252: UUMBAJI WA MBIGU NA DUNIA
“kwa hivyo mbigu na dunia zikakamilika”
Dunia iliumbwa mwanzoni (Mwanzo 1:1;. Ebr 1:10) wakati usiojulikana na kabla kazi ya ubunifu kuanza kwa siku sita. “Nchi ilikua bila umbo na tupu” (Mwa 1:02) ilikua tupu na imefunikwa na giza, maji na kukosa uhai. Ilikua mpango wa Mungu kuwapa wanadamu nchi ili onyeshe sifa na utukufu wake katika maisha yao (Hesabu 14:21) hii ilitayarisha dunia kwa ajili yamakao ya binadamu. Lengo la somo ni kuonyesha uwezo na hekima ya Mungu kutokana na matendo yake ya ubunifu kuanzia mwanzo.
Mwanzo 1; 2:1-3 KAZI YA MALAIKA (Mwanzo 1:1-2)
Mungu kupitia kwa malaika alifanya dunia kujaa uhai na kupitia kazi yake inayoelezewa katika Mwanzo 1, neno la Kihebrania ni “Elohim” ambalo linamaanisha Malaika mjumbe wa Mungu (angalia Zaburi 08:05 ambapo "Elohim" limetafsiriwa "malaika” Malaika kufanya amri ya Mungu (Zab. 103:20-21). Mungu alizungumza na Malaika wakafanya mapenzi yake (Zab. 33:6-9). Yote ilifanywa kulingana na mpango wa Mungu. Kwa hivyo anaitwa muumbaji (Mithali 3:19-20; Isa 40:28;. Matendo 17:24) na walipomaliza kazi maliaka walifurahia (Ayubu 38:4-7).
Kazi ya uumbajo ya wiki moja ilianza miaka 6,000 iliyopita wakati roho na nguvu za mungu zilikua zinatembea juu ya maji.
Siku ya kwanza: Mungu alifanya Mwanga kuangaza nchini na kufukuza giza. Siku ya kwanza kama siku zilizofuata kazi ya ubinufu ilielezwa kama usiku na asubuhi. Mf. Kipindi cha masaa isihirini na nne.
SIKU YA PILI (Mwanzo 1:6-8) Mungu aliumba anga (v.6), hewa Mwanzo 1:26 Mungu akaiita Mbigu (v.8) kisha akagawanya maji yalio juu yakawa Mawingu na ya chini yakawa Bahari.
SIKU YA TATU: (Mwanzo 1:9-13): nchi kavu iliibuka kutoka kwa maji yaliyokuwa yamefunika nchi. Kwa amri ya mungu ardhi ilimea nyasi miti na mimea zikiwa na nguvu za kuzaana.
SIKU YA NNE (Mwanzo 1:14-19): Jua, mwezi na nyota ziliwekwa katika mbingu kutoa mwanga juu ya nchi. Nyakati na majira zilipagwa kulingana na uhusiano wa dunia kwa vyombo vya mbinguni.
SIKU YA TANO (Mwanzo 1:20-23): bahari zilijaa na wanyama wa majini na anga ilijaa ndege.
SIKU YA SITA: (Mwanzo 1:24-31;, 2:07 21-22): Ng'ombe, wanyama watambaao na wanyama waliumbwa kutumia udongo (2:19). Mwanadamu aliumbwa katika sura na mfano wa Mungu, yaani "Elohim" au malaika (1:26 "Na tuumbe binadamu kwa mfano wetu, kwa sura yetu"). "Mwanaume na mwanamke wakaumbwa na Yeye" (v.27). Adamu akawapa majina wanyama na ndege, na akapewa mamlaka juu ya kila kitu kilicho hai.
SIKU YA SABA (Mwanzo 2:1-3): Mungu alikamilisha kazi yake ya ubunifu kwa siku sita na siku ya saba alipumzika "kutoka kazi yote aliyoifanya." Neno ya Kiebrania linatafsiri "akapumzika" ni "Shabath" ambapo neno "Sabato" lilitokea. Siku hii ni tofauti na zingine, kwani ni "imetakaswa" na kutengwa na Mungu (v.3). Tunaambiwa kwamba Mungu "alibariki" siku hii. Ilibarikiwa ili iwe siku mwanadamu atapumzika kutoka na na shughuli za kimiwli na kuelekeza mawazo yake kwa matendo ya Mungu, na pia ilibarikiwa kuonyesha umuhimu wake wa kinabii kuonyesha “Pumziko” ambalo litakuja katika Kristo (Mathayo 11: 29-30), na utukufu wa utawala wake wa milenia duniani (Ebr. 4:3-5, 9-11).
VISIOAMBATANA: UUMBAJI NA MAGEUZI
Kujaribu kupatanisha mageuzi na uumbaji ni kuzuia ukweli ulio wazi katika Biblia. Mageuzi yanakanusha kuwepo kwa Muumba. inadai kwamba mtu aligeuka ndani ya mamilioni ya miaka kutoka kwa aina duni ya maisha (kumbuka Zab. 100:3). Biblia inaonyesha kwamba mtu iliumbwa kutoka kwa vumbi ya ardhi. Mageuzi ni mafundisho ya ubinafsi. Uumbaji ni kazi ya Mungu. Viumbe na Mageuzi, ni mawazo tu.
Nadharia ambayo inayokataana na Muumba anamwondolea mwanadamu wajibu wake kwake. Vizuizi vyote vimeondolewa kutoka kwa dhamiri ya binadamu. Ni ajabu kwamba tunaishi katika dunia iliozama katika uasherati na maovu mengine. Dunia na hekima yote ni upumbavu mtupu mbele ya Mungu (1 Kor 1:20-28.)
TIINI ONYO LA PAULO
Mungu ana maarifa mengi yanayo pita hata wale wanaoitwa wenye 'busara' katika karne ya ishirini. Mungu alijua kuwa siku itakuja wakati binadamu atapuuza ufunuo(Warumi 1:19-20), na kutaka kumtoa kwenye kiti cha enzi. Alitabiri kuwa hii itasababisha kuvunjika kwa jamii na binadamu kujiharibu mwenyewe katika uhuru aliopewa (Warumi. 1:21-31). Lakini binadamu bado hajaelewa chanzo cha matatizo yake – ni kumkataa Mungu (Warumi 1:18, 32) Kwa sababu inamfaa kuendelea kujihusisha na mambo ya kimwili na anaendelea kuwaelimisha vijana na mambo ya nadharia amabayo hayawezekani.
Hekima ya kweli hutoka kwa Mungu na inahusiana na Mwana wake na kusudi lake tukufu Kwake (1Wakor. 1:18-31.). Elimu ya binadamu ambayo inayopinga haya ni upumbavu. Paulo alikumbana falsafa ya binadamu akiwa Korintho na akaandika, "Mtu asijidanganye. Mtu yeyote miongoni mwenu anayedhani ni mwenye hekima humu duniani, ni heri awe mjinga kusudi apate hekima. Maana, hekima ya kidunia ni upumbavu kwa Mungu Kwa maana imeandikwa, Amewanasa wenye hekima katika ujanja wao na tena, Bwana anajua mawazo ya wenye hekima ni ya bure, kwa hivyo mtu asijivunie watu "(1 Wakor 3:18.... - 21).
Basi tutii onyo la Paulo kwa Timotheo: "lindeni yale ambayo niya uaminifu, epukeni maneno ya bure na mambo ya kidunia na upinzani wa sayansi kwani ni ya uongo(1 Tim 6:20-21.).
Mwanzo ni wa Kweli
Majaribio ya kuuganisha uumbaji na mageuzi huzua swali, "Je, kumbukumbu za Mwanzo (Sura ya 1 hadi 3) ni za kweli? Je zinamaanisha vile zilivyoandikwa, ama ni mfano tu ambao unahitaji kutafsiriwa.
Kusoma kitabu cha Mwanzo wa Uumbaji kina maelezo yote isipokua yale maelezo yake halisi. Hii ni jinsi Mungu aliyvokusudia. Yesu Kristo aliamini katika Uumbaji na alitumia maelezo haya katika kusoma, inathibitisha kesi ya Uumbaji. Anaashiria Adamu na Hawa (Mk. 10:6-8), na Uumbaji (Mk. 13:19).
Mtume Paulo pia alikubali Uumbaji bila swali. Alitoa mfano wa Adam na Hawa (Warum. 5:12;. 1 Wakor 15:21-22), nyoka (2 Wakor 11:03.)Nk
Kuna baadhi wanaokadiria kuwa siku za uumbaji zilikua kipindi cha miaka 1,000 iliyopita au zaidi. Pendekezo hili huwacha nafasi kwa mawazo ya uongo. Yaani Mungu alianzisha maisha na mageuzi na kuyakamilisha. Biblia hata hivyo, haituwachi na shaka yoyote na misingi inayofuata inaeleweka. Kuna njia asili kisha maombi ya kiroho au ya kitamathali yanayofuata (1 Wakor 15:46.). kama ilivyo katika Mwanzo. Bila shaka, takwimu na mifano imetokana na rekodi halisi za kitabu cha Mwanzo, lakini hii ni recordi halisi sio kinyume.
Siku za Mwanzo 1 zimetajwa kama jioni na asubuhi na zilikua za kwanza au pili (Mwanzo 1:5, 8, 13, 19, 23, 31). Musa alielewa hizi kuwa siku za kawaida(Kutoka 31:17). Nguvu za Mungu zilitosha kukamilisha kazi ya ubunifu kwa siku sita kila moja ikiwa na masaa 24. Ni mimea gani ingeweza kuvumilia giza kwa miaka 500. Na ni vipi Adamu aliweza kuishi miaka 930 (Mwanzo 5:05) ukitumia wakati sawa na siku 1000, ni kumaanisha kitabu cha Mwanzo 1 hadi 3 kimejaa matukio halisi.
FUNDISHO YA SABATO
Siku ya saba, wakati Mungu alipumzika anazungumzia milenia ya saba katika historia ya dunia wakati ufalme wa Mungu utakapo fika huku duniani (Ebr 4:1-11). Huu ni Umpumziko ambao Mungu alituahidi - pumziko kutoka kutumikia dhambi, na wakati wa elimu katika njia za Mungu (Isaya 2:2-4).
Chini ya sheria ya Musa, Israeli iliamuriwa kutii Sabato (Kut. 30:10-11;. 9:13-14 Neh). Ilikuwa iwe siku ambayo wanapaswa kusitisha kazi zao na kufanya mapenzi ya Mungu (Isa 58:13-14). Hii ni roho ya kweli ya Sabato inayopaswa kufuatwa leo. Hata kama wafuasi wa Kristo hawatakiwi kufuata kwa kina siku ya sabato kulingana na sheria za Musa (Warum. 14:5-6; Kol 2:16-17;. 4:10-11 Gal), ni lazima waache kutumikia dhambi na badala yake kujitolea kufuata njia za Mungu. Hii si kazi ya siku moja kwa wiki bali inahitaji uwepo wete siku saba kwa wiki.
MASOMO KWETU
• Mageuzi na Uumbaji hayawezi kuwiianiishwa, kwa sababu mageuzi ni kinyume na neno la Mungu.
• Kwa kukubali nadharia ya mageuzi, Binadamu amekataa ukweli wa Mungu na sasa anajitumikia mwenyewe badala ya kumtumikia mungu.
• kusoma matukio asili ya Uumbaji katika kitabu cha Mwanzo husababisha mtu kukubali maelezo yake halisi.
•Yesu na Paulo waliamini katika Uumbaji na kufundisha ipasavyo.
MAKTABA YA KUREJELEA:
"The Visible Hand of God" (R. Roberts) — Sehemu 2
"Elpis Israel" (J. Thomas) — Sehemu ya kwanza, sura 2
"Christadelphian Instructor" (R. Roberts) — Nos. 24-29
"Evolution, Science and the Bible" (H. W. Hathaway)
"The Finger of God: Evolution or Creation?" (D. A. B. Owen)
"Wrested Scriptures" (R. Abel) — Section C
"First Principles Bible Marking Course" (C.S.S.S.) — Kurasa 12-15
MASWALI YA AYA:
1. Jinsi gani tunajua kwamba Paulo na Yesu walikubaliana na kitabu cha Mwanzo kuhusu Uumbaji halisi?
2. Jinsi gani tunajua kwamba malaika, kwa niaba ya Mungu, walijumlishwa katika wiki ya uumbaji wa dunia?
3. Kwa njia gani waumini wanapaswa kutimiza kanuni za Sabato katika maisha yao?
4. Kwa nini binadamu wanapendelea kuamini katika Mageuzi na kukataa kuamini Biblia kuhusu uumbaji.
MASWALI YA INSHA
1. Toa sababu za kukataa nadharia ya Mageuzi.
2. Onyesha kutoka maandiko sababu zako za kuamini kwamba sura za Mwanzo ni halisi.
3. Mungu akaibariki siku ya saba, akaitakasa kwa sababu katika siku hiyo Mungu alipumzika na kuacha kufanya kazi ya uumbaji (Mwa 2:03). Toa maoni kuhusuu umuhimu wa maneno haya.
UKWELI UNAO-ONYESHA NADHARIA YA MAGEUZI SI YA KWELI
1. TOFOUTI KATI YA VIUMBE
Kitabu cha Mwanzo Sura ya 1 kinaogeleea kuhusu aina mbalimbali ya viumbe, kwa mfano, "Kila ndege arukaye na aina yake" (v.21) na kila mnyama wa ardhi aina yake (v.24). Biolojia inathibitisha tofauti kubwa kati ya aina mbalimbali ya viumbe vilivyo hai. Kuzaana kati ya viumbe tofauti hakukutokea kamwe laking hutokea kudhibitiwa na binadamu. Mahuluti ndio huzaliwa bila uwezo wa kuzaa na hii ndio pigamizi inayotokea katika viumbekwa kuunganisha aina ya viumbe tofauti.
Taswira hii sio ile mageuzi ingetabiri kama kweli mageuzi yanafanyika, basi kunapaswa kuwa na ushahidi katik mageuzi kutokana kwa aina moja na nyingine. Lakini tofauti kubwa zaidi ambazo wanamageuzi hawakutarajia. Hata pale ambapo uteuzi wa makusudi unafanywa na binadamu hakuna aina mpya ya kiumbe kinachozaliwa. Wafugaji wa Mbwa wanaweza kuzalisha mbwa pekee, wapanzi wa waridi wanaweza zalisha waridi tu. Hata matunda yanaoyopitia vizazi kadhaa kwa mwaka, hawajawahi zalisha matunda tofouti.
Tofauti kubwa kati ya mtu na nyani ni ya kuaimbisha wanamageuzi. Kama binadamu nyani aliye uchi ni vipi yeye alipata ubongo ambao ijapo mkubwa kidogo una uwezo mara milioni zaidi kuliko ule wa nyani? Nini ilifanya mwanadamu awe uwezo wa kufikiri sana, iliweza kuwa mtaalamu wa hisabati, mwanafalsafa, mwanafizikia na mshairi? Mbona ni yeye pekee ana sauti inayomwezesha kuwasilisha mawazo yake, kupitisha elimu yake kutoka kizazi kimoja hadi kingine? Jinsi gani aliwezesha mikono yake ambayo inayomwezesha kutumia ubongo wake? Nini ilimpa binadamu hali yake ya ucheshi, uwezo wake kisanii, muziki, kutambua uzuri na uwezo wake wa kufahamu masuala ya maadili?
Mageuzi yanabaki bila majibu, lakini Biblia inaonyesha wazi kwamba: "Mungu aliumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba Binadamu" (Mwanzo 1:27).
2. KUKOSA USHAHIDI WA VIFUSI
Darwin na washirikarika wake walikuwa na matumaini makubwa kwamba utafiti wa kijiolojia utaonyesha vifusi ambavyo vitaonyesha mabadiliko kati ya viumbe. Baada ya miaka zaidi ya mia moja ya utafiti huo na ugunduzi wa mamilioni ya vifusi, bado kuna tofoauti kati ya viumbe. Aidha tofauti katika rekodi ya vifusi inafanana na tofauti katika dunia tunayoishi leo. Hakuna kitu kinaweza jaza pengo ou tofauti kati ya: samaki na amphibia, amphibia na nyoka, wanyama watambaao, ndege na mamalia.
Wanamageuzi wamejaribu bila mafanikio kutafuta ushahidi ili kuonyesha mageuzi ya mwanadamu, lakini vifusi vya kwanza kupatikana ni vya wanaume amabo walisimama na kutembea imara na ubongo wao ukiwa mkubwa kama ule ya mtu wa kisasa wa Ulaya. Madai ya vifusi kabla ya binadamu yamekuwa msingi wa ushahidi unaowaletea wanamageuzi jina baya.
Kama binadamu alitoka ktika viumbe duni, basi kunapaswa kua na maelfu ya hominoids amabo ni binadamu wa zamani waliohifadhiwa. Huxley, mwanamageuzi maarufu, alisema kua mageuzi yatasimama au kuanguka kutokana na rekodi ya vifusi. Hakukosea mageuzi yalianguka.
3. UTATA WA ASILI
Nadharia ya mageuzi inaamini kwamba mabadiliko yaliitokea hatua kwa hatua miaka ming iliyopita.
Jicho na vipengele vyake vyote haliwezi kuona kama haijakomaa kikamilifu. Sikio haliwezi kusikia kama vipengee vyake havipo na vinafanya kazi ipasavyo. Jinsi gani wanamageuzi wanaweza kueleza jinsi viungo kupitia mabadiliko ya polepole?
Ndege huruka kwa sababu : (1) manyoya yake (2) mwili mwepesi, (3) nguvu za misuli ya mabawa. Je, ni nini ilisababisha yote haya kutendeka kwa wakati mmoja, ikichukuliwa kua maendeleo kamili ya haya yote matatu yalitakiwa kuwepo kabla ndege angeweza kuruka, Aidha,hii haikuwa kibahati kwamba haya yote yalitendeka kwa pamoja, na sio mara tatu, ili kuweza kuruka lazima wangegeuka tofauti kwa wanyama tofauti kama ndege, popo na wadudu?
Kiungo cha sumu cha nyoka kinahitaji: (1) mtambo wa kemikali wa kutengeneza sumu, (2) mahali pa kuhifadhi sumu, (3) jisi ya kutoa sumu(4) ujuzi wa meno kama silaha (5) ulinzi ili kuhakikisha kwamba nyoka hajidugi sumu mwenyewe. Ni vipi viungo hivi viligeuka kwa hatua?
Mazingira yamejaa na hali ya kutatanisha ambazo ni ngumu kuelezea kutumia mageuzi.Jibu la kweli ni: "Ee Bwana, jinsi yalivyo, matendo yako yalivyo ya hekima na uliyafanya yote kua (Zaburi 104:24).
4. MATATIZO YA MAISHA YA ASILI
Maisha yalidhaniwa kubadilika kuanzia chembechembe halisi'. Lakini hata maisha hayo rahisi ni mbali na rahisi. Virusi ndivyo viumbe vinavyo ishi maisha rahisi ambavyo kwa kawaida ni molekuli moja kubwa iliyozungukwa na molekuli za protini.je virusi vilibadilika? Kwanza nucleic asidi ni kemikali imeunganishwa na mamia ya maelfu ya atomi ambazo zimepangwa kwa njia ya utaratibu sahihi kabisa. Pili protini ni molekuli kubwa na zenya utata. Tatu asidi nucleic haiwezi kustawi na kuongezeka bila molekuli yake protini. Nne, na la kutatanisa, virusi ni vimelea na vinaeza kuzaana na kuongeeza ndani ya mwili ya mtu ama mnyama ambapo vinaizi maisha mlefu kuliko mtu ama mnyama mwenyewe.Mageuzi yanahitaji kwanza nafasi ya uzalishaji ya kiumbe kama vile bakteria na hili kufanyika ni vigumu sana.
5. UTARATIBU WA MAGEUZI
Kwanza mageuzi yalidhaniwa kuwa yalitokea na mabadiliko ya kutafuta tabia, matumizi, mazingira, mabadiliko katika mazingira yanapitishwa kwa watoto wetu. Lakini baada ya miaka ya utafiti bila kupata mazao, nadharia hii imetupiliwa mbali.
Kisha kukaja 'neo-Darwinism' ambayo alielezea mabadiliko juu ya msingi wa mabadiliko kwa pamoja, pamoja na maisha ya waliyoafiki. Mabadiliko ya kimsingi yaliyopitishwa kwa vizazi kutoka kutoka kwa chembe zilizoharibika. Lakini mabadiliko ni zaidi ya matukio na idadi kubwa ya mabadiliko ni hatari. Mabadiliko ya kisayansi katika matunda husababisha mbawa ngwea, mbawa fupi, mbawa zilizojikunja amabzo haziwezi kupaa. Mabadiliko haya huleta machafuko na ulemavu kwa wanyama walion na maubile mazuri.
Ukosefu wa utaratibu wa mageuzi imesababisha watalamu kudhania kwamba mageuzi yalitokea katika hatua - kwa mfano unyoa ulitokea ghafla juu ya watoto wa reptilia. Binadamu atafanya chochote, ila kurejesha heshima kwa yule aliye muumba.