CSSA 3-3-322 - NEHEMIAH — MAN OF FAITH AND ACTION

Swahili

322.    NEHEMIA — MTU WA IMANI NA VITENDO

"Tuinuke na tujenge”

Baada ya kurudi kwa kwanza kwa Wayahudi ndani ya nchi chini ya Yoshua na Zerubabeli, kulikuwa marejesho zaidi chini Ezra mwandishi. Miaka kumi na mitatu baadaye Nehemia alirejea Yerusalemu kama Gavana wa  Wilaya. Wakazi walikuwa hawana matumaini na walivurugika. Ilihitaji mtu  wa maombi, Imani na vitendo kuimarisha wananchi hawa wachache na kuhamasisha wananchi wenzake na hofu ya Bwana. Nehemia alikuwa mtu wa aina hio.

Lengo letu katika somo hili ni kuona jinsi Imani kuu ya Nehemia na hali ya kusudi iliwahimiza ndugu zake na kumwezeza kushinda matatizo mengi na tofauti yaliyomkumba.

Nehemia 1 na 2

HABARI MBAYA KUTOKA YUDEA (Nehemia 1).

Nehemia alishikilia nafasi ya kuheshimiwa ya mnyweshaji wa Artashasta, mfalme wa Uajemi. Ndugu yake, Hanani, na wengine, walikuwa wamerudi kutoka Yuda na wakauliza jinsi nchi hii mpya ilikuwa inaendelea. Hili lilikuwa swali lake la kwanza.  Ingawa alifanya kazi huko Shushani mahali ambapo moyo wake ulikuwa ni Yerusalemu. Alisikitishwa sana na ripoti, “Waliobaki uhamishoni kule katika wilaya walikuwa katika dhiki  na shutuma nyingi: Ukuta wa Yerusalemu ulikuwa umevunjika na milango yake hivyo ikachomwa na moto” (1:3)

 

TATIZO LA KWANZA: KWA NJIA GANI NEHEMIA ANGEPATA RUHUSA NA KUSAFIRI HADI YERUSALEMU KUWASAIDIA WATU WAKE?

Jibu: Hiyo alipaswa kufikiria juu ya kazi hii kubwa ni alama kubwa ya ukuu wa tabia ya Nehemia, kwani alikuwa ametosheka na alikuwa akiishi vyema katika ikulu ya Uajemi. Hakuna jambo kubwa angeweza kufanya kwa hivyo alimgeukia Baba. “Alilia na kuomboleza kwa siku kadhaa, kufunga kula, nakuomba mbele ya Mungu wa Mbiguni”. Aliomba kwa dhati. Maombi aliyo-omba  yanaonyesha akili ilio na nidhamu na hofu ya Mungu na matumaini kwa Israeli. Uhamisho uliwasha na kuimarisha ari yake. Alizungumza na Mungu kulingana na huruma ya agano lake (Mst.5) akaomba kusikizwa, na kutambua haki yake na dhambi ya taifa (Mst. 6-7) kisha akakata rufaa  kwa ahadi za awali ambazo zilihakikisha marejesho baada ya mageuzi (Mst.8-9)

Maombi yamejaa nukuu kutoka kwa vitabu vya sheria, kuonyesha jinsi Nehemia alikuwa ameweka Neno akilini. Kumbuka marejeo katika pambizo na tizama uone utapata nukuu ngapi. Kisha, anasihi kwa kutaja hali ya Mungu kama baba katika kuzaliwa kwa taifa (Mst.10). Anakamilisha kwa ombi la dhati apate jibu la maombi yake. Kinachojitokeza katika maombi yake ni nia yake ya kurudi na kutumikia. Lakini pingamizi kuu ilikuwa kuajiriwa kwake na hivyo aliomba, "Nipe rehema mbele ya mtu huyu", yaani mfalme. Miezi minne ilipita (Dhibitisha 1:1, 2:1) na hakukuwa na jibu. Mfalme aliona uso wake uliokuwa umesikitika, kwani kwa kawaida alikuwa mmchangamfu. Nehemia alikuwa “ na hofu nyingi” kwamba mfalme angemkemea. Fursa hata hivyo ilitolewa ya kuelezea, “....kwanini uso wangu usiwe na huzuni, wakati mji, mahali pa mababa zangu panakaa kwa hali ya kuharibika?” kisha mfalme akasema “ Ni  jambo gani unalotaka?”  Nehemia hakuamini masikio yake. Je,haikuwa Mungu anajibu maombi yake?. Akikumbuka Mungu anaagalia maneno na matendo yake, alitoa sala kimya kabla kufanya  dua yake kwa mfalme. Hapo awali alikuwa amemfurahisha mfalme na pia, inaonekana, “pia malkia aliyekaa karibu naye” (mst. 6) Kama kweli alikuwa Esther, kama mpangilio wa nyakati hizo unaruhusu, bila shaka angeongeza msaada wake kwa ajili ya ombi lake. Hivyo mfalme akamruhusu kuondoka na kumtuma na barua zilizohakikisha usalama na kibali cha kupata vifaa vya ujenzi wa msitu wa Mfalme. Hili lilikuwa jibu la ajabu.

Ni muhimu kutambua jibu hili zuri  kwa Nehemia. Alitambua huyu alikuwa Mungu, “na mflame akanipa,kwa MKONO MZURI WA MUNGU WANGU juu yangu” (2:8)  Ilikuwa uhakika huu ambao ulimfanya  kufanya kazi dhidi ya upinzani na shida, kazi ambayo hakuacha mpaka ilipokamilika. Kuna somo katika hili. Wengi hufa moyo wakati wako karibu kupata ushindi. Tukiwa na Mungu kwa upande wetu, ukweli  utakidhiri licha ya  upinzani, hadi “mwisho dunia itajaa utukufu wa Bwana” (Hes. 14:21; Isa 50:. 7-8).

Wakati Nehemia aliwasili Yudea aliwaonyesha “watawala ng'ambo ya Mto" barua yake ya mamlaka. Lakini ole, Wasamaria wakiongozwa na Sanbalati, na Tobia, waliomboleza sana kuona kwamba amekuja mtu anayewatakia heri wana wa Israeli (2:10) Yao ilikuwa mafano wa maonyesho ya kupambana na Uyahudi ambao ulikuwa upate nguvu zaidi kama vile Nehemia aliendelea na mipango yake. Nehemia alikagua  kuta zilizobomoka  na  milango wakati wa usiku. Kwa wakati hakuwa amewafahamisha Wayahudi kile “Mungu alikuwa ameweka kwa roho yangu kufanya Yerusalemu.”

TATIZO LA PILI: ANGEWEZAJE KUWAHIMIZA NA KUWATIA MOYO WATU HAWA WALIOKUFA MOYO KWA KAZI YA UJENZI?

Jibu: Alielewa matatizo yao kabisa, “ unaona dhiki tulionayo” aliwaeleza kwamba  walikuwa watu waliopatwa na aibu na ni wajibu wao kuondoa aibu ile. Matendo yalifaa kuondoa  upotovu na hali ya kutojali: “Njooni tuujenge tena ukuta wa Yerusalemu ili tusiwe na shutumu tena”, akasema (2:17)  wakati alihusisha matukio ya Kimungu yalimfanya kuwa pale, na jinsi mflame alikuwa amempa mamlaka, wakajibu, “Hebu tuinuke na kujenga”.

Hivyo  mfano wa ari ya Nehemia uliwatia moyo watu. Ari huenea. Kama sisi tutaonyesha ari katika uanafunzi, sisi kama Nehemia, tutabarikiwa na wengine watatiwa moyo  pia (Flp.1:14 linganisha Rom 12:11.).

Lakini ari ya mabaki ya Israeli aliamsha hisia kali kutoka kwa adui zao. Sanbalati, na Tobia na Geshemu "waliposikia hayo" waliwacheka na kuwakejeli na kudai kwamba Wayahudi walikuwa wanataka kuasi dhidi ya Artashasta (2:19).


TATIZO LA TATU: JINSI GANI WATU WATAKABILIANA NA KEJELI? (Nehemia 2:19, 20; 4:1-9).

Jibu: Kejeli inaweza vunja moyo ama kuimarisha uamuzi. Nehemia alikuwa kiongozi mkuu.  Akili yake ilikuwa hai na inayowaza kuhusu masuala tofauti kwa hivyo alikuwa na jibu tayari. Kwa sababu ya imani yake ilikuwa dhabiti aliweza kukabiliana na changamoto na jibu ambalo lilionyesha kujitolea kwake. Hivyo aliwanyamazisha adui zake, na kuwatia moyo ndugu zake. “Mungu wa mbiguni, atatufanikisha; hivyo sisi watumishi wake tutainuka na kujenga lakini ninyi hamna sehemu, wala haki, wala kumbukumbu, katika Yerusalemu" (2:20).

Nehemia 3 ina kumbukumbu ya majina ya wale walishiriki na kutaja sehemu ya ukuta waliojenga.

Kama vile kazi iliendelea, maneno yakawa matendo, ghadhabu za adui zao zikazidi. Kando na kejeli, Sanbalati alichukua ripoti ya shughuli hadi Samaria na kuwaambia ndugu zake na “Jeshi la Wasamaria”.  Kuchukizwa kwao kwa mradi huo kumefupishwa kwa maneno makali ya Tobia, “Hata hiki wanachojenga, , kama mbweha  atapanda, atavunja ukuta wao wa mawe” (4: 3).  Habari za upinzani na tishio zilizokuweko  ziliwafikia Wayahudi. Lakini Yeremia hakutikiswa na akapinga kwa maombi na vitendo. Aliwaunganisha watu  katika maombi na vitendo. Aliwaunganisha watu katika sala na akaomba adui awe mwathirika wa nia yake mwenyewe: Sikia, Ee Mungu wetu, kwa tunadharauliwa; na ugeuze shutuma zao  juu ya vichwa vyao” (4.4)  Wayahudi walitiwa moyo na kuweka mawazo yao juu ya kazi ambayo iliendela kwa  kasi (4:6).

Ukuta ulio imara ulizusha uasi na chuki kati ya watu tofauti wa Samaria, na wakati huu waliishia vita. Lakini maombi ya umoja, pamoja na  hatua ya vitendo ya kuhakikisha kazi inaendelea (4: 5-9).

 

TATIZO LA NNE: JINSI YA KUSHINDA RAJUA INAYOLETWA NA UKANDAMIZAJI NA KAZI NGUMU? (Nehemia 4:10-23).

Jibu: upinzani na kazi ngumu zilianza kuwachokesha watu. Wale waliokuwa na imani hafifu walianza  kulalamika na kushusha nyoyo za wengine. Kulalamika, kama vile shauku kunaweza kuambukizwa. Baadhi yao walikufa moyo kwani kazi yao yote haikuonekana kubwa  kwa takataka na vifusi na  waliokuwa wanahisi uchovu (4:10). Wengine walikuwa wamesikia kuhusu mipango ya ushambulizi wa adui na “mara kumi” Wakarejelea: “ maeneo yote watakaoishi watatushambulia” (4:12).  Jinsi gani Nehemia angejibu changamoto hii- changamoto wakati huu ilikuwa kati yao?

Hatua ya kwanza aliyochukua ilikua kitendo. Aliweka familia pamoja na silaha zao katika maeneo maalum (4:13). Wanaume watapigana wakati familia zao zinahusika na hivyo mipaka ikalindwa. Wayahudi wa leo wanafuata wazo sawa na Kibutizi. Kisha akawakumbusha kwamba Mungu, “ambaye ni mkuu wa kutisha", alikuwa kwa upande wao na angewapigania. Lazima wawe makini kwa Mungu kuliko binadamu. Wakati maadui waliona mipango yao imejulikana na kupingwa walikata tamaa. Wayudi walirejelea kazi yao ujenzi.

Tangu wakati huo wajenzi walifanya kazi wakiwa na panga zao. Kwa sababu walikuwa wameenea umbali mkubwa na haingewezekana kuwalinda  wajenzi wote. Mpiga tarumbeta alikuwa pamoja na Nehemia na wakati alipiga kelele wangekuja na kutoa msaada. Hivyo Eklesia iliunganishwa katika kazi na kiongozi wao shujaa alikuwa katikati ya kazi yao na mbele ya ushambulizi, akiwahimiza. Msemo wao ulikuwa “Mungu wetu atatupigania” (4:20). Wale walioishi nje ya Yerusalemu waliagizwa kurudi ndani ya mji wakati wa usiku. Hivyo  walifanya kazi mchana na ulinzi usiku. Walikuwa na shughuli nyingi na hawakupata mda wa kubadili mavazi ya kulala! Wakati huu wote walitiwa moyo na mfano mzuri wa Nehemia, ambaye alitia vitendo mwenyewe kwa mambo alionena kwa watu.


TATIZO LA TANO:  JINSI YA KUKABILIANA NA HILA NA UWONGO? (Nehemia 6:1-14).

Jibu: maadui waliokuwa nje walikuwa wamejaribu kusimamisha kazi kupitia kejeli, vitisho na vurugu.  Baada ya kushindwa na hili wakachanganyikwa na kujaribu njia zingine za kikatili.  Walitaka hadhara na Nehemia, lakini lengo lao kuu lilikuwa kumdhuru. Walijua kwamba yeye ndiye alikuwa uti wa mgongo wa kazi ile ya ujenzi, na kama wangemwangamiza kazi hio ingekoma. Lakini alitambua nia yao na kuwapa jibu mwafaka kwa yeyote atakayetaka kuingilia kazi ya ujenzi, “Nafanya kazi kubwa, hivyo siwezi shuka chini: kwanini kazi isite, wakati nashuka kuja kwenyu nini?”(4:3) Walijaribu katika matukio manne tofauti kumwita Nehemia, lakini kila wakati walipata jibu lile lile.

Sanbalati aliwaza sana na akatunga barua ambayo alifikiria kwamba inaweza mshawishi  Nehemia  kufika kwenye meza ya mkutano. Alimtuma mtumishi wake kupeleka barua  ambayo ilikuwa inadai kwamba ukuta ulikuwa unajengwa kwa ajili ya uasi, kwamba Nehemia alikuwa anapanga kujiteua kama mfalme. Madai haya yangekua na madhara makubwa, hivyo ingekuwa bora kama angeshuka na kukutana nao. Nehemia alielewa nia yao na uwongo wao na akawaambia “hakukufanyika mambo kama hayo uyasemayo, lakini kwa moyo wako mwenyewe umeyabaini”.

 

YERUSALEMU KATIKA WAKATI WA NEHEMIA

 Makundi ya familia yaliyohusika katika ujenzi wa ukuta wa Yerusalemu.

Kisha Tobia na Sanbalati walifikiri  njia zingine za kikatili za kuharibu sifa ya Nehemia kwa kuonyesha kwamba alikuwa mtu mwenye hofu na mwoga.  Walimwalika Shemaia kukutana na Nehemia ndani ya hekalu milango ikiwa imefungwa. Alikuwa amwambie kwamba lazima wajifiche mle dani kwani maadui walikuwa wanaenda  kuumua wakati wa usiku. Sasa Nehemia alikuwa ameonyesha ujasiri na aliwatia moyo watu wake. Kama angekubaliana na ombi hili basi heshima yake ingeharibiwa.  Hivyo akajibu, “ je Mtu kama mimi napaswa kutoroka?” hivyo akasimama kulingana na kanuni katika sura ya changamoto hii yenye hila. Hivyo,  Shemaiya alijifanya rafiki na kusema alikuwa ametumwa na Mungu (6: 10-14)! Ilikuwa muhimu kwa Nehemia kuwa makini- hila kama nyoka lakini upole kama wa njiwa, kama vile Bwana alikuja kusema baadaye.

KUKAMILIKA KWA UKUTA (Nehemia 6:15, 16)

Licha ya jitihada zote za kupinga, kazi ilikamilika. Kuna sauti ya ushindi katika maneno haya “Hivyo kazi ya ujenzi ikakamilika katika siku ya ishirini na tano ya mwezi wa Eluli, Muda wa siku hamsini na mbili”.(Mst.15). Hili lilikuwa jambo la ajabu. Ilikuwa wazi kwamba baraka ya Mungu ilikuwa juu yao wakati huo wote. Nehemia hakuficha hili na hata adui zake walitambua hili na wakakata tamaa. Kwa Nehemia inaweza semwa kwa kweli kwamba, “ mateso kwa mwenye haki ni mengi, lakini Mungu humponya nayo yote” (Zab. 34:19).

MAMBO TUNAYOJIFUNZA:

  • Nehemia alikuwa kweli alipo taka kurudi Yuda na hivyo Bwana alijibu maombi yake.
  •  Alikuwa kiongozi mkubwa kwa sababu yeye hakufa moyo katika wakati wa matatizo, lakini alimtafuta Mungu na kujihusisha binafsi katika kazi na watu.
  • Alikuwa mtu wa maombi NA UTEKELEZAJI. Vitendo ni zaidi ya maneno. Hivyo pia leo, imani lazima iwekwe kwa vitendo - maana kwa matendo yetu tutahukumiwa.
  • Shauku na rajua zinaweza kuenezwa. Tunaweza kuhamasisha wengine katika huduma ya Mwalimu kama sisi weneywe tuna nia na ari.
  •  Nehemia alikuwa ni mtu wa mtazamo wa haraka. Kuna haja kwetu sisi kuelekezwa katika misingi ya ukweli ili tuweze kupambanua na kukataa falsafa za hila za nyakati zetu km. mageuzi, na ukombozi.

 

MAKTABA YA KUREJELEA:

"The Story of the Bible" (H.P. Mansfield)—Tol. 7, Nam. 6, 7

"Nehemiah" (R. Abel) — C.S.S.S. Notes

 

MASWALI YA AYA:

  1. Tengeneza orodha ya matatizo Nehemia alitakiwa kushinda.
  2.  Nehemia alimwomba Mungu aliposikia kwamba kuta za Yerusalemu zilikuwa zimebomoka na kwamba mabaki walikuwa matesoni. Alisema nini?
  3. Kumbuka tukio katika ukumbi wa Artashasta ambapo Nehemia alipata ruhusa kurudi Yudea.
  4. Orodhesha sifa za Nehemia ambazo zilimfanya kiongozi mkuu.

MASWALI YA INSHA:

  1.  Fanya utafiti wa tabia ya Nehemia.
  2. Eleza jinsi Nehemia alikabilianana matatizo ambayo yalimkumba wakati alichukua jukumu la kujenga upya ukuta wa Yerusalemu.
  3.  Katika njia gani Nehemia alikuwa kiongozi mkuu? Toa mifano ya uongozi wake.
  4. Ni mambo gani tunaweza kujifunza kutoka kwa mfano wa Nehemia?

 

 

 

Swahili Title
322. NEHEMIA — MTU WA IMANI NA VITENDO
Sub type
Sub sub type