285. MANENO YA MWISHO YA YOSHUA
"Ninyi ni mashahidi juu ya nafsi zenu, nimewachagueni Mimi Bwana wenu mnitumikieâ
Baada ya kufikia mwisho wa Maisha yake akiwa ndani ya utumishi wa Mungu ufanyike Yoshua aliona heri aondoke na awachie watu wa Israeli onyo la mwisho. Alifanya hivi kwa kutoa hotuba yake kwa taifa kwa mkutano wa kihistoria kule Shekemu na ili iwe kama kumbukumbu iliyoandikwa katika Yoshua 23 na 24. Mwanzoni mwa kazi yake, baada ya kifo cha Musa, Mungu alimhimizia Yoshua maswala fulani(Yos. 1:07 ). Sasa ushauri ambao alikuwa ameongezewa Yoshua ulikuwa upitishwe kwa mwingine kabla ya kufa kwake. Bwana Yesu Kristo vile vile aliwaacha ujumbee wake wa mwisho kwa wanafunzi wake kabla ya kifo chake (Yoh. 13-17 ), baada ya kufufuka kwake (Mat. 1:1-11) na katika kitabu cha Ufunuo (Ufu. 01:01 ). Kuna onyo kali kwetu sisi kufuata ushauri na mwelekeo wa njia za Mungu. Lengo letu ni kuona haja ya kumtumikia Mungu katika kweli na haki.
YOSHUA 23, 24 YOSHUA ANAWAKUSANYA WAISRAELI (YOS. 23:1-2) .
Katika wito wa Yoshua kwa WaIsrael na viongozi , wote walifurahishwa na ukuu wake na jinsi alivyotimiza yale yote Mungu aliyomwagiza na sasa akiwa kilele cha maisha yake(11:15) , Yoshua hakuwa na hali ya kujisifu na badala yake aliweka fikra na mawazo yake katika watu wa Israeli na kuwasihi kumtumikia Mungu kwa imani na kweli. Kwa kutumia maisha yake kama mfano (Mst.2) , alifahamu masuala ambayo yangewakabili na akawaonya ipasavyo. Hotuba yake inaweza fupishwa katika sehemu hizi kuu : -
⢠Sifa na shukrani kwa ajili ya mambo ambayo Mungu amewafanyia watu wa Israeli (Mst.3-5).
⢠Ushauri na kutia moyo ( Mst.6-10 ).
⢠Onyo la mwisho (Mst.11-16).
SHUKRANI, KUTIA MOYO NA ONYO (YOS. 23:3-16 ).
Kwa msingi wa wema Bwana aliyowafanyia awali mbele yao , uaminifu wake katika kutekeleza yote aliyoahidi na faida kubwa aliyokuwa amewapa, Yoshua aliwahakikishia kwamba ahadi za Mungu ni za kuaminiwa( mstari wa 5 ). Yoshua alirejelea maneno yale aliambiwa na Mungu wakati alichukua hatamu za uongozi kutoka kwa Musa : " Muwe jasiri " (Mst.6 , linganisha 01:07). Ili kufuata amri zilizotolewa katika kitabu cha Sheria inahitaji mtu kuwa jasiri ili kushindana na ushawishi wa mataifa yanayotuzunguka. Hivyo Yoshua kuwahimiza watu wawe jasiri " ili wasigeuzwe kwa upande wowote."
Aliwashawishi kuambatana na Bwana na kuepuka ushirika na watu wa mataifa. Neno " ambatana " katika kifungu cha 8, linamaanisha kuwa na uhusiano wa karibu sana kama ilivyotumika katika Mwa. 2:24 (mtu lazima " ataambatana na mkewe "), na katika Ruth 1:14 (kueleza uhusiano kati ya Ruth na Naomi). Uhusiano huu unaletwa wakati kuna upendo wa kina na Yoshua kuwahimiza watu katika Mstari wa 1 wadhihirishe upendo huu kwa Mungu. Hii ni muhimu kwa mafanikio yote na ni amri kuu ya kwanza (Kum. 6:4-5 ; . Zab. 18:01 ).
(Yoshua alitumia usemi huo katika mstari wa 12). Uhusiano huu ungesababisha upendo wao kuelekezwa kwa watu wa mataifa na ambao ungelewatea maafa ( Mst.12-13).
Mahitaji ya kwanza ni kuwa tofauti kwa ajili yetu pia , kama ilivyokuwa kwa waIsraeli. Tunaambiwa tusipende dunia au mambo yake (1 Yoh. 2:15 ), na tuwe watu tofauti (2 Kor. 6:14-18). Labda njia fupi ya maafa katika Ukweli ni kuanzisha na kuendeleza uhusiano wa kimapenzi na watu wa jinsia ya nje iliyo nje ya ukweli. Hii inasababisha mahusiano zaidi na hata ndoa kama vile Yoshua alivyowaonya waIsraeli .
Yoshua aliwahimiza WaIsraeli zaidi kwa kuwakumbusha kwamba Mungu alikuwa pamoja nao. (Mst.9-10). Musa alikuwa ametabiri kwamba mtu mmoja katika Israeli atafukuza maelfu ya watu(Kum. 32:30) . Hata hivyo uasi utasababisha kinyume cha haya.(Isa. 30:17 ).
Mungu aliwaonya WaIsraeli kupitia Musa kwamba kukubali Wakanaani kuishi kati yao itakuwa kama kuacha miiba na michongoma ambayo itawakera daima(Hes. 33:55 ). Yoshua anarejelea hili katika mstari wa 13. Yesu alitufundisha kwamba " miiba na michongoma " ambayo tunakumbana nayo, ni kama Wakanaani kwa Israeli, hatimaye miiba itasonga mbegu ya Neno la Mungu na haitakuwa vyema . Miiba kwetu sisi " ni wasiwasi, mali na anasa za maisha " (Lu. 8:14). Musa alikuwa ameambiwa kwamba maovu yote ambayo Mungu angewaletea Wakanaani pia yangewakumba wana wa Israeli kama wangekataa kutii, na Yoshua pia alirudia onyo hili (Mst.15 ; . Hes. 33:56 ; . Law 26:14-16 ; Kum. 28:15, 16, 63).
YOSHUA ANAKUSANYA MAKABILA SHEKEMU (Yos. 24:1-13 ).
Ilikuwa ni Shekemu,ambapo Ibrahimu alikuja kwa mara ya kwanza kupokea ahadi ya nchi ya Kaanani. Mungu akamwambia, " Nitawapa Uzao wako nchi hii " (Mwa. 12:07 ). Tunaambiwa kwamba wakati huo Wakanaani walimiliki ardhi hio, lakini Ibrahimu aliangalia mbele hadi siku ile ahadi itakuja kutimia. ( Ebr. 11:8-10 ).
Ilikuwa ni Shekemu pia ambapo Yoshua aliwaongoza Israel baada ya kukataa kutii amri ya Musa ( 8:30-35 ; . Kum. 27:4-26 ). Hapa baraka za Sheria zilisomwa kutoka mlima wa Gerizimu na laana kutoka kwa mlima Ebali. Sheria zote zilisomwa kwa Israeli na kuandikwa juu ya mawe, na sadaka zilitolewa juu ya madhabahu ya mawe.
Hivyo wakati wa mwisho wa maisha yake, Yoshua kwa mara nyingine aliwakusanya makabila pale Shekemu ili kufanya upya agano walilolifanya na Mungu (Kut. 24:7-8 ). Alianza kwa kuwakumbusha wito wa Ibrahimu kuondoka katika uabudu wa sanamu (Mst.2-3). Pia aliwakumbusha Waisrael kuhusu ukombozi mkubwa kutoka Misri na kuzunguka jangwani, na jinsi Mungu alivyokuwa pamoja nao katika kuwashinda Waamori kwa upande wa mashariki mwa Yorodani na jinsi nia ya Baalamu ya kuwalaani waIsraeli ilivyoshindwa. (Mst.5-10).
Walikumbushwa matukio ya hivi karibuni ya ushindi wa Nchi ya Ahadi ili kuwaonyesha wana wa Israeli uaminifu na nguvu ya Bwana, Mungu wao (Mst.11-13). Tazama jinsi neno "mimi" linapatikana katika mstari wa 1 hadi 13, hivyo kusisitiza upendo wa Mungu na ukombozi wa Israeli.
WITO KUTOA HUDUMA ( YOS. 24:14-31 ).
Baada ya kuweka msingi, Yoshua alifikia mada kuu ya kuita mkutano ule, ambao ulikuwa kutoa onyo kwa WaIsraeli: " Basi sasa mcheni Mungu na kumtumikia kwa moyo wa dhati na kweli" (Mst.14) . Hapa ndipo Bwana Yesu Kristo baadaye alikuja kumwambia mwanamke Msamaria, ambaye dini yake ilikuwa mchanganyiko wa ukweli na dhambi, Kwamba Mungu ataabudiwa kwa " roho na kweli " na kwamba " wokovu ulikuwa wa Wayahudi " (Yoh. 4:22 -23 ; . linganisha 2 Fal. 17:32-33 , 41).
Ilikuwa kitu cha kushtua kutambua kwamba tayari kushirikiana na mataifa ya Kanaani kulikuwa kumeanza kuharibu njia zao za kweli katika " Ecclesia " wa Israeli, kwani Yoshua aliwahimiza kuweka sanamu mbali. (Mst.14) . Usafi na kweli unahitaji uamuzi na Yoshua siku hio aliwapa kauli ya kuchangua. Bwana Mungu au miungu ambayo baba zao walikuwa wamekataa. Yoshua alifanya uamuzi wake na kusema: " mimi na nyumba yangu tutamtumikia Bwana" (Mst.15) . Yoshua alitekeleza yale yote aliyofundisha watu na alikuwa na ujasiri na tayari kusimama peke yake.
Watu walijitetea (Mst.16-18) , lakini Yoshua alikataa na kusimama imara na kuwaambia kwamba hawawezi kumtumikia Bwana hadi pale watakapoamua kumtumikia yeye pekee (Mst.19-20). Aliwakumbusha kuhusu wivu na utakatifu wa tabia za Mungu ambayo Musa alikuwa amewalezea, katika tukio la hapo awali, wakati walikuwa wanajihusisha na ibada ya sanamu ( Kut. 32:1; 34:6-17 ).
Israel kwa mara nyingine walitetea uaminifu wao na hamu ya kuendelea kumtumikia Bwana (Mst.21) . Basi Yoshua akawataka kushuhudia kati yao wenyewe. Ili kupima uaminifu wao Yoshua aliwapa changamoto na kuwaambia waweke mbali miungu waliokuwa nayo na kutumikia Bwana kwa mioyo yao yote (Mst.23) .
Watu walikubaliana na hayo na Yoshua akafanya agano nao. Kwa kuweka kumbukumbu la tukio hili, aliandika maneno katika kitabu cha Sheria na kuwekwa jiwe kubwa chini ya mwaloni huko Shekemu mahali ambapo Ibrahimu alikuwa amepokea ahadi na kufanya madhabahu (Mwa. 00:07 ), na mahali ambapo sanamu za wale watu ambao walikuja pamoja na Yakobo , aliporudi kutoka Padan- aramu zilifichwa (Mwa. 35:1-5 ). Hivyo Shekemu ikaja kuwa mfano wa azimio la Bwana, sanamu zao zilitupwa mbali na Mungu akaabudiwa kwa roho na kweli.
Kwetu Sanamu inaweza kuwa chochote ambacho kinashindana na upendo wetu kwa Mungu . Katika dunia ya leo , furaha, burudani , maslahi ya kijamii , michezo, tamaa na mambo mengine mengi ya anasa yanaweza kuadhiri maisha yetu ya kiroho. Mambo yanayo haribu mtazamo wetu wa Ufalme unaokuja, na kuchukua muda wa thamani ambao unapaswa kutumiwa katika utumishi wa Mungu. Nasi tusiwe kama WaIsraeli ambao walijifanya waaminifu kwa Mungu huku wakiabudu sanamu zao kwa siri. Paulo anatuambia kwamba tamaa ni mfano wa ibada ya sanamu (Kol. 3:05 ). Katika dunia ya leo tunahitaji ujasiri wa Yoshua. Viwango vya Mungu ni vile vile, lakini viwango vyetu ndivyo vinaweza badilika. Yoshua aliwahimiza watu kuwa na akili moja na akawakumbusha tabia za Bwana Yesu Kristo : "Hakuna mtu anayeweza kutumikia mabwana wawili " (Mat. 6:24) , na kulingana na Yakobo : " tu aliye na nia mbili ni mtu asiye imara kwa njia zake zote " (Yak. 1:08 ).
Kitendo cha Yoshua cha mwisho kwa umma kilichofaa maisha yake na kuwa ushahidi wake mkubwa inapatika katika mstari wa 31 : "Israel walimtumikia Bwana siku zote za Yoshua na siku zote za viongozi walioshi baada ya kufa kwa Yoshua".
MAFUNZO KWETU
⢠Ili kusimama mbali njia za kidunia na kupambana na vita dhidi ya dhambi tunahitaji ujasiri na uamuzi - "ninyi muwe jasiri", hii ilikuwa onyo la Yoshua.
⢠Kujihusisha au kuwa na urafiki na mambo ya ulimwengu kunaweza kwa urahisi kututoa katika Ukweli. Ndoa nje ya Ukweli ilikuwa ni makosa katika siku za Yoshua na inapaswa kubaki hivyo.
⢠Mungu anatuhitaji kumwabudu "katika roho na kweli".
⢠Tunahitaji kujiunga na Yoshua katika kutangaza, kwa wale wote ambao watasikiza kwamba, "mimi na nyumba yangu tutamtumikia Bwana''
MAKTABA YA KUREJELEA
"The Story of the Bible" (H. P. Mansfield)âTol. 2, Nam. 11
"Joshua" (J. Ullman) â Sura ya 23-24
MASWALI YA AYA
1. Taja mambo matatu yaliyotokea Shekemu katika historia ya awali ya taifa la Israeli na mababu zake.
2. Yoshua aliwaambia watu kumtumikia Mungu "katika imani na kweli." Alimaanisha nini? Nani alisema baadaye kwamba Mungu anapaswa kuabudiwa "katika roho na kweli"?
3. Onyo kuu katika hotuba ya Yoshua ya mwisho kwa taifa ilikuwa gani? Na onyo hili linatuathiri sisi vipi?
MASWALI YA INSHA
1. Kwa nini ilikuwa ni muhimu kwa Yoshua kuhutubia maneno yake ya mwisho kwa watu wa Israeli? Je, alitaka kuwaonyesha nini?
2. Yoshua alisema, "mimi na nyumba yangu tutamtumikia Bwana." Alisema hivi wakati gani, na alimtamka maneno haya kwa nani, na somo gani alikuwa anataka kufundisha?
3. Yoshua aliwasisitizia waIsraeli haja ya kuwa tofauti. Jinsi gani walipaswa kuwa tofauti? mambo gani duniani ambayo tunapaswa kujitenga nayo?
SEHEMU YA 3 KIPINDI CHA MAHAKIMU
Sehemu hii inashughulikia kipindi cha miaka 450 ya historia ya Israeli. Katika wakati huu Israeli haikuwa imeungana au kuwa taifa lenye umoja kama ilivyokuwa katika kipindi cha Wafalme ambacho kilifuata. Kwa sababu hiyo machafuko yalikuwa ya mara kwa mara na kila kabila likafuata njia yake tofauti. Hofu ya Bwana ikapungua na hii ikasababisha uvamizi wa mataifa jirani na kushindwa kwa waIsraeli. Kwa huruma yake, Mungu aliteuwa watu wenye imani ambao walikomboa wana wa Israeli kutoka kwa mataifa yaliyokuwa yanawakandamiza. Baadhi ya wahusika hawa wa ukombozi tutaangalia: Debora, Gideoni na Samsoni. Katika kila kesi ya ukombozi tutaona nguvu za Mungu zikitumika wakati kuna hali ya udhaifu; alitumia njia ya kipekee kuleta ukombozi ili waIsraeli wasije kudai ushindi ulikuwa wao wenyewe. Hivyo Alikuwa anasisitiza somo kwamba Yeye pekee ndiye anaweza kushinda adui zao na kutoa wokovu .
Kipindi cha Mahakimu kilifuatwa na kipindi cha utawala wa wafalme na mabadiliko ya kipindi cha mwisho cha Waamuzi na ya kwanza ya manabii, ikiwa pamoja na Samweli.
Somo la mwisho katika sehemu hii linahusu kuzaliwa kwa Samweli na ujumbe wa nyumba ya Eli.
1. Deborah anamwita Baraka kukusanyika juu ya Mlima Tabori pamoja na watu 10,000 kutoka kwa makabila ya Naftali, na Zebulon (Amu. 4:06 ).
2. Wakapambana na jeshi Sisera kule Taanaki, karibu na maji ya Megido. Magari ya Wakanaani yakaharibiwa na mto Kishoni wakati ulipofurika kwa ghafla na wakatorokea Haroshethi ( 4:15-16 ; 5:19-21).
3. Wamidiani na Waamaleki walikusanyika katika bonde la Yezreeli karibu na mlima wa More ( 6:33 ; 07:01 ).
4. Gideoni anawakusanya makabila ya Asheri, Naftali na Zebuloni pamoja na kabila lake wa Manase ( 6:34-35 ). Anachagua jeshi ndogo la watu 300 ambalo linapambana na Wamidiani (7:22).
5. Gideoni anaomba msaada kutoka kwa kabila la Efraimu kushambulia Wamidiani katika Yorodani ( 7:24).
6. Gideoni anawafuata Wamidiani kupitia Yorodani na katika kurudi kwake anaiadhibu miji wa Sukothi na Penueli kwa kukataa kumsaidia (8:1-17)