347

Swahili

347. MFANO WA MWISHO: JINSI YA KUWA NA MAARIFA NA WAAMINIFU

"Njooni, mliobarikiwa na Babangu, mridhi Ufalme"

Katika Unabii wa Mizeituni Yesu aliwapa wanafunzi wake ishara kuhusu ujio wake. Katika mifano hii ya mwisho anaelezea vile wanafunzi wake wanapaswa kujishughulisha wakati hayuko ili wawe tayari kukutana naye.

Katika Mfano wa “ Mwenye nyumba” Yesu anasisitiza kuhusu umuhimu wa wafuasi wake kukesha, kwani atakuja wakati asio tarajiwa. Akiendeleza wazo kwa wanafunzi wake kuwa mkuu wa nyumba, aliuliza swali, "Ni nani basi mtumishi mwaminifu na mwenye busara, ambaye bwana wake atamweka kama mtawala wa nyumba yake, awape chakula msimu ukifika?” (Mat. 24:45). Katika Mathayo 25 Yesu anaongea kuhusu mifano mitatu, ambayo kila mmoja alijibu swali hili.

  1. Wanawali kumi- Mfano huu unaonyesha jinsi ya kuwa na “BUSARA” (25:2) na unaonyesha haja ya kuwa waangalifu.
  2. Vipaji- mfano  huu unaonyesha jinsi ya  kuwa “WAAMINIFU” (25:21), na kutoa sisitizo kuhusu haja ya kutumia muda kwa faida yetu.
  3. Kondoo na Mbuzi- unaonyesha kile kilichomaanishwa kwa “ KUTOA CHAKULA WAKATI UKIFIKA” kwa nyumba yake na inasisistiza umuhimu wa kushirikiana na kuwasaidia wengine.

Lengo la somo hili ni kujifunza kile tunapaswa kufanya ili kuwa tayari wakati Bwana anakuja.

Mathayo 25

1. MFANO WA WANAWALI KUMI (Mt. 25:1-13).

Mfano huu unatufunza jinsi ya kuwa na hekima, ni muhimu kwetu kuelewa jinsi mfano huu unafanya hivi. Jibu linapatikana katika maneno ya Yesu ya Mwisho, “kesheni, kwani hamjui siku wala saa wakati Mwana wa Mtu atakapokuja” (Mst.13). kwa kusema hivyo, Yesu anatangaza kukesha kama ishara ya hekima. Hata hivyo, wanawali waliokuwa “tayari” pia walikuwa na jukumu la kufanya: Walikuwa wawe na mafuta ya  kutosha kwa ajili ya tukio hili kipekee la ujio wa Bibi harusi.

Kulikuwa na Wanawali kumi. Namba kumi iliwakilisha wote (linganisha Mwa. 31: 7, Hes. 14:22; Dan 1:20; Zek 8:23), na hapa kuna Wayahudi na Watu wa Mataifa (linganisha Mst.32). Ukweli kwamba kulikuwa na watano waliokubalika na watano waliokataliwa haionyeshi kwamba nusu ya wale watakao itwa wataokolewa; Yesu anashughulika na ubora wa watumishi wake na si idadi ya wale wakataopokea wokovu.

Wanawali wapumbavu walikosa mtizamo na “ hawakuchukua mafuta” (Mst.3). Wanalinganishwa na wale wenye maarifa waliojitayarisha hapo awali, na wakajibebea mafuta ya akiba. Mafuta katika maandiko matakatifu yanaashiria ya Roho ya Mungu ambayo inaangaza moyo wa mwanadamu uliojaa giza (Kut 27:20; Zab 119: 130). Leo Mafuta yanasimamia Neno la Mungu, lililotolewa na Roho Mtakatifu, ambalo ni mwanga wa Habari Njema ya utukufu wa Kristo (2 Pet.1. 19-20; 2 Kor 4: 4). Lazima tuwe na busara na tuweke ujumbe wa injili ndani yetu, ili tabia zetu zing’ae kama taa iliyojazwa mafuta (linganisha Mt. 5: 15-16). Mwanga kioo cha maisha ya Yesu Kristo inayo onyeshwa na wale wote wanaomfuata. Tutakubaliwa naye katika kiti cha hukumu (1 Yn 3: 2; Mt. 7: 21-24)

WOTE WAKASINZIA NA KULALA (Mt. 25:5).

Kauli hii inaonyesha kwamba muda mrefu utapita kabla Yesu kurejea. Karibu watakatifu wote watakuwa wamefariki, na ni wachache watakao kuwa wamebaki wakati wa ujio wake (1 The. 4:15; 1Kor 15:51). Wakati walipoitwa kwenda kumlaki bibi harusi, “wanawali wote waliinuka” na walipaswa kuwa wamejitayarisha; hivyo kuonyesha kwamba wanaojua mapenzi ya Mungu watashuhudia. Mwito ulikuja usiku wa manane, saa yenye giza kuu. Hivyo kusisitiza somo kwamba Bwana atakuja “Ghafla” na bila kutarajiwa. Kwa haraka waliinuka na kuzitengeneza taa zao ( yaani kuonyesha tabia na kazi zao)

Kwa kukata tamaa wale wajinga waliomba, “ tupeni mafuta yenu kidogo kwani taa zetu zinazimika”. Lakini walikuwa wamechelewa, na hofu yao inaonyesha utambuzi wa kutisha ambao itawakumba watumishi wale watakuwa wamepoteza fursa yao ya kumtumikia Mungu. Wale wenye maaarifa wakajibu : sivyo; hayatutosha sisi na nyinyi” (Mst.9) katika jibu hili tunaonyeshwa kwamba wakati Bwana atakapowasili muda utakuwa umekwisha wa kufanya matayarisho zaidi: Sasa ni wakati wa kwenda sokoni na kununua mafuta. Tuna wakati sasa na tunapaswa kutumia muda huo kwa busara, sio kama Wanawali wale wapumbavu.

Siku waliokuwa nazo za nafasi za kujitayarisha ziliisha wakati walipolala nasi zetu zitakuwa zimeisha wakati tutakapo aga dunia au kutokea kwa ghafla kwa Bwana.

Mafuta yana gharama- lakini sio fedha bali maombi: “njooni kwenye maji, naye asiye na fedha; nunueni mle; nunueni divai na maziwa bila fedha na bila dhamani” (Isa 55:1) .

Baada ya muda wale wanawali wapumbavu walirudi na kuomba wakubaliwe kuingia, “Bwana, Bwana,  tufungulie” (Mst.11). Ombi kama hili lilijibiwa na maneno ya kutisha: Amini nawaambia, siwajui ninyi” (Mst. 12. Kwa kweli hakuwajua kwa sababu hawakumjua: maisha yao hayakuwa yanaendana na mfano wake.

Mifano ya Yesu mara nying ina uhusiano na Agano la Kale. Tizama jinsi misingi ya mfano huu unapatikana katika Mithali 21:20 " kuna hazina ya dhamani na mafuta katika masakani ya mwenye hekima; lakini mwanadamu aliye mpumbavu hutumia yote” anaendelea kwa kurejelea mfano mwingine katika siku za Nuhu,  “ wakati hukumu ya Mungu ilisubiri” wakati maalum, na kisha “akafunga mlango” wa safina na kuwagawanyisha wenye maarifa kutoka kwa wajinga. Katika mfano huu Yesu alisema, “waliokuwa tayari wakaingia ndani... na mlango ukafungwa”(. Mst10 linganisha Mwa 7: 7, 16).

Kuwa na mafuta sio tu kuelewa Neno la Mungu, lakini utafiti ambapo moyo unageuzwa na kumpenda na kumtumikia Mungu. “Kutazama”, kwa hivyo, kunahusisha zaidi ya kuangalia ishara za nyakati kuona  dalili za kuja kwa Yesu; ni utambuzi wa haja ya kuwa tayari kumlaki Bwana wakati mwito unakuja.

Imesemwa vyema “uajizi ni mwizi wa nafasi na pia muda: na  fursa inaisha usingizi unapotujia. Tuna siku ya Leo Pekee”.

 

2. MFANO WA TALANTA (Mt. 25:14-30).

Katika mfano huu Yesu anaonyesha kwamba “mtumishi mwaminifu” anatumia wakati wake kupata faida. Neno “kwa”, inaanzisha hadithi  mpya na pia kujenga funzo la hadithi ya hapo awali. Wakati huu “Mtu” ambaye anasafiri katika nchi ya mbali anawacha mali yake chini ya uangalizi wa “Watumishi”, akigawanyisha kulingana na uwezo wao. Yesu ndiye “Mtu” na wanafunzi wake ndio “Watumishi”. Mali inagawanywa kwa misingi kwamba itatumiwa vyema ili kuongezeka zaidi katika siku ya Hesabu (Mst.19).

Jinsi mfano unavyoendelea, somo muhimu linatokea. Watumishi watatu wanapewa talanta kulingana na uwezo wao (Mst.15). Haki ya Mungu inaonekana kwamba hakutarajia zaidi ya  kile walichoweza kutoa, na yote, bila kujali uwezo, wanapewa nafasi ya kutumikia.

MTUMISHI MWEMA NA MWAMINIFU (Mt. 25:20-23)

Watumishi wawili walizidisha talanta kwa kufanya biashara ilio kubalika na Mungu. Kama talanta tuliopewa inawakilisha injili tunayoamini, basi ongezeko linawakilisha matunda ya mtu mwaminifu anayetembea kwa Ukweli (Yak. 2:17). Katika mfano huu, mtumishi mwaminifu anasemwa kuwa “mwaminifu kwa machche” (Mst.21). Zawadi haikutoshana na faida iliyopatikana ilikuwa kubwa zaidi: “Nitakufanya mtawala wa mambo makuu” (Mst.21). Kwa njia hii maoni ya kwamba wokovu unaweza nunuliwa unawekwa mbali.

MTUMISHI MWOVU NA MVIVU (Mt. 25:24-30).

Mtumishi aliyekabidhiwa talanta moja alishindwa. Ni wazi kwamba ni lazima kwa kila mtu kufanya awezavyo hata kama anakosa uwezo. Mtumishi huyu, hata hivyo, “akaenda na kuchimba ardhi na kuficha talanta aliyopewa na Bwana wake” (Mst.18): alikataa kufanya kazi. Hakupata chochote na hatimaye akapoteza hata kile alichokuwa nacho kwani alikuwa mvivu.

Wakati wake ulipofika wa kujibu alikuwa na kisingizio alichokuwa amekwisha tayarisha; kazi aliyopewa ilikuwa “nyingi sana” kwake na badala ya kuingia katika hatari ya kupoteza amana yake, aliihifadhi katika ardhi! Alifikiria hili kuwa jambo la “busara” kwani “aliogopa” Bwana wake kwani alimjua kuwa “mtu mgumu” hata kutaka mazao mahali alikokuwa hajapanda! (Mst.24-25). Bwana wake alifutilia mbali sababu zake, akisema kwamba kama huu ndio ulikuwa mtazamo wake kwake basi alikuwa na sababu zaidi za kuzalisha fedha ile. Hata faida ndogo inayopatikana katika kuwekeza kwa watoa riba ingekuwa bora kuliko kutopata kitu (Mst.26-27).

MAANA

Kila mtumishi amekabidhiwa na Ukweli na uwezo fulani na Mungu anatarajia faida na maendeleo kwa mujibu wa hayo. Wakati mtu anafanya biashara akitumia pesa anazizidisha. Lazima tufanye hivyo na Neno la Mungu. Lazima tusaidie neno kukua. Hili linafanyika, sio tu kwa kuwafunza wengine, lakini kwa kukubali Neno libadilishe maisha yetu. Wakati tunakubali nguvu za Kristo kubadili maisha yetu,  tunafanya “biashara kwa faida”.  Hatuwezi kuweka Ukweli umefungwa ndani ya nguo kama mtumishi mvivu. Talanta hazina dhamani kama hazitatumiwa kwa faida- katika kufananisha maisha yetu na Kristo, na kuleta wengine kumjua.

Umuhimu wa huduma ya bidii unatiliwa mkazo kutokana na hatma ya mtumishi yule mwovu: Mtupeni mtumwa huyu asiye na faida katika giza: kule kutakakokuwa na kilio na kusaga meno” (Mst.30). Uchungu, majuto na mauti ya milele utakuwa kwa wale watakoshindwa kuishi katika Ukweli. Basi tuwe “"watendaji wa neno"- wafanyi biashara wenye faida-  na sio wasikizaji tu” (Yak 1:22-25).

3. MFANO WA KONDOO NA MBUZI (Mt. 25:31-46).

Katika mfano huu Yesu anaelezea jinsi “watumwa waaminifu” wanafanya  katika nyumba ya Bwana wao: anaonyesha kile anamaanisha kwa kusema “chakula katika msimu” (Mt. 24:25). Hadithi sio mfano kama ile mifano miwili ya kwanza kwa sababu baadhi ya sehemu zake  zimechukuliwa zilivyo (kama kutembelea wagonjwa,Mst.36).

Picha ya hukumu ya mwisho ambapo Yesu amekaa katika kiti cha enzi na utukufu wake, na amezingirwa na “mataifa yote” yaani, wale ambao ni jukumu lake “watu wa mataifa yote, jamaa, na watu, na watu wa ndimi, (Mdo15:14; Ufu. 7: 9).  Kama mchungaji wa kondoo walio changanyika kuanzia kondoo na mbuzi, Yesu anamweka Mbuzi mtiifu kwa upande wa kulia na kondoo mtundu kwa upande wa kushoto (Mst.31-33).
 

MBUZI (Mt. 25:34-40).

Yesu anaendelea kusifu matendo ya uaminifu ya wale wenye haki. Misingi ya kukubaliwa kwao ilikuwa katika upendo wa ndugu zao kwa vitendo- mambo ambayo kila mtu, hata watoto, wanaweza wakafanya – walipaswa kuwalisha wenye njaa, kuwapa wageni malazi, kuwavika walio rarukiwa na kuwatembelea  wagonjwa. Matendo yao yalionyesha kuwa walikuwa wake. Zaidi ya hayo matendo yao hayakufanywa na maadili yanayofaa. Walipinga  kupongezwa na Bwana wao.  Lakini anafafanua hukumu yake kwao  kwa  kuwaelezea kwamba huruma inapaswa kuonyeshwa hata kwa ndugu wadogo wanatambua huduma kwake! Kwa njia hii Bwana anawahimiza wanafunzi wa kweli wawe wachungaji wa kuwatunza “ndugu zao wadogo” wao pia ni sehemu ya “Mwili mmoja” wa Kristo

KONDOO (Mt. 25:41-46)

Waliokataliwa wanatupwa katika mkono wa kushoto kwa “Moto wa Milele”, ishara ya mauti ya milele. Hawakuwa wameishi maisha ya “imani kwa vitendo”. Wanahukumiwa kwani  hawakumtendea vitendo vya huruma. Walipinga utawala wake kwa misingi ya kwamba hawakuwa wamemwona akiwa na haja kwa hivyo hawakupata fursa ya kufanya kile alichokuwa  akiwaamuru! Lakini jibu lake linawachanganya:  anawaonyesha kwamba wanapaswa kuonyesha matendo ya huruma kwa "mdogo kuliko ndugu zake" ni sawa na  matendo ya huruma kwake mwenyewe! Kila siku walikuwa na fursa hio, lakini walishindwa kufanya hivyo.

Hivyo hukumu inategemea kile tunachokifanya hapa na sasa! Hatutabadilika na kuwa mbuzi au kondoo katika siku ya hukumu; tunakuwa moja kati ya hizi mbili jinsi tunavyoishi maisha yetu sasa

MAKTABA YA KUREJELEA:

  • Wenye busara watajiandaa sasa, kwa mlango utafungwa wakati Kristo atakuja.
  • Watumishi waaminifu wanafanya "biashara" na injili na kuiruhusu injili ishawishi maisha yao na kwa kuwafundisha wengine.
  • Kristo anatumikiwa wakati tunaonyesha kwa matendo ya wema kwa ndugu wadogo.
  • Mwisho uliojaa woga unawagonja watumishi wasio waaminifu.

MAKTABA YA KUREJELEA:

"Nazareth Revisited" (R. Roberts)—Sura 32, 33, 50

"A Life of Jesus" (M. Purkis)—Kitabu 7, Sura 8

"Parables of the Messiah" (J. Carter)—Nam. 56-58

MASWALI YA AYA:

  1. Elezea kauli ya Yesu, "kadiri mlivyowatendea mojawapo wa ndungu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi" (Mt. 25:40).
  2. Eleza tabia na hukumu ya "mtumishi mwovu na mvivu" katika mfano wa Talanta.
  3. Nini kilichotokea kwa  wanawali watano wapumbavu wakati mwito ulitolewa: "Tazama, Bwana harusi anakuja"?

MASWALI YA INSHA:

  1.  Elezea mfano wa Wanawali kumi na uelezee maana yake.
  2. Elezea mfano wa Talanta. Ni masomo gani tunajifunza kutoka kwa mfano huu?
  3. Yesu alisema: "Basi ni nani mtumishi mwaminifu na mwenye busara, ambaye bwana atamweka juu ya watumishi wake ili awape chakula kwa wakati wake?" (Mt. 24:45). Onyesha jinsi kauli hii imefafanuliwa kwa mifano ifuatayo, Wanawali kumi, Talanta, na Kondoo na Mbuzi.
  4.  Eleza mfano wa Kondoo na Mbuzi.

 

 

Swahili Title
347. MFANO WA MWISHO: JINSI YA KUWA NA MAARIFA NA WAAMINIFU
Sub type
Sub sub type