CSSA 3-2-291 - SAMUEL: PREFERRED BEFORE THE HOUSE OF ELI

Swahili

291. SAMWELI: ALIYEPENDELEWA MBELE YA NYUMBA YA ELI

                                              Neno la Samweli likawafikia waIsraeli wote

Uasi ambao uliendelezewa na wana wa Eli ulikuwa wa kutisha, Hofni na Finehasi, na Eli alivyoshindwa kurekebisha hali hiyo, kulileta mabadiliko makubwa katika ukuhani. Mabadiliko haya yaliadhiri ukuhani  katika utawala wa Daudi, lakini mabadiliko haya yangekuwa na matukio mengi yaliofuata katika ukuhani.
Lengo la somo hili ni kutufundisha kwamba kuishi kwa haki ni muhimu kwa wale ambao wanataka kufanya utumishi wa Mungu kwa utukufu wa jina lake.

1 SAMWELI 2, 3 , 4 KUANGUKA KWA UKUHANI WA ZAMANI (1 Sam. 2:12-26 ).

Ingawa Eli alikuwa na bidii katika kazi ya kutunza madhabahu, alishindwa kuwatia nidhamu wanawe wawili, Hofni na Finehasi, mpaka ikawa amechelewa kufanya hivyo. Vijan hawa wawili walifuata njia zao wenyewe zisizo na maadili na wakawa na kiburi na kuamuru madhabafu yafanywe kwa ajili yao wenyewe. (Mst.13-14). Sheria iliruhusu sehemu fulani ya sadaka kuchukuliwa na kuhani (Law 7:30-34 ). Lakini wana wa Eli walichukuwa yote waliyotaka  bila kujali  umuhimu wa kutoa sadaka kwa watu. Walinyakua sehemu iliyo nzuri ya sadaka hata kabla haijateketezwa kwa mafuta " (Mst.15). Mafuta, ambayo yalikuwa sehemu nzuri ambayo iliashiria wema wa Kimungu na ambayo ilikuwa sehemu ya Mungu na haikupaswa kuliwa na mtu. (Law 3:16). Ni wazi kwamba walitaka sadaka kabla ya mafuta kuchomwa na moto ili wapate kuchoma nyama na kula na mafuta yake. Kwa njia hii wana wa Eli walidharau ibada ya Mungu bila kujali shutma kutoka kwa waumini, hii ilisababisha madhara makubwa kwani Wayahudi wengi walianza kuchukia kutoa sadaka kwa Mungu (Mst.17) .

Hali hii haingekubalika na Mungu . Uteuzi wake ulikuwa unadharauliwa na kudhalilishwa. Eli alijaribu kusahihisha uovu wa wanawe wapotofu lakini hakufanikiwa (Mst.22-25). Ilibidi wakati ufike wa Mungu kuingilia kati.

ONYO LA HUKUMU (1 Sam 2:27-36 ; . 3:1-18) .
"Mtu wa Mungu " alionya kuhusu hukumu dhidi ya ukuhani wa zamani kwa kutumiakanuni kwamba "wale watao niheshimu Mimi, Nitawaheshimu, na wale watakao nidharau pia watadharauliwa " (Mst.30). Kutakuwa na uvamizi wa maadui , wana wa Eli wataangamizwa ndani ya siku moja na ukuhani wa familia yao itaisha na mwingine kuanza- "Nami nitamtoa kuhani mwaminifu " (Mst.35).
Hii ingekuwa kazi ya awali ya Samweli ... ambayo ingefanyika katika ofisi ya kuhani katika kutoa sadaka ya kuteketezwa na sadaka na ambaye alimpaka Sauli na Daudi mafuta kama wafalme wa Israeli (1 Sam 7:9-10 , 10 . 8 ; 16:13).

Hukumu inayokuja ilifunuliwa kwa mtoto Samweli usiku mmoja akiwa huko Shilo. Mungu alimwita, " Samweli ", mara tatu na kila mara Samweli aliamka kitandani na kwenda mbio kwa Eli, akifikiria ndiye anayemwita. Hapo ndipo Eli alitambua kwamba ni Mungu aliyekuwa anamwita Samweli na akamwelekeza Samweli jinsi atakavyo jibu wakati Mungu anamwita kwa mara nyingine, " Nena, Bwana , mtumishi wako anasikia ".
Maelekezo ambayo Samweli alipokea usiku ule ilikuwa kwamba nyumba ya Eli inafikia mwisho kwa sababu ya maovu ya wana wa Eli kwani baba yao alishindwa kuwadhibiti. asubuhi yake Eli alipokea ujumbe na maagizo ya haki kutoka kwa Mungu ambaye alisema, " Ni Bwana; afanye ,kilicho chema  mbele ya macho yake ".

 

HUKUMU INAKUJA (1 Sam. 4).
WaIsraeli wakaasi dhidi ya ukandamizaji wa Wafilisti lakini walishindwa, walijaribu kutafuta msaada katika sanduku la Mungu wakati wa vita, bila mafaniko. WaIsraeli 30,000 waliuawa, ikiwa ni pamoja na wana wa Eli Hofni na Finehasi . Lakini jambo la kumshtua Eli lilikuwa kuchukuliwa kwa Agano takatifu . Aliposikia haya alianguka na kufariki (Mst.18) . Mke wa Finehasi aliposikia juu ya maafa haya pia yeye akafa alipokuwa akijifungua mtoto wa kiume, lakini sio kabla ya kumpa jina Ikabodi - " utukufu umeondoka " (Mst.17-22 ; Zab. 78:64 . ).
Agano lilipelekwa hadi nchi ya Wafilisti. Lakini uwepo wake hukuwafurahisha Wafilisti kwani ulileta aibu kwa ibada yao ya sanamu . Hatimaye Wafilisti wakarudisha agano kwa wale WaIsraeli waliokuwa wamebaki nao wakabarikiwa. Baadaye Daudi alichukua Agano na kuliweka Sayuni kwa furaha kubwa (1 Nya 15; . 16:1-3). Katika siku za Solomoni agano lilifanywa mahali Patakatifu Zaidi na akajenga hekalu kubwa ( 2 Nyak. 5:4-10 )

 

UKUHANI UNABADILIKA
Eli alikuwa ameambiwa kuwa laini ya makuhani ambayo alikuwa mmoja wao itakoma. Hii ilikuja kutokea wakati wa Daudi na sehemu ya kwanza ya utawala wa Sulemani.

Wakati wa utawala wa Daudi kulikuwa na mapadre wawili waliokuwa wanaongoza - Abiathari na Sadoki. Abiathari alikuwa wa laini ya Eli. Yeye ndiye aliyeponea kuuwawa na Sauli kwani alipewa maficho na Daudi. ( 1 Sam 22:17-21 ; . 23:06 ). Kumbuka kwamba majina ya Abiathari na baba yake Ahimeleki yaligeuzwa mara kwa mara - tazama 2 Sam 8:17; 1 Nya. 18:16 ; 24:6 .

Abiathari iliendelea kutumika wakati wa utawala wa Daudi. Lakini baadaye walipanga njama pamoja na Adonia dhidi ya Solomon na aliondolewa kutoka kwa ofisi ya kikuhani. Sadoki aliteuliwa kama kuhani mkuu badala yake. Hivyo ikatimia mabadiliko yaliyo tabiriwa katika ukuhani wa Eli (kumbuka 1 Fal. 2:26-27 ).
Pia palikuwa na unabii mwingine uliotimizwa. Wana Wawili wa Haruni, Ithamari na Eleazari, wakawa  wakuu wa familia mbili za makuhani. Eli na Abiathari walikuwa wana wa Ithamari, ambapo Sadoki alikuwa wa familia ya Eleazari (1 Nyak. 24:1-3). Mwana wa Eleazari Finehasi , alikuwa amepewa ahadi ya ukuhani wa daima " kwa sababu alikuwa mtiifu kwa Mungu na alileta upatanisho kwa ajili ya wana wa Israeli " (Hes. 25:11-13 ). Hii pia ilitimia katika utawala wa Sulemani , wakati Abiathari aliondolewa madarakani na wana wa Sadoki wakahudumu hekaluni.

 

UKUHANI WA MELKIZEDEKI (Ebr. 7).
Ukuhani ulibadilika kutoka laini moja ya makuhani hadi nyingine wakati wa utawala wa Sulemani, lakini bado walikuwa wana wa Haruni, na Walawi. Mabadiliko muhimu zaidi yangekuja kutokea baadae.

Chini ya sheria ya Musa, Makuhani wa kilawi walichanguliwa "baada ya maagizo ya kibinadamu" (Mst.16). Kwa hili, mwandishi wa Waebrania anamaanisha kwamba makuhani maalumu walipaswa kuwa na sifa fulani ambazo hazikuwa na uhusiano wowote na tabia zao au njia ya maisha. Sifa  hizi zilihusina na: -

 

• Kabila  la (Levi) na familia ya (Haruni).
• Umri (miaka 30-50).
• Nguvu za kimwili.
• Ndoa (ndani ya nyumba ya Israeli).

 

Hii ilimaanisha kwamba mtu mwovu ambaye ana sifa hizo, angeweza kuhitimu na kuwa kuhani ! Katika hili udhaifu wa ukuhani wa Walawi uliweza kuonekana.

Yesu Kristo hakutoka katika ukuhani wa Walawi,  bali alitoka katika Ukujani wa Melkizedeki. Melkizedeki alikuwa mtu aliyeishi katika siku za Ibrahimu na alikuwa mfalme wa Salemu. Kwa sababu kifo chake hakitajwa katika hadithi yake katika kitabu cha Mwanzo 14 anaonekana kama mtu aliyeishi milele.Rekodi hii ilichukuliwa na Daudi katika Zaburi 110 ambapo alisema Messiah angekuwa , kwa kiapo cha Mungu, "kuhani milele, kufuatia utaratibu wa Melkizedeki" ( Mst.3).

Katika Waebrania 7 Paulo anafafanua  kuhusu Ukuhani wa Melkizedeki. Tunaambiwa kwamba maana ya majina na hata utaratibu wa tukio ulikuwa muhimu ( Mst.2). Melkizedeki ( maana yake  "Mfalme wa haki") jina hili linatajwa na kisha anatagazwa kama "Mfalme wa Salem " (maana yake " Amani" ). Yesu alikuwa mfalme wa kwanza wa haki (kumaanisha, yeye hakutenda dhambi ) na kisha akawa  "Mfalme wa amani " na kuhani milele (angalia mst. 1-3 , 28).

 

Paulo anatumia rekodi kutoka kitabu cha Mwanzo ambayo hijataja ulezi wala kifo cha Melkizedeki, kwa kusema kwamba yeye alikuwa kama  Yesu ambaye anaishi daima kama kuhani bila kuzaliwa wazazi wa mstari wa Levi (Ebr. 7: 3, 12-15).

 

UKUHANI WA NYAKATI ZIJAZO
Katika miaka ijayo kutakuwa na aina mbili ya makuhani watakao ongoza ibada katika Hekalu kubwa ambayo Ezekiel anaeleza katika sura za mwisho akihitimisha unabii wake (sura ya 40-48). Kutakuwa na makuhani wa kibinadamu, wana wa Lawi, ambao watawasili na kumtoloea Mungu sadaka kwa haki (Eze. 44:10-11;. Mal 3:03). pia kutakuwa na aina nyingine ya makuhani wana “Sadoki” ambao hawatakuwa na hali ya kufa ( Sadoki maana yake "haki"), ambao "watahakikisha Mungu bado anatawala ", na watakuwa na ushauri mkuu zaidi na wataweza kusimama mbele za Bwana (Eze. 44:15-16).
Inaonekana kwamba wao ni sehemu ya ukuhani wa Melkizedeki kwani wamefuzu kwa "haki" – na kundeleza Utawala wa Mungu".
Leo Mungu anachukua kutoka miongoni mwa watu  taifa la  jina lake yaani , "ukuhani wa kifalme" (1 Pet 2:09;. Uf 5:9-10). Imani yao kwa Mungu inawafanya kukubalika kufanya matendo ya imani ambayo  yanafuata neema ya Mungu, atawawezesha kujivika mavazi ya kitani na kuishi milele ili wawe makuhani wa nyakati zijazo (Ufu. 19:08, 20 : 6).

 

MAFUNZO KWETU
• Wakati mwingine inaonekana kwamba haki huenda bila kuzadiwa na uovu pia huenda bila adhabu, lakini ni muhimu kukumbuka kwamba Mungu bado yupo mamlakani.
• Matendo maovu ya wana wa Eli yaliwaletea uharibifu mwishowe wakiwa vitani na kusababisha mabadiliko katika ukuhani wakati wa Solomon, miaka mia moja baada ya kifo chake.
• Bidii ya Finehasi, mwana wa Eleazari hatimaye ilizaa matunda - kulikuwa na mabadiliko katika ukuhani miaka mia baadaye.
• Mungu ametuita tuwe"Wafalme na Makuhani", sio kwa sababu wazazi walikuwa watu wenye haki, lakini kwa misingi kwamba kila mmoja wetu naonyesha upendo na uaminifu katika kazi ya Mungu.

 

MAKTABA YA KUREJELEA

 

"The Visible Hand of God" (R. Roberts)—Sura 22

"The Ways of Providence" (R. Roberts) — Sura 14

"The Story of the Bible" (H. P. Mansfield)—Toleo 3, Nam. 6

MASWALI YA AYA

1. Ni nini kilichotokea kwa agano baada ya kuchukuliwa na Wafilisti katika siku za Eli?
2. Ni mabadiliko gani yaliyotokea kwa  ukuhani katika nyakati za Solomon na ni unabii gani ambao ulitimizwa na mabadiliko haya?
• Melkizedeki alikuwa nani na jina lake lilimaannisha nini?
• Daudi alikuwa anaashiria nani alipozungumza  kuhusu "kuhani wa milele baada ya laini ya Melkizedeki"?
• Ni nini baadhi ya mambo ambayo Paulo anazungumzia kuhusu Melkizedeki na anafananisha na nini”

MASWALI YA INSHA
1. Kwa nini hukumu ililetwa kwa nyumba ya Eli? Njia gani iliyotumika kuelezea haya?
2. Nini ilikuwa sababu ya kushindwa kwa Eli na hatima ya watoto wake ilikuwa gani? Toa Maoni kuhusu masomo ambayo unafikiria yanatoka kwa nyumba ya Eli.
3. kuna tofauti gani kati ya ukuhani wa Walawi na Melkizedeki?  kwa misingi gani tunaweza kuwa sehemu ya "ukuhani wa kifalme?"

SEHEMU YA 4: MWANZO WA UFALME
Katika sehemu hii sisi tunaona jinsi Ufalme wa Mungu ulianzishwa duniani. Wafalme wawili ambao wanajadiliwa ni, Sauli na Daudi,  ambao walikuwa tofauti. Sauli alikuwa mbinafsi na asiye na imani, wakati Daudi, mrithi wake, alimtafuta Bwana kila wakati alipopata nafasi hivyo alikuwa Mtu aliyependwa na Mungu. Ilikuwa ni kwa sababu ya imani yake kubwa alifaulu, kwani Mungu alikuwa na yeye  na kumpa ushindi dhidi ya Goliath na kumwongoza katika safari yake ya kuwa mfalme wa Israel. Lakini maisha ya Daudi hayakuwa bila majaribio. Mda mwingi ulipita katika hekima ya Bwana kabla apate cheo alicho ahidiwa na Mungu. Kuna mafunzo katika haya. Muda wa majaribio kabla ya kuinuliwa ndio sheria kuu ya Mungu- ni kwa kupitia Majaribio mengi tunaweza kuingia katika Ufalme wa Mungu. (Mat. 14:22).

Uzoefu  na mateso ya Daudi akiwa Uhamishoni inatupa mafunzo ya kuwa na ujasiri, imani na haki. Mawazo yake ya ndani yamerekodiwa katika kitabu cha Zaburi, aliandika  kile ambacho kimekuwa chanzo cha starehe kwa watakatifu wa miaka yote.

 

Swahili Title
291. SAMWELI: ALIYEPENDELEWA MBELE YA NYUMBA YA ELI
English files
Sub type
Sub sub type