346. UTABIRI KATIKA MLIMA WA MIZEITUNI NA LEO
"Kesheni na kuomba siku zote"
Wanafunzi walisikiza kukanwa kwa watawala wa Kiyahudi na wakasikia hitimisho la Bwana: âTizama, nyumba yenu imeachwa kwa hali ya ukiwaâ (Mt 23:38).
Alipokuwa Hekaluni alitizama, uashi wake mkubwa na usanifu wa umbo lake kuu. Pengine maneno yake ya hapo awali ya kuja kwa ukiwa yalikuwa makubwa. Jibu la Yesu âlilikuwa uhakikisho dhabiti kwao: âHaya mnayotizama, siku itakuja ambapo hapatakuwa na jiwe juu ya lingine, ambalo halitabomolewa (Lk 21 : 6). Maneno haya ya kutisha yalikwama katika fikra za wanafunzi walipomfuata Bwana kuelekea mashariki, kushuka tambarare ya Kidroni na kuanza kupanda mlima wa Mizeituni kuelekea Bethania. Walipokuwa wanapumzika, Petro, Yakobo, Yohana na Andrea wakachukua nafasi hii kumuuliza Yesu maswali zaidi: â Tuambie, mambo haya yatatokea lini? Na ishara zikatakuwa zipi wakati mambo haya yote yanatimizwa?â (Mk 13: 1-4). Jibu la Yesu ndio âUbatabiri katika Mlima wa mizeituniâ, ulivyo andikwa kwa kina katika injili zote. Ndani yake inafunua matukio yatayofuatia hadi 70 BK, wakati Warumi watafanya mji kujaa ukiwa. Lakini cha muhimu zaidi anasonga hadi mwisho wa Watu wa Mataifa, wakati majanga yatakayotangulia kuja kwake yatakuweko nchi nzima, na wakati wa hukumu utakuwa umekaribia.
Kwa hivyo unabii unaweza kugawanywa hivi:
- Lk. 21: 8-24. Ishara inayoelekea hadi ukiwa wa Yerusalemu mwaka 70 BK.
- Lk. 21: 25-28: Matukio kabla ya kuanzishwa kwa Ufalme wa Mungu.
- Lk. 21: 29-33: mfano wa Mtini.
- Lk. 21: 34-38: Onyo la Kukesha.
Lengo la somo hili ni kuona kwamba Yesu alitabiri kwa usahihi matukio yaliyotimizwa kufikia Mwaka wa 70BK, na kwamba alitabiri matukio tunayoyaona leo katika nyakati za mwisho za Watu wa Mataifa- ambayo ni onyo kwetu sisi.
Luka 21:5-36
ISHARA ZILIZOTOKEA KABLA YA KUHARIBIWA KWA YERUSALEMU (Lk 21:8-24)
1. Kristo wa uongo (Mst.8): Utabiri huu ulitimizwa wakati idadi ya watu walipodai kuwa Masihi. Mmisri mmoja anatajwa katika Matendo ya mitume 21:38. Alijidai kuwa nabii na kuongoza kundi la watu hadi Mlima wa Mizeituni, akitangaza kwamba kuta za Yerusalemu zitaanguka na watauchukua mji. Felix akashambulia na kuwazingira, lakini Mmisri yule alitoroka. Baadaye, Simon bar Kochba alidai kuwa Masihi, na kuwaongoza Wayahudi dhidi wa Warumi. Alishindwa na Kaisari Hadrini (134 BK) ambaye alilima Yerusalemu kama shamba. Akajaza chumvi, na kubadili jina lake na kujenga Hekalu .
2. Vita na machafuko ya kisiasa (Mst 9-10): Machafuko ya Wayahudi, matokeo ya Masihi wa Uwongo, ilisababisha Roma kutumia nguvu kukomesha machafuko. Takitus (BK 58-120) analelzea nyakati hizi kama âZilizojaa majanga, woga wa vita, na uliojaa ugomvi na hofu.â
3. Mitetemeko ya Ardhi, Ukame, magonjwa na ishara (Mst.11): mitetemeko ya ardhi ilifuatia kifo cha Bwana (Mt 27:51) na ukame kama huo ulikuwa umetafsiriwa na Agabu (Mdo 11:28). Yosephusi anataja idadi ya maono ya kuogofya ambayo yalichukuliwa kama ishara za majanga na wale walioishi Yerusalemu (vita 6: 5: 3). Anaweka kumbukumbu, kwa mfano, nyota, yenye umbo la upanga, ulikuwa juu ya mji: na hii iliendelea kwa mwaka mzima.
4. Mateso ya kisiasa na Migogoro (Mst.12-15): Bwana aliwaonya wanafunzi wake kwamba kuhubiri kwa injili kungesababisha uadui wao na Wayahudi (âsinagogiâ) na Watu wa Mataifa (âWafalme na Watawalaâ) Kama vile angeteseka chini ya mikono yao, wao pia wangeteseka vivyo hivyo. Rekodi ya Matendo ya Mitume inaonyesha muungano wa upinzani wa Wayahudi na Watu wa Mataifa ni kama vile Yesu alivyotabiri: Mateso yalianzishwa na Wayahudi ambao waliwachochea Watu wa mataifa. Hii ilionekana katika maisha ya Paulo (linganisha Mdo. 21-26). Bwana aliwaambia kwamba mateso yatatoa shahidi wa Ukweli. Hivyo badala ya kuvunjwa moyo na mateso, yangekuwa ushahidi kwake, na wangeongezwa nguvu, wakijua kwamba maneno yake yametimia (Mdo 5:41). Sio hivyo tu, bali angesimama nao na kuwapa majibu dhahiri (linganisha Mdo 4:13; 5:33; 26: 31-32).
5. Chuki na Kifo, Marafiki na Jamaa (Mst.16-19): Hapo awali Yesu alikuwa amesema kwamba kuja kwake kutasababisha mgawanyiko (Lk12: 51-53). Injili ingewagawanyisha watu katika makundi kulinga na jinsi watakavyoilewa. Mahitaji yake yangesababisha kujitenga na kujitolea na matokeo yake yangekuwa mgawanyiko katika familia na mateso, hadi usaliti na kifo. Katika kuwaonya, Yesu alikuwa anaondoa shaka yoyote ambayo ingekuwa imetokea.
6. Ishara Kuu:Majeshi ya Uharibifu (Mst. 20-24): Ishara ya wazi ya kwamba wakati umefika wa kuharibiwa kwa Yerusalemu na Hekalu ni kuwepo kwa Jeshi la kirumi. Katika Mathayo 24:15 Yesu ananukuliwa akisema kwamba majeshi yalikuwa âchukizo la uharibifu lile lililonenwa na Danieli yule Nabiiâ, na kwamba watasimama katika âMahali Patakatifuâ au Hekalu. Yesu alipongeza kuelewa kwa Danieli, na kwa kurejelea unabii wa majeshi ya Kirumi, alikuwa ametia muhuri tafsiri yake (linganisha Dan 8:11, 12, 13, 24;9:27).
Yesu aliwaonya waumini kutoroka Yerusalemu pale Jeshi la Yerusalemu lilizingira mji. Nafasi ilitolewa kwa waumini kutoroka: Yosephus na Eusebius anasema kwamba Roma iliingia Yerusalemu mara ya kwanza chini ya Kestia Gallus, lakini waliondoka kwa ghafla kwa njia isiyotarajiwa, kwani wakati huo mji ungechuliwa kwa urahisi. Kwa hili ishara ilikuwa imetolewa kwa Wakristo kutoroka. Kwa sababu ya chukizo hili wengi walitorokea, Pellana wengine Mlima Lebanoni, na hivyo wakaokoa maisha yao.
Yesu aliendelea kusema kwamba hukumu hizi zitakuweko katika âsiku za hukumuâ. Hapo awali alikuwa amesema âmwaka wa neema ya Bwanaâ kwa Israeli lakini wengi âwalikuwa wamefanya licha ya roho ya neemaâ, katika kumkataa Mwana wa Mungu, hivyo kisasi kingefuata (Lk 4:19; Ebr 10: 26- 29; Isa 61: 2).
Kwa sababu alijua ukame ungekumba mji ule uliozingirwa, na kwa kukata tamaa hata watoto wangeangamia, Yesu akasema, Ole wenu nyinyi mlio wajawazito, na wale wanaonyonyesha, katika siku hizoâ (Mst.23, linganisha. Kum. 28:53). Historia iliyofuata ilidhibitisha usahihi wa maneno haya.
Kisha akaendelea kutabiri kuharibiwa kwa uasi wa Wayahudi, na kwa manusura âkuchukuliwa mateka katika mataifa yoteâ (Mst.24). Hii ilikuja kutokea na Wayahudi wakaishi uhamishoni kwa karibu miaka 1900, na wakati huu Yerusalemu ikawa chini ya kisigino cha madhalimu wa Mataifa. Maneno haya ni sahihi: na hakuna hata moja lililokosa kutimia- utabiri ukawa historia.
Lakini Yesu hakusema kwamba uhamisho wa Wayahudi na kuharibika kwa Yerusalemu kungeendelea milele; alitoa kipimo cha mda: âhadi nyakati zao zitakapotimia" (Mst.24).
MATUKIO YALIYOFUATIA KUANZISHWA KWA UFALME WA MUNGU (Lk. 21:25-28)
Zaidi ya miaka 100 iliyopita Wayahudi walikuwa wanafika katika nchi takatifu kulingana na mujibu wa matakwa ya unabii (Yer 30: 10-11; Eze 37; Zak 12: 9-10); na Mei 14, 1948 Israeli huru ilitangazwa na kuanzishwa na Sheria ya mataifa. Lakini Yerusalemu haikuwa huru kutoka kwa kisingino cha ukandamizaji wa Mataifa mpaka Juni, 1967, katika âSiku sita za Vitaâ. Hivyo wakakamilisha kipindi kirefu cha ukandamazaji wa Yerusalemu ulioanza mwaka wa 333 KK, wakati mji ulijiwasilisha kwa Alexander mkuu. Miaka kati ya 333 KK na 1967 ilikuwa jumla ya miaka 2300, na hii ni muhimu kwa sababu hiki ndicho kipindi kilichotengwa na Mungu kwa kuanguka kwa Mji (Dan 8:14). Hakika tunaishi katika nyakati za maajabu!
Yesu aliendelea kuongea kuhusu ishara zingine ambazo zingeashiria mwisho wa ânyakati za Watu wa Mataifaâ. Aliongea kuhusu ishara katika âjua, mwezi na nyotaâ. Vyombo hivi vya mbiguni ni ishara ya nguvu za kisiasa na kidini, kwani zinazo tawala mzunguko wa dunia kwa njia sawa na viongozi wanaodhibiti watu humu duniani (linganisha Isa 24:23; Yoe 2: 10-11, 30 -31; 3:15; Isa 1: 2, 10). Machafuko hayo ya kisiasa na ghasia yameonyeshwa na kuwepo kwa ishara katika âJua, Mwezi, Nyotaâ ni wazi kutoka kwa maneno yafuatayo: â na duniani hali ya dhiki katika mataifa ilikuwa ya kushangazaâ. Hali ya fikra huru, iliotolewa na kuangushwa kwa Mamlaka ya Nchi na Kanisa katika Mapinduzi ya Ufaransa (1790) ilikuwa imeanzisha harakati za Kikomunisti duniani kote. Harakati hii ina msemo wake âUhuru, Usawa na Uduguâ, na anawaita âwafanyikazi wa dunia waunganeâ na kutupa pingu za taratibu za kitambo. Hivyo uasi na mapinduzi yalianzishwa na kusambazwa katika nchi zote. Kuna âroho tatu chafu kama, chura wakifanya miujizaâ. Hali ya msusuko na wazimu ambao umewachanganya wanadamu na mataifa, ambayo sasa hayawezi kutawalika na matokea yake ya mwisho yatakuwa âkuungana ili kufanya vita katika siku kuu ya Mungu mkuuâ (Ufu 16: 13-14). Bahari zinazonguruma, zinaongea kuhusu hali ya msukasuko na kukosa utulivu iliyosababishwa na shughuli za uasi (Mst.25, Isa. 57: 20-21).
Yesu anasema kwamba madhara ya ukosefu wa matumaini utasababisha nyoyo za wanadamu kushindwa (R.V Chapa). Hakutakuwa na hata chembe ya matumaini kwenye upeo kwa wale wasio na utambuzi (Mst.26). katika nyakati hizi za kukata tamaa, wakati mataifa makuu yanaungana Katika vita vya mwisho katika milima ya Israeli, âMwana wa Mtu atakuja na nguvu na utukufu mkuuâ, na kuweka hofu zaidi kwa wale waliomkataa (Ufu.1: 7).
Lakini kwa ajili ya watakatifu hali ya dhiki itasababisha furaha na sio woga, kwani siku ya ukombozi itakuwa karibu: â na wakati mambo hayo yote yanaanza kutimia, basi tizameni juu na muinue vichwa vyenu; kwani siku ya wokovu wenu imekaribiaâ (Mst.28)
MFANO WA MTI WA MTINI (Lk. 21:29-33)
Ishara hizi zote zitakuwa kama kuchipuka kwa matawi kwa majani ya mtini, ambayo yanaashiria kwamba msimu wa kiangazi umekaribia. Lakini kunaonekana kuwa na uwongo uliofichika, kwani Mtini unatumika mara nyingi kama kielelezo cha Israeli katika manabii (Yer 8:13; 24: 1; 29:17; Yoe 1: 7, 12) na hasa na Bwana mwenyewe (Lk 13: 7; Mk 11:13-14). Kuchipuka kwa matawi kwa majani ya Mtini basi inakuwa ishara ya kuwa kutakuwa na maisha tena katika âShina lililokufa la Israeli ya siku hizi (linganisha. Isa. 6:13). Kuanzishwa tena kwa taifa la Israeli ni kutimiza.
ONYO LA KUKESHA (Lk. 21:34-36)
Kwa mtazamo wa kukata tamaa uliokuwepo, binadamu katika Agano la Kale ndio wanao gusiwa na unabii huu katika Isaya 24, wanaojipatia kila aina ya raha ya kimwili (Isa 24: 6-9). Utafutaji huu wa tamaa ya kimwili hivi karibuni utageuzwa na kuwa kuchanganyikiwa kwa mtetemeko wa ardhi (Mst.1) na hukumu (Mst.17-22) lakini hatari kwa watakatifu wa siku za mwisho ni kwamba wao pia, wanaweza kuvutiwa kwa hali ile ya anasa na mvuto wa nyakati zile. Hivyo Bwana anatoa onyo kwetu sisi: âBasi jiangalieni mioyo yenu isije ikalemewa na ulafi, ulevi, anasa na masumbufu ya maisha haya, kwani siku ile itawajia ghaflaâ (Mst.34).
Katika Mstari wa 35 ana nukuu Isaiya 24:17 ambayo inaonyesha jinsi siku hiyo ambayo haijatarajiwa itakavyokuwa. Picha ya kutisha na ya kuchanganyikiwa inaonyesha mtu akikimbia kwa hofu, akianguka kwa shimo, na kutokea akiwa na mtego shingoni! Jinsi gani siku hio itakuwa ya kutisha kwa wale hawajachukua jina la Bwana na hawatembei katika nyayo zake! Itaonekana basi kwamba huduma kwa Bwana ndiyo huduma pekee isiyo ya bure (1 Kor 15:58).
Kwa kumalizia anashauri wafuasi kuwa kukesha na kuomba kila mara, ili wasipatwe bila kutarajia, na waweze kusimama dhabiti mbele yake (Mst.36)
MAMBO TUNAYOJIFUNZA:
- Neno la Mungu ni kweli kama inavyothibitishwa na unabii ambao sasa umekuwa historia.
- Tunaishi katika nyakati za hukumu, kufuatia kuanzishwa kwa Israeli kama taifa na kukomboa Yerusalemu kutoka katika mikono ya Mataifa.
- Ni muhimu kuhusisha hali halisi ya kisiasa ya siku yetu ya unabii wa Kristo katika mlima wa Mizeituni.
- Tutaangamia kama tutavutiwa na dunia na kufuata mwongozo wake.
- Kukesha na maombi ya kila mara ni muhimu kwa ajili ya kukubalika.
MAKTABA YA KUREJELEA:
"The Ways of Providence" (R. Roberts)â Sura 24-26
"Wars of the Jews" (Yosephus)
MASWALI YA AYA:
- Ni onyo gani Yesu alitoa kwa kizazi chetu katika Unabii wa Mizeituni.
- Yesu alisema kwamba Yerusalemu "itakuwa chini ya mataifa mengine mpaka muda wa mataifa utakapotimia". Jinsi gani kauli hii ilitimia katika vita vya siku sita mwaka wa 1967?
- Jinsi gani Isaya 24 alinukuliwa katika Unabii wa Mizeituni katika Luka 21?
- Yesu alisema katika Unabii wa Mizeituni, "Wakati mambo hayo yatakapoanza kutukia, inueni vichwa vyenu juu, kwa maana ukombozi wenu umekaribia". Alimaanisha nini?
MASWALI YA INSHA:
- Ni ishara gani Yesu aliwapa wanafunzi wake kuhusu ukiwa wa Hekalu? Jinsi gani ishara hizi zilitimia?
- Katika Unabii wa Mlima wa Mizeituni Yesu alitoa ishara nyingi za nyakati kabla ya ujio wake madarakani. Onyesha jinsi ishara hizi zinakamilishwa leo. Ni maonyo gani ya kizazi chetu tunapata?
-
Onyesha jinsi ambavyo unabii katika unabii wa Mizeituni ulitimia: -
a) katika mwaka 70 BK wakati Hekalu na Jumuiya ya Israeli iliharibiwa na Warumi;
b) katika siku hizi za mwisho za watu wa mataifa. - Andika insha juu ya umuhimu wa Unabii wa Mizeituni kwako wewe.