343

Swahili

343. YESU ANAWAPA WAFU UHAI

"Ugonjwa huu si wa mauti, bali kwa utukufu wa Mungu"

Kufuatia jaribio lililofanywa dhidi ya maisha yake, Yesu aliondoka Yerusalemu na kuvuka mto Yorodani hadi mahali ambapo Yohana alimbatiza (Yn. 10: 39-40). Miaka mitatu ilikuwa imepita tangu Yohana alipombatiza, na  kazi yake ya umma ikaanza. Yesu alijua kwamba mwisho wa huduma  yake ulikuwa unakaribia. Kabla ya kifo na ufufuo wake, muujiza mkuu zaidi ulikuwa  bado haujatokea. Yesu alikuwa amewapa uhai kwa mwana wa mjane katika Nain na binti Yairo (Lk 7:14;. 8:55). Sasa Lazaro, ambaye jina lake lilimaanisha “El atasaidia” angepokea uhai kutoka kwa wafu, kupitia nguvu iliyowekwa juu Mwana wa Mungu.

Lengo la somo hili ni kuonyesha kwamba Yesu ana nguvu juu ya adui mkuu wa binadamu, kifo na kwamba kwa wale wanaokufa wakiwa ndani ya Kristo, Kifo ni kama usingizi.

Yohana 11

YESU ANAELEZWA KUHUSU UGONJWA WA LAZARO (Yn. 11:1-5)

Janga lilikuja kwa familia ndogo iliokuwa ikiishi katika kijiji cha Bethania, umbali wa kilomita tatu kutoka Yerusalemu. Lazaro, ambaye alikuwa rafiki wa Yesu na ndugu yake Mariamu na Martha, akawa mgonjwa. Akimwangalia kama alivyolala katika kitanda, dada zake waliona kwamba kifo kilikuwa karibu. Fikra zao zikaenda  kwa Yesu. Wakikumbuka miujiza yake na uhakika kwamba Yesu angeweza kuwasaidia, kwa haraka wakatafuta msaada wake.

Hivyo ujumbe ukamfikia Yesu akiwa upande wa mashariki mwa Yorodani:  Bwana, yule umpendaye yu mgonjwa”.Yesu akampa mjumbe jibu apeleke “ Huu ugonjwa sio wa mauti bali (kwa ajili ya kuinuliwa) kwa utukufu wa Mungu, Ili Mwana wa Mungu atukuzwe kwa huo”  (Mst.4).

Hii ilionekana jambo la ajabu kwamba Yesu hakujibu kama ilivyotarajiwa kwa wito wa msaada. Maneno yake yalionekana kuonyesha kwamba ugonjwa wa Lazaro haukuwa mbaya.

YESU ANACHELEWESHA SAFARI YAKE YA BETHANIA (Yn. 11:6-16)

Kwa siku mbili Yesu alichelewesha safari yake ya Bethania. Martha na Mariamu walijua kwamba kama Yesu angefika basi majonzi yao yangeisha. Aliwaelezea wanafunzi wake nia yake ya kurudi Judea. Wakikumbuka jinsi alivyoponyoka kifo kule, walishangaa (Mst 8), lakini aliwatuliza. Aliwapa sababu ya kutaka kuondoka; “rafiki yetu Lazaro amelala; lakini naenda ili niweze kumwamsha kutoka usingizini”(Mst.11). kulikuwa na mchanganyiko wa maneno. Walifikiria alimaanisha usingizi wa kawaida. Ilhali alimaanisha kifo. Yesu aliongea waziwazi, “Lazaro amekufa. Na nina furaha kwa ajili yenu kwamba sikuweko, ilimpate kuamini. (Mst 12-15).

Muujiza wa ufufuo ungekua kwa ajili ya mafunzo yao  na pia kama faraja kwa familia ilioko Bethania. Yesu alikuwa anafikiria kuhusu wengine kila wakati, na akijaribu kupanga mambo kwa manufaa yao.

MAZUNGUMZO YA MARTHA NA YESU (Yn. 11:17-27)

Bethania, mazishi la Lazaro yalikuwa yamekamilika na kaburi likazibwa. Wengi wa waombolezaji waliokuwa marafiki za Marimu na Martha walibaki nyumbani kwao kundelea kuwafariji. Wakati huo Yesu akakaribia Bethani. Kusikia kwamba Yesu alikuwa anakuja, Martha akandoka na kwenda kukutana naye. “Bwana,”  Akalia yule dada mkubwa, “kama ugelikuwepo hapa, ndugu yangu hangekufa” (Mst.21). Yesu akamjibu, "Ndugu yako atafufuka" (Mst.23). Martha alielewa kwamba atafufuka katika siku ya mwisho, lakini hakutambua kwamba angefufuka wakati ule. “Najua kwamba atafufuka tena katika ufufuo wa siku ya mwisho.” Akamjibu. Yesu akasema, “mimi ndimi ufufuo na uzima; yule aniaminiaye; hata akifa atakuwa anaishi: na ashiye na kuniamini hatakufa milele” (Mst. 25-26). Maneno yake yanatufunza mambo kadhaa:

  1. Yeye anampa uhai “ Yeyote....” Yesu ndiye uzima wa maisha, kwa Wayahudi na Watu wa Mataifa.(Gal 2.20) Wale ambao wanafanya hivyo hawataishi tu bali wataishi milele.
  2. Imani Inayoishi ni ya muhimu. Lazima tuweke imani yetu katika matendo. Kristo lazima aishi ndani yetu na lazima tujenge katika maisha yetu kwa sifa ya Mungu zinazoonekana katika Mwana Wake (Gal 2.20) Wale ambao wanafanya hivyo hawataishi tu bali wataishi milele.

Yesu akamtizama usoni, “ Je, unasadiki hayo?” kwa mara nyingine jibu dhabiti likaja, “ Naam, Bwana: mimi nasandiki kwamba wewe ndiwe Kristo, Mwana  wa Mungu, yule ajaye ulimwenguni” (Mst.27)

MARIAMU ANAKUJA KWA YESU (Yn. 11:28-37)

Baadae nyumbani, Martha alimvuta Mariamu kando na kumwelezea kuhusu kuwasili kwa Bwana. Mariamu alikimbia kwa Bwana, alitoa madai ya imani sawa na yale ya dada yake, “Bwana, kama ungekuwa hapa, ndugu yangu hangekufa (Mst.32).

Yesu aliadhiriwa na majonzi ya Martha na Mariamu na marafiki zao waliokuwa wanaomboleza. Walipokuwa wanamwongoza hadi kaburini, Yesu alilia kwa huruma (linganisha Lk 07:13) alishikwa na majonzi ya watu (Ebr. 4:15). Wale waliokuweko, walipoona machozi yake na wakijua sifa zake, walishangaa kwamba hakuwa amefika awali kumponya mtu yule mgonjwa. 

Yesu alikuwa pia analia kwa sababu aliweza kuona kwa kifo hiki huzuni ya binadamu wote, majonzi yanayoletwa na dhambi. Kwa muda mfupi yeye pia angewekwa kaburini, na njia ya kifo chake ingeonyesha  “Jinsi alivyopenda” sio tu Lazaro, lakini wale wote watakoa kuja kwake na kuishi (Yn 15:13;. 1Yn. 3:16).

MUUJIZA WA UFUFUKO (Yn. 11:38-46)

Kundi likaelekea katika eneo la kaburi. Siku nne zilikuwa zimepita kabla kifo cha Lazaro na alikuwa amekwisha zikwa . Yesu akaagiza jiwe liondolewe. Martha akashangaa: “Bwana, ananuka sasa, kwani ameshakuwa maiti kwa siku nne (Mst.39).  Huu haukuwa muujiza wa kawaida.

Jiwe likaondolewa. Yesu akainua macho yake na kumwomba Baba yake. Kisha sauti yake yenye mamlaka ikasikika, “Lazaro njoo huku nje” (Mst.43). kwa mshangao wa umati uliokusanyika, Lazaro akatoka kaburini akiwa amefungwa sada za kaburini. Watu walishangaa walipomwona Lazaro amesimama mbele ya Mwokozi wake. “Mfungueni”, akasema Yesu, “na mwache aende zake” (Mst.44) .

Muujiza huu ulionyesha utukufu wa Mungu (Mst 4, 40). Ulifundisha kwamba Yesu ndiye “ufufuo na uzima” katika mji huu wa majonzi, kwa Bethania ilimaanisha “nyumba ya maskini au ya wanaoteseka”. Lazaro alikuwa amekufa ili kuwaongoza wengine kwa Mungu. Alionyesha mfano wa Bwana katika sadaka yake ya kifo na ufufuko  na mfano huu haukuwa umepotea kwa Bwana: wala hatupaswi kusahau maana ya kweli ya kifo chake.Kifo cha Bwana katika mazingira ya kawaida kilimaanisha mwisho wa maisha, lakini Mungu alimpa nguvu, na kumfufua kutoka kwa kifo. Matokeo-UTUKUFU KWA MUNGU kwa njia dhabiti zaidi kuliko vile ilikuwa katika hali ya Lazaro.

Matukio yanayozunguka muujiza huu yanapaswa kutukumbusha sisi tangazo la Bwana kwa Musa: “kama niishivyo mimi, dunia yote itajazwa na UTUKUFU WANGU” (Hes 14:21). Mungu anaishi, na kwa sababu anaishi, nia yake na utukufu inapaswa kuonekana kwa viumbe vinavyo ishi pia.  Nguvu zake za uzima, ambazo pia amempa Mwana wake  (Yn. 5:26).

Ni sahihi kwamba hii ilikuwa ishara ya saba kati ya nane zilizoandikwa na Yohana. Nambari saba ni nambari ya agano na inawakilisha Agano ambalo linatoa ufunguo utakao fungua kifo na kaburi (Ufu 1:18). kifo na ufufuo wa Bwana unatoa uhakikisho wa agano jipya (Rum 15: 8), na  pia uhakikisho kwa wale wamo ndani yake kwa kweli kwa pia wao watafufuliwa na kupokea uzima wa milele (Rum 6: 5). Yesu ataondoa kifo kwa wale ambao amewateua (soma Heb;2:14: 1 Kor 15: 15-25; 2 Tim 1:10).
 

 SANAHEDRINI (BARAZA) WANAKUTANA (Yn. 11:47-57)

Wayahudi wengi ambao walishuhudia ufufuo wa Lazaro waliamini katika Yesu mara moja. Wengine walienda kwa haraka na kuwaambia Wafarisayo kile kilichotokea. Hii ilisababisha mkutano wa dharura. Makuhani wakuu na  Wafarisayo waliita baraza. Uharibifu a Yesu ukawa  rasmi (Mst.53) Yesu, alitambua mipango yao, na akaenda na kujificha, alitambua kwamba amepiga hatua moja kuelekea katika kusulubiwa kwake.

MAMBO TUNAYOJIFUNZA:

  • Martha na Mariamu waliongozwa na ushawishi wa mfano wa Kristo na mafundisho yake. Sisi pia, ni lazima tudhihirishe imani yenye uhai. Yote tunayofanya lazima yawe kwa ajili ya utukufu wa Mungu (1 Kor. 10:31).
  • "Maisha ni wakati wa kumtumikia Bwana". Katika kifo hakuna kukumbuka, hakuna kazi,  na wala hakuna matumaini yeyote. (Zab 88: 3,12; Mhu 9:10).
  • Wakati tunaona "mwanga wa ulimwengu" hatutakuwa na mashaka, lakini  tutakuwa na " mwanga wa uzima" (Yn.8:12; 9: 4-5, 10:10). Kwetu sisi, basi, kifo kinakuwa tu usingizi, tukisubiri siku ya kufufuka (1 The. 4: 14-16).

MAKATABA YA KUREJELEA:

"The Story of the Bible" (H. P. Mansfield)—Tol. 10, Kurasa 130-141

"A Life of Jesus" (M. Purkis)—Kitabu 6, Sura 8

"The Gospel of John" (J. Carter)—Sura 11

"Nazareth Revisited" (R. Roberts)—Sura 42

 
MASWALI YA AYA:

  1. Elezea maneno ya Yesu: "Mimi ndiye ufufuo na uzima".
  2. Katika njia gani kumfufua Lazaro kulikuwa tukio la muhimu sana?
  3. Majibu ya watu yalikuwa gani kuhusu kufufuka kwa Lazaro?
  4.  Kwa nini Yesu alichelewesha kuja kwa Lazaro aliposikia kuwa ni mgonjwa?

MASWALI YA INSHA:

  1. Kwa kifupi elezea hadithi ya ufufuko wa Lazaro, na ujadili umuhimu wake juu ya kazi ya Bwana Yesu Kristo.
  2. Ni mashauri gani ya binafsi yanayojitokeza kutokana na hadithi ya ufufuko wa Lazaro? Ni mafunzo gani ya kimsingi tunayojifunza kutokana na muujiza huu?
     

Sehemu ya 4

HADI YERUSALEMU KWA KESI, KUSULUBIWA NA KUFUFUKA

Awamu ya mwisho ya huduma ya Bwana ilikuwa imefika. Siku zilikuwa zinakaribia wakati “angekumbana na kundi la waovu”, na  “kwa mikono miovu, angesulubishwa na kuuwawa”.

Mwanzoni wa huduma yake alikuwa Yohana Mbatizaji amemtambua kama “Mwanakondoo wa Mungu aondoaye dhambi za ulimwengu". Sasa Pasaka yake ya mwisho ilikuwa inakaribia, “Mwanakondoo” aliyekuwa auwawe alikuja Yerusalemu. Alipochunguzwa na maadui zake alionekana hana makosa na kwa hivyo angeweza “kubeba dhambi zetu kwa mwili wake juu ya mti” (1 Pet 2: 21-24).

Katika siku zake za mwisho na hata katika masaa yake ya mwisho, Wasiwasi wa Yesu ulikuwa juu ya wanafunzi wake.  Aliwalekeza kupitia mifano na unabii wawe wenye busara na waamini na wavumilie hata kama yeye mwenyewe angeteseka mambo mengi na aondolewe kutoka kwao. Lakini walionekana kutosikiza; hivyo wakati wa majaribio yake makuu yalipofika, wote walimwacha na kumtoroka. Peke yake alisimama mbele ya  Pilato, lakini hakuwa peke yake kwani Mungu alikuwa pamoja naye (Yn. 16:32).

Siku hio ya hukumu alihukumiwa na Wayahudi pamoja na watu wa mataifa hadi alipopelekwa kusubishwa. Hivyo upendo Baba yetu wa mbinguni ulionekana kwa kumtoa Mwana wake Mpendwa kwa ajili ya dhambi za ulimwengu (Yn 3:16).

Maisha yaliyojaa ahadi yalionekan kuishia kwa maafa, na yote yalionekana kupotea. Siku tatu baadae, alifufuka, akashinda kifo. Kisha akaendelea kuwashauri wanafunzi wake kwa siku arobaini, alipaa mbiguni, na sasa “anaketi katika mkono wa kiume wa Mungu; akisubiri mpaka pale maadui zake wote watakapowekwa kama kibao chini ya miguu yake "(Ebr 10:12, 13).


 

Swahili Title
343. YESU ANAWAPA WAFU UHAI
Sub type
Sub sub type