336. MFANO WA MPANZI
"Tazama mpanzi alienda na kupanda mbegu . . ."
Neno la Mungu, linaonyesha mfano huu kama mbegu, bila dosari. Kama mbegu ingechukua mizizi na kukua na kuzalisha mbegu ilitegemea asili ya udogo ilipopandwa. Wakati tunapokea neno la Mungu katika nyoyo zetu ni lazima tuitunze kwa makini. Lazima tuhakikishe kwamba mvuto wa dunia na matatizo tunayokumbana nayo hayapingi ukuaji wa mbegu na kuizuia kuzaa matunda.
Lengo letu katika somo hili ni kujifunza njia ya haki na makosa kupokea Neno la Mungu.
Mt. 13: 1-23
MBINU MPYA YA KUFUNZA.
Yesu alikuwa anafunza kwa KUHUBIRI na mambo yaliyohusiana na Ufalme wa Mungu na tabia iliyohitajika kwa wale wanaoiridhi. MIUJIZA mikuu ilionyesha nguvu za Mungu na kuonyesha kwamba madai yake ya kuwa Mwana wa Mungu yalikuwa ya kweli. Kwa MFANO, alikuwa ameonyesha dhahiri njia za Mungu; Jinsi tunavyo sali, jinsi ya kusamehe, na jinsi ya kuonyesha neema.
Katika hatua hii ya huduma yake tunapata msisitizo mpya: MIFANO inakuwa misingi ya mafunzo na mahubiri yake. Bwana alifananisha mambo ya asili na mambo ya kiroho, katika hadithi kuhusu mambo ya kawaida. Hivyo mithali ni hadithi yenye maana iliyofichwa.
Mfano huu mpya ulitizamwa na wanafunzi na waliuliza maswali: "Kwa nini unasema kwa mifano?â (Mt. 13: 10). Kabla tufukirie jibu lake kwa swali hili lazima tuzingatie kwanza mambo yalivyokuwa yamebadilika. Sasa ilikuwa katikati ya mwaka wake wa pili wa huduma yake. Msisimko juu wake ulikuwa umepungua na watawala walikuwa tayari wanapanga kumuua. Katika Mathoyo 12 Bwana alipingwa na Wafarisayp ambao walihusisha miujiza yake kwa Beelzebub, mungu wa kipagani. Viongozi walikataa madai na mafunzo yake, na waliwakakosoa wafanyikazi wake. Sababu ya Yesu kunena kwa mifano, ilikuwa kama alivyowajibu wanafunzi wake âKwa sababu ninyi mmejaliwa kuzijua siri za ufalme wa mbiguni, lakini wao hawakujaliwa (Mt. 13:11). Mifano ilikuwa na kusudi-mbili: kuelimisha wale wanyenyekevu na kuwashangaza wenye kiburi. Wenye- moyo wa kunyenyekea waliomfuata walihifadhi mifano hii katika akili yao na kupitia kutafakari, ujumbe huu ulieleweka; lakini wenye kiburi ambao walimpinga, hawakuyatia mafunzo haya moyoni na hivyo hawakuelewa mafunzo yake (linganisha Mst. 0.34-35). (Hivyo kwa wale ambao âWanaâ unyenyekevu wataongezewa maarifa (Mst.12). Katika Mstari wa 13-15 Yesu aliongea kuhusu upumbavu wa wale wanaompinga. Alisema kwamba maneno ya Isaiya 6:9-10 yangetimia katika kizazi hicho. âWangesikiaâ mifano itakayonenwa, lakini âhawataelewaâ kwa sababu walikuwa âviziwi wa kusikiaâ katika mistari 16-17 Yesu aliwaambia mitume kwamba, walikuwa wamepata neema ya hali ya juu, kwani waliona na kusikia kutoka kwa kinywa chake mambo ambayo mababu zao watakatifu walitamani kuona(linganisha 1 Pet.1:10-12).
Kwa hio mifano ilikuwa njia ya ajabu ya kuelimisha na kuwachanganya. Ilikuwa rahisi kukumbukwa kwa ilichukuliwa kutoka kwa mifano ya kila siku. Wale walikuwa na hamu, fikra zao zilielimishwa na walipata kuelewa maana, ingawa hawakuelewa kamili mpaka wakati wa ufufuo wake. Mifano hii dhahiri ilielezewa vyema kutoka kwenye kinywa cha Mwalimu na ni ishara kweli alikuwa Mwana wa Mungu.
Mfano wa kwanza na wa awali ni mfano wa Mpanzi (linganisha. Mk. 4:13).
HADITHI YA MPANZI (Mt. 13:1-9)
Yesu alikuwa katika kingo ya magharibi za mto wa Galilaya wakati aliongea kuhusu mfano huu. Akiwa katika nafasi hii aina zote za mchanga zilionekana na ilikuwa wakati wa mavuno (linganisha Mt. 12:1). Mbele ya Yesu, alipokuwa ameketi kulikuwa na umati mkubwa. Maneno yake yalikuwa yanapenya kwenye masikio kama mbegu wakati zinapandwa; maneno yake yangejaribu mchanga wa akili zao na kuzigawanyisha kwa makundi. Hadithi hii ya kawaida ilikuwa ya mazingira ya kiasili ya Israeli.Tofauti na leo, mbegu hupandwa kwa kutumia mashini, mpanzi angeenda na mfuko wake wa mbegu ukininginia shingoni: akirusha mbegu kutoka kwa mfuko hadi ardhini. Katika shamba kulikuwa na njia: katika pembe kulikuwa na mkusanyiko wa mawe, ilhali katika udongo mzuri kulikuwa na miiba iliokuwa imeota. Juu yake jua liliwaka, na ndege walivutiwa na mbegu zilizotawanyika, walikusanyika nyuma yake.
Yesu alielezea kwa lugha ya wazi hatma ya ngano. Mbegu zilizoanguka kwenye njia zilinyakuliwa na kuliwa na ndege: zile zilianguka kwenye mawe, ziliota lakini zilichomwa na jua na kufa kwa kukosa udongo mzuri; zile zilioanguka kwenye miiba ziliontwa na kukua lakini zilisongwa na miiba na kunyauka: na hatimaye kuna zile mbegu zilizoanguka kwenye udongo na ziliota na kunawiri, na kuzaa mazao mara mia zaidi. Hadithi hii ilikuwa rahisi na rahisi kueleweka kama vile Yesu alivyoelezea.
MAANA YA MIFANO (Mt. 13:18-23)
Katika mfano wa mpanzi, tuna faida kubwa kupata utafsiri kutoka kwa kinywa cha Yesu. Ni mafunzo gani Yesu alikuwa anataka kufundisha wale âwaliokuwa na masikio ya kusikiaâ kutoka kwa mfano? Ni wazi kwamba sisitizo lilikuwa kwa aina tofauti za udongo. Mbegu ya aina moja ilipandwa- mbegu nzuri, Neno la Mungu au Neno la Ufalme (Mst.19) lakini zilianguka katika mchanga wa aina tofauti. Neno la Mungu ni kama mbegu, ndogo na yenye uwezo wa kuzaa na kujizindisha mara nyingi, kulingana na moyo wa anayesikiliza (linganisha 1 Pet. 1:23; Yak. 1:21; 1 Yn. 3:9). Mkulima yeyote anajua maana ya kuwa na udongo sawa, uliotayarishwa kama kazi itafuatiliwa na mafanikio. Mbegu itajaribu udongo, hivyo ndivyo Neno la Mungu, lililotawanywa na Mungu na wafuasi wake. Udongo, unawakilisha watu tofauti; na jinsi wanavyopokea Neno la Mungu âlinapandwaâ katika mioyo yao. Yesu anaelezea makundi manne ya watu- injili inagawanyisha wanadamu katika makundi. Kundi kubwa kati ya haya ni wale wanaokataa Neno, akili yao inafananishwa na barabara sugu. Kuna wengine, wanaosikia, ndani yao mbegu inachukua mizizi. Lakini kwa, kuamini sio mwisho:ni mwanzo tu na katika makundi haya kunapatikana migawanyiko mingine. Wacha tuangalie maagizo ya kila kundi.
- Barabara au Njia (Mst. 19):
Iliyokauka na kuwa ngumu kama jiwe, hakuna fursa ya kuota. Mbegu iliyoanikwa juu ni rahisis kunyakuliwa na ndege. Mtu wa aina hii huwa hapokei Neno la Mungu. âMtu Mwovuâ ("Shetani" katika Mk. 4:15; "Shetani" katika Lk. 8:12), kama ndege, wanavyonyakua kabla iote. Katika nyakati za Yesu, Wafarisee walikuwa hivi. Walisikia Neno kutoka kinywani mwake, lakini kama kundi la watu â wasiosikiaâ (linganisha Mst, 14-15 Yn: 8:43-47). Upofu na Kiburi ni tabia ya asili ya binadamu na zilikuwa zimewaadhiri sana na hawangeweza âkusikiaâ neno la uzima. Wale walioweka imani katika viongozi wa ulimwenguni wangekumbwa na hatma moja. Kama vile ndege walivyonyakua mbegu, hivyo kwa ushawishi wao walishawishiwa kutomfuata Yesu: Aliye kipofu akiongozwa na Kipofu.
Kwa njia gani tunaweza tumia hili katika siku zetu? Kutoamini kumekidhiri sana leo kwa sababu binadamu wanataka kutimiza tamaa zao kwa njia tofauti za kutafuta anasa. Tamaa kama hizi zinaweza adhiri ushawishi wa Neno. Katika kesi zingine, dini za uwongo zinaadhiri fikra za watu na Neno linakosa kupokelewa.
- Mahali Penye Mawe (Mst. 20, 21):
Hakuna udongo wa kutosha kwa Neno kujishikilia, na kuota. Lakini udongo hapa ni mgumu na mizizi haiwezi ingia ndani kwani kuna mawe mengi chini ya udongo huu. Ukosefu wa unyevunyevu, ukuaji wa mbegu hii unasitishwa. Matokeo yake ni kuota kwa haraka, ikifuatiwa na kunyauka na kifo cha haraka wakati jua linaangazia mmea huu. Jua na joto lake linasimamia mateso yatakayotokea hadi kukiri kwa Ukweli. Kuna wale wanaosikia Neno na kulipokea kwa haraka na kwa hamu, lakini hawana kina cha ufahamu. Wana tabia na fikra hafifu. Wakati wanahitajika kusimama kwa ajili ya Ukweli na wanapata aibu, âwananyaukaâ na wanaonyesha kwamba wanawaogopa binadamu kuliko Mungu. Kwa njia gani mitume walikuwa tofauti na kundi hili (linganisha Mdo. 3, 4, 5). Je tunachukulia kama jambo la furaha wakati tunahitajika kuteseka kwa jina la Kristo? Ama tunakosa msukumo wa kiroho na kutenda yale wenzetu wataona kuwa sawa?. Bwana anatoa maoni katika mahali pengine, "Yeye atakayevumilia mpaka mwisho, ataokolewa." (Mt.10:22).
3. Kati ya Miiba (Mst. 22):
Miiba ilikuwa inakua vizuri pamoja na mbegu nzuri ikapata nafasi kati ya miiba, ikaota na kuanza kukua, lakini pakawa na mashindano kwa ajili ya rutuba ya udongo, mwanga na hewa. Miiba ilikuwa tayari ishamea hapo awali na mimea ile michanga ikasombwa na kushindwa kupambana.
Hapa tuna picha ya kutisha. Sio kwa kukosa nguvu kundi hili âudongoâ au mtu anashindwa; ni kwa sababu ya nguvu hii inatumika vibaya. Watu hawa wanajiingiza kwa mambo mengine ambayo ni ya kuharibu. Mbegu nzuri na ile mbaya zinakua pamoja- lakini kwenye udongo mbegu mbaya ina nguvu kuliko nzuri âkujali mambo ya ulimwengu huu, anasa na tamaa za kila namna huingia na kulisonga hilo neno, nalo haliwezi kuzaa matunda" (Mk. 4:19). Hapa basi, tumetambua mkasa wa maisha ya uanafunzi bila kuwa na matunda ya kiroho ya kuonyesha mwishowe- maisha ya bure. Huduma kuu ingeweza kuleta Ukweli, kwani udongo una nguvu za kukuza. Lakini mambo mengine pingamizi yalichukua nafasi ya kwanza- mizizi yake iliiba unyevunyevu na rotuba kutoka kwa udongo na matawi yake yakazuia mwanga na kuzomba mbegu nzuri; Hamwezi kumtumikia Mungu na mali" (linganisha Mat 6:24; Hag. 1: 5-6) linganisha kama mfano kijana mdogo tajiri (Mt. 19:22).
4. Udongo Mzuri (Mst. 23):
Mbegu inapoanguka kwa udongo uliochimbwa vizuri, kutayarishwa na usio na magugu, kuna kila nafasi ya kupata mazao mazuri. Mchanga huu unawakilisha kundi la wanadamu ambao bila shaka, wataridhi ufalme wa mbiguni. Mara mbili hapo awali katika injili ya Mathayo Yesu alitangaza kwamba binadamu watajulikana kwa matunda yao (7:20; 12:33). Kusikia, kuelewa na âkupokeaâ Neno (Mk. 4:20), tofauti na kundi la barabaraniâ wana kina cha akili, Neno linachukua mizizi ili liweze kustahimili siku ya kesi (linganisha Kol 2: 7), tofauti na âkundi la udongo wenye mawe; maisha yao hayazaombwa na tamaa za mambo ya dunia na anasa na hivyo neno Neno linaweza kunawiri bila ushindani, tofaiti na âkundi la udongo wenye miibaâ;.Tunda la Kweli linaweza kuendelezwa kwa ushirikiano na Kristo (Yn.15: 4). Tunda la Roho, matokeo ya mwisho ya ushawishi wa Neno juu ya walio na moyo wa kweli na wa dhati, yameorodheshwa katika Wagalatia 5:22, yaani, "upendo, furaha, amani, uvumilivu, wema, fadhili, uaminifu, upole, na utulivu "(yaani kujizuia). Wana wa ufalme wataonyesha sifa hizi kama ushahidi kwamba wamejua Mwana wa Mungu
HISTORIA YA AGANO LA KALE
Manabii walitumia mafumbo na mifano ili kusisitiza na kufanya wazi ujumbe wao. Wazo la Mungu la kupanda na nyoyo za binadamu kufananishwa na mchanga, zinafanana na fumbo la nabii hosea: rejelea mistari, ukitambua kwamba jona Yezreel linaamisha âMungu anapanda -Hosea 1:11; 2: 22-23; 8: 7; 10:12. Wazo kama hili linapatikana kwengineko (kwa mfano Isa. 55:10) wakati Yeremia akiwa na fikra sawa na Bwana, aliwaambia Waisraeli, âlimeni udongo, na msipande kwenye miibaâ (Yer. 4: 3)
MASWALI YA INSHA:
- Mfano ni nini? Kwa nini Yesu alitumia mifano?
- Katika mfano wa mpanzi, mbegu ilipandwa juu ya aina nne za udongo. Elezea kile kila aina ya udongo inawakilisha na jinsi mbegu zilivyofanya.
- Elezea maana ya mfano wa mpanzi. Taja mambo ambayo yanaweza kusitisha ukuaji wetu katika Ukweli.
TAFAKARI ZA KUHITIMISHA.
Mfano ni uchambuzi wa matokeo ya mahubiri, akitafakari jinsi kupita kwa muda kungeonyesha uzoefu wa Yesu. Wasikilizaji wake waliwekwa katika âmakundiâ kulingana na majibu yao kwake. Hadi sasa wale kumi na wawili walihusika, mfano huu lazima uliwavunja moyo hasa walipoana majibu ya watu kwa Kristo. Sisi, kama wao, tumekatazwa kukata tamaa wakati tunatambua kwamba sio kila mtu ayasikia neno la Mungu. Aidha, tunapaswa kutafakari tuko kwa kundi lipi na hili linapaswa kuboresha mtizamo wetu.
MAMBO TUNAYOJIFUNZA:
- Mvuto mbaya, uwe wa ndani au wa nje, unaweza kunyakua Neno kabla lipate muda wa kuota ("njiani").
- Wenye akili dhaifu wataanguka wakati wa majaribu kwa sababu imani yao ni hafifu ("penye mawe").
- Moyo ambao utamtumikia Mungu na wakati huo huo kutafuta mambo ya ulimwengu na utajiri utazombwa na magugu na hutaazaa matunda ("ardhi yenye miiba").
- Mioyo yetu lazima iwe tayari kama udongo mzuri na kisha Neno litanawiri kwa utukufu wa Mungu na wokovu wetu.
MAKTABA YA KUREJELEA:
"Parables of the Messiah" (J. Carter)âNam. 27 na 28
"Nazareth Revisited" (R. Roberts)âKurasa. 216-218
MASWALI YA AYA:
- Nini kilichomfanya Yesu kuzungumza kwa mifano?
- Ni masomo gani tunafundishwa na ardhi yenye mawe na ardhi yenye miiba katika mfano wa mpanzi?