CSSA 3-2-279 - THE DEATH OF MOSES

Swahili

                                                       279. KIFO CHA MUSA
                                   "Jicho lake halikuwa na kiza ​ wala nguvu zake hazikupunguka"



Pale Kadeshi, Mungu alimwamuru Musa kuliamuru jiwe kutoa maji. Musa alikataa kumtii Mungu na badala yake aligonga jiwe kwa hivyo hakuruhusiwa kuingia katika nchi ya Ahadi.

"Kwa maana yule anayepewa mengi, mengi yanatakiwa kutoka kwake. (Luk. 12:48). Umuhimu wa mawazo yetu na umakini wa neno la Mungu unatiliwa mkazo katika tukio hili kwa maisha ya Musa aliyekuwa Mteule wa Mungu.
Tukio hili, pamoja na kifo cha Haruni na Miriamu, pia linaonyesha kwamba Sheria haiwezi kumpa mtu uhai ila ni kwa njia ya Yesu (Yoshua) ndipo njia ya kuingia katika Nchi ya Ahadi itapatikana.

Lengo la somo hili ni kuoyesha jinsi Mungu anawajali watu wake katika jangwa na inaashiria kazi ya Bwana Yesu Kristo.


Hes. 20 , 21:4-9; Kum.34

 

MUSA AADHIBIWA (Hes. 20:1-13 ).
Kwa miaka 38 WaIsrael walitanga tanga  jangwani kati ya Kadeshi na Elathi . Na wakati wa kutangatanga ulipofika mwisho, walielekea kaskazini mwa Kadesh . Kule Miriamu akafa ( Hes. 20:01 ). Watu walimlalamikia Musa kwa kukosa maji.  Musa aliambiwa achukue fimbo ya Haruni aende “ANENE” na mwamba. Badala yake aliupiga ule mwamba na akasema, "Lazima tupate maji kutoka kwako? " (Zab. 106:32-33 ). Hivyo basi hakuasi tu, lakini alitoa matamshi mabaya kinywani mwake.

Paulo anasema kwamba mwamba uliwakilisha Kristo (1 Kor . 10:04 ). Mapema, kule Refidimu, Musa alikuwa ameambiwa kugonga mwamba ili kutoa maji ya uzima (Kut. 17:5-6 ). Kupiga mwamba kwa mara ya pili  kule Kadesh hakukuwa na maana kwani Yesu alisulibiwa mara moja tu , wakati  nguvu za nyoka zilimjeruhi, sasa lililokuwa muhimu ni  " kuzungumza na mwamba" .

Mungu alimwadhibu Musa kwa vitendo vyake. Alimwambia kwamba hataingia  Nchi ya Ahadi. Katika kufanya hivyo, Mungu alisisitiza kwa watu umuhimu wa utii. Kama mtu kama Musa, mwaminifu na mwenye bidii aliadhibiwa na sisi je?

Somo hili ni muhimu kwetu. Neno la Mungu linatutaka sisi kutii amri zake kama tuna matumaini ya kuingia katika Ufalme wake. Na kama vile iliwabidi wana wa Israeli  kumchagua kiongozi mpya (Yoshua) kuwapeleka katika Nchi ya Ahadi, hivyo vivyo hivyo sisi tunamfuata Yesu ( sawa na ' Yoshua ' ) kutupeleka ndani ya ufalme wa Mungu.

 

KIFO CHA HARUNI (Hes. 20:14-29).
Kufuatia tukio hilo kule Kadeshi, wana wa Israeli walinyimwa ruhusa ya kupitia Edomu (mst. 14-21). Kwa hiyo walisafiri kusini kuelekea Ghuba ya Elathi.
Hii iliwapeleka kupita Mlima Hori (mst.22), uliokuwa umeinuka na unatizamia nyika kali  walioweza kuiona. Hapa Haruni naye akafa. Mavazi yake ya kikuhani yalipewa Eleazari mwanawe, wakipanda Mlima Hori, ambapo angeweza kwa mara ya mwisho kutizama nyika ambayo WaIsraeli walikuwa wakitangatanga kwa muda mrefu, kisha akafariki.

 

NYOKA WA HASIRA JAGWANI (Hes. 21:4-9 ).
Safari ilikuwa ya kukatisha tamaa, na waIsraeli  walidhani kwamba wangeangamia jagwani kama mababa zao,  kwani Mfalme wa Edomu alikuwa amewakataza njia ya kupita.  Walikuwa wamekata tamaa kabisa kiasi cha kwamba waliona huu ndio mwisho wao na pia wakiwa wamechoshwa na chakula kimoja kila siku: Manna. Je wangeendelea kukosa imani kama kizazi kilichopita?


 Mungu akawaadhibu kwa kumtuma nyoka aliwauma na wengi walikufa, (Mst. 6) . Watu waliona jambo hili  kama adhabu kutoka kwa Mungu - kwamba kifo kililetwa dhambi. (" Uchungu wa mauti ni dhambi" , 1 Kor. 15:56). " Tumetenda dhambi ", walitangaza na wakamshawishi Musa kuwaombea msaada kwa Mungu ( mst.7 ).
Musa akafanya hivyo . Akaambiwa na  Mungu amtengeneze nyoka kisha amtundike juu ya mlingoti wote watakao mtizama nyoka wa shaba aliyetundikwa juu ya mlingoti  wangepona. Lakini walipaswa kutizama kwa imani  na kuamini kwamba wangeokolewa. Wale ambao wangemtizama nyoka bila imani wangekufa kwa ukosefu wao wa imani.


Miaka mingi baadaye, Bwana Yesu alifananisha tukio hili kama mfano wa kifo chake ( Yoh. 3:14-15 ). Somo hili ni la ajabu na linaturejesha hadi Shamba la Edeni na Ahadi iliyotolewa kuonyesha sadaka ya Bwana wetu Yesu kristo. (Mwa. 3:15)

 

Jinsi gani mfano huu unafananishwa na  Yesu? Tunaweza kufananisha asili ya binadamu na nyoka. Yesu aliwaita walimu wa Sheria na Wafarisayo, " nyoka " (Mat. 23:33) . Walikuwa kama nyoka wenye sumu iliyo wadhuru wale wote waliowasikiliza. Yesu alikuwa wa asili moja kama wao (Ebr. 2:14), lakini yeye hakutenda dhambikwa hiyo aliwakilishwa na nyoka -  na wale si yule nyoka halisi ambaye alileta kifo , bali yule nyoka ya shaba ambaye alikuwa ametundikwa kwa mlingoti , kama vile yeye alitundikwa msalabani ili wote waone kusulubiwa kwake.

 
Na jinsi  wana wa Israeli walivyotimzama  nyoka wa shaba kwa imani  walipata kuishii , licha ya kuwa walikuwa wameumwa na nyoka halisi,  kwa hivyo basi  sisi ambao " tumeumwa " na asili ya binadamu lazima tumtizame Yesu aliyesulubiwa ili tupate kuishi. Lazima  tu usulubishe mwili na tamaa zake ili tupate kuwa washindi.  (Gal. 5:24).

Kwa hivyo, katika safari ya kuelekea nchi ya ahadi ,WaIsrael walifunzwa  jinsi ya kutumainia  njia za Mungu ili waweze kushinda dhambi na mauti.

 

KUELEKEA NCHI YA AHADI.
Juu ya Ghuba ya Elathi, Israel wakageuka na kuelekea upande wa mashariki, baada ya kufikia mpaka wa Edomu, walisafiri  kaskazini karibu na misitu na malisho upande wa mashariki mwa Yorodani. Jinsi walivyokaribia Nchi ya Ahadi watu wakapatwa na msisimko na furaha. Hii ilionekana kwa mashairi yao ya ushindi na furaha. Jangwa likabaki nyuma, kwa upande wa mashariki mwa Yorodani waliweza kuona uzuri wa ardhi ambayo wangeridhi.
Wafalme wawili wakapinga - Sihoni, aliyekuwa Mwamori, na Ogu mfalme wa Bashani (Hes. 21:23, 33) - lakini hawa waliangamizwa vitani. Mfalme wa Moabu alimwajiri nabii wa Babeli aitwaye, Balaamu, ili awalaani WaIsraeli, lakini laana yake iligeuka na kuwa baraka,  Moabu, pamoja na Balaamu wakaadhibiwa.
Hatimaye WaIsraeli wakafikia  mipaka ya Nchi ya Ahadi na wakajitayarisha kuingia na kuchukua urithi wao.

 

KIFO CHA MUSA (KUM. 34).
Kitabu cha Kumbukumbu kina ujumbe wa mwisho wa Musa, wakati wa mwisho wa maisha yake. Aliwakumbusha WaIsraeli yote yaliyo tokea taifa lao. Alitoa mwito "wazidi kuwa na nguvu na moyo wa ushujaa" (Kum. 31:6), Aliwaambia waendelee kuweka imani yao na imani kwa Mungu ambaye hatawaacha kushindwa. Aliwaonya kuhusu uasi (Kum. 31:29), akawambia kwamba wakati utakuja ambapo wangeweza kuondoka kutoka katika njia za Mungu, na hii itakuwa ni changamoto kwa wale kati yao ambao wangetaka kuendelea katika njia za haki .
Kiongozi mpya, Yoshua, aliteuliwa (Kum. 31:7-8), na akamriwa kuweka imani yake kwa Mungu,na kuwa na "nguvu na moyo wa ushujaa", Yeye ndiye angewaongoza wana wa Israeli hadi Nchi ya Ahadi ". Musa Alimhakikishia Yoshua kwamba Mungu hato muacha.

 

Na sasa wakati ukafika kwa kiongozi mkuu kufa. Nguvu zake kimwili hazikuwa zimeadhirika ( Kum. 34:7) , lakini kazi yake ilikuwa imemalizika. Akaondoka  kambi ya Israeli, akapanda Ml. Nebo,  mbele  akaona  Nchi ya Ahadi. Chini yake kulikuwa kambi ya Israeli iliyo gawanya kwa  tarafa nne, wakisubiri amri ya kuingia Nchi ya ahadi. Kwa upande mwingine wa Yorodani aliweza kuona ngome of Jericho ( muhimu kwa nchi ya Palestina ), bonde la Esdraeloni , milima pacha ya Ebali na Gerizimu, bonde lenye rutuba la Shekemu.  Pia aliweza kuona milima ya Yudea na ngome kuu ya Yebusi iliyokuja  baadaye kuitwa Ml. Sayuni. Kama vile Musa alitizama maeneo haya yote alijua kwamba, ingawa hangewaongoza  watu wake kuingia Nchi ya Ahadi , siku moja angeweza kusimama juu ya mipaka yake. Pamoja na Ibrahimu na wengine, na chini ya uongozi wa Bwana Yesu, atapata urithi wake. Kama wengine wengi , Musa "alikufa katika imani , bila kupokea ahadi , bali waliziona kwa umbali ..." (Ebr. 11:13). Alifariki katika imani kwamba siku moja atapata urithi wake na utukufu.

Hivyo Musa alipitia kifo chake akiwa mtu mtukufu sana . Katika kuongoza,  kuwajali na kuwa mtetezi wa wana wa Israeli.  Pia aliwaunga  mkono, akawaongoza katika jangwa kuelekea Nchi ya Ahadi, kuwafundisha sheria ya Mungu, kuwasaidia kuvuka  bahari ya Shamu – na kwa njia hizi na nyingine nyingi walimwona kama mfano wa Bwana Yesu (ona Kum. 18:18-19 . ) Lakini  mfano wa Musa haukuwa kamili , kwa hivyo mtu mwingine alichaguliwa kuongoza WaIsrael  kupitia Yorodani- Yoshua, mtu wa imani.

Na Mungu alipompumzisha  mmoja wa wafanyakazi wake ,mwigine alichukua kazi hio. Kwani, ingawa wafanyakazi hufa, kazi lazima iendelee.

 

MAFUNZO KWETU
 

• Kama Musa alivyohisi huzuni kubwa , Mungu anatutaka sisi kufuata neno lake kwa uaminifu. Wokovu na kuingia ndani ya " Nchi ya Ahadi " hautapatikana kwa wale ambao hawatii amri zake .
• Kama wana wa Israeli, ni lazima tumtafute kiongozi mpya (Yesu / Yoshua)ili atupeleke ndani ya Ufalme . Hii ni jambo ambalo sheria ya Musa haingeweza kufanya .
• Wokovu kutoka uchungu wa dhambi unahitaji imani ndani ya " Kristo aliyesulubiwa " na kazi ya upatanisho ilitokea kwa njia yake. Mungu alitoa mwanawe mpendwa " ili kila mtu amwaminiye asipotee , bali awe na uzima wa milele " (Yoh. 3:14-17).
• " Uwe na nguvu na moyo wa ushujaa " ni ushauri ambao Musa alimpa Yoshua , ushauri ambao pia baadaye Daudi alimpa mwanawe Solomon, na  unaweza tumika kwa mtu yeyote leo ambaye amekabiliwa na masuala ya ukweli na kidunia .
• Uzoefu wa Israeli ulifananishwa na wa safari yetu kwa Ufalme wa Mungu (1 Kor. 10:1-11) . Ni lazima tujitenge na mambo ya dunia , tubatizwe katika Kristo, tusikilize neno lake,  tupitie majaribio na kupitia hukumu ambapo kuna wale watakao kubalika na wengine kukataliwa.

 

MAKTABA YA KUREJELEA:

"The Visible Hand of God" (R. Roberts)—Sura 19

"The Story of the Bible" (H. P. Mansfield)—Tol. 2, Nam. 8 &9

"Moses My Servant" (H. Tennant)—Kurasa 148-165

 

MASWALI YA AYA:
1 Ni somo gani tunajifunza kutokana na adhabu ya Mungu aliyompa Musa?
2. Ni kwa njia gani nyoka wa Shaba alikuwa aina ya Yesu?
3 "Wale wote waliokufa katika imani, bila kupokea ahadi, bali waliziona kwa umbali na wakakubaliana na kukumbatiana". Jinsi gani hii inafananishwa na  maelezo ya Musa?

MASWALI YA INSHA:
1. Kwa nini Musa alikatazwa kuingia Nchi ya Ahadi? Ni somo gani tunajifunza kutokana na hili?
2. Elezea tukio la nyoka na uonyeshe jinsi  gani hii inatabiria kazi ya Kristo katika kuishinda dhambi na kifo.
3. Ni jinsi gani kutangatanga kwa WaIsraeli na mwishowe kufikia mlango wa Nchi ya Ahadi kunafananishwa na safari yetu ya kutafuta Ufalme.

 

1. Mwishoni wa safari ya kuzunguka jangwani, Israeli walirudi Kadeshi ambapo Miriamu alikufa (Hes. 20:01; 33:16-36).
2. Dhambi ya Musa katika kuupiga mwamba kutoa maji (20:2-13).
3. Mfalme wa Edomu aliwakataza WaIsraeli kupitia katika nchi yake, hivyo iliwabidi waIsraeli kuelekea kusini kwa mipaka ya Edomu (20:14-22; 21:04;. Kum 02:08).
4. Aaron ilipanda Mlima Hori uliopakana na  Edomu na akafa (Hes. 20:23-29).
5. Watu walilalamika tena na Mungu akamtuma nyoka wa hasira aliyewauma na wale waliomtizama nyoka ya shaba juu ya mlingoti waliweza kuponywa (21:4-9).
6. Israel, kupanda mlima  wa Arnoni, kupatikana kwa ushindi mkubwa juu ya Sihoni mfalme wa Waamori kisha Ogu mfalme wa Bashani (21:13).
7. Musa kupanda Mlima Nebo, ambapo alitazama Nchi ya Ahadi, na kisha akafa (Kum. 34:1-8).

SEHEMU YA 2: KUTEKWA KWA NCHI
Kuanzia somo 5 hadi 10 la Kitabu cha Yoshua tutazingatia mambo  kadhaa. Tutajifunza kuhusu kuingia kwa ushindi katika Nchi ya Ahadi na kuanguka kwa ukuta wa Yeriko.
Kufuatia kampeni hii, kampeni nyingine mbili zilitekelezwa na Yoshua dhidi ya majeshi ya muungano wa  Wakanaani kwa pande zote mbili za kusini na kaskazini. Mataifa yenye nguvu yalishindwa na kilichobaki ni makabila binafsi kuingia na kuchukua sehemu zilizobaki na kuondoa upinzani uliobaki. Kwa hio Mungu alikuwa ametimiza ahadi yake ya kuwatoa wana wa Israeli kutoka Misri na kuwaleta Kanaani.


Lakini ushindi huu haukuwa bila mafunzo, wakiwa Ai na Wagibeoni. Ingawa  walipata mafanikio, iliwabidi kufuata maagizo ya Mungu kwa kufanya maamuzi. Kama hawangefanya hivyo wangekubwa na majanga. Kwa upande mwengine tunaona kwamba  watu, waaminifu walizawadiwa kama vile Yoshua na Kalebu walivyopata urithi wao.
Sehemu hii inamalizia na maneno ya mwisho ya  Yoshua kwa taifa ambalo alikuwa amelitumikia kwa uaminifu. Aliwakumbusha baraka walizopokea kama Taifa kuanzia wito wa Ibrahimu hadi sasa. Mungu alikuwa amewaongoza katika safari ya maisha, kuwaokoa katika nyakati za hatari . Utambuzi huu unaonekana kama  mwito wake wa  mwisho kwa watu wake wazidi kumtumikia Bwana katika roho na kweli. Kwa hiyo, kuna mengi ya kujifunza katika katika sehemu hii.

 

 

 

Swahili Title
279. KIFO CHA MUSA
English files
Sub type
Sub sub type