35. KUSHAMBULIA AI
"Israeli wamefanya dhambi na wamelivunja agano langu"
Shabaha.
Kuonyesha kwamba uasi wa Akani haukufichwa mbele za Mungu. Ni lazima aadhibiwe kabla ya Mungu hajawa pamoja na Israeli tena.
Muhtasari
Waisraeli walikuwa wameona nguvu za Mungu alipoiangamiza Yeriko na akawaruhusu kushinda vita. Maana walimtumainia Yeye, Mungu akawapa ushindi. Huu ni mfano mwingine unoonyesha umuhimu wa kutii maagizo ya Mungu sawasawa. Huu ni mfano unohuzunisha kwa sababu unoharibu furaha yote ya ushindi dhidi ya Yeriko.Yoshua 7na8
SHAMBULIO LA KWANZA DHIDI YA AI JOSHUA 7:2-5
Wakati Israeli walipingia Kanaani wakazi wake walikuwa ni waovu na waabudu sanamu. Mungu akasema ni "lazima waharibiwe kabisa". Wana wa Israeli walitiwa moyo na shambulio lao lililofanikiwa walipouteka Yeriko. Ilionekana kana kwamba mambo yao yangeendelea vizuri kuanzia hapo. Hali wakiwa na matumaini walitazamia kushinda mji uliofuata.
Mji wa Ai ulikuwa km 19 kutoka mji wa Yeriko. Ilikuwa ni muhimu sana kwa nchi ya Ahadi ya Israeli walitumaini sana wautwae urithi wao. Yoshua alituma wapelelezi waichunguze Ai,na taarifa ya wapelelezi walisema kwamba Ai ni mji mdogo. Wakashauri kwamba waisraeli maaskari wasiende wote lakini waende watu "elfu mbili au tatu" (mst 3) .Kwa hiyo watu wa vita walichaguliwa; nao wakaenda kushambulia. Kwa shangao waisraeli walifadhaishwa kwa kupigwa haraka na walifukuzwa na kurudishwa nyuma na jeshi la Ai, hadi kwenye makambi ya wana waisraeli.
Katika vita hivi waisraeli 36 walikufa. Kambi yote walishikwa na "hofu kuu ya ghafla ikawashika na mioyo ya watu ikayetuka ikawa kama maji" (mst5) .
SABABU YA KUSHINDWA JOSHIA 7:6-15
Yoshua akiwa Mkuu wa jeshi la watu wake,Yosha alifadhaika na kuhuzunika. Akamwomba Mungu ili awambie sababu maana vinginevyo wangeshindwa na kuangamizwa na Wakanaani. "Israeli wametenda dhambi" Mungu akasema "Mimi sitakuwa pamoja nanyi tena"(mst 12).Kuna kitu kimechukuliwa kutoka Yeriko na kufichwa katika vyombo vyenu ndani. Na hili lilikuwa limeshakatazwa (mst 11) vitu vyote vilitakiwa kuharibiwa kwa moto au kuwekwa katika hazina ya Mungu.Hili lilikuwa ni tatizo kwa Yoshua.Ilimpasa kumpata aliyetenda dhambi kati ya maelfu ya askari walioshiriki kuteka Yeriko.
Lakini Mungu akamwambia awakusanye Israeli wote ili Mungu amwonyesha mwenye kutenda dhambi.
USHAURI WA KUMPONYA YOSHUA 7:16-26
"Yoshua akaondoka asubuhi na mapema akawasogeza Israeli kabila na kabila" (mst 16) .
Bila shaka Mungu alijua aliyetenda dhambi na kuchukua vitu kutoka Yeriko na kuvificha.Yeye anajua yote tunayoyatenda yawe ya kweli au makosa. Kabila la Yuda likatwaliwa yamkini kwa njia ya kura. Kutoka familia ya Yuda mtu mmoja aliyeitwa Akani alitwaliwa. Ilikuwa ni taabu sana na huzuni kwa Wairaeli wote waliokuwa na majonzi wakisubiri zamu Akani aliposimama mbele ya Yoshua na kukiri mambo aliyoyafanya "kweli nimefanya dhambi mbele za BWANA, Mungu wa Israeli" (mst 20). "Wakati nilipoona katika nyara joho nzuri ya Baberi na shekeli mia mbili za fedha na kabari ya dhahabu uzani wake shekeli hamsini basi NALIVITAMANI,,nikavitwaa;tazama vimefichwa machangani,katikati ya hema yangu na ile fedha chini yake (21mst).
Akani alikuwa amejitwalia mali ya Mungu iwe yake. Kwa uasi huu yeye na wote waliomsaidia waliuwawa kwa mawe, chungu kubwa la Mawe ikakusanywa juu ya waliokufa na mahali hapo paliitwa "Bonde la Akori" maana yake "taabisha".
FUNDISHO KWETU
Ilikuwa ni vigumu kwa Israeli kujifunza ya kwamba Mungu alikuwa ana maana kwa kila neno alilosema. Akani alitakiwa kufahamu hili na kumpatia Mungu utukufu; kwa kutii neno lake. Jina Akani maana yake taabisha na tunaona jinsi dhambi ya mtu mmoja ilivyosababisha Israeli wote wakataabika sana.
Akani alivunja amri ya kumi "Usitamain" Akani alitenda dhambi ile na aliiba kitu kile alichotamani ;kwa hiyo akawa amevunja amri ya nane "Usiibe", dhambi moja hukuongonza kutenda nyingine na Akani aliiba vitu ambavyo ni mali ya Mungu(Yos 7:11).
Yesu anatuambia kuhusu amri mbili ambazo tukizitii tutaweza kumpendeza Mungu. Zisome katika Math 22:37-39 "Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote na kwa akili yako yote. Hii ni amri iliyo kuu tena ni ya kwanza. Na ya pii ya fanana na hiyo Umpende jirani yako kama nafsi yako".
UKUMBUSHO WA NYONGEZA KUTWALIWA KWA AI: Yoshua 8
Baada ya dhambi ya Akani kuondolewa Mungu akamwambia Yoshua,"Usiogope ...Mimi nimemtia mikononi mwako huyo mfalme wa Ai ,nawatu wake na nchi yake "(mst1). Shauri moja rahisi la kushambulia liliweza kuwapatia ushindi ulio kamili.
Yoshua aliwatoa watu wa vita 5000 usiku wakajificha nyuma ya mlima upande wa Magharibi kati ya Betheli na Ai. Mapema asubuhi waliongoza watu wa vita wapigane maaskari 25,000 ya Ai upande wa kaskazini ndipo wa Ai wakatoka ili kupigana ,na Israeli wakafanya kana kwamba wameshindwa wakawakimbia nao adui wakawafuatia kama walivyofanya mwanzo.
Watu wa Betheli wakawafuatia wakiungana na wale wa Ai hakusalia mtu yeyote ndani ya Ai au Betheli asiyewafuatia Israeli waliacha mji wazi bila walinzi. Mungu akamwambia Yoshua "unyoshe mkuki ulionao mkononi kuelekea upande wa Ai" (mst 18) hii ilikuwa ni ishara ya watu 5000 wajitokeze. Waliukimbilia mji ulioachwa wazi bila walinzi na kuutia moto.
Ndipo watu wa Ai walipouona moshi wakaanza kukimbia kurudi kwao mjini wakiacha kuwafuatia Israeli, wakakimbia wakirudi mjini kwao hao waliokuwa wakiwafuatia kukutana na wale maaskari waliokuwa wamejificha.
Jeshi lote la Yoshua wakawageukia na hivyo wakawa wameingia katikati ya mtego wa makundi mawili ya waisraeli.
Yoshua alisimama kwenye kilele cha kilima hali mkuki wake akiwa ameuonysha kama alivyokuwa amefanya mwanzo.
Israeli wakaendelea kushinda vita kwa hiyo hata mji wa pili ukaangamizwa. Israeli waliambiwa wawaangamize watu wote wa Ai, isipokuwa mifugo na mali zote waliruhusiwa wachukue kuwa mali zao.
Kwa hiyo mji ukateketezwa kabisa kwa moto. Baadaye Yoshua alijenga madhabahu katika mlima Ebali akamtolea BWANA dhabihu hapo.
Kisha Yoshua akakutanisha Israeli wote, nusu ya makabila yote aliwaweke katika mlima Gerizimu na nusu iliyobakia aliwaweka katika mlima Ebali ;alisoma maneno yote ya baraka na laana ilivyoandikwa katika kitabu cha Torati kama Musa alivyoagiza kabla ya kufariki (Yoshua 8:35, Kum 27:1-3).
MASWALI MAJIBU MAFUPI
1. Baada ya Yeriko kuangamizwa ni mji upi uliofuatiwa kushindwa
2. Ai ilikuwa sehemu gani?
3. Ni waisraeli wangapi waliokwenda kupigana na Ai.
4. Ni jambo gani liliwatokea Israeli walipokwenda kupigana kwa mara ya kwanza na Ai?
5. Ni kwanini waisraeli walishindwa katika vita na Ai?
6. Ni njia ipi Yoshua alitumia kumpata mtu aliyetenda dhambi?
7. Je Akani aliadhibiwaje gani?
8. Ni amri ipi Akani aliivunja?
MAJIBU YA KINA
1. Israeli waliposhambulia Ai kwa mara ya kwanza walishindwa
a. Ni kwanini walishindwa?
b. Yoshua alifadhaika sana. Alifanya nini?
c. Yoshua alitumia njia gani kumpata mwenye dhambi?
2. a. Eleza dhambi ya Akani ilikuwa ipi?
b. Aliadhibiwa namna gani?
c. Ni fundisho gani tunalipata kutokana na tamaa ya Akani?
MAJIBU YA NYONGEZA.
3. Ni jinsi gani Akani alivunja amri Mungu.
4. Eleza ni jinsi gani Waisraeli walivyowashinda watu wa Ai mwishowe.
