319. WAYAHUDI UHAMISHONI
"kwa mito ya Babeli, tulikaa chini,tukalia, tulipokumbuka Sayuni"
Kijana Danieli wa nyumba ya kifalme ya Yuda alikuwa miongoni mwa wale mateka waliofukuzwa wa kwanza kwa mkono wa Nebukadreza. Baada ya kukatizwa katika harakati zake Wamisri na habari za kifo cha babake, Nebukadreza kwa haraka alimweka Yehoyakimu chini ya kodi, akanyukua samani na mateka wachache hadi Babeli. Danieli angeungana na wengine wengi kufuatia kuhamishwa, hadi kiti cha enzi kilipo-pinduliwa na miaka sabini ya uhamisho ikaanza, adhabu kali ya kusafishwa ikashuka kwa watu wa Mungu waliokuwa wameasi.
Lengo letu katika somo hili ni kuona jinsi adhabu ilisafisha na kurudisha imani kwa Wayahudi wakiwa uhamishoni.
Danieli 1 na BABELI 3
Babeli ilikuwa inachukuliwa kama âUtukufu wa falme, uzuri wa fahari ya Wakaldayoâ (Isa.13:19).
Herodoti inasema kwamba Babeli ilikuwa imezingukwa na ukuta wa matofali mita 26.7 na upana wa mita 107.7. juu ya kuta kulikuwa na safu mbili za nyumba na barabara katikati. Kiingilio cha mji kilikuwa kupitia milango 100 ya shaba. Mto frati uligawanya mji kwa sehemu mbili ambazo ziliunganishwa katikati na dayaja la upana wa mita 9.2. Mfalme aliacha maneno yafuatayo katika kumbukumbu â Nimemaliza kuta mbili kuu za Babeli.Nimeimarisha mji kwa matofali yaliochomwa na kuwa magumu kama mawe, na kupanga vikundi vikubwa kama milima. Hivyo nimeimarisha ulinzi wa Babeli. Na udumu milele.Babeli mji ambao ni furaha ya macho yangu ambayo nimefanya kuwa tukufuâ.
Ibada ya sanamu ilipenya kila mahali katika maisha ya Wababeli. Mamia ya hekalu na madhabahu yalihudumia mahujaji na wafanyi biashara. Mamlaka ya Hekalu yaliendesha idara ya Maduka, vituo vya ununuzi, maghala, mabenki na taasisi za mikopo. Hivyo mazingira ya ibada ya sanamu ikawazingira Wayahudi walio kuwa wamechuliwa mateka. Walihisi hisia kali za msiba wakiomboleza nchi yao na hekalu. Walilia na kukumbuka Sayuni (Tazama Zab. 137). Walivyotazama kuwasili kwa mateka zaidi Wayahudi na udhalilishaji wa viongozi wao, kama vile Sedekia, walitubu kwa ajili ya uovu wa taifa lao na kuacha ibada ya sanamu ya watekaji nyara wao. Walitiwa moyo na unabii wa ajabu wa nabii Isaiya (Sura.13,) na Yeremia(Sura ya 51) Ishara ya Ezekieli na imani na ujasiri wa Danieli na wenzake ulizindisha utegemezi wao wa Mungu. Walitiwa adabu na uhamisho huu na wakarudi kuwa watu wa kumwabudi Mungu mmoja.
Wayahudi waliokuwa uhamishoni waligawanyika katika makazi mbalimbali ya Babeli, kule ambako waliunda vikundi vidongo vidongo vilivyokuwa na ushikiano na uhuru wa kuabudu (tazama pia Yer.29: 4-7).
Kundi moja kama hilo lilikuwa Tel-Abibu (Eze. 3:15), ambako nabii-kuhani Ezekiel na mke wake waliishi 24:18). Walikuwa wamefukuzwa katika kundi la tatu la uhamisho pamoja na Yekonia (1: 2).
EZEKIELI: MTU WA ISHARA.
Ezekiel alijitahidi kuonyesha kwa maneno na ishara kwamba uhamisho wa Wayahudi ulikuwa uwe wa miaka 70. Hili lilifanywa kuwa ngumu kwa ndoto za uwongo kutoka wa manabii wa Uwongo na washiriki wao, ambao walidai kwamba Yerusalemu haitaanguka na kwamba wale walioko Yerusalemu hawataondolewa (Eze. 11:15; 33:24). Wale waliokuwa tayari uhamishoni walifurahia kusikia habari ya ukombozi (Eze. 13:16, 19). Nabii wa uwongo katika Yerusalemu, Hanania, alitabiri kwamba watarudi baada ya miaka miwili wakiwa na vyombo vya hekalu (Yer. 28). Lakini kuwasili kwa wahamiaji zaidi, kifo cha Hanania na onyo la Yeremia, huduma ya Yeremia na kuanguka kwa Yerusalemu kuliondoa matumaini yote ya kurudi kwa haraka kwa mji wao mpendwa. Ilikuwa ni kazi ya Ezekieli kutilia mkazo akilini mwao utambuzi na kukiri dhambi zao. Matamshi yaliorejelewa ya unabii wa Ezekieli âWatatambua kwamba mimi ni Munguâ. Utambuzi huu ulikuwa usisitizwe katika akili za Wayahudi waliokuwa uhamishoni.
Tuna ujumbe wa Ezekiel, pamoja na maandiko, yanatuhimiza sisi kumtambua Mungu na kuweka imani yetu kwake. Lengo lake alilokiri ni kurejesha kiti cha Daudi chini ya utawala wa Mwana mkuu wa Daudi.
DANIELI: MKUU WA MAKUHANI
Nabii mwingine ambaye alitekeleza jukumu kuu katika kuelimisha watu wa Mungu walio uhamishoni alikuwa Danieli, ambaye maisha yake yalikuwa karibu kuchukuliwa katika matayarisho ya Kurudi. Danieli alikuwa na miaka pengine 17 au 18 wakati alipelekwa katika mahakama ya kifalme ya Nebukadreza. Aliishi zaidi ya miaka ile 70 ya uhamisho (Dan. 1:21) na kwa hiyo huduma yake ndefu na ya imani ni ya muhimu kwani ilichangia kuboresha hali ya kiroho ya Wayahudi waliorejea.
Tukichukulia kuwa Danieli alikuwa na miaka 17 wakati alifukuzwa, basi tutapata kwamba alizaliwa katika kipindi cha mageuzi ya Yosia (2 Nya. 34: 8, 29-33) na hivyo alilelewa katika mazingira ya mageuzi na msisimko wa amri na sheria za Mungu. Imani ya Danieli katika miaka ya ujana wake lazima iwe ilitokana na mafunzo aliyopokea tangu aliwa mchanga. Hivyo ni muhimu kwetu sisi kukumbuka Muumbaji wetu katika siku za ujana wetu wakati tunakumbwa na majaribio ya kutatanisha ya nyakati zetu.
HEKIMA YA KIPANGANI INAHUKUMIWA (Daniel 1)
Unyakuzi wa Nebukadreza wa vyombo vya hekalu na mateka wachanga lilikuwa jaribio la kuonyesha ukuu wa mungu wake, Bel, juu ya Mungu wa Israeli. Alitaka kuwapotosha Daudi na Washirika wake kutoka chochote kinachohusiana na Mungu na kuwaingiza katika tamaduni za Kibabeli, ambazo zilikuwa zimeendelea sana kote ulimwenguni. Mahitaji yalikuwa rahisi- Kuendana na uwezo wao wa kielimu, walitakiwa kuwa na elimu ya dini na Sayansi kila wakati. Lakini kulikuwa na hatari ya kuingilia hali ya kipangani, kwani Yeremia alionya kwamba â ni nchi ya sanamu za kuchongwa, na wameingiwa na wazimu kwa ajili ya sanamu zao â (Yer. 50:38).
Danieli aliazimia kwamba hatakuwa kwa njia yoyote akishirikiana na ibada ya sanamu (Mst.8) alipanga kwa siri kudhibitisha uhalali wa uamuzi wake (Mst.12), kwani alikataa masharti ya Mfalme ambayo ingeleta hasira ya mfalme kwake yeye na kwa watu wake. Imani yake ilidhibitishwa wakati chakula chake kisicho na dhambi kilidhibitishwa kutosheleza zaidi, na Mungu akampa yeye na marafiki zake mafanikio katika masomo yao na kuwashinda wasomi wale wengine wote.
Msimamo wa Danieli wa kimaadili, pamoja na busara, ulipokea jibu tayari kutoka kwa Bwana. Sisi, pia, tunajaribiwa katika majukumu ya kila siku katika nafsi zetu na tunahakikishiwa kwamba tukimtambua Mungu katika njia zetu zote, kwani ataongoza na kufaniskisha njia zetu (Mit. 3: 1-7.).
IBADA YA KIPANGANI INAHUKUMIWA (Danieli 3)
Wakati Nebukadneza alitengeneza picha ya dhahabu na kuamuru watu wake kuiabudu au kupata adhabu ya kifo, marafiki watatu wa Daniei (Hanania, na Mishaeli, na Azaria) waliwekwa katika nafasi ngumu. Majibu yao kwa ombi hili yangekuwa utii kwa sababu ya heshima kwa Mfalme na nguvu za Babeli, na kusahau pingamizi yoyote ya Israeli ya zamani. Mtazamo wa Wayahudi hawa watatu, hata hivyo ulikuwa ule wa utii wa amri za Bwana, licha ya kuondolewa kutoka kwa Hekalu na Nchi. Hawakuamini kuweko kwa milele kwa Babeli, mji mkuu duniani. Kuabudu Sanamu, ambayo iliwakilisha Babeli na utawala wake, ulikuwa ibada ya utukufu wa mwili.
Nebukadreza alikuwa amejenga sanamu kwa sababu ya tamaa ya Babeli na yake mwenyewe kutukuzwa (tazama mtazamo wake katika Isa. 14: 4, 13-16; Yer. 51:53.). Babeli katika fikra zake ilikuwa iishi milele. Hivyo alitaka kupinga kusudi la Mungu kama ilivyokuwa funuliwa kwake wazi na ndoto ya Danieli 2. Katika picha ya ndoto, dhahabu (ikiwakilisha utawala wa Babeli) ilitumika tu kama kichwa, kwani utawala huo ungeanguka karibuni. Lakini Nebukadreza alitengeneza picha katika Danieli 3 kwa dhahabu.
Ni kweli kwamba Babeli hapo awali ilikuwa imeonyesha roho sawa katika kujenga mnara wa Babeli (Mwa. 11: 2-4),bali walisitishwa na Bwana.
UJASIRI NA IMANI (Danieli 3:8-18)
Wayahudi watatu walienda kwa kujitolea, kukubaliana na agizo la Mflame kuhudhuria (tazama 1 Pet. 2:. 13-15). Lakini, walipoamriwa kuabudu ile samanu, walimtii Mungu kuliko binadamu (Mt. 5:29; Kum. 5:. 6-10). Walijitenga kwani walikataa kusujudu mbele ya sanamu inayotukuza mwili. Walikuwa waasi waangalifu. Kuna wakati hatupaswi kutikiswa kutoka kwa mitizamo yetu licha ya aibu inayoweza kutuletea. Wacha tujiunganishe na imani yetu kwa mfano huu wa ujasiri katika uso wa mashaka.
Wapinzani wao, wakionyesha roho ya awali ya kupambana na Uyahudi, taarifa ya kukataa kwa Wayahudi kuabudu mchoro ulikuwa kama tusi na kitendo cha uhaini dhidi ya Mfalme na miungu yake (Mst.8-12). Nebukadreza alipandwa na hasira. Nafasi yake ya nguvu na ujasiri katika mwili ilijaa ndani yake na katoa changamoto, sio kwao, bali kwa Mungu wao. Kwa upofu akifuata njia ya kiburi na ujinga wa wanaume kama vile Goliathi, Rabshake na Senakeribu, alidai â naye ni nani huyo Mungu atakayewaokoa ninyi kutoka kwa mikono yangu?â (Mst.15) katika uwepo wa nguvu kuu ya huyu mfalme walishikilia msimamo wao, wakionyesha ujasiri wa ajabu katika mtizamo wao. Wokovu ulionekana kuwa mbali sana. Hata marafiki wa Daudi walikuwa tayari kutoa maisha yao kwa Mungu kama Muumbaji mwenye imani (angalia 1 Pet. 4:. 12-19). Lao lilikuwa zaidi ya kukataa, ulikuwa ushuhuda, ulinzi usio na woga wa Imani.
UKOMBOZI WA KIMIUJIZA (Danieli 3:19-30)
Makali ya moto yaliongezewa mara saba Zaidi, hivyo kuonyesha ghadhabu kamili ya watu Mataifa kwa Watu wa Mungu.
Marafiki watatu walitupwa motoni, wakati wale walio watupa motoni wakichomeka na joto la moto wao wenyewe. âYule ambaye anawagusa ninyi anagusa kipendezacho jicho languâ, Mungu alikuwa amesema. Hatima yao ya kusikitisha ni mfano wa hatima ya wote ambao wanatesa watu wa Mungu (Taz. Yoe. 3: 9-16). Israeli katika vita vya mwisho watasafishwa na moto, kwani Mungu alikuwa amesema kwamba âAtaleta sehemu ya tatu kupitia motoâ (Zek. 13: 9).
Marafiki watatu jasiri waliokolewa kwa njia ya ajabu (24-27). Lakini kile kilichomshangaza Nebukadreza zaidi kilikuwa kutokea kwa mtu mwingine,malaika kando ya mateka. Malaika (Mst.28) alikuwa amewazunguka wale wanaomwogopa Mungu na kuwakoaâ (Zab.34: 7.), Mungu alikuwa amejionyesha mwenyewe kwa niaba ya wale ambao wana moyo kamilifu (2 Nya. 16:. 9). Imani yao ilikuwa âimepunguza makali ya motoâ (Ebr. 11:34).
Kwa ishara kubwa ya ukuu wa âMungu aliye Juuâ, Nebukadreza alilazimika kukiri upumbavu wake na udogo wake mbele ya Mungu (Mst.26-30). Alitambua kwamba Wayahudi walikuwa watumishi wa Mfalme mkuu kuliko yeye mwenyewe na imani yao ilikuwa imezawadiwa licha ya mateso yake. Basi akafanya amri ya kuheshimiwa katika himaya yake kubwa, kwamba Mungu wa Wayahudi ni wa kuheshimiwa, "kwa sababu hakuna Mungu mwingine ambaye anaweza kuokoa kwa njia ya aina hiiâ (Mst.30)
UHARIBIFU WA BABELI NA ROMA
Babeli ililetwa kwa uharibifu wakiwa katikati ya kuponda raha na ufisadi (Dan.5). Wakati wa sikukuu ya Belshaza, mjukuu wa Nebukadreza, mkono ulionekana ukiandika kwenye ukuta. Danieli akatafsiri maandishi kwamba ufalme ulikuwa umeisha (Mst.25-28), na usiku huo Dario, Mmidiani aliingia kwenye mji akipitia kingo za mto Frati uliokuwa umekauka na kupitia milango iliokuwa wazi. Belshaza aliuliwa na ufalme ukapinduliwa. Ufalme ulilipa adhabu kwa uharibifu wake wa ufalme wa Daudi. (Dharau yake kwa Mungu wa Israeli ilionyeshwa bayana na matumizi Belshaza, usiku wake wa mwisho wa kusherehekea, wa vyombo vitakatifu vilivyotolewa katika Hekalu ya Bwana katika Yerusalemu miaka mingi hapo awali mst.2-4).
Mfumo wa Kikatoki wa Roma unaitwa âBabeli Kuuâ na maovu yake yalizidi yale ya Babeli ya zamani (Ufu. 17: 5). Kwa hivyo adhabu yake ya baadaye itakuwa kubwa zaidi (Yer.51:51-64).
Ufunuo 18 unaelezea kuangushwa kwa Roma kwa njia ya ghasia kwa sababu ya usherati wake wa kiroho, mafundisho ya uwongo, na kuteswa kwa Eklesia. Roma ingeteseka kwa pigo la mtetemeko wa ardhi, kisiasa na kimwili. "Tokeni kwake, watu wangu" (Mst.4) ni wito wa kujitenga ndani ya Eklesia katika wakati wa Babeli, katika nyakati za Roma na hasa katika nyakati zetu.
MAMBO TUNAYOJIFUNZA:
- Miaka 70 ya mateka iliwatia adabu na kuwasafisha Wayahudi waliohamishwa. Kutoka mitazamo ya fahari ya kuamini mkono wa mwili waliletwa kwa utegemezi wa Bwana.
- Kazi ya manabii Yeremia, Ezekieli na Daniel ziliwatia moyo Wayahudi kujiandaa kwa uaminifu kwa ajili ya marejeo.
- Tunapaswa kuishi kama wageni, wakimbizi, tukitayarishwa na manabii kwa ajili ya "kurudi" kwetu Sayuni.
- Tunapata nidhamu kwa majaribu ya imani yetu.
- Tunatiwa moyo na maandiko kudumisha kujitenga kutoka kwa mambo maovu ya ulimwengu na kuangalia kwa ujio mkubwa kuliko Koreshi ambaye ataharibu Roma na wapinzani wa watu wa Mungu.
MAKTABA YA KUREJELEA:
"The Story of the Bible" (H.P. Mansfield)âTol. 6, Nam. 9-11
"The Apocalypse Epitomised" (H.P. Mansfield)
"Exposition of Daniel" (J. Thomas) â She. 1
"The Prophet Ezekiel" (W.H. Boulton)
MASWALI YA AYA:
1. Yapi yalikuwa Matokeo ya kuchukuliwa mateka katika Babeli kwa mateka Wayahudi?
2. Kwa kifupi toa muhtasari wa matukio wakati marafiki watatu wa Danieli walionyesha imani yao katika Mungu wa Israeli.
3. Marafiki watatu wa Danieli walikataa kuabudu sanamu, ambayo mfalme Nebukadreza alikuwa amesimamisha. Ni kwa mambo gani kanuni hii ya pingamizi kwa "amri ya mfalme" inatokea siku ya leo?
4. Jinsi gani mfumo wa Katoliki ya Roma unalinganishwa na Babeli? Toa Maoni kuhusu kuanguka kwa kila mmoja.
MASWALI YA INSHA:
- Ni Jukumu gani Ezekiel alikuwa nalo kwa mateka Wayahudi?
-
(a) Ni changamoto gani Daniel alishinda, kama ilivyoandikwa Dan. 1?
(b) Ni changamoto gani sawa tunayo kabiliana nayo leo na jinsi gani tunaweza kushinda nazo? - Onyesha jinsi kupitia imani, watu watatu waliokuwa rafiki wa Danieli "walizima nguvu za moto" (Ebr. 11:34).
- Eleza baadhi ya njia ambazo uhamisho wa Wayahudi katika Babeli na Uajemi ulileta kuzaliwa upya kwa imani katika uod