308. KUGAWANYIKA KWA UFALME
"Hivyo Israeli wakaasi dhidi ya nyumba ya Daudi hadi leo"
Dhambi ya Sulemani ilikuwa ya kuleta mateso mengi katika taifa. Upumbavu huu ulileta mgawanyiko na uadui ambao unaweza kuponywa wakati Yesu atakaporudi (Eze.37:22). Hilo lililetwa na mtu aliyewacha alama ya uovu katika historia ya Israeli na kujulikana kama mtu âaliyefanya Israeli kutenda dhambiâ (1 Fal. 14:16). Jina lake lilikuwa Yeroboamu.
Lengo la somo hilo ni kuona majanga makuu yanayotokea wakati Mungu anasahaulika katika Mioyo na Akili za binadamu.
1 Wafalme 11: 26-43; 12
MTU YEROBOAMU (1 Wafalme 11:26-28)
Yeroboamu alikuwa mtu mwenye uwezo na ushawishi wa kutosha. Akiwa bado mdogo, Sulemani alitambua dhamani yake na kumweka kama msimamizi wa wafanyikazi wake kutoka Ephraimu waliotengeneza na kufanya ukarabati wa Yerusalemu. Maneno ya Zaburi 22:29 yanatumika kwake âTizama mtu mwenye bidii katika kazi yake? Atasimama mbele ya wafalme: hatasimama mbele ya binadamu wakatiliâ kwa hakika, Yeroboamu alikuwa awe mfalme.
UNABII WA AHIYA (1 Wafalme 11:29-40)
Nabii Ahiya, alikuwa ameagizwa na Mungu kukutana na Yeroboamu katika safari yake ya Yerusalemu. Ahiya alikuwa amevaa vazi mpya alipokutana naye, Ahiya akararua vazi lake vipande kumi na viwili, kuonyesha nia ya Mungu ya kugawanya taifa. Akampa Yeroboamu vipande kumi na kubaki na viwili. Akamwambia Yeroboamu kwamba kitendo hiki kilikuwa mfano wa kile ambacho Mungu alikuwa anataka kutenda Israeli. Vipande kumi na viwili vilikuwa makabila kumi na mawili ya Israeli, kumi ambayo Mungu alikuwa anataka kuondoa kwa mkono wa Sulemani wakati kabila moja (pamoja na kabila la Sulemani la Yuda) lingebaki hii ni katika ahadi iliofanywa kwa Daudi na pia kwa sababu ya utakatifu wa Yerusalemu ambayo ilikuwa imepakana na Beyamini (Mst.31-32, 36). Sababu ya hukumu hii ilielezwa kwa makini katika maelezo ya Yeroboamu: â kwa sababu wameniacha mimi na kuabudu Ashotorethi.......wala hawakuenda katika njia zanguâ (Mst.33) aliambiwa wazi kwamba kama atashika Amri za Mungu, basi atajengewa ânyumba ya kweliâ.
Yeroboamu alifurahishwa na maneno haya, kwani alikuwa anapenda nguvu. Lakini ujumbe huu ulikuwa na uwezekano wa hatari. Kama Sulemani angetambua haya, basi maisha yake yangekuwa hatarini. Lakini badala ya kuficha ujumbe huu, Yeroboamu kwa ujinga wake aliwaambia wenzake kwamba Sulemani alikuwa na sababu nzuri ya kuwa na shaka na umakini, kwani Bwana alikuwa amemwambia kuwa atamwinua yule atakaye gawanya ufalme kufuatia kifo chake (1 Fal. 11:11-13) Wakati ujumbe wa Ahiya ulimfikia, hakupoteza muda na alifanya hima kutambua adui huyu. âSulemani alimtafuta Yeroboamu ili amwangamize. Naye akatorokea Misri kwa mfalme Shishak wa Misri, na alibakia Misri hadi kifo cha Sulemani.â
MKUTANO HUKO SHEKEMU (1 Wafalme 12:1-5)
Sulemani alifariki baada ya kutawala kwa miaka arobaini. Mwanawe Rehoboamu, ambaye mama yake alikuwa Mwamoni, akaridhi kiti cha enzi (1 Fal. 11:42; 14:21 linganisha Kum 23: 3).Kutawazwa kwa mfalme yule mdogo kulifanyika hadharani kule Shekemu na watu walikusanyika kwa hafla hii.
Lakini wazee wa Israeli walikuwa wamemwita Yeroboamu kutoka Misri baada ya kifo cha Sulemani. Yeroboamu bila shaka alikuwa na hamu ya kutimiza ahadi ya Ahiya kwake. Lakini hili ingetokea kwa njia ngani?
Kulikuwa na masuala mawili ambayo Yeroboamu alitumia kutimiza nia yake.
- Kulikuwa na wivu na uadui kati ya mataifa kumi ya kaskazini na yale ya Kusini (Mst. 16; Linganisha 2 Sam. 19:41-43).
- Watu walikuwa wamesikitishwa na mzigo mzito wa kodi walizopaswa kulipa ili kudumisha kazi za Sulemani.
Yeroboamu alichanganya mambo haya mawili na kuwakilisha kesi kwa watu. Muda na nafasi zilikuwa kwa upande wake. Wakati Rehoboamu alipofika kulikuwa na hali ya wasiwasi. Rehoboamu aliongoza kesi hii na ombi likatolewa â Baba yako amefanya kazi zako kuwa ngumu: sasa basi fanya kazi zetu ngumu kuwa zako baba, na mzigo aliotuwekea kuwa mwepesi nasi tutakuhudumia.â
Hili lilikuwa ombi zuri ambalo linaonyesha jinsi Yeroboamu alikuwa mjanja. Kama Rehoboamu angekataa basi angeonekana kama mjeuri. Kama angekubali, basi heshima ya Yeroboamu ingeongezeka. Chochote ambacho kingetokea lazima kingekuwa katika faida ya Yeroboamu aidha Rehoboamu hangeweza kukataa ombi hili lenye uhalali. Hangeweza kusema kwamba Yeroboamu ni mfanya ghasia, ama kumhukumu kwa uhaini. Kwa kweli Yeroboamu alikuwa anaonekana kama mzalendo, na mwenye hamu ya kumtumikia mfalme na nchi badala ya kusababisha ghasia yoyote.
UJINGA WA REHOBOAMU (1 Wafalme 12:6-15)
Rehoboamu aliwaambia watu kuondoka kwa muda wa siku tatu na kisha kurudi naye angewapa jibu lake. Katika wakati huu aliomba ushauri kutoka kwa washauri wa Sulemani, ambao walikuwa wameshuhudia hekima yake na hukumu, hata pia kwa vijana, na watu wa rika lake. Sauti ya umri na uzoefu ikashauri umakini: â Nena maneno mazuri kwao, na watakuwa watumishi wako mileleâ (Mst.7)Walitambua umuhimu wa mfalme huyu mchanga na mpya kupata neema dhidi ya watu wake, na walitambua hisia za watu, na tamaa ya Yerobaomu na hatari ya hali hii. Walimsihi Rehoboamu kukubali masharti yaliyowekwa mbele yake.
Lakini Rehoboamu hakushika ushauri wao. Pengine alikuwa tayari ameshafanya uamuzi wake hapo awali. Pengine uwepo wa adui yake, Yeroboamu ulimfanya awe mgumu dhidi ya maelewano. Hivyo akawaendea vijana nao walikuwa wenye pupa na waliokosa maono ya mbali. Kulingana na maoni yao kodi ilipaswa kuongezwa. Kuwapa watu yale waliodai ingeonyesha udhaifu.
Kwa siku tatu watu walikaa kwa hali ya kusubiri. Mfalme katika ukosefu wake wa maarifa akachukua ushauri wa vijana; âkidole changu kidogo kitakuwa kikubwa kuliko kiuno cha babangu, nitaongeza mizigo yako na kuwaadhibu kwa nge.â Aliwafanya wahisi nguvu ya nafasi yake, na kutangaza mateso yao yataongezewa. Hili lilidhibitisha hofu yao: kwani hili lilikuwa tendo lake la mwisho la dhuluma.Matokeo yake yangekuwa uasi.
Ujinga wa Rehoboamu ulionekana wazi kwa wote. Hata bila kutafuta sababu kwa ajili ya Rehoboamu, andiko linasema kwamba mambo haya yaliyoletwa na Bwana ili maneno wa Ahiya yapate kutimia (Mst.15).
UFALME UNAGAWANYIKA (1 Wafalme 12:16-24)
Wakati watu wote walipoona kwamba ombi lao limekataliwa, walikasirika. âTuna sehemu gani katika Daudi ...kwa mahema yenu, O Israeli: Sasa itunze nyumba yako mwenyewe, Daudi." Hii ilikuwa lugha ya kugawanyika. Yeroboamu akahisi kwamba mipango yake ilikuwa inazaa matunda. Jibu la ujinga la Rehoboam lilichochea uasi. Rehoboam alitaka kuzima uasi huu. Akatumtuma Adoramu kuongea na watu. Hili lilikuwa chaguo mbaya zaidi kwani Adoramu alikuwa anasimamia kodi, na uwepo wake uliwakasirisha watu zaidi. Walichukua mawe na kumpiga hadi akafa. Rehoboamu akatorokea Yerusalemu akihofia maisha yake na kupanga kisasi. Akakusanya jeshi kubwa la kuangamiza uasi, lakini alikatazwa na Shemaya, nabii, kuendeleza na mipango yake, kwa yale yaliyotokea ni ya Mungu.
Yeroboamu alichaguliwa kuwa mfalme kwa mapenzi ya Israeli yote. Sasa mgawanyiko ukakuwa dhabiti na Israeli ikagawanyika kwa mataifa mawili. Kwa sababu ya uovu, Sauli, mfalme wa kwanza, aliona ufalme wake ukichukuliwa kutoka kwa familia yake na kupewa Daudi. Daudi alijidhibitisha kuwa mtu anayefaa na akaahidiwa âNyumbaâ kwa uhakika (2 Sam 7:. 11-16, 26). Sasa mwana wa Daudi alikuwa hafai hivyo ufalme ungeweza kuchukuliwa kutoka kwake, kama vile ulikuwa umechukuliwa kutoka kwa Sauli kama haingekuwa ni kwa ahadi na huruma ya Mungu: âLakini huruma yangu haitaondoka kwake kama vile niliiondoa kwa Sauli hapo awaliâ (2 Sam. 7:15). Kwa hiyo, makabila haya mawili yakabaki kama ukoo wa Daudi. Hii itakuwa mpaka kurudi kwa kristo ndipo makabila haya kumi na mawili yataunganishwa tena (Mt.19:28; Lk. 1: 32-33; Eze. 37:22.).
HOFU YA JEROBOAMU NA UASI (1 Wafalme 12:25-33)
Yeroboamu hangefaidika na makosa ya Sulemani na Rehoboamu. Angeweza kuimarisha nafasi yake na kudumisha neema na Mungu. Lakini kudumisha mamlaka yake lilikuwa jambo la muhimu kwake kuliko kudumisha mamlaka ya Neno la Mungu. Alitambua kwamba ingawa Israeli ilikuwa imegawanywa katika sehemu mbili kumaanisha sasa kulikuwa na sehemu mbili za ufalme, uabudu wa Bwana ulikuwa Yerusalemu na bila kutoa ushawishi ambao ungekuwa wenye nguvu kuliko nguvu zilizotaka kuwatenganisha. Sheria ilihitaji kila mwanaume kufika mbele ya Bwana mara tatu kwa mwake(Kut. 23:17). Bila shaka hii ingefanya ushawishi wake kuisha wakati nafasi ya Rehoboamu ungeimarishwa, akatoa hoja.
"Kama watu hawa wataenda na kutoa sadaka katika nyumba ya Bwana Yerusalemu, basi mioyo ya watu hawa itageuka na kumrudia Bwana, hata Rehoboamu, mfalme wa Yuda, nao watakwenda tena kwa Rehoboamu, mfalme wa Yuda" (Mst.27).
Jinsi gani angeshughulikia swala hili? Suluhisho lake linaonyesha njia zake za hila. Kwa kutumia hila ya kidini, alipotosha ukweli kwa njia ambayo wengi walishindwa kutambua uovu huu na mchanganyiko wa mema na mambaya. Alifanya mambo matatu:
- Mistari ya 28-30: Yeye alikana mafundisho ya msingi na kutengeneza ndama wawili wa dhahabu ambao aliwaweka kaskazini na kusini, kule Dan na Bethel (linganisha Kut. 20: 3-4; 32: 7-8). Alihoji kuwa ilikuwa ni mbali kwenda hadi Yerusalemu na isitoshe Mungu alikuwa kila Mahali. (Yosephus)
- Mst.31: Hakukana haja ya ukuhani, lakini hakubadilisha vigezo vyake; badala ya kutoka katika wana wa Aaron, alifanya makuhani kutoka kwa watu wa kawaida (Hes. 3:10.).
- Mst. 32-33: Hakukataza haja ya kuwa na sherehe, lakini alibadilisha siku: ikawa kuwa sherehe ya mahema/vibanda iliteuliwa kuanzia katika siku ya kumi na tano ya mwezi wa saba, sherehe ya Yeroboamu ianze siku ya kumi na tano ya mwezi wa nane.
Hivyo dini yake ikawa ibada ya mapenzi ya binadamu. Lakini Mungu anahitaji binadamu kumwabudu kwa njia ambazo yeye ameweka; kwamba âWamwabudu kwa roho na kweliâ (Yn. 4:24). Yote ni ushirikina.
Kwa ajili ya dhambi zake Yeroboamu akawa mtu mwenye alama katika Israeli. Wafalme wote ishirini na tatu waliotawala baada yake walifuata njia zake. Wote isipokuwa wa mwisho na Neno linasema: â alitembea kwa njia zote za Yeroboamu mwana wa Nebati, na katika dhambi yake aliwafanya Waisraeli kutenda dhambi...â Ndama wa Betheli na Dani wakawa kama mtego kwa mataifa yale kumi na kuwa chanzo cha dhambi ambayo mwishowe ilileta uhamisho (linganisha 2 Fal. 17: 21-23; Hos. 10: 5-6).
Kulingana na Yeroboamu, Mungu alikuwa ametangaza nia yake kwa kuharibu nyumba yake kabisa (1 Fal.14: 7-16). Hivyo miaka ya dhahabu na utukufu chini ya Sulemani ikafuatiwa na miaka ya mgawanyiko na uasi.
Uasi kutoka kwa Ukweli bila shaka ungeleta madhara kwa maisha ya binadamu. Ukuu na tutukufu wa utawala wa Suleimani ukapotelea mbali baada ya kutotii amri za Mungu.
- Kama Mungu ni haki na sawa katika njia zake zote, hivyo tunapaswa kuwa katika shughuli zetu na watu wengine. Rehoboamu akajibu watu wake katika njia ambayo ni sawia na maneno ya babu yake Daudi: "Yule atawalaye watu lazima awe mwenye haki, atawale kwa kumwogopa Mungu (2 Sam. 23.3.).
- Tunapaswa kuthamini sauti ya uzoefu miongoni mwetu. Rehoboamu asikiliza vijana wasio na uzoefu na hivyo kupoteza sehemu kubwa ya ufalme wake.
- Mfano mbaya unaishi katika fikra za binadamu. Yeroboamu ilianzisha ibada ya uongo, na kusababisha Israeli kutenda dhambi, na wafalme ishirini na watatu waliotawala baadae walifuata njia hiyo hiyo.
-
Dini ya Yeroboamu alikuwa mambo ya ibada ya kweli katika kuweka maeneo ya ibada, makuhani na sikukuu, lakini kila moja ilikuwa tofauti na vile Mungu alihitaji kwa hivyo alikataa. Mungu si wa kudhihakiwa. Katika ibada yetu sisi lazima tuzingatia amri za Mungu na viwango vyake.
MAKTABA YA KUREJELEA:
"The Story of the Bible" (H.P. Mansfield)âTol. 4, Nam. 11
"The Ways of Providence" (R. Roberts)âSura. 19
"The Visible Hand of God" (R. Roberts)âSura. 25
MASWALI YA AYA:
- Ni kwanini ufalme uligawanyika na ni kwanini makabila haya mawili yalipewa Rehoboamu?
- Jinsi gani Yeroboamu aliambiwa kwamba ufalme utagawanywa na angekuwa mfalme?
- Kwa kifupi taja ombi ambalo watu walimwomba Rehoboamu huko Shekemu. Ni ushauri gani alioupokea na jinsi gani aliwajibu watu? Ni somo gani tunajifunza kutokana na tukio hili?
MASWALI YA INSHA:
- Elezea sababu na matokeo ya mapungufu ya Rehoboamu na Yeroboamu.
- Eleza jinsi mgawanyiko wa ufalme ulitokea baada ya kifo cha Sulemani.
- Jinsi gani na kwa nini Yeroboamu alianzisha ibada ya uongo ndani ya Israel na nini ilikuwa na athari juu kwa wafalme ambao walimfuata? Je, ni masomo gani makuu tunayojifunza kutokana na hili?