Utukufu unamwendea Mungu
Mhubiri ni sehemu ya mchakato ambao Mungu anadhibiti. Mungu ndiye anayewaita watu kwenye imani (1 Wakorintho 1:26). Mhubiri ni mtu ambaye Mungu anamtumia. Mhubiri lazima akumbuke kwamba ni Mungu anayetawala.
Mwitikio wa injili unafananishwa na kukua kwa mbegu, ambapo mbegu ni neno la Mungu. Paulo alituambia hivi, “Basi Apolo ni nani? Na Paulo ni nani? Ni wahudumu ambao kwao mliamini; na kila mtu kama Bwana alivyompa. Mimi nilipanda, Apolo akatia maji; bali mwenye kukuza ni Mungu. Hivyo, apandaye si kitu, wala atiaye maji, bali Mungu akuzaye. Basi yeye apandaye, na yeye atiaye maji ni wamoja, lakini kila mtu atapata thawabu yake mwenyewe sawasawa na taabu yake mwenyewe. Maana sisi tu wafanya kazi pamoja na Mungu; ninyi ni shamba la Mungu, ni jengo la Mungu.” (1 Wakorintho 3:5-9).
Ikiwa kuna mafanikio kutoka kwa kazi yako, ni mafanikio ya Mungu. Utukufu unamwendea. Tuna pendeleo la kuwa sehemu ya kazi ya Mungu. Tumebarikiwa kwa sababu Mungu ameturuhusu kufanya kazi yake na kuona kazi hiyo ikibarikiwa.