327

Swahili

327. YESU ANABARIKIWA NA KUJARIBIWA

"Huyu ni mwanangu mpendwa, ninaye pendezwa naye"

Tumefikia hatua wakati Yesu alikuwa tayari kuonyeshwa hadharani kwa Waisraeli. Matayarisho yake kule Nazareti kwani kazi  hii ilikamilika wakati sawa na ule watu walikuwa wanatayarishwa kwa ajili ya kuonekana kwa mahubiri ya binamu yake, Yohana Mbatizaji. Lengo la somo hili ni kuona mfano ambao Mungu ameweka mbele yetu katika masuala ya ubatizo na majaribu.

Mathayo 3; 4:1-11

WITO WA YOHANA WA TOBA (Mt. 3:1-6)

Yohana Mbatizaji alikuwa sawa na mtangulizi wake maarufu, Eliya wote walikuwa wanavaa mavazi mabaya ambayo yalikuwa alama ya manabii, na walikuwa wakali wenye matendo ya haraka (mst 3-4; 2 Fal. 1: 8). Kusudi la Yohana lilikuwa kuharakisha akili ya watu wa Israeli ili wawe tayari kupokea neno la Ufalme kutoka kwa Masihi. Watu walikuwa wametosheka katika mbinu zao kwa Bwana na walihitaji kubadili nyoyo zao ili mbegu ya Injili iweze kuchukua mizizi  iliyokita ardhini  (Mst.3). Ujumbe wa Yohana ulitoka Isaya 40: 3-8. Alikuwa sauti ya yule anayelia jagwani kwa mioyo ilio mbele yake, kwa watu waache njia zao mbaya na wakiri dhambi zao na wabatizwe ili watambue hali yao. Utukufu wa Mungu ulikuwa  tayari kufunuliwa. Katika maandalizi Mungu alihitaji watu wote kukiri kwamba “miili yote ni nyasi, na uzur wate ni kama  ua la shamba” kama msingi kwa ajili ya toba. Mahubiri ya Yohana yalikuwa na ufanisi na yalienea (Mst. 5), hata kwa  viongozi wa Mafarisayo na Masadukayo, walikuja kumsikiliza.

UWAZI WA YOHANA NA UTABIRI WAKE (Mt. 3:7-12).

Yohana hakuwa na woga katika kushutumu watawala wa Israeli. Aliwaita "nyoka" na uzao wa nyoka. Walionyeshwa kuwa hivyo kwa matukio yaliyofuatia (Isa 59: 2-8). Haikuwa vyema kutegemea kama walivyofanya, kwa kutegemea nasaba za kimwili,  za kipindi cha Ibrahimu. Kwa sababu mada kuu ya ujumbe wa Yohana ilikuwa “Mwili ni nyasi”. "Mungu anaweza kuyafanya mawe haya yawe watoto wa Abrahamu" (Mst9). ilikuwa inafaa kwamba Yohana alifaa kuhubiri katika sehemu moja ambapo Yoshua alivuka mto Yorodani kwani pale Yoshua alipanga kama ukumbusho wa utoaji wa Mungu kwa watu wake na pale Israeli walitahiriwa. Hivyo kukana “mwili” (Yos. 4:20, 5: 8-9). Shoka la hukumu ya Mungu ilikuwa hivi karibuni ikate miti hiyo yote na kuleta ile miti itakayozaa matunda na Yohana kwa bidii aliwaonya kwamba unafiki wao haukuwa umefichwa mbele ya macho ya Mungu. Aliwaambia wazi “zaa tunda linalofaa kutubu” (Mst. 8 RSV). Lakini Yohana alikuwa mtangulizi wa Masihi na hivyo ikawa mada kuu ya mahubiri yake. "mwenye uwezo zaidi kumliko yeye” alikuwa tayari kuonyeshwa hadharani. Ubatizo wa Yohana ulionyesha mwili jinsi ulivyo, lakini huyu anayekuja alikuwa awapatie nafasi ya kuchagua- nguvu za Roho Mtakatifu au hukumu: ngano itakusanyika kwake, lakini wale wasio na maana watakuwa kama makapi na watachomwa kwa moto usioisha (Mst. 12). Hukumu ya kukataa kutubu ingeleta ukiwa na kutawanyika, lakini nafasi ya uchaguzi ilikuwa mbele yao.

UBATIZO WA YESU (Mt. 3:13-15)

Ubatizo wa Yohana ulikuwa ule wa kutubu dhambi, hivyo wakati Yesu alimjia, Yohana alipinga kwamba “anahitaji kubatizwa” na Yesu na sio kinyume chake (Mst. 14). Yesu, hata hivyo, alisisitiza kwamba kwamba Yohana ambatize akisema “hivyo itupasavyo kuitimiza haki yote" (Mst. 15). Kwa nini ilikuwa hivyo? Bila shaka Yesu hakuwa na dhambi za kukiri, lakini alijua na kutambua asili aliyozaliwa nayo, iliyofanana na ya watu wote. Katika ubatizo alikiri kwamba Mungu ni mwenye haki ilhali :Mwili ni nyasi.  Ingawa  yeye hakuwa na dhambi, mwili wake ungepita kama wa binadamu yeyote ila kwa ajili ya Neno la Mungu. Sisi pia, tunakiri kanuni hii wakati tunabatizwa. Tunapokea msamaha kupitia huruma ya Mungu, lakini tunatambua haki ya Mungu katika kuhitaji asili ya binadamu na uzoefu wao wa kutenda dhambi lazima wauawe (Rum. 3: 23-26; 6: 6-7). Kama Yesu aliona ikiwa muhimu abatizwe, basi ni jambo la maana kwamba kila mmoja wetu kufikiria jambo hili, hasa kwa sababu sisi, ni tofauti na yeye, na tunahitaji msamaha.

JIBU KUTOKA MBIGUNI (Mt. 3:16-17)

Baada ya ubatizo wa Yesu, palifuata uthibitisho wa nafasi yake kama Masihi, kwani Roho wa Mungu alikuja juu yake (Mst.16). Yohana alikuwa ameambiwa na Mungu kwamba hii itakuwa ishara ya kumtambulisha kama Masihi (Yn.1: 32-33). Njiwa siyo ishara pekee iliyotolewa- sauti kutoka mbinguni pia alitangaza maneno haya, "Huyu ni Mwanangu mpendwa, ninaye pendezwa naye” (Mst.17) hivyo huduma ya Mwana wa Mungu ikaanza. Alikuwa ametangulizwa na ishara dhabiti, na maneno yaliyofuata hayakuacha shaka kwamba alikuwa Masihi wa Israeli.

MAJARIBU NYIKANI (Mt. 4:1-11).

Mamia ya miaka hapo awali, Mungu aliwajaribu wana wake wa kitaifa, Israeli, kwa miaka arobaini kule nyikani. “Mwana” huyo alishindwa. Sasa Mwana wake mpendwa alikuwa anaelekea kujaribiwa kwa mambo yote “kama vile sisi, ingawa hakuwa na dhambi” (Ebr. 4:15). Wakati huu ushindi ungekuwa wa Mungu na njia ikafunguka kuleta wana wengi katika utukufu. Yesu alijaribiwa kupitia njia tatu mabazo dhambi hutokea, "tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha maisha" (1 Yn. 2:16). Alishinda mapendekezo haya yote ya ushawishi na hivyo kufanya Mungu aheshimiwe. “Adamu wa pili” alifaulu pale ambapo wa kwanza alishindwa, kwani katika shamba la Edeni tamaa sawa na hizi zilisababisha kuanguka kwa Adamu na Hawa.jedwali ifuatayo inalinganisha matukio haya.

 

"YALE YOTE YALIKUWA DUNIANI"1 Yn: 2:16

KUANGUKA KWA EDENI Mwanzo. 3:6

 

KUJARIBIWA KWA YESU Mat:4

 

MAJIBU YA MUNGU KWA SHETANI

Mat:4

 

‘Tamaa ya mwili’

‘mti ulikuwa mzuri wa chakula’

mst.3-"amrisha mikate hii iwe mkate"

Mst.4-"binadamu hataishi kwa mkate pekee”

‘Tamaa ya macho’

"ulifurahisha macho"

Mst.8-"akamwonyesha ufalme wote wa dunia"

Mst. 10- "Msujudie Bwana Mungu wako"

" kiburi cha maisha"

"mti uliotamaniwa kumfanya mtu awe na hekima"

Mst6-"kama wewe ni Mwana wa Mungu jitupe chini

Mst.7-"Usimjaribu Bwana Mungu wako"

 

Majibu ya Yesu yote yalitoka katika kitabu cha kumbukumbu la Torati. Hii inaonyesha kwamba Yesu alikuwa anafikiria kuhusu uzoefu wa Waisraeli wakiwa jagwani na makaripio na mashauri yale Musa aliwapa kwa sababu walishindwa. Yesu alishika mafunzo haya na na kupitia nguvu iliyotokakwa Baba yake, alishinda udhaifu ule ambao ni  kawaida kwetu sote.

USHAWISHI WA TAMAA YA MWILI: JIWE KUWA MKATE (Mt. 4:2-4).

Yesu alikuwa katika mawasiliano ya karibu na Baba yake na alikuwa amefunga kwa siku arobaini mchana na usiku. Nambari hii arobaini ni muhimu kwani inahusiana na muda wa  kupimwa na kujaribiwa (linganisha Hes 14 33-34; Yon 3: 4-10). Ni lazima Yesu alikuwa na njaa kupita kiasi na maoni ya Mshawishi yaligusia jambo hili. Mshawishi alitaka Yesu kuonyesha ukweli kwamba alikuwa Mwana wa Mungu na angeweza kutosheleza haja za kimwili kwa kugeuza jiwe kuwa mkate. Lakini Yesu akakumbuka kwamba Mungu alikuwa amesababisha waisraeli “kuteseka na njaa” ili wapate kijifunza kuweka imani yao kwa Bwana na sio kwa nguvu za mwili (Kum 8: 3). Roho wa Mungu haukutolewa ili utimize haja za kibinafsi. Akili ya Yesu ilirejelea maneno ya Musa alivyokumbuka kwamba ni Mungu aliyewaongoza wana wa Israeli wakiwa jagwani kama dhibitisho kwao wajue kile kilichokuwa mioyoni hasira - "mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu"- alionyesha kwamba chakula na kinywaji chake kilikuwa neno la Mungu na hangengatuliwa  kutoka kwa kusudi lake (Mst.4).

USHAWISHI WA KIBURI CHA MAISHA: JITUPE CHINI KUTOKA KWA HEKALU (Mt. 4:5-7).

Mshawishi kisha akatumia mbinu tofauti kwa kumshawishi Yesu kuonyesha kweli alikuwa Mwana wa Mungu kwa kuruka kutoka juu ya mnara wa hekalu na aokolewe na malaika. Kwani, si  zaburi imetabiri kwamba malaika “watakuchukua mikonono mwao ili usijikwae mkuu wako katika jiwe”  (Zab. 91: 11-12)? Lakini mshawishi alitumia vibaya Zaburi. Yesu hakudanganyika na hili. Alijua Zaburi imeweka vigezo maalum jinsi Mungu angemlinda. Zaburi inaelezea kwamba ulinzi wa Mungu ulikuwa unapatikana kwa sababu alikuwa ameweka imani yake kwa Mungu na sio katika njia za watenda dhambi  (Zab 91: 2-4, 8-10). Kutumia kinga hii ni kuoyesha kiburi cha mwili jambo ambalo lilikuwa kinyume cha roho wa Zaburi. Kwa mara nyingine fikra za Yesu zikaenda kwa Waisreali wakiwa jagwani. Wakiwa Masa na Meriba waisraeli walishikwa na kiu na wakaanza kunungunika na kutilia shaka uwepo wa Mungu "Je, Bwana yu kati yetu au la" (Kut. 17: 7). walikuwa  wametoa changamoto, na  walikuwa wanatafuta kuona namna ya tabia waliyokuwa wakishauriana na waliyokuwa wakimfanya Mungu kutimiza mapenzi yao wenyewe. Walikuwa wakimwambia Mungu kile alihitaji kufanya, kwa uchungu wa kutoamini kwao kwake, hakufanya walivyotaka. Kama Kiumbe mkuu wa ulimwengu, sio Mungu bali ni binadamu ndio walikuwa  wanapswa kujaribiwa, kama  inavyosema katika Kutoka 15:25 “ Pale Aliwadhibitishia”.  Mungu si wa kufanywa chombo cha kutimiza mapenzi ya binadamu: wao ndio wanapaswa kumtii yeye, na  wala sio yeye. Lilikuwa somo hili ambalo Musa aliwasisitizia kutoka kwa uzoefu wake wakati aliangalia historia yao katika mwisho wa kuzunguka kwao (Kum. 6:16). Katika jibu lake kwa jaribio la pili, hivyo, Yesu akadhibitisha ukuu wa Mungu kwa kukataa kufanya mapenzi ya Mungu kumtumikia yeye binafsi "Usimjaribu Bwana Mungu wako." Alijua kwamba Mungu alikuwa pamoja naye-kwa ubatizo wake wa hivi karibuni nguvu za Mungu zilikuja juu yake na sauti Yake ilikuwa imetoa dhibitisho- na kuhitaji dhibitisho lingine ilionyesha ukosefu wa imani kwa upande wake na kumjaribu Mungu.

KWA TAMAA YA MACHO: UTUKUFU WA UFALME (Mt. 4:8-10).

Hatimaye, mshawishi akaonyesha mbele ya macho ya Mungu utukufu wa falme za dunia, akimwahidi kumpa zote, japo tu atamsujudia- yote haya nitakupa kama utanguka chini na kuniabudu” (Mst.9) Yesu angepokea mara moja utawala wa ulimwengu wote bila kuteseka msalabani. Lakini alijua kwamba msalaba lazima uje kabla ya  taji. Kwa mara nyinginw bila kusita katika uamuzi wake. Alikumbuka kwa mara nyingine maneno ya Musa kwa Waisraeli kwamba Bwana alikuwa amewapa ushindi na alikuwa amewaleta hadi nchi ya ahadi. Hakuna kitu kingepatika kwa israeli kuabudu miungu ya mataifa yaliyowazunguka, kwani nguvu zao na ushindi ulikuwa kwa Bwana (Kum. 6: 10-15). Israeli walishindwa kwa jambo hili, lakini Yesu alikubali kusudi la Mungu, licha ya huzuni na mateso. Hangekubali  njia nzuri ya maisha na kwa hivyo akajibu “msujudie Bwana Mungu wako, na umwabudu yeye pekee (Mt. 4:10;.Kum. 6:13) mshawishi akamwondokea Yesu “kwa msimu” na malaika wa Mungu wakashuka “wakamtumikia” (mst.11). Tunaweza japo kwa umbali kufikiria ushirika mzuri unaohusishwa, wakati malaika walimwongeza Yesu nguvu kimwili, kiakili kwa siku zijazo.

KUSHINDA MAJARIBU.

Rekodi hii ya majaribu ya Yesu inatusaidia katika kuyashinda majaribu yetu sisi. Yakobo anatukumbusha kwamba “kila mmoja hujaribiwa wakati yeye anavutwa na kunaswa kwa tamaa yake mwenyewe" (Yak 1: 14-15). Wakati mshawishi alikuja kwa Yesu, Bwana alipuuzilia mbali mapendekezo yake na akafanya fikra zake kufikiri kuhusu masomo ambayo Musa alikuwa anawasisitizia wana wa Israeli kabla kufa kwake. Kutoka kwa rekodi hii alipata nguvu na jibu kwa mapendekezo ya mshawishi. Hapa kuna masomo muhimu kwetu sisi. Njia ya kushinda majaribio ni kufikiria kuhusu neno la Mungu na litatupa nguvu ya uamuzi na pia majibu ya matatizo yetu. Maombi kwa Baba yetu wa mbinguni yanaweza kusaidia pia. Kama vile Yohana anasema, “Huu ni ushindi ambao  unashinda ulimwengu, hata imani yetu” (1 Yn. 5: 4). Amani hio inakuzwa kwa kushika neno la Mungu na akili ya Kristo, ili majaribu yakose mahali ambapo yanaweza  kuchukua mizizi. Akili yetu daima imechangamka na fikra za kila aina hutokea. Kwa njia gani tutaweza kuweka msururu wa fikra safi? Yesu kama Mzaburi,  aliwaza usiku na mchana kuhusu sheria ya Bwana (1 Zab: 2). Fikra nzuri  zitaondoa mawazo mabaya kwani hakutakuwa na nafasi. Kwa hivyo  mitume wanatuhimiza kufikiria fikra nzuri: “yote yaliyo kweli.....haki....staha....safi.....na yote ya kupendeza....ya sifa njema: ikiwapo sifa yoyote, FIKIRIA MAMBO HAYA” (Flp. 4: 8). Ushindi wetu dhidi ya majaribu, kama ushindi wa Yesu, huanza katika akili.

MAMBO TUNAYOJIFUNZA

  • Ujumbe wa Yohana Mbatizaji una umuhimu katika kizazi chetu. Leo mtu hujivuna katika ubatili na tunahitaji kutambua kwamba "mwili ni nyasi" (1 Pet. 1: 23-25; Yak. 4: 13-17).
  • Kuja kwa Yesu kulileta hukumu; watu walikuwa wachague aidha kumtumikia au kumkataa. Kristo akiwa mlangoni tuna huo uchaguzi na hisia ya haraka. Hebu tuchague nguvu za Mungu katika neno lake na kuendeleza tabia yake (2 Pet 3: 11-14; Lk. 21: 34-36).
  • Yesu aliona ni muhimu kutambua haki ya Mungu katika ubatizo. Kiasi gani hili ni muhimu kwetu sisi wenyewe, tunao hitaji kuomba msamaha wa Mungu (Mdo 2: 37-38; 19: 1-5).
  • Yesu alishinda mapendekezo ya mshawishi kwa sababu akili yake ilikuwa imezama katika Neno la Mungu-"Kuweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwako ndani ya Kristo Yesu" (Flp 2: 5-11).

MAKTABA YA KUREJELEA:

"The Story of the Bible" (H. P. Mansfield)—Tol. 8, Kurasa: 69-89

"A Life of Jesus" (M. Purkis)—Kitabu 2,Sura 3, 4

"Nazareth Revisited" (R. Roberts) Sura 11

MASWALI YA AYA:

  1. Yesu alimaanisha nini alipomwambia Yohana Mbatizaji: "Hivyo itupasavyo kutimiza haki yote"?
  2. Jinsi gani Yesu alionyeshwa kuwa Masihi wakati wa ubatizo wake? Jinsi gani Yohana alimtambua akiwa hivyo?
  3.  Je, ni njia gani tatu ambazo mtume Yohana anasema dhambi hutokea? Linganisha njia hizi tatu na majaribio matatu ya Yesu.
  4.  Orodhesha lengo kuu la huduma ya Yohana Mbatizaji.

MASWALI YA INSHA:

  1.  Kwa nini Yesu alibatizwa? Taja katika jibu lako kwa nini ni muhimu kwetu sisi kubatizwa.
  2.  Jinsi gani Yesu anatofautiana na Adamu na Hawa pamoja na Israeli katika suala la majaribu yake?
  3. Jinsi gani Yesu aliweza kushinda Majaribio? Ni masomo gani tunaweza kujifunza kutokana na mfano wake?

 

 

Swahili Title
327. YESU ANABARIKIWA NA KUJARIBIWA
Sub type
Sub sub type