CSSA 3-2-300 - GOD'S PROMISE TO DAVID

Swahili

300. AHADI YA MUNGU KWA DAUDI

"Lakini huruma yangu haitawahi mwondokea"

Ahadi ambayo Mungu alifanya kwa Daudi ni ya tatu na ya mwisho kubwa ya ahadi ya ujio wa mshindi. Ahadi ya kwanza kuu “Mbegu ya Ahadi” ilifanywa katika shamba la Edeni na ilihushisha uzao wa mwanamke ambao utashinda kifo (Mwa. 3:15). Ahadi ya pili ilifanywa kwa Ibrahimu na ilihusisha Nchi ya Israeli kuridhiwa na wale walio kwa Kristu(Mwa. 12:1-3; 13:14-17; 22:16-18;. Gal 3:16 , 26-29). Ya tatu inahusiana kiti cha enzi, Ufalme na kuja kwa mteuliwa wa Mungu.

Umuhiwa wa ahadi hizi unaweza kuonekana kutokana na kwamba mstari wa kwanza katika Agano jipya unamuunganisha Yesu Kristo na mababu zake kama Ibrahimu na Daudi (Mat. 01:01). Wakati wa kuzaliwa kwake alidhibitishwa kuwa wa uzao wa Ibrahimu na Daudi (Lu. 1:32-33, 54-55, 69-73). Kifo chake hivyo hivyo, kilidhibisha “ Ahadi walizopewa mababu zake” (Rum. 15:08). Ahadi zilitimizwa katika Kristo na zikawa misingi ya habari njema iliohubiriwa na mitume (Mat. 2:29-31; 3:13, 25-26; 13:22-36; 26:6-7, nk).

Lengo letu litakuwa kuelewa ahadi kubwa ya Mungu kwa Daudi na kuona jinsi gani inahusiana na Kristo na wokovu wetu.

2 Samweli 7

DAUDI ANATAMANI KUMJENGEA MUNGU NYUMBA (2 Sam. 7:1-7)

Mungu alikuwa amewaambia waIsraeli kwamba wakati atakuwa amewasaidia kuangamiza maadui zao wote, kutakuweko na mahali patakapochaguliwa na Yeye ambapo “Jina lake litakapo kaa" (Kum. 12:10-11). Wakati huu ulikuwa umefika kwani Daudi alikuwa amekaa katika nyumba ya mierezi adui zake wakiwa chini ya miguu yake(2 Sam. 7:01). Alijua kwamba kuna jambo lisilokuwa sawa kwani Agano la Bwana likikuwa katika hema, ilhali Mflame alikuwa anaishi kwenye nyumba ya mierezi. Daudi hakufurahishwa na hili. Hivyo akamwita Nathani nabii na kumjulisha nia yake kuhusu agano. Nathan akamjibu “tenda kile kilicho moyoni mwako, kwani Bwana yu nawe” (Mst.3).

Lakini jibu la Nathani halikuwa sawa kwani lilikosa idhini kamili  ya Mungu. Usiku huo kwa ufunuo wa Mungu Daudi alipata jibu na kuelezwa nyumba kubwa na ya kupendeza kuliko vile Daudi alivyodhania. Daudi alitumainia kumjengea Mungu nyumba ya miti na mawe, lakini alimfunulia kwamba angemjengea Daudi nyumba sio ya miti, lakini ya watu- yake itakuwa nyumba ya kifalme. Hii ingekuwa zaidi ya ile binadamu yoyete angeweza kujenga.

Daudi alisikiliza, akishangazwa na kuguswa na maneno ambayo Nathani alirudia  “nani atanijengea nyumba ambayo nitaishi? (mst. 5).  Labda kwa mara ya kwanza Daudi alielewa ukuu wa jambo ambalo alihitajika kufanya.

Je binadamu anaweza kumjengea Mungu nyumba? Je Mungu anweza kuishi ndani yake? Kwa utaratibu Daudi aliongozwa kwa njia ya kuelewa. "Tangu wakati niliwatoa watoto wa Israeli kutoka Misri, hadi sasa (sijakaa kwa nyumba yoyote) lakini nimetembea katika hema na Maskani"(Mst.6-7). Mungu kuishi katika hema ni somo muhimu kwetu. Mungu bado hakuweza kuishi na binadamu. Hata Solomoni aliona upungufu wa hekalu alilomjengea Mungu(1 Fal. 8:27, Mat. 7:48).Mungu anaishi katika nyoyo zinazonyenyekea na kuogopa neno lake (Isa. 66:1-2; 57:15;. Efe 3:17; 04:06; 2 Kor. 6:16.), wale ambao ni sehemu ya jiwe la msingi ambalo ni Yesu Kristo amblo limewekwa na Mungu (Isa. 28:16;. Efe 2:20;. 1 Kor. 3:11;. Zab. 118:22).

KAZI YA MUNGU (2 Sam. 7:8-16)

Daudi alipokea ujumbe huu na kuelewa kwa undani. Mungu alimkumbusha Daudi kwamba kuinuliwa kwake kutoka mchungaji hadi kuwa mflame ullikuwa chini ya mkono wake na kwamba  angeendelea kumwinua na kufanya jina lake kuu. Kazi hii yote ingekuwa kazi ya Mungu; “Mimi nilikuchukua kutoka kwa zizi la mbuzi, Ilikuwa ni mimi Nitayechagua mahali pa watu wangu katika  Israeli.....Pia Bwana alimwambia kwamba Nitakujengea nyumba...na kuweka uzao wako.....Nitaanzisha Ufalme wako. Atajenga nyumba kwa jina langu, nami Nitakuwa baba yako... . "(Mst.8-16).

Mahali pa mwisho pa kupumzika pa Jina la Mungu, nyumba atakayoishi, itajengwa na mwana wa nyumba ya Daudi ambaye atakuwa Mwana wa Mungu. Hata nyumba zilizojengwa katika nyakati za wafalme hazitajengwa na Daudi kwa sababu alikuwa amemwaga damu nyingi, kama ilivyoelezwa katika (1 Nyak. 22:8-10). Ni kweli kwamba hekalu ilijengwa na Solomoni, ambaye jina lake lilimaanisha "Amani", hivyo kuashiria kazi ya Messia na utawala wa amani.

MAELEZO YA AHADI (2 Sam. 7:10-16)

Kuna mambo sita katika ahadi ambayo ni muhimu kwa injili: -

1) WaIsraeli wawe na makazi katika ardhi na waishi na amani na mataifa yote: "Nitachagua mahali kwa watu wangu Israeli, ambapo wataishi katika nafasi yao wenyewe, bila kuondoka, wala kuteswa na watu wauovu tena"(Mst.10). Hili bado halijatimia. Manabii, hata hivyo, wanaonyesha kwamba masharti haya yatatimia wakati Kristo Mfalme atatawala Sayuni (linganisha Eze 34:28-29;. Amo. 9:14-15;. Sef 3:15; Yer. 33:11, 14-15). .
2) Uzao ulioahidiwa utakuwa wa mwili na damu ya Daudi -Mwana wa Mtu-na hivyo  wakukufa: "Mimi nitaanzisha uzao wako baada yako, ambao utatoka ndani ya mwili wako" (Mst.12).
3) Uzao huu utajenga Nyumba kwa jina la Mungu: "atajenga nyumba kwa jina langu" (Mst.13). Nyumba mbili zinajulikana kama: -
a) Nyumba halisi - Hekalu la Ezekieli, "nyumba ya sala kwa mataifa yote" itajengwa Yerusalemu (Isa. 2:2, 3;.. Mk. 11:17; Zak. 14:16; 06:12 -13).
b) Nyumba ya kiroho” iliyojaa watu "katika Kristo" (Ebr. 3:1-6;. Efe 2:19-22;. 1 Pet. 2:05;. 2 Kor. 6:16).
4) Mungu (kama vile Daudi) kuwa Baba  yake-Yeye atakuwa Mwana wa Mungu: "Mimi nitakuwa baba yake, naye atakuwa mwanangu" (Mst.14). Hii ni hulka kuu ya Yesu Messiah. Kwa hio alikuwa amefaa kuwa Mwokozi Asiye na dhambi (linganisha Lk. 1:32-35;. Isa 7:14; 9:6-7; Yohana 1:14, 49; 3:16).
5) Huruma ya Mungu kubaki kwa uzao wa Daudi licha ya uovu wa jamaa zake wengi, ambao waliadhibiwa ipasavyo (kwa mfano Solomon katika 1 Fal. 11:11-14): "Kama atatenda uovu, nitamwadhibu kwa fimbo yakibinadamu, na kwa mapigo ya wana wa binadamu, lakini fadhili zangu hazitamwondokea, kama nilivyomwondolea Sauli "(Mst.14-15 linganisha Zab. 89:28-33; 132:12 .. sehemu ambayo  ahadi hii  inaelezwa zaidi;. Yer 17:24-27).
6) Enzi ya Daudi kuanzishwa milele mbele yake wakati wa kurudi kwa Kristo: "Na nyumba yako, na ufalme wako utaanzishwa na kudumu milele: nacho kiti chako cha enzi kitadumu milele" (Mst.16). Marejesho ya Ufalme wa Israeli pamoja na Kristo, mwana wa Daudi, kama Mflame ni mawazo ya manabii na mada ya matumaini ya Israeli (linganisha Isa 9:6-7;. 11:1-5, 10 ., Yer 33:14-26; Eze 37:25-27; Amo. 9:11-15; Lk. 1:30-33; Mat. 19:28; Mat. 1:06; 2:30; 3:19 - 21; 13:23-36; 15:16; 28:20; n.k)

KUTIMIZWA KWA AHADI

Uzao wa ahadi ni upi? Kutoka kwa yale yaliosemwa ni dhahiri kwamba Yesu Kristo ni Mwana wa Daudi ambaye kupitia kwake ahadi itatimizwa, Hata hivyo, ahadi hairejelei uzao wa Daudi waliokalia kiti cha Enzi, hasa Solomon. Angalia jinsi suala linatumika kumrejelea Solomon katika 1 Fal. 1:48; 5:05; 8:20; 9:4-6. Ahadi likuwa na masharti kama uasi ungetokea. Solomoni aliasi, na akadhalalisha ahadi na hivyo “aliadhibiwa na fimbo ya binadamu" (2 Sam 7:14;. 1 Fal. 11:11-14). Sababu zifuatazo pia zinaonyesha ni kwa nini Solomon hakutiza ahadi ila ni kwa  kifupi-

  1. Kama ilitimizwa na Solomoni, hakuna kutajwa zaidi na Mungu katika kutimiza baada ya kifo chake, yaani.
    • Miaka 250 baada ya kifo chake - Amo. 9:11;
    • Miaka 450 baadaye - Yer. 33:14-26;
    • Miaka 500 baadaye - Zek. 12:6-8;
    • Miaka 1000 baadaye - Lk. 1:32-33.

Kwa hiyo ni lazima itaje mtukwa muda mwingine baadae. Maneno ya malaika kwa Maria yalioandikwa katika Luka 1 yanaonyesha kwamba inataja Yesu Kristo.

  1. 2 Sam. 7:14  inanukuliwa na kutumika kwa Yesu Kristo katika Ebr. 1:05
  2. Sedekia alikuwa mfalme wa mwisho kutawala kwa kiti cha Daudi. Lakini kwa sababu ya uovu wake alikataliwa na Mungu an akatangaza kwamba Ufalme utakuwa bila mtu “Mpaka pale atakapokuja yule anayestahili” (Eze. 21:25-27).

Yesu alidai haki hii (Yoh. 18:36-37) na Peter na Paulo wote walimtangaza kuwa mrithi halali kwa ufufuo (Mat. 2:29-32; 13:22, 23;. Rum 1:3-4).


MAFUNDISHO YA MSINGI YA MKATABA WA DAUDI WA UFUFUO

 Kulikuwa na kutodhihirika kwa ahadi. Hili linaweza keulezewa ka misingi ya ufufuo. Mungu alitoa ahadi akijua kwamba ufufuo utakuwa muhimu katika kutimizwa kwa agano (kama vile alivyotoa ahadi kwa Ibrahimu amazo zilihitaji ufufuo)

  1. Mfalme aliyeahidiwa agekuwa mwana wa Daudi na hivyo binadamu wa wili wa kukufa lakini ufalme wake ungedumu milele. Kwa Jinsi gani? Kupitia ufufuo. Daudi aliongea vilivyo katika Zab. 16:8-11. Petro na Paulo wote walielezea kwamba Zaburi hii inatufunza ufufuo wa kristo (Mat. 2:24-31; 13:35-37).
  2. Daudi anaambiwa kwamba atakufa (“alale na baba zake”), lakini pia anaambiwa kwamba mwanawe atatawala milele “kabla yake” ama katika uwepo wake. Swali linaibuka-kiaje? 2Licha ya kufahamu kwamba uzao wake utakuwa mtu aliyefufuka, alielewa kwamba, yeye pia itabidi afufuliwe kama angekuwa shahidi wa ufalme wa Kristo “ Wewe....utaniharakisha mimi tena, na kunifufua tena kutoka chini ya ardhi. "(Zab. 71:20-21).

MUHURI WA KIAPO CHA MUNGU.

Kipengele kingine muhimu cha ahadi ya kiapo ya Daudi ni kiapo cha Mungu kudhihirisha: "Bwana ameapa kwa ukweli kwa Daudi; yeye hatogeuka kwa ukweli huo" (Zab. 132:11). Kama agano la Ibrahimu, ahadi kwa Daudi haingevunjwa wala kubadilika (Zab. 89:3-4, 34-36;. Yer. 33:20-26;. Linganisha Lk. 1:69-74).

 

ADHARI ZA AHADI YA DAUDI (2 Sam. 7:18-29)

Nathani akaondoka, kazi yake ikiwa imekamilika, Daudi akaamka na kwenda hadi pale Agano lilikuwa na kufunga pazia zake. Akakaa  kwa unyenyekevu mbele ya Mungu, akishangazwa na maajabu na neema ambazo Mungu alikuwa amemwahidi. Hakuwa tu mfalme wa nyumba yake aliyetafuta baraka kwa Agano la Mungu kwa kuliweka katika mako ya kudumu Yerusalemu. Alijirudia and akaanza kuomba "Mimi ni nani, Ee Bwana Mungu, na ni ipi nyumba yangu, kwanini umenifikisha hadi hapa? Na hili ni jambo dogo mbele ya macho yako, ewe Bwana Mungu pia umenena kuhusu nyumba ya mrumisho wako kwa muda mrefu ujao"(Mst.18-19).

Mungu Mkuu alikuwa amenena na Daudi na kumfanya atetemeke kwa neema aliyopokea. Alipotafakari yule atakayepokea ahadi hii na Mwana wa Mungu “ni mwana wa Binadamu” “Sheria ya binadamu”) baadaye alitambua kwamba Mwanawe atakuwa mkuu kumliko, kwani alimwita “Bwana wangu” Zab. 110:1;. Mat. 22:44). Mwana wa Dausi alikuwa Bwana wa Daudi kwani alikuwa Mwana wa Mungu.

Daudi aliendelea na kumshukuru na kumtukuza Mungu kwa ufufuo Wake (Mst.21-22). Kisha akaongea kuhusu ukuu wa taifa la Israeli, lililokombolewa na Mungu (Mst.23-24). Aliomba kwamba jina la Bwana litukuzwe kupitia kutekelezwa kwa ahadi ilionywa juu ya nyumba yake. (Mst.25-26). Maneno yake ya mwisho yaliomba kwamba baraka bila shaka ishuke kwa nyumba yake(Mst.29).

MAFUNZO KWETU:

• Kuelewa sahihi kwa ahadi za Daudi ni muhimu sana kwa Injili ya Ufalme kwani hii ndio mising ya  Mkataba wa Daudi.
• Daudi alihisi kwamba anatakiwa kufanya kitu kwa ajili ya Mungu ili kuwezesha ufalme kutulia, lakini Mungu alionyesha kwamba kazi yoyote kwa ajili ya mema ni kazi ambayo Mungu tayari amekwisha andaa.
• Daudi alinyenyekea alipogundua kuwa Mungu alikuwa amefunga  "nyumba" yake katika mpango wa milele. Hivyo pia, wote ambao ni wa familia katika Ukweli wamepata upendeleo wa hali ya juu.
• Mungu ametualika kwa "nyumba yake" kushiriki katika kiti cha enzi na Ufalme wa Daudi.

 

MAKTABA YA KUREJELEA:

"The Ways of Providence" (R. Roberts)—Sura. 17

"Elpis Israel" (J. Thomas)—Kur. 302-307

"Christendom Astray" (R. Roberts)—Somo 12

"The Story of the Bible" (H. P. Mansfield)—Tol. 4, Nam. 2

"The Man David" (H. Tennant)—Kur. 119-124

"God's Way" (J. Carter)—Sura. 6

"First Principles Bible Marking Course" (C.S.S.S.)—Kur. 63-66

MASWALI YA AYA:

1) Mungu alimwambia Daudi kwamba atamjengea nyumba. Elezea kile Mungu alimaanisha.
2) Ni hali ipi iliyokuwepo ambayo ilisababisha Mungu kumwahidi Daudi nyumba?
3) Nini Daudi alifanya na kusema wakati ahadi kuu ya nyumba ilifunuliwa kwake?
4) Mkataba wa Daudi haurejelei Solomoni pekee. Toa sababu ya kauli hii.

MASWALI YA INSHA:

1) Ni somo gani kuu ambalo Daudi anajifunza wakati anatoa mapendekezo ya kujenga nyumba ya Mungu?
2) Ni kwa jinsi gani agano la Daudi linahusiana na injili?
3) Elezea jinsi ufufuo ni muhimu katika kutimiza Agano la Daudi.
4) Eleza ni jinsi gani agano lililofanywa kwa Daudi linarejelea Yesu Kristo.
5) Orodhesha nyanja nne kuu za ahadi kwa Daudi na uelezee kutimia kwake.

 

 

Swahili Title
300. AHADI YA MUNGU KWA DAUDI
English files
Sub type
Sub sub type