CSSA 3-2-290 - SAMUEL: HIS BIRTH AND MISSION

Swahili

290 SAMWELI: KUZALIWA KWAKE NA KAZI YAKE
          "Israel yote ... Ilitambua kwamba Samweli amechanguliwa kuwa nabii"



Kazi ya Samweli Nabii ilikuwa kugeuza taifa lililojaa machafuko ya nyakati za Waamuzi ili kuwezesha uanzishwaji wa "Ufalme wa Mungu" chini ya Daudi, mfalme wao. Samweli ndiye alikuwa Mwamuzi wa mwisho na kuanzia kwake Manabii walifuata (ona Mat. 3:24). Samweli anahusishwa na Musa katika kukadiria jinsi Mungu alitaka kuwa na uhusiano wa kudumu na binandamu. (Yer. 15:01). Anaweza kulinganishwa na Yohana Mbatizaji kama mtangulizi aliye tengeneza njia  kabla ya upako wa Bwana. Somo hili linaonyesha maandalizi ya Mungu kwa ajili ya kuanzishwa kwa ufalme wake kwa kumtumia nabii na kiongozi mwaminifu.

Lengo la somo hili ni kuonyesha umuhimu wa mafunzo ya  mapema ya watoto wa Mungu.

 

1 Samweli 1 , 2:1-11

KUZALIWA KWA SAMWELI (1 SAM. 1).
Mlawi mmoja aitwaye Elkana aliishi Raman karibu na Mlima Ephraim na wake zake wawili, Penina na Hana. Hana alikuwa mpendwa wa mumewe, lakini alikuwa tasa hivyo alidhihakiwa na Penina ambaye alikuwa na watoto.
Kila mwaka kila Familia ilifanya Hija  kwa kwenda Shilo, ambapo hema zilitundikwa na  watu  kuabudu na kutoa sadaka kwa Mungu. Sherehe hizi zilikuwa za huzuni kwa Hana kwani hakuwa na mtoto.


katika tukio moja karibu na  mlango wa madhabahu, Hana aliomba kwa dhati na akaapa Kwamba kama Bwana atasikia ombi lake na kumbariki na mtoto  basi atamtoa kwake amtumikie maisha yake yote. Angekuwa kama Samsoni, Mnadhiri, aliyejitenga na kumtumikia Mungu (tazama Hes. 6.). Maisha yake yangekuwa ya kikuhani na ya huduma kwa Mungu, ingawa hangekuwa kuhani halisi wa asili ya Haruni (Hes. 18:07).

 

Eli kuhani mkuu ilikuwa amekasirishwa na tabia ya Hana ya kwanza ya ulevi na kumkemea sana. Alijitetea na kukanusha madai ya ulevi akisema kwamba anamtengemea Mungu na moyo wake wote. Baada ya kutambua tabia yake ya ucha Mungu, Eli aliongeza maombi yake na yale ya Hana: "Mungu wa Israeli akujalie haja yako" (Mst.17).
 
Mungu alijibu maombi ya Hana na baada ya mda mtoto alizaliwa, na akampa jina Samweli, ambayo ina maana ya "habari za Mungu." Mtoto alipoachishwa maziwa, Kwa furaha Hana alifunga safari kwenda Shilo kumpeleka Samweli kwa huduma ya Bwana ambaye alikuwa amejibu maombi yake kwa njia ya ajabu (Mst.26-28, tazama pia nguvu za maombi katika Yak. 5:16. Lk. 11:1-13;. Yos 1:05; 5:11;. Mat. 17:20, 21).

 

MAFUNZO YA SAMWELI (1 Sam. 2).
Hakuna maelezo mengi ambayo yametolewa kuhusu elimu na mafunzo ya Samweli. Hata hivyo, mambo mawili yalifunzwa Samweli. Kwanza aliwekwa chini ya uangalizi wa Eli, kuhani mkuu, huku akifunzwa  mambo ya Mungu : pili , alitembelewa mara kwa mara na wazazi wake ambao walimpa ushauri na upendo (Mst.19) .
Mafundisho hayo ni muhimu kwa vijana ili kuendeleza tabia za Mungu - wakati wanakabiliwa na ukosefu wa maadili na uasi unaowazunguka. Tunaweza fikiria mshtuko wa Samweli wakati aliposhuhudia uovu wa wana wawili wa Eli, Hofni na Finehasi, na uamuzi wake katika umri mdogo ili kuepuka kushirikiana nao. Somo la Samweli ni lile la kujitenga na mafunzo ya kuanzia utotoni . Baadaye Yesu alisema, " hawa ni kama ufalme wa mbinguni" ( Mat. 18:03 ; 19:14). Mafundisho ya watoto katika sheria za Mungu ni kama wajibu, na amri ya Mungu, (Kum. 6:7-9 ). Methali huonyesha hekima ya " mafunzo ya mtoto ili akue kwa njia ipasayo , maana wakati atakapo komaa hataiacha hio njia " (Mit. 22:06 )

Janga kubwa lilimpata Eli kwani alishindwa kuwadhibiti wanawe (1 Sam 2:12-17 , 22-25 ; . 3:11-14 ). Jambo ambalo linashutumuwa katika methali ( 29:15-17 ; 13:24). Tofauti kati ya Samweli na wana wa Eli imetajwa na kusisitizwa katika kumbukumbu katika mistari ya 11-12 kwamba mtoto Samweli alikuwa "mjumbe wa Bwana mbele ya Eli kuhani. Sasa wana wa Eli walikuwa wana wa Beliali ; hawakumjua Bwana. " ; na tena katika mistari 17-18, "dhambi za wale vijana zilikuwa kubwa sana .. lakini Samweli alitumika mbele za Bwana, akiwa kijana, aliyevaa nguo  ya kitani "; na tena katika aya 25-26, " hawakusikiliza sauti ya baba yao ... na huyo mtoto Samweli akakua akipendwa na Bwana na watu. " Hapa tabia Samweli inaashiria ile ya Yesu ambaye, kama vijana, " akazidi kuongeza hekima akipendwa na Mungu na watu" (Lk. 2:52) .
Ni kinaya kuona kwamba Eli ambaye alimwongoza Mtoto Samweli kwa njia za Kimungu na Utiifu alishindwa kuwangoza wanawe walio asi  na kukataa mafundisho ya baba yao. "Watoto watiini wazazi wenu mkiwa ndani ya Bwana ",  haya ndiyo  mafundisho ya Paulo (Efe. 6:01 ), na anaongeza, " maana hii ndiyo haki ." Dunia inawaonyesha watoto kutowaheshimu wazazi wao kukataa yale wanayoambiwa. Watoto wanaolewa kwa njia ya ukweli hawapaswi kufanya hivyo. Heshima kama ile mtoto Samweli Alionyesha ni mfano mzuri tunaopaswa kufuata. " Waheshimu baba na mama , kwani hii ndio amri ya kwanza yenye ahadi, ili iwe nzuri kwenu na mpate kuishi kwa muda mrefu humu duniani" (Efe. 6:2-3).

SAMWELI NA YOHANA MBATIZAJI.


Ni muhimu kuwa kuna sehemu nyingi za kufanana ambazo zinapatikana katika kulinganisha kuzaliwa kwa Samweli na Yohana Mbatizaji, wote ambao waliteuliwa kuwa katika "mstari wa mbele" kwa kuandaa njia kabla ya ujio wa Bwana.
• Hana alikuwa tasa (1 Sam 01:05.);  pia Elizabeth (Lk. 01:07).
• Wanawake  hawa  wawili waaminifu walipeleka kilio chao kwa  Bwana kwa njia ya sala ambaye Alisikia maombi yao (1 Sam 1:10-11, 19-20;. Lk. 1:13).
• Watoto hawa wawili walifanywa wa nadhiri na walitengwa kwa utumishi wa Mungu (1 Sam 1:11;. Lk. 1:15;. Hes. 6:1-5).
• Katika maadhimisho ya huruma na baraka waliyopewa na Mungu, wanawake hawa waliimba nyimbo za sifa na shukrani (1 Sam 2:1-10;. Lk. 1:42-55).
• Tizama maana ya majina ya watoto hawa wawili: -
o Samweli-"habari za Mungu" (1 Sam 1:20.);
o Yohan-"ambaye Mungu amemtoa kwa neema" (Ebr. "Yohana”)

 

Samweli na Yohana walikuwa Mitume waliotumwa kuandaa njia ya Bwana, na kuwatayarisha  watu kwa ajili ya Bwana (Mk 1:2-3). Samweli alibadilisha taifa lilokuwa kubwa kwa ajilli ya ufalme wa Mungu na pia akawaandikia katiba, (1 Sam 10:25.), Wakati Yohan alitayarisha njia ya kuja kwa Bwana Yesu Kristo. Katika siku za usoni ilibidi Eliya aje kwanza na kufanya kazi ambayo ni sawa na ile waliofanya Samweli na Yohana. Ali tayarisha mambo  yote, na kugeuza mioyo ya baba na watoto wa watoto wao ili wawe kama babu zao wa kale kabla ya "siku ya kutisha ya Bwana" (Mat. 17:11;. Mal 4:5-6).

 

KAZI YA SAMWELI

 Samweli alikuwa Mlawi wa wana wa korah kutoka katika familia ya Kohath familia ambayo Daudi aliteua kutunga wimbo wa madhabahu (1 Nya. 6:31-38 - . " Shemueli " katika mstari wa 33 ni " Samweli " , Linganisha . mstari wa 28 )
 

Ijapokuwa hakuwa wa ukoo wa Haruni na hivyo hakuwa kuhani, Samweli alimtolea Mungu sadaka ya kuteketeza na sadaka (1 Sam. 10:8), Na aliteuliwa kumwagilia mafuta  Sauli na Daudi kama wafalme wa Israeli (1 Sam. 9:16 , 10. : 1; 16:13)

 

Kama moja wa wale waliogeuza taifa kutoka kwa machafuko na uovu wa siku za Waamuzi hadi wakati  wa kumkubali kiongozi mwenye haki katika Mfalme Daudi, kazi Samweli kubwa ilikuwa kuwafundisha watu . ( 1 Sam. 7:15-17) . Mtume Petro alimpa jina kama mnabii wa kwanza (Mat. 03:24 , Linganisha 13:20;  Heb 11:32 ;  1 Sam 3:20). Hapo awali kulikuwa na waonaji (1 Sam. 9:09 ), hivyo kazi Samweli ya inaonekana kuwa ya kuanzisha utawala wa manabii, ambao katika siku za kifalme walikuwa na ushawishi mzuri juu ya mfalme.

 

Maisha na huduma ya Samweli inatuonyesha matumaini pamoja na onyo kali "Ataweka miguu ya watu wake imara na wale wauovu watanyamazishwa katika giza, kwani kwa  nguvu za mwili hakuna mtu atatawala. wapinzani wa Bwana watavunjwa  vipande vipande; radi itatoka mbinguni  na  Yahweh atatawala hadi mwisho wa nchi; naye atampa mfalme nguvu  na kuitukuza pembe ya masihi wake (Masihi) "(1 Sam . 2:9-10).

 

MAFUNZO KWETU


• Samweli ni mfano mkuu wa kanuni ya "kumbukeni Muumba wenu katika siku za ujana wenu."
• Mamake Samweli alimtoa kwa utumishi wa Mungu kama shukrani kwa kumpa mwana ili kuanzia utotoni ahusishwe na madhabahu.
• Mafunzo ambayo Samweli alipokea kutoka kwa mama yake na chini ya mkono wa Eli na akaanzisha huduma ya ibada ya Bwana.
• Biblia inatoa wito kwa watoto waheshimu wazazi wao.

 

 

MAKTABA YA KUREJELEA

"Elpis Israel" (J. Thomas)—Kurasa 451, 452

"The Ways of Providence" (R. Roberts)—Sura 14

"The Visible Hand of God" (R. Roberts) — Sura 22

"The Story of the Bible" (H. P. Mansfield)—Tol. 3, Nam. 6

 

MASWALI YA AYA:


(1) Jinsi gani Eli alikuwa na makosa katika malezi ya watoto wake?
(2) Andika maelezo mafupi kuhusu tabia ya Hana.
(3) Ni muhimu kwanini kuwapa watoto mafunzo ya Kimungu kuanzia utotoni? Toa jibu lako kwa kurejelea Samweli.

MASWALI YA INSHA:
1. Ni masomo gani tunayojifunza kutoka kwenye mafunzo ya Samweli?
2. Kazi ya Samweli ilikuwa gani?
3. Linganisha kati ya Samweli, Elia na Yohana Mbatizaji.
4. Andika insha kuhusu hali iliyozingira kuzaliwa kwa Samweli.

 

 

Swahili Title
290 SAMWELI: KUZALIWA KWAKE NA KAZI YAKE
English files
Sub type
Sub sub type