329

Swahili

329. KUKUBALIKA KWA NJIA YA AJABU SAMARIA

"Yeyote atakaye kunywa maji ninayompa hataona kiu kamwe"

Baada ya Yesu kuongea na Nikodema akaingia Yudea pale alibatiza wengi. Wakati huo huo Yohana Mbatizaji alikuwa anabatiza watu huko Ainoni. Ukweli ni kwamba wote wawili walikuwa wanabatizana kuliibua maswali katika akili za wafuasi wa Yohana. Ni mamlaka gani Yesu alikuwa nayo  ya kubatiza? Katika jibu lake, Yohana alijiondoa kutoka kwa nafsi yake na kutoa ushahidi kwa asili na mamlaka ya Yesu na hivyo haja ya wanafunzi wake kuweka utii wao kwake. “ Lazima yeye azidi mimi nipungue”, Yohana akasema, na hivyo ni muhimu kwamba katika Yohana 4:1  tunaambiwa kwamba Yesu “alibatiza wanafunzi WENGI kuliko Yohane”. Wakati Bwana  alipitia Samaria “Wasamaria wengi wa mji huo waliamini". Hivyo Yohana 4 inaonyesha jinsi injili ilitambaa na kuleta matokeo mazuri katika jamii hii iliojaa watu wa Mataifa. Lengo letu katika somo hili ni kuona jinsi Yesu ni mtoa maji ya uzima  kwa Wayahudi na watu wa mataifa mengine, na kuona mahitaji ya ibada ya kweli.

Yohana 4:1-42

AKISAFIRI KASKAZINI KUPITIA SAMARIA (Yn. 4:1-6).

Habari zilifikia mamlaka kwamba idadi kubwa walikuwa sasa wanamfuata Yessu kama walivyokuwa wamefanya Yohana. Tabia yao ilifanya mahubiri zaidi kutohitajika kwani walikuwa na wivu wa ushawishi wake na walitaka kumshika. (Mst.1) hivyo aliondoka Yudea na kuelekea Kaskazini. Kulikuwa na njia mbili zilizoelekea Galilee. Njia moja ilikuwa inapitia Samaria, lakini ilichukuliwa na Wayahudi wakiwa kwa makundi kwani ilikuwa na hatari nyingi. Njia hio nyingine mashariki mwa Yorodani ilikuwa rahisi, lakini kwa Yesu ilikuwa na hatari kutoka kwa utawala na hivyo alichagua njia ya Samaria: "Naye alikuwa hana budi kupita katikati ya Samaria." Akafika Sikari, moja kati ya miji ya Samaria, iliyokuwa karibu na Shekemu, ambapo Mungu alimpa Ibrahimu ahadi ya kwanza ya nchi ya Ahadi, na pia karibu na sehemu ya ardhi ambayo Yakobo aliwapa wana wa Yusufu (Mwa. 12: 6-7; 48:22). Waliwasili katika kisima cha Yakobo saa sita mchana na Yesu akakaa chini, akiwa amechoka  wakati wanafuzi wake  wakinunua chakula katika mji.

FUMBO LA MAJI YA UZIMA (Yn. 4:7-15)

Hata akiwa amechoka,Yesu alikuwa tayari kusahau mahitaji yake kwa ajili ya mahitaji ya wengine . Alizungumza na mwanamke Msamaria aliyekuja kutafuta maji kisimani, na hatua kwa hatua alimleta mpaka akapata utambuzi wa kwamba angeweza kumpa maji yanayoishi ya uzima wa Milele. Kulikuwa na sababu nyingi ambazo zingemfanya Yesu kumpuuza mwanamke huyu: sio tu kwa sababu alikuwa amechoka, lakini kwa sababu Wayahudi walikuwa na ubaguzi dhidi ya kabila la Wasamaria lililochanganyika, na alijua alikuwa mtenda dhambi. Hata hivyo, alisema, "Nipe maji ninywe." Lilikuwa swali lililochaguliwa kwa makini kwani Yesu alijua jinsi mwanamke yule angemjibu na jinsi yeye angemjibu. Alionyesha mshango kwamba anaweza dhubutu kuongea na yeye, Msamaria. Angeharibu msimamo wake kwa ajili ya maji (Mst. 9)! Lakini Yesu hakushughulika na utamaduni ambao haukuwa na maana na ulikuwa na misingi ya chuki na tamaa. Hakushughulika sana na jibu lake ila kwa upole alimpa changamoto ya utambulisho wake. Alijua alikuwa Myahudi lakini sio nani! Alijibu * "Kama tu ungalijua zawadi ya Mungu, na ni nani anaye kuambia umpe maji anywe, ungalikwisha mwomba, naye angekupa maji yaliyo hai "(linganisha. Yn. 3:16). Visima mara nyingi viliitwa "zawadi ya Mungu", na "maji yaliyo hai" ilikuwa  maelezo ya kawaida ya maji yanayotiririka  kutoka kwa kisima.

Hiyo ndio maana mwanamke yule alichukua maneno ya Yesu kama ya kawaida, lakini Yesu alitaka ayachukue kwa maana yake ya Kiroho. Hakuelewa kwamba katika mambo ya kiroho alikuwa amechoka na nafsi ilio na kiu katika kisima cha uzima. Mwanamke alidai kwamba Yesu hawezi kutoa maji ya uzima kwani hakuwa na njia za kuchota maji kutoka kisimani, na kisha akamkaripia kwa kudai kuwa mkuu kuliko Yakobo, ambaye aliwapa kisima kile kwa ajili ya watoto na mifugo. Hapa palikuwa na changamoto katika kulinganisha. Yesu alijibu vipi? Hakukuwa na dharau bali kuweka masuala makuu katika mstari wa mbele. Alisisitiza kati ya tofauti ya maji ambayo angetoa na yale alikuwa anaomba. Maji ya kisima yangesababisha kiu tena; lakini "maji yaliyo hai"(yaani Neno la Mungu ni "chemchemi" -Yer 2:13; Isa. 12:3; 49:10; 55: 1-3), ambayo angeweza kutoa na ingekuwa chemichemi ya kudumu ya uzima wa milele (Mst. 13-14). Hivyo kwa njia isiyo ya moja kwa moja ikawa ni ulinganishi wake na Yakobo.Bila kuelewa maana ile kikamilifu aliomba “maji ya uzima” kujipumzisha kutoka safari za usoni kisimani. Hatua nyingine ilikuwa imefikiwa. Mazungumzo yalikuwa yamegeuka. Badala ya Yesu kuomba maji, yeye ndiye alikuwa anaomba maji yake! Yesu sasa lazima ampatie misingi ya imani.

YESU ANAJITAMBULISHA NA MWANAMKE ANAAMINI (Yn. 4:16-30)

Mwanamke aliomba maji ya uhai lakini Yesu alimjibu, "Nenda ukamwite mumeo uje naye hapa." Kwanini alisema hivi, kwani haikuwa na uhusiano na ombi lake? Kwanza kabisa ombi la kwenda kumtafuta mumewe lilikuwa la dhati, kwani kama zawadi ingetolewa basi ingekuwa bora ingawanywe kati yao. Lakini cha muhimu zaidi, Yesu alikuwa anampa misingi ya imani yake kama Masihi kwa kufanya kauli ambayo alijua kwamba ingempa fursa ya mwanamke yule kuonyesha historia yake ya awali. Hii ingekuwa ishara dhabiti kwamba alikuwa nabii, na hivyo alipswa kutilia maanani kile Yesu alichosema ni "maji yaliyo hai". "Nenda ukamwite mumeo ..." alijibu kwa haraka, "Mimi sina mume." Yesu alionyesha ujuzi wa hali ya juu wa maisha yake ya hapo awali ambayo yangekuwa yametoka kwa Mungu: “Umesema kweli, kwamba huna mume: Maana umekuwa na waume watano, na hata yule unayeishi naye sasa si mume wako." Maneno ya Yesu hayakuwa sahihi tu lakini “kutoka kwa Mungu”, yalipenya moyo wake: na yalikuwa yamesemwa ili kufunua dhambi zake na haja zake. Alitambua kwamba alikuwa nabii. Kwa muda alikimya kwa aibu, akiepuka amri yake, akauliza swali lenye utata kuhusu pale Mungu angekubali kuabudiwa-Yerusalemu au Samaria. Wayahudi walichukulia Yerusalemu kama “mahali panapo paswa kuabudiwa”, lakini katika siku za Nehemia, Sanbalati alijenga hekalu pinzani juu ya Mlima Gerizimu karibu Shekemu, ambapo wasamaria walienda kuabudu. Jibu la yesu katika  mistari 21-24 ni mfano wa kuigwa.

 Anapita maswali madogo ya uaminifu na kurejelea swali kuu la uhusiano wa mtu binafsi na Mungu. Daima Yesu aliweka mambo katika mtazamo sahihi na sisi tunapaswa kufuata mfano wake. Aliongea kwa njia yenye utulivu. “mwanamke niamini mimi” (sasa alikuwa na sababu nyingi za kumwamini), “wakati unakuja” (33 BK na hatimaye 70 BK wakati Yerusalemu na hekalu zitakapoharibiwa) “wakati  nyinyi wala mlima huu hata Yerusalemu, mtamwabudu Baba” (mst.21) Yesu alionyesha kwamba alikuwa "Mwokozi wa ulimwengu" (Mst. 42), kwani  baadaye kungekuwa na "majira ya Mataifa" wakati watu wa mataifa  watakapoitwa pia (Lk. 21:24). Katika Matendo ya Mitume 10 tunasoma Petro alikuwa ametumwa na Mungu kwa Jemedari wa mataifa Kornelious, wakati kwa mara ya kwanza, “mmoja wa taifa lingine” alibatizwa rasmi kwa jina la Yesu Kristo. Hivyo Mungu anaweza kuabudiwa inavyokubaliwa kwa mahali popote, Yerusalemu ingawa ilikuwa mahali muhimu katika uabudu wa Mungu kwani ingekuwa mahali muhimu kwa ibada miaka ambayo ingefuata(Mk 11: 15-17; Zek. 14:16). Yesu akafanya ulinganishi kati ya dini ya Wasamaria na Wayahudi; Wasamaria “hawakujua kile walichokuwa wakiabudu” walikuwa taifa lililochanganyika  na ibada yao ilikuwa mchanganyiko wa machafuko ya sanamu na hofu ya "Mungu wa nchi" (2 Flm. 17: 24-41). Walishikilia tu sehemu ya Pentatau kama walivyoongozwa, ambapo Wayahudi walishikilia Agano la Kale Yesu alisema kwamba "wokovu ulikuwa wa Wayahudi". Yesu kisha aliendelea kuelezea aina ya waabudu wanaokubalika na Mungu (Mst. 23-24).

Alielezea kwamba tofauti na sanamu, Mungu ni Roho, anayetambua, kujua, kuhisi na anatarajia binadamu walioumbwa katika "sura na mfano wake" kuelewa kusudi lake na upendo, na kujibu  kwa ibada na huduma. Mungu amewapa binadamu rekodi ya Njia zake na anawataka wamfahamu na “wamwabudu kwa roho na kweli” Ni dhahiri kwamba Yesu alinukuu maneno ya Yoshua yaliyonenwa katika sehemu hio (Yos. 24:14). Katika sura hiyo Yoshua alikuwa amechukua umakini wa Waisraeli kwa  matendo makuu ya Mungu dhidi yao na kuwaita waje wamtumikie Mungu "kwa moyo wa dhati na kweli". Israeli yote haikuwa imefanya hivi kwa Yoshua wakati aliwauliza watu wachangue kati ya ibada ya Sanamu na ibada ya Bwana Yesu (ambaye alikuwa mfano wa Yoshua) alikuwa anatoa wito huo. Mwanamke alijua ya kutosha kuhusu agano la kale kuunganisha dhana hii kuu ya Masihi (mst. 25;. linganisha "yeye atatuambia mambo yote" na Kum.18:18). Wakati ulikuwa umefika wa Bwana kujitambulisha, alimwambia kwamba alikuwa Massia. Katika kuangalia matamshi yake, tunaona jinsi kwa utaratibu alimwongoza yule mwanamke kutoka hali ya kukosa imani mpaka pale alipoamini. Wakati huo wanafunzi wake wakawasili na kukatiza mazungumzo yao. Tofauti na Bwana wao hawangeweza kuzungumza na mwanamke yule Msamaria, Ingawa  hawakusema hivyo. Mwanamke akenda akiwa amejaa ajabu ya imani hata akasahau kile alichokuwa amekuja kufanya kisimani- akaondoka kisimani! Punde tu alipofika mjini akatangaza imani yake mpya “njooni mumuone mtu, aliyeniambia mambo yote niliyoyatenda: he siye kristo? Wasamaria walioamini walianza kumiminika na YESU ALIWAONA.  

NYAMA YA KWELI: KUTENDA MAPENZI YA MUNGU (Yn. 4:31-42).

Wanafunzi walimlazimisha Yesu ale chakula lakini juhudi zao hazikufanikiwa. Furaha ya huduma na kudhirika katika kuhudhuria mwitikio wa mwanamke, ilikuwa imechukua nafasi ya chakula kwa muda.  Hakuwa na ufahamu wa harakati zao karibu na yeye. Wakati Yesu aliwaambia kwamba alikuwa na nyama ya kula ambao hawaijui, walifikiria kwamba alikuwa ameipata kutoka mahali pengine. Kisha akawalezea kwamba NYAMA YAKE  ilikuwa kufanya  mapenzi ya Yule aliyemtuma (linganisha Zab 40: 7-8). Ilikuwa miezi minne kabla ya mavuno lakini Yesu alisema kwamba mashamba yalikuwa sasa meupe na tayari kuvunwa Alimaanisha nini? Macho yake yalikuwa yameinuliwa na  aliweza kuona kundi kubwa la watu wakija kutoka vijinini kujifunza kumhusu kwa sababu ya maneno ya yule mwanamke (linganisha. Isa. 49:18). Wanafunzi walikuwa na kazi kubwa ya kufanya: walikuwa wanapaswa kuvuna mavuno wa watu kwa ajili ya Mungu. Yesu alikuwa amepanda mbegu ya Neno. Lazima wangeingia kazini ambayo ilikuwa imeshanza tayari na kuimaliza kazi ile. Matokeo yake ni kwamba Wasamaria wengi waliamini kwa sababu ya ripoti ya mwanamke, na wengine wao wenyewe waliamini wakati waliposikia wao wenyewe katika siku mbili ambazo Yesu alikuwa nao (Mst. 39-42).

MAMBO TUNAYOJIFUNZA:

  • Yesu pekee ndiye anaweza kutoa maji ya uhai ya uzima wa milele.
  • Ibada ya kweli leo haitegemei mahali, lakini juu ya tabia yetu kwa Mungu.
  • Mungu amemuumba mtu kwa mfano wake na anabudiwa inavyokubalika wakati watu wanamtambua na kujibu kutoka moyoni katika ukweli na usafi.
  • Nyama ya kweli ni kufanya mapenzi ya Baba na kuteseka kwa ajili yake katika mavuno ya watu.

MAKTABA YA KUREJELEA:

"A Life of Jesus" (M. Purkis)—Kurasa 76-80

"The Gospel of John" (J. Carter)—Sura 4

"Nazareth Revisited" (R. Roberts)— Sura 14

 

MASWALI YA AYA:

  1.  Nani walikuwa wasamaria na waliamini nini? Je,  nini Yesu alimwambia mwanamke Msamaria kuhusu ibada ya kweli?
  2.  Elezea jinsi Yesu alimwonyesha mwanamke Msamaria kwamba yeye alikuwa nabii.
  3.  Ni masomo gani tunajifunza kuhusu ibada ya kweli kutokana na tukio la mwanamke Msamaria?

MASWALI YA INSHA:

  1. Kumbuka matukio ambayo yalitokea wakati Yesu alikutana na mwanamke msamaria kisimani.
  2. Orodhesha hatua ambazo mwanamke Msamaria alichukua ili kukiri Yesu kama Masihi.
  3. Ni masomo gani wanafunzi na watu walijifunza kutoka kwa mkutano wa mwanamke Msamaria? Yesu aliwafunza haya kwa jinsi gani?

SEHEMU 2: MASOMO KATIKA UANAFUNZI

Mtume Paulo anasema kwamba Yesu “ataleta wana wengi  wafike kwenye utukufu” (Ebr 2:10). Baadaye ananukuu kutoka Zaburi 22:22 ambapo Kristo anasema: "Nitalihubiri jina lako kwa ndungu zangu, katikati ya  mkusanyiko nitakusifu”. Kazi ya Bwana ilikuwa  kuwaita  waume na wanawake kutoka kwa dunia wawe wawe wafuasi wake.  Jinsi huduma ya  Bwana ilivyoendelea na “akifundisha katika masinagogi na kuhubiri Habari Njema ya Ufalme, huku akiponya kila aina ya magonjwa” alifuatwa na "umati mkubwa wa watu” (Mt. 4:23-25). Miongoni mwa hawa kulikuwa na wale waliokuwa wamefurahishwa kwa dhati na "maneno ya neema yaliyotoka kinywani mwake" na walitaka kupata mafundisho. Wakawa wanafunzi wake. Kutoka kwa kundi hili, Yesu akachagua kumi na wawili ambao watakuwa wakifuatana na yeye katika huduma yake na baada ya kufufuka, watatumwa kuwa wanafunzi wake. Wanafunzi inamanisha (wasomi) wanaopaswa kufunzwa,  kama jina lao  lingemaanisha kitu chochote. Kupanua mafunzo yake, Yesu aliwachukua mpaka kwa milima ya nchi na “alipokaa chini, wanafunzi wake walikuja kwake, na  alifungua kinywa chake na kuwafunza” (Mt. 5: 1-2). Katika njia ya ajabu, pale Bwana alibainisha sifa za uanafunzi wa kweli katika kile sasa tunachojua kama hotuba au Mahubiri ya Mlimani.

 

 

Swahili Title
329. KUKUBALIKA KWA NJIA YA AJABU SAMARIA
Sub type
Sub sub type