335

Swahili

335. BETHESDA: UPONYAJI SIKU YA SABATO

"Inuka, chukua kitanda chako utembee"

Katika somo hili, Yesu anakuja Yerusalemu kwa tukio la pili lililo rekodiwa la huduma yake na katika kisima cha Bethesda anaponya kiwete mwenye miaka 38 siku ya Sabato. Hii ni ishara ya tatu iliyo rekodiwa katika Injili ya Yohana. Kitendo hiki kilisababisha kusumbuliwa na Wayahudi na kikasababisha mazungumza marefu kutoka kwa Yesu ambapo alionyesha maana ya kweli ya sheria ya Sabato ambayo walikuwa wameshindwa kuelewa kabisa. Aliendelea  kuongea kuhusu ushirika wa karibu aliokuwa nao na Mungu, na mamlaka aliyokuwa amepewa. Alimalizia kwa kuorodhesha mashahidi wa madai yake na kuwaonya kwamba, wasipobadilisha tabia zao kuelekea kwake, watakosa uzima wa milele.

Lengo la somo hili ni kuona mamlaka na nguvu za Yesu kupitia mashahidi hawa watatu.

Yohana 5

MTU MGONJWA ANAPONYWA (Yn. 5:1-9).

Kulikuwa na birika karibu na kona ya kaskazini-mashariki mwa hekalu iitwayo Betheseda, kumaanisha “Nyumba ya Rehema” kulikuwa na idadi kubwa ya wagonjwa waliokuwa wamekusanyika wakiwa na hamu ya kuwa wa kwanza kuingia katika birika lilochemka maji. Birika ile ilipata maji yake kutoka kwa  chemichemi iliokuwa na madini ya kimatibabu baada ya kutibuliwa. Jambo hili la kawaida lilisemekana kufanywa na malaika.Yohana anaelezea hili katika mstari wa 4, ambayo iko kwenye mabano. Hakuna uhalali wa kuondolewa kwa aya hii katika tafsiri zingine.

Yesu alielekea kwa barabara na akasimama katikati mwa kundi la watu wagonjwa waliojaa matumaini ya kuponywa. Maji yalikuwa bado hayajatibuliwa na hali ilikuwa ya ukimya kama vile wagonjwa, marafiki na jamii walimakinika kwa uchoyo uliokuwa umetokana na ukubwa wa uchungu wao na haja, ya kuona maji yakichemka.

Yesu aliwatazama na kuona jambo la kusikitisha zaidi: mtu alikuwa amelala bila mtu wa kumsaidia (Mst.6) kwa miaka thelathini na nane alikuwa amepitia mateso ya ugonjwa. Hali ya kukata tamaa ilikuwa imejaa usoni mwake. Yesu akasimama karibu na mtu huyo lakini uwepo wake haukutambulika. Mtu yule hakumjua, hivyo hakuwa na imani kwake, na hakumwitisha chochote. Hili lilionyesha mfano wa Israeli: kwa sababu ya kukosa imani ya kizazi cha hapo awali kilikuwa kimeadhibiwa kwa miaka 38 na leo walikuwa “Wasimame” na wawe na imani zaidi katika ushirikina na nguvu zao wenyewe kuliko Mwana wa Mungu aliyechaguliwa (Mk 4:7; Hes. 14: 33-34; Kum. 2:14).

Ghafla akasikia sauti ikinena naye, “je, unataka kuponywa?” (Mst.6 RSV) Yesu bila shaka alijua kwamba alikuwa amejikokota pale na kwamba wengine walikuwa na haraka kufika kwenye maji. Hali ya kukata tamaa iliokuwa machoni mwake ilisisitzwa na sauti yake “Bwana, mimi sina mtu wa kunitia birikani wakati maji yanapotibuliwa” (Mst.7) Macho yake yalikuwa katika maji meusi yaliyokuwa chini. Mwishowe alikuwa amepata rafiki ambaye angemsaidia kuingia kwenye maji? Lakini Yesu alielekeza mawazo yake kutoka kwa matarajio hayo hafifu, na kwa sauti yenye nguvu akatoa amri , “inuka, chukua godoro lako, utembee” ghafla mtu akatii:akainama  na kukuja godoro lake na kusimama. Alipata uhuru ambao hakuwahi ujua kwa miaka 38.  Aligeuka kumtizama yule alikuwa amempa amri ile, lakini Yesu alikuwa ameshatoweka.

Macho yote yalimgeukia mtu huyu, yule aliyekuwa amekosa furaha kuliko kila mtu alikuwa sasa anatembea miongoni mwao akiwa amejaa furaha. Maji ya birika yangechemka bila yeye kugundua kwani sasa kulikuwa na chanzo kikubwa cha uponyaji Israeli.

YESU ANAELEZEA MAANA YA KWELI YA SHERIA YA SABATO (Yn. 5:10-20)

Tiba ilikuwa imefanyika katika siku ya Sabato ambayo hakuna kazi ilipaswa kufanyika. Mtu aliyebeba godoro alisimamishwa na Wayahudi na wakamkea kwa kuvunja sheria. Mtu yule alihalalisha matendo yake kwa misingi ya kwamba mponyaji wake alikuwa na nguvu za Kimungu na hivyo mamlaka ya Kimungu pia. Alikuwa amemwambia achukua godoro lake! Nini alichofanya makosa? Upofu wa Wayahudi unaweza kuonekana wakati inapokumbukwa kwamba alikuwa mtu anayejulikana, kiwete wa miaka mingi. Walifutilia mbali kutoka akilini mwao muujiza wa uponyaji wake ambao ungewaongoza kumdhamini Yesu zaidi na Sheria ya Sabato.

Katika Hekalu, aliyeponywa na mponyaji walikutana ana kwa ana, na Yesu alikamilisha uponyaji alioanzisha katika birika. Uponyaji wa kiroho ulifuatia ule wa kimwili: “Tizama, umekuwa mzima; usitende dhambi tena" Dhambi ni sababu kuu ya mateso na itaendelea baada ya Uponyaji basi ingesababisha jambo baya zaidi: kifo (Mst.14). kwa shukrani, kuna uwezekano kwamba, mtu yule aliwaambia Wayahudi nani aliyekuwa amemponya. Lakini nia yao ilikuwa ovu na kama ndege wa kuwinda, walishambulia, bila kutambua muujiza. Walimhukumu na kutaka kumwangamiza kwa kile walichoona kama ukiukaji wa sheria ya Sabato- kuonya mtu na kumwambia abebe godoro lake siku ya Sabato (Mst.16)

Miujiza mingi ya Kristo ilifanyika siku ya Sabato (kwa mfano Mk 2: 23-28; 3: 1-7) Wayahudi walisema, Yesu, angesubiri. Lakini nyuma ya matendo ya Yesu,  kulikuwa na ukweli wa kina. Alisema: “Baba yangu bado anafanya kazi, na mimi pia nafanya kazi” (Mst.17 RSV). Mungu alikuwa anafanya kazi kurejesha “Pumziko” kwa waliotakaswa naye wakati wa uumbaji, lakini walioharibiwa na dhambi ya binadamu. Mungu alikuwa nafanya kazi bila kuchoka kwa ajili ya binadamu na sasa alikuwa amemtuma Mwana wake ili pumziko la kweli lipatikane kupitia kazi yake ya wokovu (Mt.11: 28-30). Yesu alikuwa anafanya  kazi anafanya kazi ya Mungu, kuendeleza mfano na malengo. Ushahidi wa uamuzi wa Mungu kuleta “Pumziko” la kweli kwa binadamu katika Ufalme inaweza kuoneka katika baraka yake ya siku ya saba na kufanya maadhimisho yake jambo la masharti (Mwa. 2: 3; Kut. 31: 15-17 ). Kuona kwamba Yesu alikuwa na  malengo sawa na Mungu ( kuwapa uhuru wale waliofungwa katika katika utumwa wa dhambi) hakuna siku ingekuwa inafaa zaidi kuliko Sabato, kwa Yesu kufanya kazi ya miujiza ya uponyaji.

Katika tukio hili Yesu alichukua hoja iliyokuwa ya juu zaidi- kwamba matendo yake yalikuwa mfano wa Baba Yake. Baadaye Yesu alihalalisha kitendo cha wafuasi wake kuvuna nafaka siku ya Sabato kwa kutaja kwamba Mwana wa Mtu alikuwa Bwana wa Sabato. Mwana wa Mtu alikuwa ameahidiwa utawala juu ya “kila kitu” na hii ilikuwa ni pamoja na sheria ya Sabato (Mk. 2: 27-28; Zab. 8: 2-6).alifunza kwamba “Sabato ilikuwa kwa ajili ya Binadamu” ilikuwepo kwa ajili ya ustawi wake wala sio uharibifu wake. Binadamu hangeikiuka ila katika nyakati za hitaji, wakati wema wake mkuu ulipingana na sheria ya Sabato.

Baadaye tena Yesu alifunza somo kwa ajili ya matumizi yao wenyewe. Aliwauliza kama ingekuwa halali mtu kumtoa ngombe au punda kutoka kwa kisima katika siku ya Sabato (Lk.14 5; 13: 15-16). Alifunza kwamba Sabato ilikuwa inaadhimishwa zaidi wakati matendo ya huruma na wema yanatendeka. Hivyo Yesu hakujitetea kwa kukiuka sheria hii ya Sabato, lakini alitaka kuwaongoza ili wapate kutambua kusudi la Mungu ndani yake.

Lakini maneno yake hayakutambulika na, yalifanywa msingi wa madai zaidi: kwa sababu alimwita Mungu Baba Yake, alishtakiwa “kwa kujifanya sawa na Mungu” (Mst.18). katika maneno yaliyofuatia Yesu anapinga madai yote mawili: "Mwana hawezi kufanya kitu peke yake" (Mst.19). Katika ujumbe huu wa ajabu, anaongea kuhusu utegemezi wake kwa Mungu wala sio Usawa, na kwa kazi, Baba alikuwa amezifanya  hivyo alikuwa anazidhibitisha. Kisha akaelezea uhusiano wa karibu na Baba yake: Baba “anampenda mwanawe” na “Anamwonyesha” kile anachokifanya, na Mwana anaona kile anachofanya na kufanya vivyo hivyo. Ana Ujuzi wa matendo na nia ya Baba yake, ambayo ni mwongozo wake. Kama walishangazwa na onyesho la uponyaji, je “Kazi kubwa” zingekuwa na adhari gani kwao (Mst.19-20)?

"KAZI KUU" ZA YESU KUTIMIZA ISHARA YA SABATO (Yn. 5:21-30)

Yesu alielezea kwa makini kwamba  Baba yake alikuwa  ameweka heshima kubwa juu yake; alikuwa  amepewa mamlaka, kufufua, kuhukumu na kupatia uhai “kwa yule atakaye”. Majukumu ya Baba yalikuwa yametwikwa Mwana. Basi nafasi ya wale waliokuwa nampinga na walitaka kumuua ingekuwa gani?

Katika mistari 24-28 Yesu alitangaza mamlaka yake kwa wale waliomsikiliza. Kwa kumbali Yeye na Baba yake, wangekuwa wamehusishwa na uzima badala ya kifo-  ahadi yake ilikuwa na uhakika kwamba utiifu ungehakikisha uzima wa milele. Tazama kwamba uzima wa milele sio mali  ya sasa lakini ni tumaini(Tit. 1: 2), au ahadi (1 Yn 2:25), itakayopatikana katika ufufuo (Mst.29). Dhamana inapatikana kwa Ukweli kwamba Baba ndiye, “chemchemi ya uzima" (Zab. 36: 9; 1 Tim. 6:16), alikuwa amempa guvu sawia za kuwapa binadamu uzima wa milele,  zaidi hayo alikuwa  Mwana wa Mtu, na hivyo “aligusa hisia za unyonge wetu”, alikuwa amechaguliwa na Mungu kwa ajili ya sadaka ya binadamu, kuhani mkuu wa binadamu, mwamuzi wa binadamu (Ebr. 2:13 -18, 4: 14-16; Yn. 5:27) kwa  njia hii kazi ya ukombozi wa binadamu, ilioanzia kwa imani (Mst.24), ingekamilika kwa ufufuo wa maisha. Lakini katika kesi ya wale waliokataa,kungekuwa na  hukumu (Mst.29). Hapa palikuwa na onyo kwao. Wala hawangeweza kutoroka: wale waliosikia na kuona kazi zake kuu wote wangewajibika kwake. Binadamu wote hawangefufuliwa (Zab. linganisha 49:20; Efe. 2: 1, 12); “wote” katika Mstari wa 28 inahusu makundi yote mawili ya wasikilizaji- wanaokataa na wanaokubali.

MASHAHIDI WATATU WALIOSHUHUDIA UHALALI WAKE (Yn. 5:31-47)

Kama ingedaiwa kwamba Yesu alikuwa najishuhudia mwenyewe, basi kungekuwa na mashahidi wengine wangethibitisha madai yake. Kwa kweli, madai yake yalikuwa ya kuunganisha, hivyo akitarajia pingamizi, aliyaweka mbele ya mashahidi wawili.

  1. Ushahidi wa Yohana— Mst.31-35.

Walikuwa wametumwa kwa Yohana na waliambiwa wazi kwamba hakuwa Kristo, lakini hivi karibuni Yesu atawasili  na alikuwa anatayarisha nyoyo za watu kwa ajili yake (Yn.1: 19-27). wakati ushahidi wa Yohana ulipokelewa “kwa muda”, Yesu alikiri kwamba uhusiano wake na Baba ulikuwa wa karibu sana kwamba alihitaji ushahidi wa mtu zaidi ya mmoja: Mungu pekee angetoa ushahidi, ambapo kila aina yeyote ya usaidizi ingekataliwa, hivyo haja ya shahidi wa pili:-

  1. Ushahidi wa Baba kupitia kazi—Mst.36-38.

Mara kwa mara Yesu aliwaelezea kuhusu maana iliokuwa nyuma ya kazi zake kuu- kwamba Mungu alikuwa  naye (linganisha Yn. 10:32, 15:24). Kukataa kwao kwa ushahidi huu dhahiri ulidhibitisha kwamba hawakutambua maana ya kweli ya mahubiri ya Neno ya Baba (Mst.37-38). Hivyo walipuuza shahidi wa tatu:

  1. Shahidi wa Neno —Mst.39-47.

Mistari 39-40 katika RSV inasoma “Mwayachunguza maandiko, kwa sababu mnadhani kwamba mna uzima wa milele ndani yake: Na hayo ndiyo yanayonishuhudia MIMI, wala hamtaki kuja kwangu mpate uzima”. Hapa kulikuwa na jambo la ajabu; Kristo alikuwa kiini cha mtazamo katika maandiko waliochunguza, na  bado walimkata. Nini kilikuwa chanzo cha upofu huu?  Walitaka sifa na utukufu wa binadamu wala sio kukubaliwa na Mungu. Walipokonywa tumaini lao la mwisho wakati Yesu alisema kwamba Musa, ambaye kwa Sheria yake walitafuta uhalali, angekuwa mshtaki wao: ilikuwa vigumu kuamini Musa na kumkataa Yesu, kwa sababu Musa aliandika kumhusu (Kum.18: 15-18).

MAMBO TUNAYOJIFUNZA

  • Yesu amepewa nguvu ya ufufuo na hukumu ambayo yeye binafsi atasimamia. Kutoaminiwa kwake leo kutaleta kukataliwa naye kesho, lakini kumkubali sasa kutamaanisha furaha na uzima wa milele pamoja naye katika Ufalme.
  • Ishara ya Sabato ilizungumzia kazi ya Mungu inayoendelea kwa ajili ya wokovu wa binadamu na pumziko, na sio uharibifu wake. Katika Yesu Kristo tunaweza pumzika sasa kutoka kwa shughuli zisizo na manufaa za binadamu na kufanya kazi katika shamba la Mungu "kuingia katika pumziko" la miaka 1000.
  • Yesu anadhibitisha madai yake makubwa kwa kutumia mashahidi watatu, Mungu pamoja na binadamu, ambayo haiwezi kukataliwa.

MAKTABA YA KUREJELEA:

"The Gospel of John" (J. Carter)—Sura 5

"A Life of Jesus" (M. Purkis)—Kitabu 3, Sura 5

"Law and Grace" (W. F. Barling)—Kurasa 192-193

MASWALI YA AYA:

  1. Mtu aliyekuwa kiwete katika Birika la Bethsda alikuwa mgonjwa kwa muda wa miaka 38. Kwa njia gani aliwakilisha taifa la Israeli?
  2. Kwa nini ilikuwa ni haki kwa Yesu kumponya mtu katika siku ya Sabato?
  3. Wayahudi walimshataki Yesu baada ya kumponya mtu yule kiwete katika birika la Bethesda na kwa kudai usawa na Mungu. Jinsi gani Yesu alionyesha hili kuwa uongo?
  4. Toa maoni kwa kifupi juu ya mashahidi watatu kwa kazi ya Yesu ambao aliongea kuwahusus baada ya uponyaji katika bwawa la Bethesda.
     

MASWALI YA INSHA:

  1. Toa sababu ya kile kilichotokea katika bwawa la Bethesda wakati Yesu alimponya mtu aliyekuwa kiwete?
  2. Yesu alisema: "Baba yangu anafanya kazi daima, nami pia nafanya kazi" (Yn. 5:17). Eleza alikuwa anamaanisha nini?
  3. Ni mashahidi gani Yesu alielezea kuunga mkono madai yake wakati alikemewa na Wayahudi baada ya uponyaji katika bwawa la Bethesda?

 

 

Swahili Title
335. BETHESDA: UPONYAJI SIKU YA SABATO
Sub type
Sub sub type