345

Swahili

345. KUWAJIBU WAPINZANI WAKE

"Na hakuna  aliyedhubutu kumuuliza maswali yeyote"

Viongozi wa Kiyahudi walikuwa wamejawa na hasira kwa Yesu. Alikuwa ameonyesha mapungufu yao hadharani kwa kutumia mfano na “walijua kwamba alikuwa anaongea kuwahusu” (Mk. 12:12).

Waliamua kwamba Yesu lazima aangamizwe na kwa njia ambayo ilionekana sawa kwa macho ya watu. Walifikiria maswali matatu. Walikuwa na uhakika kwamba kama angejaribu kujibu bila shaka angesema kitu ambacho wangetumia kumdhalilisha mbele ya macho ya watu ili wamtie nguvuni. Hivyo wakamwendea Yesu wakijifanya kuwa na nia nzuri lakini kwa kweli walikuwa wanafiki tu (Mt. 22:18) na wapelelezi (Lk. 20:20).

Lengo la somo hili ni kuonyesha ukamilifu wa busara ya Yesu wakati alijaribiwa na watawala wa Wayahudi.

Marko 12

SWALI LA KWANZA: KULIPA KODI KWA KAISARI AU LA? (Mk. 12:13-17).

Mafarisayo walikuja pamoja na Maherodi. Walikuwa wapinzani wa kisiasa lakini hawakuangalia tofauti zao ili waweze kumwangamiza adui yao- yule ambaye walimwona kama tishio kubwa kwao kuliko vile walikuwa wao wenyewe. Mafarisayo walikuwa na kiburi, ubinafsi na wenye uzalendo mkali. Waliwachukia Warumi na kuwadharau wale wote waliowaunga mkono, kama vile kikundi cha Herode na watoza ushuru, kama Mathayo (Mk. 2:16). Walilipa ushuru kwa kusita, kwani walielewa kwamba  sheria ilipinga. Kundi la Herode walikuwa waaminifu kwa utawala wa Herode na Roma, na walilipa  kodi na kuhimiza wengine kufanya hivyo. Hivyo wakati walienda pamoja kwa Yesu na swali hili la muhimu: "Je, ni halali kulipa kodi kwa Kaisari, au la? Kulikuwa na hisia ya uhalali kwa swali hilo.

Walisifia ujasiri wake: “Bwana, tunajua wewe wasema na kufundisha yaliyo haki na wala hujali cheo cha watu, bali unafundisha njia za Mungu kwa kweli”. Kwanini walifanya hivi? Kwa sababu walitarajia “La” kama jibu ili waweze kumshtaki mbele ya mkuu (Lk. 20:20). Lakini kama wangepata jibu la “ndio”, basi Mafarisayo wangesema kwamba  yeye si mzalendo. Walisisitiza kupata jibu “Ndio” au “La” : Je, sisi tutoe, au tusitoe?”. Walifikiria kwamba hakuna njia yoyote Yesu angeweza kuponyoka mtego waliokuwa wameuficha katika swali lile.

Lakini lengo la msingi na hila ilkuwa  wazi kwa Mwana wa Mungu; "alijua yaliyomo ndani  ya roho ya mwanadamu", na bila kuogopa binadamu alitambua unafiki wao na kubaini nia yao: “kwanini  mnanijaribu? Nileteeni dinari ili nipate kuiona”.

Yesu alikuwa ameamua: na hakukuwa na kusita katika mizamo wake kwa swali lile: Warumi walikuwa wamekuja Yudea kwa  sababu ilikuwa  nia ya Mungu na mpangilio ulikuwa umewekwa kwa watu. Hivyo haikujalisha “kama wangetoa?”- hawakua na uchaguzi.

Senti au dinari ililetwa kwake. Akawauliza swali, swali ambalo liliwapa jibu kutoka vinywani mwao “ina sura na anwani ya nani?” wakamjibu “Kaisari” Kichwa cha mkuu wa Tiberia, Mfalme wa milki ya Kirumi, kilikuwa kimechorwa upande mmoja wa sarafu, na upande mwingine ulikuwa na maandishi “Pontifex Maximus" (maana ya Pontifa Maxima-Kuhani Mkuu) kwani Tiberia alitaka watu wake wamchukue kama mungu.

Jibu la Yesu lilikuwa rahisi, lililojaa maana. Ndani alijibu swali ambalo liligawanyisha falme. “Mpeni Kaisari vilivyo vya Kaisari na mpeni Mungu vilivyo vya Mungu (Mst.17). Walishangaa! Kwani hawakuweza kumshaki mbele ya mkuu au kumshtumu kwa kutokuwa mzalendo dhidi ya Wayahudi. Walikuwa wamemwonyesha sarafu ya kifalme iliokuwa na sura ya Kaisari juu yake. Kwa hivyo ilikuwa ya Kaisari na ilikuwa haki kwamba ipewe Kaisari.

Lakini kulikuwa na vitu vilivyokuwa vya Mungu na vile waliokuwa wamepokea kutoka kwake. Kama vile- upendo, maisha na ibada- mambo yaliyo mazuri maishani-yalikuwa yametoka kwa Mungu, na ilipaswa “kutolewa” kwake.  Vitu hivi havingeweza kununuliwa kwa fedha (Isa 55: 1-2; 1 Pet 2:19). Badala ya kwenda kumuua Yesu, walipaswa kumrudishia Mungu upendo ambao alikuwa amewaonyesha kwa kumtuma Mwana Wake wa Pekee duniani ili kuokoa ulimwengu. Walikuwa wameubwa kwa sura na mfano wa Mungu ili kudhihirisha utukufu wake (Mwa.1:26, 27; 1 Kor 11: 7). Walikuwa wanatoa huduma kwake? Walikuwa wanajaribu kutengeneza tabia inayofanana ya mwokozi wao? Walikuwa tayari kumsulubisha, kumwanika na kumwaibisha, na wakaondoka.

SWALI LA PILI 2: UFUFUO NA NDOA (Mk. 12:18-27)

Kisha wakaja Masadukayo-kundi la watu ambao hawakuamini ufufuko na waliamini vitabu vitano vya sheria vilivyo julikana kama “Pentateuch, vitabu vitano vya kwanza katika Biblia, ambavyo havina urejeleo wa moja kwa moja wa ufufuo (Mdo: 23:8). Walikuwa na swali ambalo walifikiria lilikuwa na maarifa na walikuwa na uhakika kwamba lingeaibisha yeyote aliyeamini ufufuo. Lakini badala yake udhaifu wa msimamo wao ulidhihirishwa, na kutoka katika vitabu vya sheria! Wakamuuliza kuhusu mwanamke aliyeolewa na mandugu saba kwa zamu, na kila mmoja anafariki kabla mtoto yeyote kuzaliwa: “ katika ufufuo, wakati watafufuka, yeye atakuwa mke wa nani? Kwani ndugu zote saba walimwoa”

Tafakari jinsi swali hili lilivyowekwa kwa njia nzuri, na utazame hali ya kuridhika iliokuwa katika nyuso za “Mbwa mwitu hawa wenye ngozi ya kondoo”. Nyuso zao zilibadilika haraka! Yesu alitoa jibu la waziwazi: “Je hampotei kwa sababu hii”. Hawakuwahi kuongeleshwa kwa namna hii. Hawakuwa wamezoea “watu wa kawaida” kupinga maoni yao, na isitoshe kuambiwa kwamba walikuwa wanakosea katika utafsiri wao wa sheria. Lakini “hawakujua andiko, wala nguvu za Mungu” na Yesu aliendelea kuwaonyesha hili kwao (Mk.12.24-25).

 Kwanza kabisa walikuwa na mawazo yasiyo sahihi kuhusu ufalme na ndoa. Ndoa ilikuwa imetengenezwa mwanzoni kwa anjili ya kuongezeka kwa watu wenye Umungu ili dunia ijae na binadamu na kuinyakua (Mwanzo 1: 26-27). Katika nyakati za baadaye lengo la ndoa katika Israeli ilikuwa kuzaana kwa mbegu ya kimungu (Mai 2:15; Ezr.9: 2). Lakini katika ufalme kizazi hiki kingetukuzwa na kupewa mamlaka na Kristo (Ufu 5: 9-10). Kwa hivyo, nia ya ndoa, kulingana na watakatifu, ingekuwa imetimizwa. Ufisadi hauwezi kuridhi usawa: kifo, ndoa na kuzaana hakutakuwa sehemu ya maisha  ya wale wanaofufuka “tutafanywa kuwa sawa na malaika, na hatutakufa tena” (Mk.12:25; Lk 20:34 -36). Ilikuwa kwa sababu Masadukayo walikuwa wamejawa na usherati na walikuwa hawajui maandiko ndio maana walikuwa wamepotea sana.

Yesu alichukua nafasi hii kuwafundisha mafundisho ya msingi juu ya sheria yao wenyewe: kama kugusa waliokufa, ili wafufuke: hamjasoma vitabu vya Musa, jinsi katika kichaka Mungu alinena naye, akisema, Mimi ni Mungu wa Ibrahimu, Isaka, na Yakobo? " hawakuwa wametambua maana ya maneno haya. Mababa hawa wa Israeli walikuwa wakuu kulingana na Mungu na hata kama walikuwa wamekufa na wakazikwa kitambo, Aliongea kuwahusu kama kwamba bado wako hai. Alikua amechagua kujulikana kupitia majina yao na adi zake kwao (Ebr 11:16;. Mwa 17.7). Hii ilimaanisha kwamba watafufuliwa kwa Nguvu zake, ambazo Yesu alisema hawakuelewa. Yawhe ndiye Mungu aishiye na ni nia yake kwamba hakuna yeyote atakayepotea. Hivyo wale wanaokufa na wanapendwa naye bila shaka wataishi tena, na njia ya uzima ni ufufuo: Yeye si Mungu wa waliokufa bali wa walio hai (Mst.27, linganisha Rum 4:19). Kuhusu ahadi za Abrahamu, Isaka na Yakobo zilikuwa na umiliki wa Nchi ya Kanaani milele (Mwa 13:15). Ibrahimu alikufa bila kuimiliki (Mdo 7: 5., Heb 11:13), kwa hivyo uridhi wake ni wa siku za usoni. Hivyo ufufuo unafunzwa kwa kuahidiwa kitu ambacho kinahusishwa.

Ujinga wao kwa hivyo ulikuwa mkubwa sana “Nyinyi mmekosa sana!” (Mst.27)

SWALI LA TATU: AMRI NGANI KUU ZAIDI? (Mk. 12:28-34).

Masadukayo walinyamazishwa, lakini Mafarisayo walirudi na shambulio hilo. Mmoja wao, ambaye alikuwa mwandishi na mwanasheria, alijua nguvu ya maoni ya Yesu na aliuliza swali la udadisi (mst.28, Mat: 22:35). Yesu alimtambua mtu huyu kama mdadisi halisi (Mst.34), hivyo wakati tunasoma katika Mathayo 22:35 kwamba “alimjaribu” Yesu ni dhahiri kwamba kutoka kwa swali lake ilikuwa majaribio bila nia mbaya.

Yesu alichukua msimamo wake kutoka ufunuo wa Agano la Kale na kujibu, "Sikiliza, Israeli, Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja; nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili yako yote, na kwa nguvu zako zote "(Mst.29, 30).  Kwa sababu Mungu ni umoja usiogawanyika, lazima abudiwe kwa ibada isiogawanyika: Hatagawanya utukufu wake na sanamu  (Isa 42: 8), au aina ingine yeyote ya ibada (Kol 3: 5). Kwa sababu yeye ni umoja usiogawanyika, viumbe vyote lazima waletwe kwa Umoja na Yeye (1 Kor. 15:58). Lazima tutoe nyoyo zetu katika huduma ya Mungu- fikra, maneno na matendo yetu.

Yesu hakusitia hapo.  Kukiri kwa upendo wa Mungu ni rahisi, lakini Yesu aliongeza jaribio lingine pale ambapo kukiri kwa upendo kungejulikana kama ni dhahiri. Kama mtu anapenda Mungu kwa kweli basi atapenda wanadamu wenzake: “na ya pili ndio hii”, akasema, “mpende jirani yaka kama unavyojipenda wewe mwenyewe”. Ilikuwa ni hapa upungufu wa kukiri kwa upendo wao kwa Mungu ulionekana (Mst.38-40). Kutowajali maskini, wajane, pamoja na ubinafsi wao wa kidini, ulionyesha wazi kwamba Mfarisayo hakumpenda Mungu wala binadamu bali yeye mwenyewe. Yesu alikuwa na amri mbili ambazo hazingeweza kutenganishwa na Yohana anaziunganisha pamoja kwa njia sawa: Yule anayempenda Mungu anampenda nduu yake pia” (1 Yn. 4:21). Upendo wetu au kwa wenzetu, unatoa jaribio kama sisi ni wanafunzi wa Yesu, kuna haja kubwa ya kujichunguza sisi wenyewe tabia na matendo yetu.

Waandishi wakajibu kwa pamoja na wakafanya ulinganishi kati ya maadili ya upendo na sadaka. Alijua kwamba, kama Samweli, upendo huo na utiifu ulikuwa wa maana zaidi kwa Mungu kuliko sadaka, ambayo inaweza tolewa hata kwa roho yenye uovu (1 Sam 15: 22-25; Hos. 6: 6, Mk. 6: 6-8; Zab 40: 6-8; Mit 15: 8). Yesu alipongeza jibu lake na akatoa maoni kwamba hakuwa mbali na Ufalme wa Mungu.  

KRISTO—MWANA WA MUNGU (Mk. 12:35-37)

Hekima ya Mungu ilikuwa imeonyeshwa na wote wakanyamazishwa. Yesu akawauliza swali, “ Jinsi Waandishi wanasema Kristo ni Mwana wa Daudi”, wakati Daudi mwenyewe alimwita “Bwana” (Zab. 110: 1)? Wakitambua maana ya swali lile, walikataa kumjibu. Katika Israeli vijana walikuwa wanachukuliwa kuwa chini ya baba zao. Hii ingekuwa hivyo kwa Daudi, mfalme mkuu wa Israeli aliyeteuliwa na Mungu. Hivyo hali isiyo ya kawaida ya Daudi kumwita mwana wake Bwana huikulingana na ukoo wake: Mwana wa Daudi alikuwa Bwana wa Daudi kwa sababu pia alikuwa mwana wa Mungu (2 Sam 7:14). Ilikuwa ni hili walilokuwa wanakataa kutambua,  kwani ingewabidi kukubali madai ya Yesu, mafunzo na Mamlaka. Walielewa kwamba alitambulikana kama Mwana wa Daudi  (kwa mfano Mk.10:47) na mara kadhaa Yesu alidai kuwa Mwana wa Mungu, na kwamba miujiza yake ilikuwa ushahidi wa haya (Yn. 8:42, 54 , 10: 24-25, 36-38). Kwa upofu viongozi walikataa kumkubali kama Mwana wa Mungu, lakini watu wa kawaida walimsikiza kwa furaha.

UTAJIRI WA MASKINI (Mk. 12:41-44)

Yesu aliwashutumu watawala kwa kuwa na upofu katika ucha Mungu, ibada yao iliyopangwa ili kupokea sifa kutoka kwa binadamu, kwa maonyesho yao ya kutoa (linganisha Mathayo 6:2). Alikuwa anaongea kwa ujasiri karibu na hazina ya hekalu pale ambapo aliweza kuona “matajiri wengi wakitoa”. Lakini pia tofauti kabisa aliweza kuona mjane maskini aliyetoa sarafu mbili ndogo. Kwa macho ya binadamu hii ilionekana kama sadaka ya ubahili, wakati ya matajiri ilionekana kama ya ukarimu. Lakini Yesu aliona tofauti: walikuwa wametoa “ ya wingi wao”, lakini ilikuwa kidogo, mwanamke yule alitoa nyingi, kwani alitoa zote alizokuwa nazo!

Mfano wake, katika hali fulani, unalinganisha matukio matatu ya siku

  1. Alikuwa maskini mno kusumbuliwa na kodi. Alitoa kile alikuwa amekopa na kilichobaki alimtolea Mungu. Mahitaji yake hayakujali.
  2. Alikuwa mjane-kundi ambalo nyumba zao ziliporwa na matajiri (Mk.12:40)! Alimtegemea Mungu na kusubiri siku njema.
  3. Maisha yake yote  - alikuwa anajitolea kwa Mungu, kama amri ya kwanza inavyosema. Yesu alimpongeza lakini aliwakemea Mafarisayo wanafiki.
     

MAMBO TUNAYO JIFUNZA:

  • Yesu angeweza kuwarundikia aibu wadadisi wake lakini badala yake alichukulia maswali yao kwa umakini na katika kila kesi alijibu swali kwa umakini mkubwa.
  •  Mtazamo wetu kuhusu Neno la Mungu lazima uwe wa dhati na unaoletwa na hamu na moyo wa kumtumikia Yeye na wala sio sisi wenyewe. Hatupaswi "kuweka onyesho" kama vile Mafarisayo walivyofanya mbele ya Bwana Yesu Kristo.
  • Utajiri unaweza kuwa baraka katika maisha yetu kama unatumika kwa usahihi. unaweza pia kuwa mtego kwetu. Hatupaswi kutamani au kuruhusu uchukue muda wetu wote.
  • Mungu bado ni Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo na tunaweza kushiriki katika urithi wa watu hao waaminifu kwa kuweka imani yetu katika uzao wao, Bwana Yesu Kristo, na kwa kubatizwa katika jina lake (Gal 3: 27- 29). Maisha katika utii wa Mungu yatahamasisha ndani yetu upendo si wa Mungu pekee, bali wa kila mmoja wetu. Tutakuwa makini kueneza "Habari Njema" kwa wengine na kuwasaidia kufikia lengo hilo tukufu.
  • Hatupaswi kuwa matajiri ili kumtumikia Mungu. Mungu amewachagua maskini katika ulimwengu huu ambao ni matajiri katika imani ili wawe warithi wa ufalme wake (Yak 2: 5).

 

MAKTABA YA KUREJELEA:

"The Story of ihe Bible" (H.P. Mansfield)—Tol. 11, Kurasa 71-88

"Nazareth Revisited" (Robert Roberts)—Sura 49

"A Life of Jesus" (M. Purkis)—Kitabu 7, Sura 7

 

MASWALI YA AYA:

  1. Jinsi gani Yesu alidhibitisha katika Zaburi 110 kwamba alikuwa Mwana wa Mungu?
  2. Yesu alimaanisha nini aliposema kwamba mjane maskini alikuwa ametoa kuliko wote?
  3. Jinsi gani kauli "Mimi ni Mungu wa Ibrahimu, Isaka, na Yakobo" inadhibitisha ufufuko?
  4. Yesu alimaanisha nini aliposema, "Mpeni Kaisari yaliyo ya Kaisari, na Mungu yaliyo ya Mungu" (Mk 12:17)?

MASWALI YA INSHA:

  1. Wakati Yesu alijaribiwa na watawala kuhusu masuala ya Wayahudi: -
    1. Kutoa kodi kwa Kaisari,
    2. ufufuo, na
    3. Amri ya kwanza,
      Aliwajibu kwa umakini na hivyo akaonyesha kanuni za thamani zaidi. Jadili kanuni hizi.
  2. Jadili jibu la Yesu kwa swali, "Je, ni halali kulipa kodi kwa Kaisari, au la?" na maoni yako juu ya matumizi yake.
  3.  Je, unaelewa vipi amri mbili kuu ambazo Yesu alitoa alipoulizwa ni ipi ilikuwa amri ya kuu kuliko zote?
  4.  Yesu aliwajibu vipi swali la Masadukayo kuhusu ufufuo kuhusiana na mwanamke ambaye alikuwa ameridhiwa na ndugu saba walipokufa mmoja baada ya mwengine?

 

Swahili Title
345. KUWAJIBU WAPINZANI WAKE
Sub type
Sub sub type