CSSA 3-2-296 - SAUL'S JEALOUSY AND JONATHAN'S LOVE

Swahili

296. WIVU WA SAULI NA UPENDO WA JONATHANI

"Na Jonathani akanena wema wa Daudi kwa baba yake".

 

Urafiki kati ya Daudi na Jonathan ulikuwa wa karibu kama ilivyoelezewa na maandiko, Jonathani alivutiwa na Daudi wakati alionyesha imani kamili kwa Mungu katika ushindi wake dhidi ya Goliathi. Hii ilikuwa roho sawa na ile alikuwa ameonyesha katika tukio la hapo awali (1 Sam. 14:06) misingi wa urafiki wao ilikuwa sawa na upendo wa Yahweh. Kila mmoja alikuwa amejawa na Imani ya Israeli kwa hivyo walivutiwa pamoja. Urafiki wao haukuwa na kiburi wala uchoyo, kila mmoja alikuwa tayari kujitoa sadaka kwa ajili ya mwengine. Kwa hili walikuwa walifanana na Yesu Kriso ambaye aliyatoa maisha yake kwa ajili ya marafiki zake, sisi ni marafiki yake kama tutafanya kama tunavyoamriwa (Yohana 15:13-15, 1 Yohana 3:16).

Kwa upande mwingine mafanikio na umaarufu wa Daudi ukawa kikwazo kwa Sauli. Mafanikio yakaleta wivu na rekodi inaonyesha taswira ya kuchukiza ya Mfalme wa Israeli aliyejivika aibu kwa kumwaga damu isiyo na hatia. “Moyo safi ndio uhai wa mwili” lakini  wivu ni ubovu wa mifupa” (Mit. 14:30). Jinsi gani binadamu anaona ugumu wa amari “kuwa na huruma kwa kila mtu na uwe na upendo wa kindungu; kwa heshima na kutanguliza mwingine” (Warumi 12:10).

Lengo letu katika somo hili ni kuona mfano mkuu wa misingi ya urafiki wa kweli.
 

1 Samweli 18 to 20

DAUDI NA JONATHANI WANAVUTWA PAMOJA (1 Sam. 18:1-4)

Ingawa alikuwa hali ya kifalme na ukuu, Jonathani alivutiwa na Imani na Upenod wa Daudi kwa Yahweh; “ Nafsi ya Jonathani ilikuwa imeunganishwa na ile ya Daudi, na Jonathani alimpenda kama alivyojipenda yeye mwenyewe. “ Neno la Kiyahudi “kuunganishwa” limetumika pia kuelezea upendo mkuu aliokuwa nao  Yakobo kwa Yosefu (Mwa. 44:30) hata Sauli alipendezwa na upole wa Daudi na alitamani azidi kubaki katika ikulu yake. (mst.2)

Kufuatia kushindwa kwa Goliatho, Jonathani na Daudi waliingia katika ahadi kuu ya urafiki. Jonathani alijivua mataji yote ya ofisi yake kuu kama vile, vazi lake, silaha, na hata upinde na mshale wake (RSV). Na ikawa katikati ya ukuu wa ikulu ya Sauli, Daudi alitiwa moyo na upendo wa yule aliye wafanya wengine kuwa bora kumliko” (Flp. 2:3). Mridhi wa  kiti cha Ufalme cha Sauli alitambua kwamba Mungu amemtayarisha mtu aliyekuwa mkuu kumliko atawale watu wak.

MAFANIKIO YANALETA WIVU (1 Sam. 18:5-11)

Chini ya uongozi wa Mungu Daudi alizidi kupanda gazi, alichanguliwa Generali wa majeshi ya Sauli na alikubalika katika jeshi na watu pia na watumishi wa Sauli. Hakuna aliyemchukuia au kumwonea Wivu (Mst.5) kama ilivyorekodiwa katika 1 Samweli 16:21, "Sauli alimpenda sana".  

Lakini jinsi umarufu wa Sauli ulivyozidi kuongezeka ndivyo shaka ilimpata Sauli, ushindi wa WaIsraeli uliongozwa na Daudi ulimfanya apokelewe vyema na wanawake wa Israeli walikuja kumkaribisha kwa nyimbo na kucheza “Sauli ameangamiza maelfu na Daudi ameangamizi kumi ya maelfu” Wivu wa Sauli ukaamka. Samweli alikuwa amesema wazi kwamba Yahweh atampomkonya Sauli ufalme na kumpa jirani aliye bora kumliko(Zab. 13:13-14; 15:28). Wivu huu ulikua polepole kwa miaka ndani yake na kwa ghafla ukazinduka na wivu huu ukaelekezwa kwa Daudi “ nini anachoweza kupata zaidi ila Uflame”? aliuza Sauli (MST.8) kwa miaka bila shaka  alikuwa anangalia mridhi ambaye Mungu alisema atakuja. Sasa alikuwa na shaka kwamba ni Daudi kwani alikuwa mpendwa wa watu.

Sauli alianza kumwangalia Daudi kuanzia ile siku (mst.9) upendo aliokuwa nao kwa Daudi ukageuka na kuwa chuki kali. Kama vile woga wa kwamba Daudi atakuja kumridhi ulivyozidi kukua ndani ya akili yake, Sauli akawa mwenye hasira. Kesho yake akawa  na usumbufu. Daudi akacheza kinubi ili kujaribu kumtuliza, kwa Ghafla Sauli akachukua mkuki na kumrushia mara mbili ili amdhuru Daudi, lakini Daudi alikwepa(Mst.10-11).

SAULI ANAPANGA KIFO CHA DAUDI (1 Sam. 18:12-30)

Akivumilia vitisho vya maisha yake, Daudi alizidi kubaki katika ikulu ya Sauli, Hapo ndipo Sauli alipanga njama pale Wafilisti wangekuwa wauuaji wa Daudi. Alimpa Daudi Merabu bintiye mkuu awe mke wako kwa masharti kwamba atakuwa akipigana vita vya Yahweh. Akamtoa katika ikulu yake na kumpeleka vitani, na badala ya kuuliwa akawa mshindi- lakini harusi  aliyopanga Sauli kwa Daudi haikutimia. (mst.19)

Punde tu fursa nyingine ikajitokeza, akamwambia kwamba bintiye mdogo Michal alikuwa anampenda Daudi, Sauli kwa mara nyingine akapaga kifo cha Daudi. Sauli wakati huu angempa Daudi bintiye kwa masharti ya kuwa Daudi amletee mahari ya Ngovi 100 za wafilisti (Mst.20-25). Sauli alifikiria hili litafanya Daudi kuuwawa kwa mkono wa Wafilisti” (Mst.25) lakini Daudi alienda na kuwauwa Wafilisti 200 na kuleta mahari mara mbili ya ile mfalme alikuwa ameitisha na akamchukua Michal kama mke wake. (Mst.26-27)

Daudi sasa akawa mkwe wa mflame, lakini  zaidi ya hapo chochote alichofanya kilifanikiwa. Uadui wa Sauli haukuwa na mipaka na hata katika nyakati ngumu Daudi alizidi kukaa mtu mwenye busara kuliko watumisho wote wa Sauli; hivyo jina lake lilikuwa la dhamani. " (Mst.30)

Sauli alionyesha picha mbaya ya mtu amabye ni mwathirika wa kiburi chake mwenyewe kwani alikuwa amekataa kukubali uchanguzi wa Mungu. Alijua kwamba Mungu alikuwa pamoja na Daudi (Mst.12, 28), lakini alikataa kumpa heshima ya wito wake. Kwanini? Shetani wa majivuno alikuwa ameyapofusha macho yake, hivyo kwamba alikuwa mwathirika aiye na matumaina wa wivu, woga (Mst.29), hasira (MST.8) na ujinga.

ULINZI KUTOKA KWA JONATHANI (1 Sam. 19:1-7)

Jinsi Daudi alivyozidi kuwa maarufu ndio chuki ya Sauli ilivyozidi na tamaa yake ya kumwangamiza. Hata akamwambia Jonathani nia yake ambaye alimwambia Daudi na akaanza kumlinda (Mst.2-3).  Akawa anamtetea kwa mfalme na kumlinda kutokana na dhuluma za baba yake. Alitaka mateso dhidi ya Daudi kufikia mwisho na akamtaka babake kutoa kiapo mbele ya Daudi na Mungu kwamba Daudi hatauwawa (Mst.4-6). Hili lilikuwa tendo la huruma ambalo Jonathani alifanya  na lingeweza kumgahrimu nafasi mbele ya baba yake. Matendo yake yalionyesha kuelewa na upendo wa kweli. Hivyo Daudi alirudishwa kwenye ikulu na kuchukua nafasi alikuwa nayo hapo awali (MST.7).   

DAUDI ANATOROKEA KWA SAMWELI (1 Sam. 19:8-24)

Wakati huu wote hali ya Sauli ilizidi kuwa mbaya, wakati vita vilipozuka na Daudi akarudi na ushindi, mfalme hakuweza kuvumilia tena. Wakati huu alitaka kumdungilia Daudi kwa ukuta na mkuki wake, lakini Daudi akatoroka kutoka kwa ikuli yake. (Mst.8-10). Daudi alienda nyumbani lakini Michal alimshauri kuondoka mara moja. Alimsaidia Daudi kutorokea kupitia dirisha. Alikuwa mwanamke mwerevu na akatafuta njia ya kuficha kitu mfano wa Daudi kwa kitanda ili mjumbe wa kwanza atakapofika  atajifanya kwamba Daudi ni mgonjwa na yupo kitandani. Wakati wajumbe waliporudi kutoka kwa Sauli kumchukua Daudi kutoka kitandani alidai kwamba Daudi alikuwa akimtishia maisha yake na hivyo hakuwa na busi ila kumwacha aende. (Mst.11-17).

Wakati huo Daudi alitorokea kwa Samweli kwa kukata tamaa. Wakati Sauli alipojua alikokua alituma wajumbe kwenda kumchukua Daudi, lakini roho wa Mungu uliwageuza kutoka watekaji hadi manabii. Kwa mara tatu mkono wa Bwaba uliingilia kati na kusitisha mipango ya Sauli. Kisha yeye mwenyewe akaenda na jambo lile likamtokea. Akitabiri alifika mbele ya Samweli kule Nayothi katika Raman, ambapo alilala uchi mchana na usiku kucha” ishara dhahiri ya ujinga wa kusudi lake(Mst.18-24).

FARAJA KUTOKA KWA JONATHANI (1 Sam. 20)

Daudi alipata nafuu kidogo wakati Sauli alivyotabiri, nani angemgeukia? ni Jonathani tu?. Hivyo alirudi kwa Gibeah ambapo alimtafuta Jonathani. Kwa nini Sauli alitaka kumuuua aliuliza? Ni hapa  tabia ya ukarimu na unyenyekeve ya Jonathani inapoonekana, kwani hata sasa hakuwa tayari kuamini kwamba baba yake angevunja ahadi yake na kutimiza mpango wake wa kumwangamiza Daudi (Mst.1-3)

Marafiki hawa walikubaliana kumjarinu Sauli ili wajue kusudi lake. Sikukuu ya Mwezi mpya ambapo jamaa wa karibu walikuwa wamealikwa. Ilimbidi Daudi  kuhudhuria shehere hio iliyoandaliwa katika ikulu ya Sauli, lakini angemwomba ruhusa Jonathan kwa kisingizio cha kuweka sherehe ya familia yake Bethlehemu.  Angekaa kwenye uwanja mpaka pale angepokea ujumbe kutoka kwa Jonathani kumjulisha atoroke au abaki, ujumbe huu ungepitishwa kwa kurusha mishale karibu  au mbali na mwamba wa Ezeli (kumaanisha “ondoka”) ni dhahiri kwamba ushindi wa Daudi ulikubaliwa na Jonathani bila swali. Kile alichotaka kutoka kwa Daudi ni kuzidisha ukarimu wake kwake na kwa wanawe atakapokuwa Mflamena hii ikawa msingi wa agano kati yao (Mst.14-17).

Mpango huu ukaanza kutekelezwa. Kuanzia mwanzo wa maandiko kumerekodiwa kusudi la mauaji la Sauli (Mst.25-26). Siku ya pili utetezi wa Daudi na Jonathani ulimkasirisha babake “wewe mwana wa mwanamke muasi” akasema Saul “ si ninajua ya kwamba wewe amemteua mwana wa Jesse ili kunichanganya mimi na uchi wa mamamngu? Kwani kwa muda wote mwana wa Jesse atakapoishi ulimwenguni ufalme wako hautaanzishwa. Hivyo nenda umlete kwani ni lazima afe "(Mst.30-31).

Jonathani alijaribu kumsihi babake bila mafanikio. Sauli alikuwa na hasira nyingi kwamba alimrushia mkuki na Jonathani akaondoka akiwa na hasira akikataa chakula na akiwa na huzuni nyingi moyoni kwa sababu babake alikuwa amemdhalilisha Daudi (linganisha mst. 34.)

Asubuhi iliyofuata mshale wa Jonathani ulirushwa upade wa jiwe la “Kuondoka” an hapo Daudi akapewa ishara iliyopangwa ya kutoroka. Wakiwa wamejawa na majonzi warafiki wale wawili walitengana, wasiwahi onana tena isipokuwa kwa muda mfupi wakati Sauli alikuwa anamfuata Daudi na Jonathani alimtembelea kwa siri kumtia nguvu ndani ya Yahweh and kufanya upya agano lao. (23 :16-18).

Uaminifu wa Jonathani ulimfanya abaki kwa upande wa baba yake. Daudi sasa alikuwa mkimbizi nana aliomba makazi ajifiche waliokuwa wanamfuata. Akiwa uhamishoni Daudi aliamua kuendelea kumtumainia Mungu na hakuna kwa wakati  wowote angeinua mkono  kwa mtu aliyeteuliwa na Bwana.

MISINGI YA URAFIKI WAO WA KWELI

Baadae wakati Jonathani alipouliwa na Wafilisiti, Daudi alilalamika na kusema “upendo wako kwangu ulikuwa wa ajabu, kushinda upendo wa wanawake " (2 Sam. 1:26). Hii ilikuwa kwa sababu misingi ya urafiki wa kweli ni mfano wa upendo wa mambo ya Mungu. Marafiki hawa wawili walikuwa na jambo moja la kawaida- imani yao kuu kwa Mungu wa Israeli kumtumainia na kuwamini kwa kila jambo. Ni jambo hili lililovunja vikwazo vyote vya umri, utajiri, cheo kati yao na kuwafanya kitu “kimoja”

Kiini cha urafiki wa kweli ni sawa hadi lee. Marafiki wana nafasi kubwa katika masihs yetu na wanatushawishi kutenda mema au maovu. Tunapaswa kuchagua marafiki kama waandani wetu wa kweli. Wale ambao wanampenda na kumtii Bwana Yesu ndio marafiki na kama vile Jonathani na Daudi, hawatatutoroka wakati wakati wa matatizo. "Msifungwe nira pamoja na wasioamini" (2 Kor. 6:14).

MAFUNZO KWETU:

• Jonathani kama mrithi dhahiri angepoteza mengi kwa kukubali Daudi kuwa mridhi wa kiti cha enzi cha Israeli. Hata hivyo kwa hiari alikubali kusonga kando akiomba  uhifadhi wa wazawa wake, na haki ya kumtumikia Daudi yeye binafsi katika ufalme.
• Alikuwa mfano wa kuigwa wa upendo katika Kristo Yesu aliopongezwa kwa Wafilipi: " chochote kisifanyike kwa ajili ya ubinafsi au kujisufu, bali kwa unyenyekevu, tuwachukue wenzetu kama walio bora kutuliko sisi" (Flp 2:03).
• Upendo wa Jonathan ulionyesha fadhila ya uaminifu na matumaini, ukarimu, unyenyekevu na ujasiri (linganisha 1 Kor. 13:1-13).
• Licha ya tabia za  Sauli, Jonathan na Daudi walimheshimu kama mtu aliyeteuliwa na Mungu.
• Wivu usiokuwa na mipaka utachimba moyo wa mtu naye atakuea amezamwa kwa wivu kama vile Sauli alizama kwa wivu wake kwa Daudi (Mit. 6:34).
• Urafiki wetu anastahili kuwa na wale ambao wanamheshimu Mungu wa Israeli.

 

MAKTABA YA KUREJELEA:

"The Ways of Providence" (R. Roberts)—sura 15.

"The Story of the Bible" (H. P. Mansfield)—Tol. 3, Nam. 9

"The Man David" (H. Tennant)— kurasa 32-45

 

MASWALI YA AYA:

1. Kwa nini Sauli alimwonea wivu Daudi? Nini husababisha wivu na jinsi gani tunaweza shinda?
2. Elezea kwa kifupi matukio mawili ambapo Sauli alipanga kumuua Daudi.
3. Jinsi gani Jonathani alijaribu kumsaidia Daudi wakati baba yake alitaka kumuua?
4. Msingi wa urafiki wa kweli ni nini? Je, hii inaonekana kwa njia gani kati ya Daudi na Jonathani?
 

MASWALI YA INSHA:

1. Kwa nini Sauli alitaka kumuua Daudi? Alijaribu hili kwa jinsi gani?
2. Jinsi gani mfano wa Daudi na Jonathani unatusaidia kuchagua marafiki zetu?
3. Andika kuhusu utafiti wa tabia ya Jonathan.
4. Linganisha tabia za Jonathan na Sauli kama zinavyoonyeshwa katika kusudi lao kwa  Daudi.

 

 

Swahili Title
296. WIVU WA SAULI NA UPENDO WA JONATHANI
English files
Sub type
Sub sub type