349. KESI NA KUSULUBIWA
âYeye ni kama mwana kondoo wa kuchinjwa"
Mtume Paulo aliandika kwamba âYesu Kristo... mbele ya Pontio Pilato alikiri vyemaâ. Kwa kweli kulikua na msusuru wa kesi, hakuna hata moja ilionyesha dhambi au kosa la Bwana. Kila moja lilikuwa kejeli ya haki. Hivyo alichukuliwa, kama mwanakondoo asiye na dhambi kwenda kuchinjwa, kwa mikono miovu, alisulubishwa na kuchinjwa. Ilikuwa â wakati wao na nguvu za gizaâ. Wakati Baba wa mbiguni aliwaruhusu kufanya kitendo chao kiovu, Alionyesha furaha yake kwa ishara ya ajabu, na kutoa mazishi ya heshima kwa ajili ya Mwana wake mpendwa.
Lengo la somo hili ni kuonyesha jinsi upendo wa Mungu ulivyo mkuu kwetu sisi kwa kutoa Mwana wake kama sadaka kwa dhambi zetu: na kuonyesha ukumbwa wa majaribio na utii wa Mwokozi wetu, Yesu Kristo, ili awe mkamilifu
Mathayo 26: 57-75; 27: 1-61; Yohana 18: 28-40; 19: 1-18
MAJARIBIO MBELE YA WAKUU WA KIYAHUDI-
JARIBIO LA KWANZA: Mbele ya Anasi (Yn.18:13, 19-24).
Kesi ya Yesu ilifanyika katika hatua sita, tatu mbele ya wazee wa Wayahudi na tatu mbele ya viongozi wa Mataifa. Ni Yohana pekee ambaye aliyeandika kuhusu sehemu ya kwanza ambayo ilikuwa mbele ya Anasi, ambao ingawa walitolewa madarakani na makuhani wakuu wa Kirumi, bado walitambulika kati ya Wayahudi (mfano Lk 3: 2; Mdo 4: 6). Alikuwa mkuu wa Baraza aliyekuwa tajiri na mwenye nguvu. Anasi alimuuliza kuhusu wanafunzi wake na mafundisho yake. Yesu alimwelekeza kwa wale waliomsikiza, kwani kama alivyoelezea, alikua ameongea wazi kokote alikokwenda. Kwa kusema hili alizabwa kofi na mmoja wa maafisa. Kofi la kwanza lilikuwa kwa shavu lake. Hili lilikuwa pigo la kwanza kati ya mapigo mengi aliyopata ambayo yaliharibu mwili wake mpaka pale akawa âamejeruhiwa kuliko binadamu yeyote yuleâ (Isa. 52:14). Anasi kisha akamfunga Yesu na kumtuma kwa Kayafa (Mst.24)
Jaribio la Pili: Kesi Mbele ya Kayafa kabla ya machweo (Mt. 26:57-68).
Kesi ya Yesu ilifanyika wakati wa usiku wa manane (linganisha Yohana 18:3; Mt. 26:43, 74; 27: 1). Hivyo Yesu akaletwa mbele ya Wakuu, kukiwa na baridi, kabla ya machweo. Kesi kama hii haikuwa halali kwani hakuna kesi kuu zilizofanyika kabla ya kutua kwa jua. Kayafa alikuwa ameita kundi kubwa la viongozi waaminifu kwake ili kumsingizia makosa â ili wamuueâ. Walipitisha hukumu yao kabla ya kusikiza ushahidi.
Idadi ya mashahidi wa uongo walitoa ushahidi lakini hali ya kuchangikiwa ilionekana kwani walijichanganya wao wenyewe (linganisha Kum 17: 6-7; 19:15-21). Mwishowe mashahidi wawili walijitokeza wakisema kwamba Yesu alikuwa amedai kwamba ataharibu na kujenga hekalu kwa siku tatu. Ilionekana kwamba walikuwa wanapotosha kauli Bwana ya hapo awali (Yn. 2:19). Kauli yao ilionyesha kufuru na uchawi. Madai haya mawili yangetumika kuleta adhabu ya kifo kulingana na sheria ya Wayahudi. Lakini Kayafa alihitaji zaidi ya hayo, kwani Pilato hakujali kuhusu kufuru na uchawi? Lazima kungekuwa na kosa kubwa kuliko hili. Kayafa alikuwa anakata tamaa. Muda ulikiwa unasonga na hakuna kitu kilichokuwa kinatokea. Masaa machache yajayo mahujaji wa Pasaka wangejaa katika mji wakielekea katika mahakama wakimtafuta Nabii wa Galilee. Kuhani Mkuu alikuwa katika hatari ya kumpoteza mfungwa wake. Hali ya ukimya ya mfungwa wake ilifanya hali hii kuwa ngumu zaidi. Ilikuwa ni vita vya tabia.
Bwana alisimama ametulia na akiwa na ushujaa katikati mwa vurugu lililojaa hofu. Kayafa alimkemea Yesu kwa kutojibu mashataka yaliyomkabili, lakini yeye alitulia (linganisha Zab. 26: 4; Isa 53: 7). Akihisi mzigo, Kuhani mkuu aligeukia sheria ya uapisho, âtuambie kama wewe ndiye Kristo, Mwana wa Munguâ (Mt. 26:63; linganisha Law 5: 1) Jibu la yesu lilikuwa uhakikisho wa wazi, akichanganya maonyo ya (Zab. 110:1 na Dan. 7:13: â Mtaona Mwana mtu akiwa ameketi katika upande wa kulia wa Nguvu, akija katika wingu kutoka mbiguniâ. Hapa palikuwa na kukiri ambako Kayafa alikuwa akitaka: sasa angemshitaki Yesu kwa kosa la kukufuru mbele ya Wayahudi na uhaini kabla Warumi. Aliwaongoza viongozi katika kurarua nguo zake, kwa sababu ya madai ya âkufuruâ hawakuhitaji mashahidi zaidi! Kurarua nguo zake, kulikuwa ishara iliyokubalika kwa kosa la kukufuru, lakini ilikatazwa kufanywa na kuhani mkuu (Law. 21:10)! Hivyo Kayafa, akisimama mbele ya Kuhani Mkuu wa Kweli (ambaye, katika suala la Zaburi 110 alikuwa amenukuliwa akisema kwamba, atawaangamiza adui zake wote na kuanzisha utaratibu mpya wa Ukuhani wa Melkizedeki), alirarua vipande vipande nguo zake maalum na kijidhalilisha yeye mwenyewe! Hata hivyo kwa muda huu matendo yake yalileta matokeo yaliyotarajiwa. Wale waliokuwepo walisimama kama vibaraka na kutangaza kwamba Bwana alikuwa na âHatia ya Kifoâ. Wakamtemea mate, wakampiga, na wakadhihaki madai yake. Maandiko na nguvu za Mungu zilihibitishwa na matendo haya (Mt. 20: 17-19.; Mk 10: 33-34; Isa 50: 5-8).
Jaribio la Tatu: Hukumu Rasmi Mbele ya Baraza (Sanhedrin) Alfajiri.
Mathayo na Marko wanaelezea kwamba Alfajiri mkusanyiko wa wakuu 70 waliitwa kukubaliana na uamuzi (Mt. 27:1; Mk 15: 1; Lk 22:66). Walidhibitisha hukumu ya kifo, lakini kwa sababu hawakuwa na uwezo wa kutekeleza hukumu, walimtuma Yesu akiwa amefungwa kwa Gavana wa Kirumi, Pontio Pilato (Yn. 18:31).
KESI MBELE YA UTAWALA WA MATAIFA
Kesi Ya Kwanza: Kuja Kwa Mara Kwanza Mbele Ya Pontio Pilato.
Haikuwa ajali kwamba Mwana wa Mungu aliletwa mbele ya utawala wa Mataifa. Binadamu wote walikuwa wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu. Ilikuwa inafaa, kwamba, Wayahudi na Watu wa mataifa waungane kutenda dhambi kubwa zaidi katika historia ya binadamu
(Rum. 3: 9, 20, 23).
Aidha, maandiko yalikuwa yametabiri kwamba wangefanya hivyo. Katika Zaburi 2 ( imenukuliwa katika Matendo 4: 25-26 na kupewa matumizi katika ujio wa kwanza), imetangazwa kwamba Wayahudi na Watu wa Mataifa wataungana na kupokea ushauri dhidi ya mteuliwa (Mst.l, 2). Maandiko na Yesu alikuwa ametabiri kwamba angekufa kwa âkusulubishwaâ- njia ya kifo ambayo ilitekelezwa na Warumi (Yn 3:14; 12: 32-33 Isa 11:10), tofauti na mtindo wa Wayahudi wa kupiga mawe (linganisha Yohana 18:30-32).
Umbo la mamlaka la Pontio Pilato lilikuwa tayari limewakasirisha Wayahudi: Mapungufu yake yalikuwa yameripotiwa Roma. Angepoteza nafasi yake kama mageuzi mengine yangetokea. Hivyo, ingawa Pilato hakupata makosa kwa Yesu, alitaka âkukubaliana na Watuâ (Lk. 23: 4; Mk 15:15). Katika ukumbi wa Hukumu aliendelea kumuuliza maswali Yesu ambaye alikuwa amehukumiwa na kosa la âkupotosha taifa, na kuwakataza watu kulipa kodi kwa Kaisari, akisema kwamba yeye mwenyewe ni Kristo Mfalmeâ (Lk. 23: 2). Madai haya yalikuwa makubwa sana, na Pilato, akikumbuka nafasi yake hafifu mamlakani, na angeweza kuyachukulia kwa urahisi. Hata hivyo hakutaka kukubaliana na madai yao kwa sababu alijua kwamba âkwa sababu ya wivuâ walikuwa wamemleta kwake (Mk.15:10). Hakuweza kuamini kwamba mtu huyu aliyepigwa na mnyeyevu angeweza kuwa mwanzilishi wa fitina! Kando na haya, Mke wake alimletea habari mbaya, akimsihi kwamba asihusike katika kuamuru kifo chake âmtu huyu mwenye hakiâ kwani mkewe alikuwa "ameteseka mambo mengi siku hio katika ndoto kwa sababu yakeâ.
Baada ya Pilato kumhoji Yesu, kama ilivyorekodiwa kwa kirefu katika Yohana 18: 33-38, alipitisha uamuzi wake, âmimi sioni hatia yoyote kwakeâ (Yn 18:38; Lk. 23: 4). Lakini Wayahudi walipinga kwa nguvu, "Anawachochea watu kwa mafundisho yake katika nchi yote ya Yudea, kuanzia Galilaya hata mahali hapa" (Lk. 23: 5). Alipotambua kwamba alikuwa Mgalilaya, alichukua nafasi kuchelewesha. Angemtuma kwa jengo lililopakana na hilo akahukumiwe na Herode wa Antipa.Hili lilikuwa kosa baya. Kuanzi wakati huo Pilato akawa chombo cha makuhani, na hakuna kitu kingemwoka sasa. Chini ya shinikizo alifungua kesi ambayo ilikuwa imeisha tayari.
Kesi Ya Pili: Mbele Ya Herode (Lk. 23:8^12).
Ni Luka pekee aliyerekodi tukio hili. Heredo Antipa, âMbwehaâ alitaka kutosheleza udadisi wake juu ya Yesu ambaye alikuwa amesikia mengi kumhusu. Alitarajia kuona muujiza. Kutofurahishwa kwa Yesu na mtu huyu mwovu kunaonyeshwa kwa kimya chake: âHakumjibu chochoteâ (Mst.9, Lk 13:32). Kwa hasira, Herode aliwatuma majeshi wake kumpiga Yesu, ambao walidhihaki madai yake ya kifalme kwa kuweka mataji ya kifalme juu yake (linganisha 9 Mk. 33-35; Isa 52:14; 53: 3)! Hivyo Yesu akarudishwa kwa Pilato na Herode âWakawa Marafikiâ.
Kesi Ya Tatu: Kutokea Mara Ya Pili Mbele Ya Pontio Pilato (Mt. 27:15-24; Lk. 23:13-25; Yn. 18:33; 19:16).
Haki haingeweza kutarajiwa kutoka Pilato. Alikuwa amebadilisha akili yake pale alipotambua kwamba ingembidi akubaliane na shinikizo la Wayahudi. Alijaribu kumweka Yesu kama mfungwa atakaye wekwa huru wakati wa Pasaka, kwani hii ndio iliokuwa desturi. Lakini watu, wakiwa wameshinikizwa na makuhani wakuu, walikataa hili na kumlilia Baraba aliyekuwa amehukumiwa kwa ajili ya mauaji na fitina dhidi ya Roma, madai sawa na waliokuwa wamemwekea Yesu bila ushahidi (Mk 15:7; linganisha Isa 53 : 12; Mk 14:48)! Kumbukumbu ya Yohana inatoa maelezo na kuonyesha kwamba masumbuko ya kiroho ya Gavana huyu alipojaribu kuzuia hukumu ya kifo ya mtu huyu asiye na hatia. Ili kuwafurahisha wayahudi, aliamuru Yesu apigwe mijeledi. Askari walimkejeli na kumdhihaki na kumvika taji la miiba na kumvika vazi la zambarau (Yn 19: 1-3). Baada ya hili kufanyika, Pilato akamleta mtu yule aliyepigwa mbele ya Wayahudi, na akisihi utu wao, akasema, âTazama, mtu huyu!" lakini hakukuwa na huruma. Wakiogopa kwamba Pilato atamsamehe, Makuhani wakuu na maafisa wakalilia damu yake, âMsulubishe, msulubishe".
Kisha wakapanga njama ya ujanja, wangeshtumu Pilato kwamba hakuwa mwaminifu kwa Roma kama angemsamehe Yesu: "Ukimwachilia huyu mtu, wewe si rafiki yake Kaisari; kila mtu anayejifanya kuwa Mfalme hamfitini Kaisari (Yn 19:12). Akiwa amekubwa na changamoto hii ya uaminifu kwa Roma, Pilato, licha ya maneno yake mengi kuhusu kutokuwa na hatia kwa Yesu, alikubaliana na Wayahudi na akamtoa Yesu asulubishwe (Mt. 27:24).
âAkachukua maji na kuosha mikono mbele ya umati, akisema, â'Mimi sina hatia ya damu ya mtu mwenye haki; kama mlivyoona wenyeweâ. Hili lilikuwa onyesho la kuchukiza la kujaribu kujiondoa katika dhambi ambayo udhaifu wake ulikuwa ameukubalisha. Lakini doa ya dhambi haiwezi kuondolewa kwa urahisi.
Wengine walikuwa tayari zaidi ya wengine kukubali hatia; Wayahudi wakasema, âDamu yake na iwe juu yetu na juu ya watoto wetu" (Mt. 27: 24-25). Huu ulikuwa unabii wa kutisha: Mateso ya Wayahudi kwa zaidi ya miaka 1900 yanatokana kwa kumkataa Masihi.
ASULUBIWE!
Kuchukua taswira ya askari ya Kirumi akipigilia misumari mikubwa katika mikono na miguu ya Bwana kwenye mbau, kunajaza mtu na hasira ya haki. Hata kama alisulubiwa saa tatu asubuhi (Mk. 15:25), nje ya kuta za mji, mahali paitwapo "Golgotha" (au kwa Kigiriki "Kalvari"), maana yake "Fuvu la Kichwa" (Ebr 13:12; Law 16:27;Mk 15:22; Lk 23:33). Kwa ajili ya kiu chake wakampa mchanganyiko wa siki na nyongo (Mt. 27:34; Zab 69:21). Pia wakamsulubisha pamoja na wezi wawili na wakawaweka, mmoja kwa upande wa kulia na mwingine kwa upande wa kushoto (Mst.38, Isa 53:12; Lk 22:37). Wote walijiunga katika kudhihaki Mwana wa Mungu. Miongoni mwa wadhihaki wake walikuwa Askari wa Kirumi, makuhani wanafiki, wapita njia na pia wale wezi wawili waliosulibishwa kando yake (Mst. 36, 39, 41, 44; linganisha Zab 22: 6-8). baada ya kugawana mavazi yake askari wale walikaa chini na kumtizama, kama kundi la mbwa mwitu wakitazama windo lao (Mst.35-36; Zab 22: 16-18). Pilato alindika â Yesu Wa Nazarethi; Mflame wa Wayahuduâ na akaweka juu ya msalaba juu ya mwili wa Yesu aliyekuwa amefifia na akimwaga damu (Yn.19:19-22). Wayahudi walitaka kubadilisha andiko lile kwa kumwambia Pilato kuongeza maneno, âalisema....â lakini Pilato alikataa na kuwafukuza.
Matusi yalishindwa kuleta jibu (linganisha 1 Pet. 2:23; Isa. 53:7). Akili ya Yesu iligeukia matumaini ya kuwabadili wale ambao walimwonyesha chuki; âBaba, uwasamehe kwa maana hawajui watendalo" (Lk 23:34). Alitoa ahadi ya wokovu kwa mwizi aliyekiri; pia alitoa hakikisho na kuondoa wasiwasi kwa mama aliyekuwa na huzuni (Lk. 23:43; Yn. 19: 26-27). Upendo kama huo kwa wengine katika wakati wa aibu na mateso unamwacha mtu akishangazwa na utiifu wa Mwana wa Mungu kwa kweli yeye ni mfano kwetu; "Wale walio wa Kristo wameisulubisha hali yao ya kidunia pamoja na upendo na tamaa" (Gal 5:24). Matendo ya Yesu yalimtukuza Baba yake; Mapenzi ya Mungu yalifanyika na mwili ulionyeshwa kwamba unahusiana na kifo (Yn 12:27, 28; Rum: 3:25-26).
Ingawa ilikuwa mapenzi ya Mungu kwamba yeye afe, alionyesha kutofurahishwa kwake kwa kutuma giza juu ya nchi pamoja na mtetemeko wa ardhi (Mt. 27: 50-54; Lk 23:44).
MAZISHI (Mt. 27:57-66; Yn. 19:38-42)
Kwa mara nyingine Agano la Kale lilidhibitishwa, kwani wawili walio ubeba mwili wa Yesu walikuwa matajiri na viongozi walioheshimiwa (Isa 53: 9). Yosefu wa Arimathaya, mzee mwaminifu na mwanafunzi wa siri wa Yesu, aliomba mwili wa Yesu kutoka kwa Pilato (Mk.15:43; Lk 23:51; Yn 19:38). Alijiunga na Nikodemu, aliyekuwa pia mwanafunzi wa siri wa Bwana, na sasa mwanafunzi wake mwenye ujasiri. Pamoja, na kwa upendo wakaupaka manukato mwili wa Masihi wao, wakauzungushia sada ya kitani, na kuuweka katika kaburi jipya la Yosefu lilichongwa katika Mwamba. Maria Magdalena alibakia katika bustani, akitazama kila kitu kilichofanyika mpaka jiwe kubwa lililofunga mlango wa kaburi lilipowekwa katika nafasi yake(Mst.60-61; Lk 23:55)
MAMBO TUNAYOJIFUNZA:
- Yesu aliomba kwamba Mungu awasamehe maadui zake ambao walimsulubisha. Hivyo tunapaswa kuwapenda wale wanaotuchukia.
- Tukiwa wafuasi wa Kristo sisi pia lazima "tusulubishe mwili na upendo na tamaa zake".
- Kama tutawafurahisha wanadamu hatutakuwa watumishi wa Mungu.
- " Mwili hauna faida yeyote; ni Roho inayotupa uhai".
- Wajibu wetu wa kwanza katika maisha ni kumtukuza Mungu kwani Ametuonyesha neema yake juu yetu kwa kumtoa Mwana wake Mpendwa (Yn. 3:16).
- " Hakuna mtu aliye na upendo kuliko huu, kwamba mtu anatoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake". Upendo wa Kristo kwetu unatulazimisha kutoa huduma kwa upendo na utii.
MAKTABA YA KUREJELEA:
"A Life of Jesus" (M. Purkis)âKitabu 7, Sura 12-14
"The Gospel of John" (J. Carter)âSura 18 na 19
"The Story of the Bible" (H. P. Mansfield)âTol. 12, Kurasa 56-134
MASWALI YA AYA:
- Ni Mashtaka gani yalioletwa dhidi ya Yesu katika kesi yake?
- Jinsi gani Yesu alipewa mazishi ya heshima?
- Kayafa akararua mavazi yake. Je, kitendo hiki kilimaanisha nini?
- "Walipokuwa wakimtukana, yeye hakuwatukana" (1 Pet. 2:23). Jinsi gani kanuni hii inaonekana katika kesi na kusulubiwa kwa Yesu.
- Jinsi gani huduma ya Yesu kwa wengine inaonekana wakati wa kusulubiwa?
MASWALI YA INSHA:
- Tengeneza orodha ya matukio katika majaribu, kifo na mazishi ya Kristo ambayo yalikuwa yametabiriwa katika Agano la Kale.
- Tengeneza muhtasari wa majaribio ambayo Yesu alipitia kabla ya kusubiwa kwake. Ni mafunzo gani tunapata katika majaribio hayo?
- Andika insha fupi juu ya aibu, mateso na upweke wa Yesu wakati alisulubiwa.
- Elezea kesi ya Yesu mbele ya Pilato ukionyesha jinsi Pilato alibadili mawazo yake.
- Orodhesha kesi ya Yesu mbele ya baraza.
- Ni mafunzo gani sisi tunajifunza kutokana na mfano wa Yesu juu ya msalaba?