22 - 13. Kurudi Kwa Yesus

Swahili

13. Kurudi Kwa Yesu

Yesu sasa yuko mbinguni lakini atarudi duniani (Matendo 1:10,11; 3:20-21; Yohana 14:2,3). Atakapokuja, atawatuza waumini kulingana na maisha waliyoishi (Mathayo 16:27, Ufunuo 22:12). Jambo la kwanza atakalofanya ni kuwafufua wafu na kuwahukumu (1 Wathesalonike 4:16; 2 Timotheo 4:1).

Ufufuo

Waumini waliokwisha kufa watafufuliwa kutoka kwa wafu. Hakuwezi kuwa na maisha baada ya kifo isipokuwa wafufuliwe. Ufufuo unafundishwa katika sehemu nyingi (Yohana 5:24-29; Yohana 11:25-26; 1 Wakorintho 15; Matendo 24:15; Warumi 6:5; Wafilipi 3:10,11).

Masadukayo hawakuamini ufufuo na walisahihishwa na Yesu.(Mathayo 22:23-32). Wakorintho wengine hawakuamini ufufuo na walisahihishwa na Paulo (1 Wakorintho 15:12-23). Baadhi ya Wathesalonike na wengine walifikiri kwamba ufufuo umekwisha na walisahihishwa na Paulo (1 Wathesalonike 4:13-16; 2 Timotheo 2:16-18). Watu bado wamechanganyikiwa leo.

Si kila mtu aliyewahi kuishi atafufuliwa (Warumi 2:12; Danieli 12:2; Isaya 26:13,14, Yeremia 51:57). Wale wasio na imani hawawezi kumpendeza Mungu (Waebrania 11:5) hivyo wale ambao hawakuwa na imani kamwe hawatafufuliwa.

Waamini waliofufuliwa watakusanywa mahali pa hukumu (1 Wathesalonike 4:16,17; Luka 17:30,36). Hii inaelezea usafiri wa anga kwa njia ambayo Filipo, Eliya, na wanafunzi walisafirishwa (Matendo 8:39-40; 1 Wafalme 18:12; Yoh 6:21).

Hukumu

Waumini watahukumiwa kulingana na maisha yao ( Zaburi 62:12; Mhubiri 12:14; Yeremia 17:10; Mathayo 16:27; Warumi 14:10-12; 2 Wakorintho 5:10; 2 Timotheo 4:1; Ufunuo 22 :12). Mifano mingi inafundisha hivyo - ngano na magugu ( Mathayo 13:24-30, 36-43 ), samaki katika wavu (Mathayo 13:47-50), kondoo na mbuzi (Mathayo 25:31-46).

Mwili na damu haviwezi kuingia katika ufalme wa Mungu (1 Wakorintho 15:50; Wafilipi 3:21). Wale walio na haki watapata heshima na uzima wa milele (Warumi 2:7; Mathayo 25:21,34). Wale ambao ni waovu watapata aibu na kifo (Danieli 12:2; Mathayo 8:11,12; Warumi 2:5-11).

Ufalme

Waamini wakishahukumiwa, wenye haki wataingia katika ufalme wa Mungu.

Yesu atatawala kutoka Yerusalemu (Luka 1:32; Yeremia 3:17). Wenye haki watapewa vyeo vya kutawala juu ya ufalme wa Mungu (Danieli 7:27; Ufunuo 5:10).

Bado kuna watu wanaokufa wamebaki duniani wakati huu (Isaya 65:17-20). Kipindi hiki kinachukua miaka 1000 na kinaitwa 'Milenia' (Ufunuo 20:1-6). Ni mwisho tu wa kipindi hiki ambapo kifo kitaharibiwa, na Yesu atakabidhi utawala wa ufalme kwa Mungu ( 1 Wakorintho 15:22-28; Ufunuo 20:14; 21:4 ).

Swahili Title
13. Kurudi Kwa Yesu
African text
John Mathias
Translator 1
Carl Hinton
Literature type