302. DHAMBI YA DAUDI NA MATOKEO KWETU
""Jambo ambalo Daudi alikuwa amefanya halikumpendeza Bwana"
Somo hili linatufanya kuelewa kwamba kuna adui mkubwa zaidi ndani ya nafsi ya binadamu kuliko adui wote wa nje. Daudi alikuwa amebarikiwa sana na Mungu na utukufu wake ulizidi kwa kila ushindi wa adui kwa mkono wake. Hata akiwa mkuu hivyo mtu ambaye zamani angesema âNimezishika njia za Bwana, na sijatoka kwa Munguâ, kulikuwa na adui waliojificha. Tamaa ya ndani na msukumo wa kawaida wa dhambi, unaokuja wakati wa mapumziko wakati tunaruhusu akili kutulia na kuwacha kufukiria yale Neno la Mungu linatuamuru. Somo la dhambi ya Daudi ni "Yule afikiriae amesimama ajihadhari asije kuanguka".
Lengo letu katika somo hili ni kuona majanga makuu ambayo dhambi huleta katika maisha yetu na mtazamo ambao Mungu hutizama dhambi.
2 Samweli 11 na 12
DHAMBI YA DAUDI (2 Samweli 11:1-15)
Pamoja na mabadiliko ya msimu, jeshi la Israeli chini ya Yoabu likarudi kumaliza vita na Waamoni. Daudi, ambaye sasa alikuwa anakaribia miaka 50, alibaki nyumbani. Akiwa amepumzika alasiri, alienda hadi kwa paa. Huu ulikuwa wakati mzuri kupumzika, akiwa kwa umbali wa vita pahali Uria alipigana na jeshi la Israeli. Bathsheba, mke mzuri wa Uria, alikuwa akioga katika ua lake mbele ya macho ya mfalme. Daudi aliadhiriwa na urembo wake na kutuma mpelelezi akamchunguze. Kuitwa na mfalme ni jambo la kufurahisha; na kukataa wito na tamaa ya mfalme kulihitaji uamuzi imara ambao Bathsheba alishidwa kuonyesha.
Daudi hakuwa na sifa mbaya na tabia yake ilikuwa imeonekana kama ya heshima katika ufalme wake; lakini sasa kupitia tamaa alikuwa anachukua mkondo wa janga âYule anayezini hana akili; yule afanyaye hivi anajiharibu mwenyewe, atapata majeraha na kukosa heshimaâ na aibu yake haitaondoka kamwe. (Mit. 6: 32-33).
DAUDI ANAFICHA DHAMBI. (2 Samweli 11:6-25).
Dhambi ya Daudi ilikuwa ni dhambi wengi wetu wanaweza kuelewa. Tunaweza hata hivyo elewa umbali ambao tunaenda kuficha dhambi. Lakini matendo ya Daudi yalifuata mfumo huu wa mwili kuanzia kwa Adamu, kwa kutotaka kuleta dhambi kwa uwazi. Isitoshe Daudi alikuwa na nguvu ya kutimiza chochote alichotaka.
Muda si mrefu baada ya tukio hili, Daudi alikumbana na ujumbe wa Bathsheba asio utarajia wala kuutaka â Mimi ni mjamzitoâ. Daudi alitaka kuficha kuhusika kwake na kila jaribio lake lilikatisha tamaa kwa kila mara hakufanikiwa.
Uria alitolewa vitani na Daudi akamsihi apumzike nyumbani. Daudi alielezwa kwamba Uria amekataa na akampa Daudi sababu zake. âSaduku la Agano, na Israeli na Yuda ziko katika hema; na Yoabu bwana wangu na watumishi wa Mungu wangu wako vitani; Je nitaenda nyumbani, kula na kunywa na kulala na mke wangu? Kama uishivyo na kama moyo wangu uishivyo, sitafanya jambo kama hilo?â Maneno hayo ya uadilifu na utiifu yalisababisha msukumo wa dhamira mbaya ndani ya nafsi ya Daudi. Uria alitiwa kizuizini siku iliofuata na ingawa alikuwa amepewa chakula na mvinyo na Daudi, Uria alikataa kwenda nyumbani kwa mkewe Bathsheba.
Daudi alikasirishwa na hali ya kujinyima ya Uria na akatafuta njia nyingine ya kujiondolea matokea ya dhambi. Uria akatumwa kwa Yaobu akiwa na ujumbe ambao ulikuwa ni kibali chake cha kifo â Mweke Uriah kwenye mstari wa mbele pale vita vilivyochacha, kisha umwondokee ndio apate kuuawa. Dhambi moja hufuatiwa na nyingine, na kama dhambi zote Daudi hangeweza kujiondoa katika dhambi bila kujuta. Tatu kati ya amri kumi zinahusu kumpenda jirani yako ilikuwa imevunjwa âUsimtamani mke wa jirani yako ... Usizini na Usiue" (Kut. 20: 13-17). Akawa na dhambi tatu jinsi siku zilivyosonga, Daudi alikuwa chini ya hukumu ya kifo âWazinifu wote watauwawaâ (Law. 20:10.).
Njama ovu ya kumwacha Uria katika mahali ambapo pangesababisha kifo chake ilitekelezwa. Mbinu ambayo kwa kawaida Daudi angeikashifu. Baada ya kuelezwa kwamba Daudi Uria alikuwa ameuawa na bada ya muda wa maombolezi ya mumewe Bathsheba alitwa na akawa mke wa Daudi. Kwa nje hakukuonekana kama kulikuwa na mpango kwa yale yaliotokea. Lakini dhambi ya Daudi ilikuwa hajaikiri na mazao yake yenye giza yalikuwa mbele yake â lakini jambo ambalo Daudi alikuwa amefanya halikumpendeza Munguâ (2 Sam.11.27)
KUKIRI NA MSAMAHA (2 Samweli 12:1-14)
Miezi kadhaa baadaye, Nathani, kuhani alikuja kwa Daudi. Aliongea kwa mafumbo kuhusu mtu tajiri âAliye na mifugo wengiâ ambaye alikataa kuchukua kondoo kutoka kwa mifugo wake kama chakula kwa msafiri ambaye alikuwa amefika nyumbani kwake, lakini alichukua kondoo mmoja wa mtu maskini. Hali ya kawaida ya haki ya Daudi iliamka. Akatangaza hukumu kwa kitedo hiki kiovu, âMtu yule amefanya kitendo hiki lazima afe; na kulipa mara nne....ââ lakini kwa kusema hivyo alikuwa amejihukumu yeye mwenyewe kwani Nathani alimjibu â wewe ndiye mtu huyoâ Maneno haya Daudi hakuyatarajia na yalidunga moyo wa Daudi.
Daudi aliadhirika. Nathani alimwelezea yote, na hata kutumia maneno yale Samweli alikuwa amemwambia Sauli â"Kwa nini umedharau amri ya Bwana?" (2 Sam.12: 9; 1 Sam. 15:23) kwa sababu alikuwa ametumia upanga, aliambiwa kwamba upanga hautaondoka katika nyumba yake, kwani alikuwa amechukua mke wa mwingine, hivyo jirani zake watachukua wake zake. Majaribio ya Daudi kuficha dhambi yalikuwa bure. Neno,ambalo linaishi na lenye Nguvu (Ebr. 4:12, Diagloti),lilikuwa limefumbua âfikra na nia ya roho yakeâ na kumwacha na aibu â ulifanya hivi kwa siriâ akasema Nathani. Daudi alikuwa ametenda kitendo kama Mungu hakuwepo na kwa sababu hii adhabu yake itakuwa wazi.
Hapakuwa na kusita kwa jibu la Daudi, hakutoa sababu wala kuomba adhabu ndogo, hakumlaumu Bathsheba; alijibu; â Nimetenda dhambi dhidi ya Munguâ. Kukiri kwa Daudi kulileta majibu ya haraka kutoka kwa Nathani; âBwana amekuondolea dhambi; hivyo hutakufaâ lakini hata kwa msamaha, kutakuwa na matokeo. Muda wa dhambi ungeleta miaka ya machungu- kama ukumbusho wa udhaifu na mahitaji ya binadamu. Daudi alibadilika kuanzia hio siku. Hakuweza kutoa hukumu kwa wengine hata kama walikuwa na makosa. Ilibidi aishi kwa kukemewa na watu kama Yoabu na Shimei na kuwacha mambo katika mikono ya Bwana.
Nathani alimwonyesha Daudi matukio ya matendo yake â kwa sababu ya matukio yako umewapa adui nafasi ya kumdharau Mungu, mtoto atakayezaliwa atakufa.â Kwa sababu heshima ya bwana imedharauliwa, Daudi lazima angelipa kwa njia ya kweli kwani mtoto ambaye angezaliwa angekufa, Kifo kilifuatia kifo.
MSAMAHA KWA NEEMA (Zaburi 32 and 51)
Msamaha wa Mungu wa Daudi una somo kuu. Hakukuwa na kitu Daudi angefanya, hakuna dhabihu angetoa, kubadilisha adhabu ya kifo kulingana na sheria ya Musa.Hata hivyo aliokolewa kutoka kwa kifo. Katika hili kuna matumaini kwa watu walio na dhambi- kama watatubu. Wokovu sio kazi ambayo wanadamu wanapaswa kujivunia, lakini ni kwa neema kwa anayetubu na aliye mwaminifu (Rum.3: 26-28; Efe. 2: 8.). âDaudi pia anaelezea kubarikiwa kwa mtu yule, ambaye Mungu amempa uadilifu bila matendo, akisena, âWamebarikiwa waliosamehewa makosa yao ambao makosa yao yamefutwa. Heri ni mtu yule ambaye Bwana hamhesabii dhambi "(Rum 4: 6-8.) Maneno haya ya Daudi, yamenukuliwa kutoka Zaburi 32 ambayo ilikuwa imeandikwa kuhusu tukio hili (mst.1-2) Daudi anaongea kuhusu dhiki iliokuwa ndani yake, wakati alificha dhambi yake na âKukaa kimyaâ (Mst.3-4), na hali ya radhi ilioletwa na kukiri na msamaha (Mst.5).
Zaburi 51 iliandikwa "wakati Nathani alikuja kwake", kama vile chapa inatuarifu. Katika Zaburi hii roho ya Daudi inakosa ile hali ya kujiamini ilionekana katika zaburi ya hapo awali (kwa mfano Zab. 139:. 23-24), lakini yeye anatubu udhaifu na haja yake ya kutakaswa na Mungu. Anatangaza kwamba dhabihu haina dhamani, kwani"Dhabihu za Mungu ni roho iliyovunjika". Aidha, anawashauri wenye dhambi (hakuna asiyetenda dhambi) kufuata mfano wake na kutambua kwamba âKuna msamaha kwa Mungu ili apate kuogopwaâ-"Ndipo mimi nitawafundisha wakosaji njia zako; na wenye dhambi watageuzwa kwako "(Zab. 51:13; linganisha Zab. 130: 4).
MTOTO ANAKUFA (2 Samweli 12:15-23).
Daudi alikuwa ameambiwa kwamba mtoto wa Bathsheba angekufa kama matokeo yake kuwapa adui wa Bwana nafasi ya kumdharau. Ukiangalia haya kwa kina hili lilikuwa tendo la huruma kwa Daudi, kwani kama mtoto yule angeishi basi ingekuwa kumbusho la kila mara, mfano uishio wa dhambi ya Daudi. Hata hivyo Daudi alisujudu na kufunga ili apate kubadili hukumu ya Mungu ya kifo. Kilio cha watumishi wake kumfanya ale chakula hakukisikiza. Na Baada ya siku saba mtoto akafa, bila kutahiriwa ama kupewa jina. Hakuingia katika agano la watu na dhambi ya Daudi ilivyosahaulika pia yeye akasahaulika.
Majonzi juu ya majonzi ndivyo alivyokuwa nayo Bathsheba. Lakini jinsi muda ulivyosonga ndoa yao ilichukua mkondo wa furaha. Matumaini yakachipuka tena kwa ahadi ya mtoto mwengine. Kama vile Nathani alivyotokea wakati wa kuzaliwa kwa mtoto wa kwanza pia akatokea tena wakati wa kuzaliwa kwa mtoto wa pili. Alikuja na ujumbe mwingine kutoka kwa Bwana, dawa ya uchungu na woga, ishara ya baraka ya Bwana kurejeshwa. Nathani alimwita mtoto yule wa Kiume âJedidaâ kumaanisha âMpendwa wa Bwanaâ na kumbukumbu inaonyesha alifanya hivyo âkwa ajili ya Bwana.â Wazazi wake walimwita âmwenye Amaniâ âSulemani. Katika kumpa jina mtoto kulikuwa na ahadi ya mtoto mwingine, yule ambaye atakuwa amekuja âkwa ajili ya Bwanaâ kamili, âKijana Mpendwaâ âMwenye Amaniâ naye in Bwana wetu Yesu Kristo. Bathsheba akafarijika na Daudi akahisi kwamba Mungu alikuwa amemrudishia neema.
MATOKEO YA DHAMBI YA DAUDI
Ingawa Daudi alikuwa amesamehewa, nafasi ya kubadilika ilikuwa imepita na Maisha ya Daudi hayangekuwa kama kawaida kuanzia wakati ule. Kwa njia nyingi Daudi angekuwa mtu mkuu zaidi. Furaha, ushirika na ujasiri wa miaka ya hapo awali haukuwepo. Yoab alikuwa ameona udahifu wa Daudi. Kwa hivyo Daudi angekuwa chini ya nguvu zake. Maneno yake kwa Daudi akimwita kwenda kuchukua mji wa Raba, mji wenye kumbukumbu za machungu, ili auchukue na ku upa jina lake, hii ilionyesha kukosa kwa heshima inayostahili kuwepo kati ya kamanda na Mfalme (2 Sam.12:. 27- 28). Familia ya Daudi na wale waliouzunguka ufalme na pia wengine walioko mbali walio-ona mfalme akichukua mke wa mume mwingine katika mazingira yaliyokuwa ya kutatanisha, hili liliwapa kibali cha kufanya hivyo. Familia yake iliadhirika sana. Baadhi ya vijana wake walikuwa wameshakomaa na tabia zao zilihitaji kuangaliwa, lakini baba yao alikuwa hawezi kuwaangalia tena. Kifo cha mtoto wa Bathsheba kilifuatiwa na vifo vya wana wa Daudi watatu. Muasi Amnon aliangamia kupitia upanga wa Absalom aliyekuwa na kiburi na muasi (2 Sam.13:. 28-29). Naye akaangamizwa na Yoabu (2 Sam. 18:14). Baadaye Adom-ja yule mtundu, ndunguye absalomu akauawa na upanga wa haki wa Sulemani (1 Fal. 2:25). Ilikuwa ni kupitia kwa Daudi ambapo alirejesha mwana-kondoo aliyemchukua mara nne (2 Sam.12: 6; linganisha Kut. 22:1.).Bwana alikuwa amesema âUpanga hautaondoka nyumbani kwakoâ
MAFUNZO KWETU
- Dhambi ni ya muda mfupi, inaweza toa radhi ya muda mfupi lakini matokeo yake maovu yanadumu na yana machungu.
- Tunaishi katika dunia ambayo majaribio yanajitokeza kila mahali. Wana wa Mungu lazima wawe macho na kutambua matokeo ya kujihusisha na dhambi kama ilivyoelezwa katika hadithi ya Daudi na Bathsheba.
- Kumbukumbu yenye uchungu ilibaki katika fikra za Daudi na Bathsheba na fikra hizi hazikutolewa hata baada ya kupokea msamaha. Msamaha unaondoa matokeo ya milele, lakini Mungu huleta adhabu ya muda mfupi kwa mtenda dhambi ili yawe funzo la kujitakasa.
- Dhambi hutia madoa, na kutia kovu maisha ya mtenda dhambi na hukwamilia kwenye kisigino chake daima.
âJiepusheni na usheratiâ âWasherati......na wanaozini hawataridhi ufalme wa Munguâ (1 Kor. 6:18, 9-10).
MAKTABA YA KUREJELEA:
"The Man David" (H. Tennant)âSura 7
"The Story of the Bible" (H.P. Mansfield)âTol. 4, Nam. 3
"The Ways of Providence" (R, Roberts)âSura 17
MASWALI YA AYA:
- Kwa nini Daudi alisamehewa dhambi yake na Bathsheba?
- Jinsi gani dhambi ya Daudi iliadhiri familia yake?
- Ni amri gani katika zile kumi ambazo Daudi alivunja katika matukio yaliyozunguka dhambi yake na Bathsheba? Je, hili linatufundisha nini sisi?
-
Ni masomo gani Daudi anataka tuelewa katika Zaburi 32 na 51 ambayo aliandika baada ya dhambi yake na Bathsheba?
MASWALI YA INSHA:
- Eleza jinsi Daudi alimuua Uria baada ya dhambi yake na Bathsheba na jinsi Nathani yule nabii aligundua uovu wa vitendo vya Daudi.
- Jinsi gani dhambi ya Daudi ilimuadhiri yeye na familia yake? Ni fundisho gani kuhusu dhambi tunajifunza kutokana na hili?
- Ni masomo gani tunaweza kujifunza kutoka kwa dhambi ya Daudi na Bethsheba?