341. YESU ANAFUNZA KUHUSU MSAMAHA
"Hadi mara sabini mara saba"
Baada ya kumponya mtoto mwenye kifafa, Yesu na wanafunzi walibaki Galilaya kwa muda mfupi. Wakiwa katika eneo hilo Yesu aliwaambia wanafunzi wake kwamba angesalitiwa katika mikono ya binadamu, auawe na afufuke tena katika siku ya tatu (Mt. 17:22, 23). Wafuasi hawakuelewa kile Yesu alichomaanisha kuhusu kifo na ufufuko wake. Mathayo alirekodi kwamba âwalihuzunika sanaâ, naye Marko alisema â hawakuelewa neno alilosema, na waliogopa kumuulizaâ (Mst. 9:32).
Badala yake, wakati Yesu alikuwa anaongea kuhusu mateso yake yajayo, wanafunzi wake walikuwa wanajadiliana kuhusu nani atakakuwa mkuu zaidi katika ufalme. Wasiwasi wao ulikuwa mkubwa mpaka kukatokea mgogoro miongoni mwao. Wakiwa wamenoga kwa majadiliano yao walisahau kwamba Bwana alijua mawazo yao. Hata hivyo wangetambua kwamba hakuna kitu kinachoweza kufichwa kwa Mwana wa Mungu- Jambo ambalo hata sisi tunapaswa kuzingatia.
Lengo la somo hili ni kuonyesha kwamba mtazamo wetu kwa wenzetu unaadhiri mtazamo wa Mungu kwetu: kama tutasamehe, atasamehe, na kama Anasamehe, pia sisi tunapaswa kufanya hivyo.
Mathayo 18
YESU ANAFUNZA KUHUSU UNYENYEKEVU. (Matt. 18:1-5)
Yesu aliwauliza wafuasi wake kile walikuwa wanabishania wakiwa njiani kuelekea Kapernaumu (Mk. 9:33). Wote waliona aibu na wakaepuka kumjibu moja kwa moja kwa kumuuliza, ânani mkuu katika ufalme wa mbiguni?â (Mt. 18.1). akikaa na wale kumi na wawili, Yesu aliwapa jibu wasilotarajia. Maoni yake ya ukuu yalikuwa tofauti na yao. Aliwaonyesha kwamba yule anaye shughulika na cheo katika Ufalme, anaweza kosa kufika kwenye ufalme huo; âYeyote atakaye kuwa wa kwanza lazima awe wa mwisho wa yote" (Mk. 9:35).
Kuonyesha âukuuâ aliotamani kuona, Yesu alichukua mtoto mikononi mwake, na kuwaambia wanafunzi wake: "Hakika, nawaambia, msipogeuka na kuwa kama watoto wadogo, hamtaingia kamwe katika Ufalme wa mbinguni. Kila anaye jinyenyekeza kama mtoto huyu, huyo ndiye aliye mkuu katika Ufalme wa mbinguni "(Mt. 18: 3-4). Ukuu hauhusishi vitendo vikuu ili kufurahisha wanadamu wenzetu. Lazima tugeuke kwa kukandamiza kiburi cha asili ya binadamu, na kuchukua hali ya kufunzwa na kutumainia kama mtoto mdogo. Maneno ya Mika ni sheria ya maisha katika ulimwengu ambao daima unasifia mafanikio ya binadamu. "Bwana anataka nini kwako, ila kutenda haki, na kupenda rehema, na kwenda kwa unyenyekevu na Mungu wako?" (6 Mik.8).
MBEGU YA UASI (Mt. 18:6-7)
Yesu hakuwa tu na wasiwasi kwamba wanafunzi wake walipaswa kuwa na roho wa unyenyekevu, lakini pia alikuwa na wasiwasi kwamba wangeweza kuona hatari ya kufuata njia tofauti. Aliona kwamba kama kiburi kingeruhusiwa kuendelea, hivi karibuni ubishi ungeibuka kuhusu nani mwenye mamlaka kwa kundi hilo na kanuni za utumishi kwa kila mmoja zingesahaulika. Hivyo, Yesu akawaambia wanafunzi wake: "Kila mmoja atakayewakosesha mmoja wa hawa wadogo waniaminio, ingekuwa afadhali kwa mtu huyo afungwe jiwe la kusagia shingoni mwake, na kutupwa baharini" (Mst 6). katika kutumia maneno haya mazito, Yesu alikuwa analinganisha hatma ya mtenda dhambi anayeinua mkono wake juu ya kundi lake, pamoja na hatma ya Babeli ya zamani. Kuongea kuhusu kuangamizwa kwa Babeli, Yeremia aliambiwa: âtena itakuwa utakapokwisha kukisoma kitabu hicho, utakifunga kwa jiwe na kukitupa katika mto Frati: na kisha utasema: âHivyo ndivyo utakavyozama Babeli, na hautainuka tena kutoka kwa maovu nitakayoleta juu yakeâ (Yer 51: 63-64). Yesu alijua kwamba kwa kupita kwa mda âMtu wa dhambi, mwana wa kuzimuâ angekuja na kupotosha ukweli (2The. 2: 3-12). Mtu huyu angeongoza mfumo wa ukristiano bandia ambapo ushirikina na uovu wa Babeli ya zamani ungekuweko: "Ole wake ulimwengu kwa sababu makosa hayana budi kuja mambo ya kukosesha, lakini ole wake mtu yule aletaye jambo la kukosesha! " (mst.7).
Yesu alikuwa anaongea kuhusu kuanzishwa kwa Upapa na Babeli Kuu, uasi wa Katoliki ya Kiroma. Kama vile Babeli ya zamani ilivyoharibiwa, hivyo pia itakuwa kwa "siri ya uasi." Kristo akirudi: âna malaika mwenye nguvu akachukua jiwe kama lile kubwa la kusagia, na kulitupa baharini akisema, kama hivi kwa nguvu nyingi utatupwa chini Mji mkuu wa Babeli, wala hautaonekana tenaâ (Ufu . 18:21).
Si ajabu kwamba Yesu alitumia maneno haya mazito kuwaonya wanafunzi wake dhidi ya kiburi na tamaa ya nguvu na mamlaka.
HAJA YA KUONDOA TABIA MBAYA (Mt. 18:8-9)
Tunapaswa kuwa waangalifu tusije kusababisha mwingine kupotea, na tuwe waangalifu tusije tukaanguka sisi wenyewe. Yesu akawaambia wanafunzi wake, "Basi, ikiwa mkono wako au mguu wako utakukosesha ukate ukautupe mbali: ni bora kuingia katika uzima ukiwa umepungukiwa, kuliko kuwa na mikona na miguu miwili na kutupwa katika moto wa milele. Na kama jicho litakukosesha, lingoe, ukalitupe mbali: kwani ni bora kuingia katika ufalme wa mbiguni na jicho moja, kuliko kuwa na macho mawili na kutupwa katika Jehanamu ya motoâ (Mst.8-9).
Yesu bila shaka hakuwa anamaanisha maneno katika hali halisi. Macho ni ya kuona, mikono ni ya kufanya kazi. Yesu alikuwa anawaelekeza wanafunzi wake kuepuka maono, kuepuka matendo na kuepuka mahali patakapo tufanya sisi kuanguka. Maneno ya Bwana wetu yanafaa vijana wa leo. Katika siku hizi za kisasa kuna mengi ya kuona na kutenda, na pia mahali kwingi kwa kwenda. Lakini katika haya yote kuna majaribu ambayo hatuwezi kupinga na yakiendelea yanaweza kutugharimu uzima wa milele.
Macho, mikono na miguu ni ya kutumiwa, lakini kwa mambo ambayo yanaweza kutufikisha katika Ufalme wa Mungu. Kama mambo tunayojihusisha nayo yanasababisha tuanguke, basi Yesu anaamrisha uchungu wa kuyaondoa. Wokovu ni kitu cha muhimu na tamaa au mambo mengine ambayo yanaweza pinga safari yetu lazima yaondolewe. Kama sivyo katika siku ya hukumu tutapata kwamba, hatuwezi kuingia katika ufalme. Ni bora kuteseka hasara katika maisha haya kuliko kupoteza yote mwishowe.
HAJA YA KUWAJALI WENGINE (Mt. 18:10-14)
Katika kumtumikia Mungu mfuasi lazima awajali wengine. Hata katika wakati wa majaribio yake makuu, Yesu alifikiria kuhusu wanafunzi wake na aliwaombea (Yn 17: 9-11). Katika macho ya Mungu sisi ni "watoto wadogo" ambao wanahitaji huduma na makini. Kama tutawajali wengine kwa mtazamo huu, tunaweza tambua maneno ya Yesu, "Jihadharini! Msimdharau mmojawapo wa wadogo hawa; kwa maana nawaambieni, malaika wao mbinguni siku zote huutazama uso wa Baba yangu aliye mbinguni "(Mst.10).
Mara nyingi sisi husahau huduma hii ya malaika. Pengine tunawafikiria kama wajumbe wenye nguvu wa Mungu wanaotimiza nia zake kuu katika hafla kubwa. Lakini hapa tunawaona katika mtizamo mpya kabisa- wanawajali watoto wa Mungu kibinafsi. Tunasoma pia kwamba wao ni â roho waliotumwa kuhudumu kwa wale watakaouridhi ufalme wa mbiguniâ (Ebr 1:14; Zab. 34: 7). Hivyo inaonyesha kwamba Mungu anawapenda wale wanaomheshimu na amewateuwa Malaika kuwa nao kila wakati. Wanawaongoza katika njia ngumu na kuwasaidia katika nyakati za hatari za kiroho, na kuwatetea mbele ya Baba. Tusiwahi sahau kwambu hatuko peke yetu.
Uvumilivu na upendo wa Mungu unaonekana katika mfano mfupi wa kondoo aliyepotea (Mst. 11-14). Katika ulimwengu wa leo âkila mtu ako kivyakeâ, lakini miongoni mwa wanafunzi lazima iwe âkila mtu kwa ajili ya wengine". Ingekuwa rahisi kwa mchungaji kusahau kondoo mmoja aliyepotea na kupoteza muda akiitafuta. Lakini kila jitihada ilitumika mpaka pale kondoo aliyepotea amepatikana.
ROHO WA MSAMAHA (Mt. 18:15-22)
Wanafunzi walikuwa wamemsikiza Bwana wao kwa makini kuhusu sifa za mfuasi wa kweli, lakini Petro hakuwa na uhakika kuhusu mara ngapi alipaswa kusamehe. Luka anatuambia kwamba: âJilindeni, kama ndugu yako akikukosea, mwonye, akitubu msamehe. Na kama akikukosea mara saba katika siku moja na kuja kwako mara saba akisema, Nimetubu: Msameheâ (Lk. 17: 3-4). Petro alitaka kuweka kipimo kwa msamaha, hivyo akaja kwa Yesu na kumuuliza, âBwana, ndugu yangu anikosee mara ngapi, nami nimsamehe?â (Mst.21). Jibu la Yesu liliondoa shaka yoyote Petro aliyokuwa nayo na kuonyesha roho wa msamaha. Alimwambia Petro kwamba kila siku inapaswa kuchukuliwa kama siku mpya na msamaha haupaswi kuwa na kiwango: âNawaambieni, hadi mara saba mara sabiniâ (Mst.22).
Katika Mwanzo tunasoma kwamba Mungu alitishia kisasi mara saba kwa yeyote atakaye mshambulia Kain, muuaji wa Habili. Lakini Lameki wakati alipotenda mauaji, alijigamba kwamba hakuhitaji ulinzi wa Mungu na kwamba atajilipizia kisasi yeye mwenyewe: âkama Kaini angelipiziwa kisasi mara saba, kwa hakika Lameki mara saba mara sabiniâ (Mwa 4:24). Inaonekana kwamba Yesu alielewa kuhusu kijivunia kwa Lameki wakati aliongea kuhusu msamaha, kinyume cha kisasi. Lameki alijigamba hakutakuwa na kipimo kwa kisasi chake. Yesu alishauri kwamba hakupaswi kuwa na kiwango cha msamaha.
MFANO WA MKOPESHAJI ASIYE SAMEHE (Mt. 18:23-35)
Kuonyesha umuhimu wa kuwasamehe wengine, Yesu alitoa mfano wa Mkopeshaji asiye samehe. Mfalme fulani alichukua hesabu ya watumishi wake na kupata kwamba mmoja wa watumishi wake alikuwa na deni lake la talanta elfu kumi. (Talanta moja ilikuwa sawa na miaka kumi na tano ya ajira.) Mtumishi yule alipokosa njia ya kumlipa, mfalme yule aliamuru mtu yule na familia yake kuuzwa. Lakini mtumishi yule alianguka chini na kuomba msamaha akisema, â Bwana, nivumilie, nami nitakulipa yoteâ.Mfalme aliguswa na maneno yale na kumsamehe deni lile.
Baadaye mtumishi yule akaondoka na kukutana na mtumishi mwenzake aliyekuwa na deni lake la dinari mia moja, dinari moja ya kirumi ilikuwa sawa na ajira ya siku moja. Bila ya huruma alimkaba koo yule mtumishi na kutaka malipo ya papo hapo. Mtumishi yule alianguka miguuni pake na kuomba aongezewe mda: â Nivumilie nami nitakulipa yoteâ. Lakini hakupewa muda na akatupwa gerezani, âmpaka atakapolipa lile deniâ.
Wakati watumishi wengine waliona hivyo na wakamwelezea mfame. Alimwita mtumishi yule asiye na huruma na kumkemekea: Ewe, mtumwa mwovu, nimekusamehe wewe deni lako lote, uliponisihi: nawe, je huwezi kumrehemu mjoli wako, kama vile mimi nimekurehemu?â. Mtumishi yule alikosa jambo la kusema. Bwana wake akamtupa gerazani na kumtaka alipe deni lake ambalo alikuwa amesamehewa hapo awali.
âHali kadhalika baba yangu aliye mbinguni atakavyowatendea nyinyi, msiposamehe kwa mioyo yenu kila mtu ndugu yake makosa yakeâ. Kila neno hapo limejaa maana.
Sisi sote tumetenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu, na kama Mungu anaweza âtizama mapungufu yetuâ hatuwezi tukasimama mbele yake. (Zab 130: 3). Mungu atatusamehe: kwa maana hakabiliani na sisi baada ya dhambi zetu, wala kutuzawadi kulingana na mapungufu yetu. Kama vile âMashariki ilivyo mbali na Magharibi, hivyo ndiyo Mungu ameweka mapungufu yetu mbali, kama tutamgeukia kwa unyenyekevu, kukiri na kutubu (linganisha Zab 103: 8-14).
Katika Lugha ya mfano, dhambi ni deni ambayo hatuwezi kulipa, lakini Mungu ametuondolea. Lakini baada ya kusamehewa deni kubwa kiasi hicho, tunapaswa kuonyesha mtindo huo kwa wenzetu kwa kuwasamehe wenzetu âmadeni yao madogoâ. Tusipowaonyesha wenzetu huruma leo, sisi pia hatutaonyeshwa ikifika siku ya hukumu: âatakuwa na hukumu bila msamaha, kwa yule hakuonyesha hurumaâ (Yak 2:13). Tunapaswa kusamehe âkutoka moyoniâ. Hatupaswi kuna na fikra kwamba-ânaweza samehe lakini siwezi sahauâ. Mungu ameahidi kusamehe dhambi zetu nyingi, lakini misingi ya msamaha wake ni kwa sisi pia kuwasamehe wenzetu (Mt. 6:12). Hatuwezi kuwa na machungu na kisasi dhidi ya wenzetu. Umuhimu wa kuwa na roho yenye unyenyekevu ambayo inaweza kusamehe inaonekana kwani baada ya kutoa "Sala ya Bwana", Yesu alirudi mara moja suala hili la maombi (Mt. 6:14, 15).
Maneno ya Paulo kwa Waefeso yanatoa maoni juu ya mfano huu: âUchungu wote, ghadhabu, hasira, kelele, masingizio na kunena kwa uovu kuwekwe mbali na nyinyi na kila namna ya ubay: na muwe na hurum kwa wenzenu, msameheane, kama vile Mungu kwa ajili ya Kristo alivyowasamehe ninyi (Efe. 4:31, 32).
MAMBO TUNAYOJIFUNZA:
- Hatupaswi kutafakari ukuu wa baadaye lakini kustawisha unyenyekevu kama wa watoto.
- Kiburi na dhuluma zinaweza kusababisha uasi.
- Tabia ambazo zinaweza kututoa katika Ukweli lazima ziondolewe.
- Lazima tutafute waliopotea kama mchungaji.
- Nia yetu ya kuwasamehe wenzetu itaamua kama Mungu atatusamehe.
MAKTABA YA KUREJELEA
"A Life of Jesus" (M. Purkis)âKitabu 5, Sura 10
"The Gospel of the Son of God" (L. G. Sargent)-Kitabu V, Sura 2
"Parables of the Messiah" (J. Carter)âNam. 39, 40
"Nazareth Revisited" (R. Roberts)âKurasa 262-263, 325-326
MASWALI YA AYA:
- Yesu alimaanisha nini aliposema, " Basi, ikiwa mkono wako au mguu wako utakukosesha ukate ukautupe mbali: ni bora kuingia katika uzima ukiwa umepungukiwa, kuliko kuwa na mikona na miguu miwili na kutupwa katika moto wa milele. Na kama jicho litakukosesha, lingoe, ukalitupe mbali: kwani ni bora kuingia katika ufalme wa mbiguni na jicho moja, kuliko kuwa na macho mawili na kutupwa katika moto wa milele"?
- Orodhesha kwa kifupi onyo ambalo Yesu aliwapa wanafunzi wake wakati walimuuliza, "Ni nani aliye mkuu katika Ufalme wa mbinguni" (Mt. 18: 1)?
- Yesu alimaanisha nini aliposema, "Jihadharini! msimdharau mmojawapo wa hawa wadogo, kwa kuwa mimi nawaambia, kwamba malaika wao mbinguni siku zote huutazama uso wa baba yangu, aliye mbinguni" (Mt.. 18:10)?
MASWALI YA INSHA:
- Andika insha kuhusu mafundisho ya Yesu wakati wanafunzi wake walimwuliza swali: "Ni nani aliye mkuu katika Ufalme wa mbinguni?" (Matt.18: 1).
- Kwa nini Yesu alifundisha kwamba ni muhimu kwetu kuwasamehe wenzetu?
- Elezea hadithi ya mfano wa mkopeshaji aliyekataa kusamehe. Ni masomo gani yanaibuika kutoka kwa mfano huu?