334. MIUJIZA YA UPONYAJI KAPERNAUMU
"Na Yesu akamwonea huruma, akanyoosha mkono wake ..."
Kapernaumu ikawa makao makuu ya huduma ya awali ya Yesu, Galilaya ilikuwa ni mji wa nyumbani wa mitume wake maarufu kama, Petro, Andrea, Yakobo na Yohana, wote ambao walikuwa wavuvi. Sifa ya Yesu ikaanza kuenea kwa mataifa baada ya kumponya pepo katika sinagogi la Kapernaumu. Watu walifurahi, sio kwa nguvu za miujiza yake lakini pia kwa mamlaka ya mafundisho yake. Matokeo yake, umati mkubwa ukaja kwake â kutoka sehemu zote zilizozinguka Galileeâ.
Lengo la somo hili ni kutafakari juu ya umaarufu wa Yesu, kujitolea na huruma yake, na pia mamlaka yake na nguvu.
Marko 1: 29-45; 2: 1-12
UPONYAJI KATIKA NYUMBA KAPERNAUMU (Mk. 1:29-34)
Baada ya miujiza katika sinagogi, Yesu aliondoka mara moja na kuelekea nyumbani mwa Petro ambapo aliishi na ndugu yake Andrea, mke wake na mama mkewe. Walikumbwa na hali ya ugonjwa- mama mkwe alikuwa mgonjwa homa. Mitume walikuwa wanajifunza kumtegemea Mungu kwa usaidizi wakiwa na wingi wa Matumaini, âwalimwambia habari zakeâ; anaweza kuponya pepo hivyo anaweza kumponya rafiki yake wa dhati. Aliweza kunena na ugonjwa ukapotea! Katika tukio hili na matukio yaliyofuatia jioni hio, walijifunza kwamba licha ya Yesu kuwa na Nguvu, alikuwa amejaa huruma. Bwana alipochukua mkono wa mama mkwe wa Petro, alijitambulisha yeye mwenyewe na mwanamke yule mgonjwa aliyelala mbele yake. Mguso wake ungempa mwanamke yule imani. Yesu hakujiondoa kutoka kwa hisia za wale ambao alishirikiana nao. Kwa kweli âameyachukua magonjwa yetu" (Isa 53:4; Mt. 8:17). Yesu âakamwinuaâ, kuashia kitendo cha kuinua wengi wanaoweka matumaini yao ndani yake. Yeye ndiye analeta wale waliohusishwa naye kutoka kaburini wakati atarudi kutoka mbiguni katika ujio wake wa pili (37:34 linganisha Zab; 30: 3; 40:2).
Ripoti ya uponyaji wa pepo hapo awali ulifufua matumaini ya wengi waliokuwa wamepigwa na magonjwa yasiyopona. Katika mwisho wa Sabato, âwakati jua lilituaâ, wote waliokuwa na magonjwa na wenye kichaa waliletwa kwake. Kumbukumbu inasema kwamba, âwote wa mji ule wakakusanyika nje ya mlango." Yesu akawaponya wote. Fikiria mabadiliko ya hisia kutoka dhiki hadi furaha. Kumbuka adhari kwa wale waliokuwa wamekuja kutazama. Ilikuwa onyesho la ajabu la Nguvu za Mungu!
Katika yote haya kulikuwa na hitaji kuhusu uvumilivu wa Yesu. Alikuwa ameadhirika mwili na akili kwani hakuponya tu bali, alitaka kuona kwamba kila mmoja alitambua wema wa Mungu. Vitendo vya Yesu vya kuponya vilikuwa zaidi ya nguvu: lakini ni matendo ya kutoa kile kilichokuwa cha Mungu na kuwapa wengine.
SALA YA ASUBUHI (Mk.1:35-39)
Ingawa alikuwa amechoka kimwili kwa shughuli ya kuponya watu usiku kucha, mwili wake uliburudishwa kwa kupata masaa machache ya usingizi. Lakini akili yake ilitamani uwepo wa Baba yake na nguvu mbali na umati mkubwa wa watu. âMapema kabla ya siku kuanzaâ, Yesu aliamka na âkuondoka hadi mahali pa faragha na kuomba (linganisha Mat. 6: 6). Mbali na masuala ya binadamu ndiyo aweze kufikia chanzo cha nguvu zake za ndani bila kukatizwa wakati wa mawasiliano na baba yake.
Alfajiri kulikuwa na ishara kwamba matukio ya usiku yangerejelewa, lakini Yesu hakupatikana ndani ya nyumba. Petro aliongoza shughuli ya kumtafuta na mwishowe walimpata Bwana akiwa faraghani akisali, lazima liwe tukio ambalo hawangeweza kusahau. Walikuwa wanaanza kujifunza kwamba matendo yake ya upendo na Nguvu, ndio chanzo cha ndani cha maisha yake. Alikuwa na ushirika mtakatifu na Baba yake. Kama sala ilikuwa hitaji kwake, je ina umuhimu gani kwetu sisi tunaokosa urithi wake wa kimungu na maono?
Petro akaja na ujumbe: âWatu wote wanakutafuta ' akitarajia bila shaka kwamba Yesu ataharakisha kurudi kwa nyumba. Je angekubali fursa hii ya kujionyesha kwa umati kupita? Jibu la Bwana lazima liwe liliwashangaza sana; âTwendeni kwa mji mwingine, ili niweze kuhubiri huko pia; ndio maana nilikuja (Mst.38). Je alikuwa tofauti na hakujali mahitaji ya binadamu? Huduma yake ilikuwa na sehemu mbili, Kuponya na Kuhubiri. Kuponya kungerejesha afya ya binadamu kwa muda mfupi lakini kuhubiri kungeweza kuwaokoe milele. Kuokoa kulikuwa ishara ya kuonyesha mamlaka yake ya kuongea. Kuhubiri kulikuwa jukumu lake kuu, na hio ndio ilikuwa sababu ya kutumwa kwake (linganisha Isa. 61:1). Kulikuwa na hatari kwamba umuhimu uliokuwa umewekwa kwa uponyaji ungeadhiri jukumu lake kuu. Hivyo akaondoka Kapernaumu kutimiza jukumu lake. Pengine kuondoka kwake kulikuwa uamuzi uliotokana na Sala yake. Zaidi ya hayo watu wa Kapernaumu wangefaidika; baada ya msisimko kuisha, wangekuwa na nafasi ya kutafakari maneno yake kufuatia matendo yake (linganisha Yn 5: 36-38).
MTU WA KWANZA MWENYE UKOMA ATAKASWA (Mk. 1:40-45)
Sheria ya Musa iliwachukulia walio na ukoma kama waliokataliwa na jamii. Walikuwa wanapaswa kuishi nje ya mji (5 Hes. 1-4) Kwa umbali mtu yule mwenye ukoma alishuhudia nguvu za Yesu; aliona machungu ya walio wagonjwa yanageuka furaha, afya na alitamani kutakaswa. Kwa ujasiri na unyenyekevu mkubwa alikuja kwa Yesu. Akipiga magoti alimsihi Bwana, âukitaka, waweza kunitakasaâ. Imani yake kwa nguvu za Yesu kumwokoa hazikutoshana na ujasiri wake kwa nia ya Yesu kufanya hivyo. Alihisi kwamba kile kitu kilichokuwa katikati yake na kutakaswa ni nia ya Yesu ya kufanya kitendo kile. Je Yesu huyu hangebangua watu wa aina yake kama wanadamu wengine? Jibu la Yesu ni muhimu:
âYesu akamhurumia na kunyoosha mkono wake, na kumgusa, akamwambia, ânataka, uwe msafiâ (Mst.41).
Hakukuwa na hali ya kusita katika Yesu. Haikuwa na haja kumbembeleza aonyesha huruma. Huruma ilikuwa inahusika katika miujiza yote ya Yesu na mtu mwenye ukoma angetambua kwamba ingeonyeshwa kwake.
- âAlimgusaâ. Hili lilikuwa jambo la ajabu kwani watu wenye ukoma hawakupaswa kuguswa kwani iliashiria âkujinajisi".
- âNataka, uwe msafiâHapa palikuwa na maneno ya furaha na kufariji. Yana maanisha nini kwetu? Neno âMimiâ kutoka kwa Bwana halijapoteza umuhimu wake katika nyoyo za wanaomini anaweza kuokoa.Yesu hakuwakataa hao. Daima aliwaalika watu âwaje kwakeâ (linganisha Isa 55: 1-3; Mt 11: 28-30). Hapa bila shaka palikuwa na nguvu za Mungu.
Matokeo yalikuwa uponyaji wa haraka. Badala ya Bwana kuambukizwa unajisi, alitoa utakasaji. Ukoma ulikuwa ugonjwa ambao ungeweza kuondolewa kwa mkono wa Mungu (Kut: 4: 7; Hes: 12: 10-15, 2 Flm. 5:7-8). Hapa bila shaka palikuwa na nguvu za Mungu.
Yesu alimwambia mtu yule asimwambie yeyote kilichotokea na ajionyeshe kwa makuhani âkama ushuhuda kwaoâ na kutoa sadaka iliohitajika kulingana na sheria ya Musa. Yesu hakutangaza nguvu au kujisifu. Mambo haya ni ya kibinadamu ambayo hayana nafasi katika heshima ya mtumishi wa Mungu (Isa. 42. 1-4; Mt 12: 16-20).
Ukoma uliwakilisha laana ya kifo katika njia ya kuonyesha wazi jinsi mwili unavyooza wakati mwadhiriwa yuko hai. Kama vile kifo kimetokea kwa ajili ya dhambi, hivyo ugonjwa huu ulikuwa kama adhabu katika matukio fulani ya dhambi (Hes.12:10; 2 Fal. 5: 7-8; 2 Nya. 26:19). Sadaka iliohitajika kwa utakaso wake ilifanana na kazi ya ukombozi ya Bwana. Katika muujiza huu tunaona utabiri wa kazi ya Bwana, kwani kupitia kwake kifo kitamezwa na uzima.
UPONYAJI WA DARINI (Mk. 2:1-12)
Mtu yule mwenye ukoma hakutii maagizo ya Yesu âkutomwambia mtu kitu chochoteâ, lakini aliwatangazia wote kuhusu uponyaji wake. Matendo yake yalifanya makundi makubwa ya watu kukusanyika kwa Yesu, na kufanya akae jagwani, lakini licha ya hili âwakaja kwake kutoka kila upande" (Mk. 01:45). "Baada ya siku kadhaa" wakati msisimko wa hapo awali ulikuwa umepungua, Yesu akaingia katika âNyumbaâ katika Kapernaumu.
Habari za kurudi kwake zikaenea, watu kwa mara nyingine, wakamzingira. Milango ilikuwa imejaa watu wale walikuwa wanataka kumwona. Hili lilileta tatizo kwa kundi la wanaume waliotamani kupata uponyaji wa rafiki yao aliyekuwa amelazwa kwa kitanda. Kwa njia gani wangeweza kumpeleke kwa mponyaji katikati ya umati huo wote! Imani ikapata njia. Walimwinua hadi juu ya paa wakaondoa upande moja na wakamshusha mpaka pale Yesu alikuwa mbele ya kila mtu! Mahubiri ya Yesu yalikatizwa na mtu yule mwenye ukoma. Jambo hili lingeonekana kama la kiburi. Je angepata majibu gani?
Yesu alifurahishwa na imani iliotokana na mtu huyu kuja kwake âBila Imani, ni vigumu kumfurahisha Munguâ. Mtu aliye na ukoma aliamini, na alisamehewa na kuponywa: mahitaji ya wokovu sio tofauti leo. (Mk. 16:16). Kuna soma nzuri katika yote haya- Yesu hawatoroki wale wanaomtafuta na moyo wa kweli (Mt.7: 7-8).
Lakini kuna wale katika umati ule waliomkosoa kwa kusamehe dhambi: â kwanini mtu huyu anaongea hivyo? Nani anaweza kusamehe dhambi isipokuwa Mungu pekee?â Hisia kali zikaanza kuamka katika nyoyo za walimu wa Sheria, ambao sifa na cheo chao kilikuwa kinaadhirika kwani Yesu alikuwa amepata umaarufu miongoni mwa watu. Tayari walikuwa wamekosa umaarufu (Mk.1:22), mbegu ya wivu ilikuwa inaanza kushika mizizi, na kwa muda usio mrefu ingekua chuki na mauaji ya hadharani. Yesu alielewa hisia zao. Hakukuwa na kosa kuuliza kama binadamu alikuwa na ruhusa ya Mungu kusamehe dhambi. Lakini kulikuwa na makosa kutia shaka wakati ushahidi ulioanzisha mamlaka haya ulikataliwa. Yesu alikuwa anaenda kuwapatia sababu ya kukubali kwamba alikuwa na mamlaka hayo. Ilikuwa ni rahisi kwa binadamu yeyote kusema, âdhambi zako zimesamehewaâ ilikuwa vigumu zaidi kusema kwa mtu mwenye ukoma, âInuka, chukua kitanda chako uendeâ. Ushahidi wa kuponywa ungejaribiwa na watazamaji, lakini msamaha si jambo ambalo linaweza kuonekana-katika kumponya yule mtu, Yesu alikuwa anatoa ushahidi wa kutosha kwamba alikuwa na Mamlaka kutoka kwa Mungu kusamehe dhambi.
Muujiza huu uliwafanya wengi kuamini, kwani walimtukuza Mungu wakisema, "Hatujapata kamwe kuona jambo kama hiliâ. Kinyume na, kukataa kwa viongozi kuona Yesu alikuwa amechaguliwa na Mungu katika kazi zake kubwa zilisababishwa kuangamizwa kwao.
MAMBO TUNAYOJIFUNZA:
- Yesu alifahamu hisia na udhaifu wa wale waliokuwa karibu naye.
- Mguso wake na kazi zake zilileta amani ya akili na faraja kwa watu wanaoteseka ambao walimtafuta. Tunaweza kuwa na uhakika wa haja yake kwetu na wasiwasi wake kwa ajili ya ustawi wetu wa kiroho.
- Uponyaji alikuwa shahidi mkumbwa uliotumiwa na Yesu kutoa msisitizo kwa Ukweli aliokuwa akihubiri.
- Yesu alifunza kwamba ugonjwa na kifo zinaweza tu kushindwa kwa imani katika nguvu ya Mungu. Kama tunaweza kukuza imani sawa na ile ya watu wale ambao waliponywa, basi sisi pia tunaweza kuepuka madhara ya dhambi wakati wa kurudi kwa Bwana Yesu Kristo.
MAKTABA YA KUREJELEA:
"A Life of Jesus" (M. Purkis)âKurasa 101-113
"The Gospel of the Son of God" (L. G. Sargent)âKurasa 25-35
"Law and Grace" (W. F. Barling)âKurasa 191-192
MASWALI YA AYA:
- Kwa jinsi gani Yesu alitafuta faraja kutoka kwa Baba yake kufanya kazi iliokuwa mbele yake? Onyesha jibu lako kwa kurejelea matukio ya Kapernaumu,
- Yesu "ameyachukua magonjwa yetu", alisema nabii Isaya. Onyesha ukweli wa kauli hii kwa kurejelea matukio kule Kapernaumu.
- Elezea uponyaji wa mtu aliyepooza kule Kapernaumu. Jinsi gani Yesu alidhibitisha katika tukio hilo kuwa alikuwa na mamlaka ya kusamehe dhambi?
- Kwa nini Yesu alifanya miujiza?
MASWALI YA INSHA:
- Andika kuhusu miujiza iliyofanywa na Yesu katika mkoa wa Kapernaumu wakati wa huduma yake ya awali ya Galilaya. Ni masomo gani tunaweza jifunza?
- Andika kuhusu uponyaji wa mtu mwenye ukoma aliye kuja kwa Yesu. Jinsi gani Yesu alivuka sheria ya Musa katika kukabiliana na mtu mwenye ukoma?
- Andika insha juu ya njia ambayo Yesu alitumia miujiza kuonyesha kwamba alikuwa na mamlaka ya Mungu.