CSSA 3-4-326 - JESUS’ EARLY LIFE

Swahili

326. MAISHA YA AWALI YA YESU

“Yesu akazidi kuongeze maarifa na kimo na kupendwa na Mungu na binadamu”

Somo letu la mwisho la sehemu ya pili linatuelezea matukio yaliyozunguka kuzaliwa kwa Yesu hadi ibada ya wachungaji katika uwanja wakati walipopata wajumbe malaika, na wakamwona Masihi wa Israeli. Tunaendeleza maisha ya Yesu kuanzia hapa.

Lengo letu katika somo hili ni kuangalia Bwana akitayarishwa kwa kazi yake kuu na kijifunza haja kwetu sisi ya kijitayarisha kwa huduma yake katika ujana wetu.

Lk: 2: 21-52; Mt: 2

TOHARA NA SAFARI YA KWANZA HEKALUNI (Lk. 2:21-38)

Siku nane baada ya kuzaliwa kwake, Mwana wa Mungu alitahiriwa kulingana na Sheria na alipewa jina Yesu (Bwana ataokoa) kama vile malaika alikuwa amemweleza Mariamu wakati alipopata mimba (Lk. 1:31). Asili ya tohara ilikuwa wakati wa Ibrahimu kama ishara ya agano kati ya Mungu na yeye (Mwa 17: 9-11). Hivyo ni sahihi, na pia ilikuwa muhimu (Gal 4: 4), kwa Yesu, ambaye alikuwa atimize agano, kwa kutahiriwa. Tunafuata mfano wake wakati tunakataa “mwili pamoja na upendo na tamaa" (Gal.5:24, 25;. 2:28 Rum, 29).

Siku thelathini na tatu baadaye, kwa mujibu wa Sheria (Law. 12: 4, 6), Maria alimchukua Yesu na kwenda na Yosefu hadi kwenye Hekalu kutoa sadaka iliohitajika kwa ajili ya utakaso, na "ili wamweke mbele ya Bwana ". Tangu wakati Mungu aliwaua Wazaliwa wa kwanza Wamisri na kuwaokoa Waisraeli waliokuwa hai, alikuwa amedai Wazaliwa wa Kwanza kama wake mwenyewe (Mst.23, Kut. 13: 1, 2). Jinsi gani hii ilikuwa kweli kumhusu Yesu, ambaye alikuwa “mtakatifu,mpole, asiye na dosari, tofouti na wenye dhambi” (Ebr. 7:26).

Yusufu na Mariamu inaonekana walikuwa miongoni wa watu maskini wa Israeli, kwa sababu sadaka yao ilikuwa " jozi ya hua wawili au makinda wawili" (Law 12: 8). Kwa nje, safari hii haikuwa tofauti na safari nyingine yoyote. Lakini mbali na Yusufu na Mariamu, kuna watu wengine wawili waliojua zaidi na walikuwa tayari kutangaza furaha wakati wa kukamilishwa kwa miaka mingi ya kutazama na kutumainia. Simoni alikuwa ameambiwa na Roho wa Mungu kwenda Hekaluni siku hio, kwani “kusubiri kwa hamu kwa ukombozi wa Israeli” kulikuwa kumefika mwisho (Mst. 25-27). Je, tunaweza kadiria matarajio yake wakati alielekea hekaluni? Kuadhimishwa kwake kutakamilika wakati “atamchukua Yesu mikononi mwake huku akimtukuza Mungu" (Mst.28). Mtoto yule angekuwa wokovu wa Mungu na nuru yake ingeenea kwa Watu wa Mataifa na Wayahudi pia (Mst 30-32). Kwa mshangao mkubwa Yusufu na Mariamu walisikiza maneno haya- Mwanga wa kungazia Watu wa Mataifa” (Mst.32). Lakini haya hayakuwa yote; Mariamu mwenyewe angeteseka zaidi kabla “maneno yote yaliyo kuwa moyoni mwake” yapate maana kwake (Mst. 35, 51). Wakati Simoni alikuwa anamaliza unabii wake, mjane wa miaka 84, Anna, aliingia na kunena kuhusu ukombozi utakao kamilishwa na Yesu (Mst. 36-38).

ZIARA YA MAMAJUSI (Mt. 2:1-12)

Pengine ni wachache tu katika Yerusalemu waliokuwa wamesikia kuhusu matukio ya ajabu wakati Yesu aliwasilishwa kwa Bwana katika Hekalu, lakini tukio sasa lilitokea ambalo lilisababisha Waisraeli wote kuongea (mst.3) Watu wenye hekima kutoka mashariki waliwasili wakimtafuta “yule aliyezaliwa Mfalme wa Wahayudi” (mst. 2). “Watu hawa hekima” ("Mamajusi") wanaweza kuwa wamehusishwa na shule ya watu wenye hekima ilioelekezwa na Danieli katika Babeli miaka mia sita hapo awali (Dan. 2:48). Pengine walikuwa wamesikia kuhusu utabiri wa Danieli wa majuma sabini (Dan. 9:24 25), kama inavyo kisiwa katika maelezo mwishoni mwa mstari wa 16. Kuangalia kwa mamajusi hakukuwa bila matunda: nyota waliokuwa wakisubiri ilitokea na kuwaongoza hadi alipokuwa Yesu. Tofauti na mtizamo wa Herode na wakazi wote wa Yerusalemu: Watu wa mataifa mengine wakawa wanamtafuta, lakini watu wake wenyewe walikuwa wameingiwa na wasiwasi wa habari hii. Maneno Simeoni ya muda mfupi uliopita sasa yalianza kupata maana. Herode, ambaye mikono yake tayari ilikuwa imemwaga damu na fitina, aliona katika kuzaliwa kwake yule “atakuwa Mfalme wa Wayahudi” tishio kwa nafasi yake bora kabisa. Alijulishwa na makuhani wakuu na waalimu kwamba Masihi angezaliwa Bethlehemu (4-6 Mst, Mik. 5: 2). Ili kuepuka kuwashtua watu, yeye binafsi aliwaita watu wenye hekima na kuwaambia waripoti kwake pindi watakapompataYesu ili aweze "kuja na kumwabudu pia" (Mst. 7-8). Bethlehemu,Watu wenye busara walivyoanza safari yao kuelekea Bethlehemu, nyota ilitokea tena na kuwaongoza hadi mahali walipokuwa wanaenda. Mariamu na Yosefu kwa sasa walikuwa wamepata nyumba (mst.11) Na huko Majasusi walianguka na wakamwabudu Yesu na kutoa zawadi zao. Zawadi hizi zote zilikuwa za gharama kubwa na zilifaa tukio hili: -

Dhahabu - kama vile mfano wa maisha milele ambayo hutokana na imani iliojaribiwa, dhahabu ni zawadi inayofaa Mfalme (linganisha 1 Fal. 10).

Ubani - inatumika kama kiungo katika uvumba ambayo ni ishara ya maombi (Kut. 30:34). Kwa jina lake maombi yatafanywa kwa baba (Yn. 16:23).

Manemane –kiungo kinachotumika katika mafuta kwa kuwateua makuhani wakichukua ofisi. Yesu ni "Kristo", Nabii Mteule. kuhani na mfalme wa Mungu (Kut. 30:23; Yn. 3:34). Manemane pia inaongea uchungu na kifo, hivyo kazi ya Yesu ya kujitoa sadaka imetajwa.

Baada ya kuwasilishwa zawadi zao na heshima zao kwa Masihi wa Israeli, walionywa na Mungu kutorudi na kuripoti kwa Herode (Mst.12) Wakarudi nyumbani wakitumia njia nyingine, bila shaka waliondoka wakifurahia, wakimwacha Herode akiwasubiri kwa hamu na kulaaumu kuchelewa kwao.

KUTOROKEA MISRI: MAJIBU YA HERODE (Mt. 2:13-18).

Herode alikuwa na hasira wakati alitambua kwamba Majasusi walikuwa wamekosa kumtii na kumuepuka. Kwa hasira za kikatili aliamuru kuuwawa kwa watoto wote waliochini ya miaka miwili, Bethlehemu na wilaya zilizo karibu. (Mst. 16) matendo yake yalikuwa ya kinyama na kikatili. Historia ilikuwa inajirudia; “Rakeli”, ishara ya mama wa asili ya Israeli, kwa mara nyingine alikuwa analia kwa kupoteza watoto Maneno ya Yeremia 31:15 yalitamkwa wakati “Rakeli” aliomboleza misururu mirefu ya mateka waliokuwa wakipelekwa Babeli. Alifarijiwa na ahadi ya kurudi. Sasa, kupitia pigo la kikatili la Herode, “Rakeli” alikuwa analia tena. Rakeli, mke wa Yakobo, alikuwa ishara inayofaa ya israeli halisi, kwani alikuwa amepitia huzuni kwa kutoweza kupata mtoto kwa muda mrefu (Mwa. 30: 1), na wakati wa kifo chake akajifungua Beyamini (ambaye alimwita "ben-oni", mwana wa huzuni yangu, Mwa 35: 16-19). Alizikwa katika maeneo jirani ya Bethlehem (Mwa. 48: 7),eneo la uovu wa Herode. Wivu na ghadhabu kali ya Mfalme Herode haikutoshana na riziki ya Bwana. Hakuna binadamu, hata awe na nguvu aje anaweza kupinga kusudi la Mungu. Malaika wa Bwana alimtokea Yusufu katika ndoto, na akamwonya atoroke hadi Misri. Hivyo Yesu akaokolewa kwa mapenzi ya Baba yake wa Mbiguni. Sisi, pia, tunaweza pata faraja kwa ukweli kwamba Mungu anatupenda na anatujali na atatuokoa kutokana na maovu yote. Isitoshe, kitendo cha unyama cha Herode kilipelekea kutimizwa kwa unabii! Mungu alikuwa anatumia njama za binadamu kuendeleza kusudi Lake. Israeli ya asili, mzaliwa wa kwanza Mwana wa Bwana, alikuwa ameitwa atoke Misri hadi kwa taifa (Kut. 04:22), na sasa Yesu alikuwa arejelee tukio hilo la kihistoria (mst. 13-15; Hos 11:1). Kanuni hii inatufikia sisi wenyewe pia. Sisi, pia, kama wana wa Mungu, tumeitwa kutoka kwenye kiza cha (Misri) kuonyesha utukufu wa Bwana (1 Pet. 2: 9-10; Efe. 2: 1-3, 13). Israeli asili kwa mara nyingine wataishi tukio hili katika msafara wa pili baada ya kurudi kwa Kristo (Mik. 7: 14-15; Isa. 11: 10-16).

KUTOKA MISRI HADI NAZARETI (Mt. 2:19-23)

Wakati Herode alikufa, malaika wa Bwana alimtokea Yosefu katika ndoto akiwa na ujumbe arudi Israeli (mst. 19-21). Alipofika, Yosefu alisikia kwamba Arkelao alikuwa anatawala mahali pa babake Herode. Kwa mara nyingine Yusufu aliambiwa na Mungu kile alichopaswa kufanya.Yusufu akafika Galilee ambapo Herode Antipa, mtu mpole kidogo, alitawala, na akafanya makazi Nazarethi (Mst. 22-23). Mathayo anatuambia kwamba hii ilifanyika “kwamba litimie neno lililonenwa na manabii. Naye ataitwa Nazarene”. Hakuna unabii maalum kuhusu jambo hili katika agano la kale, lakini neno Nazarethi lina umuhimu wa “tawi” na kuna unabii ambao unaongea kuhusu Yesu kama tawi (linganisha Isa 11: 1; Yer. 23: 5-6; 33: 14-16; Zek. 3: 8., 6:12). Nazareti ilikuwa imechukiwa na Wayahudi, kama inavyoonekana katika (Yn. 1:46, 7:41, 42, 52). Tena hekima ya Mungu huangaza katika kazi ya Mwanawe na yule ambaye hana uhusiano na utajiri, hadhi au cheo katika maisha haya. Hatuna rekodi ya maisha ya utotoni ya Yesu ila tu kwa maoni yalifanywa na Luka: "Mtoto akakua, akazidi kupata nguvu, akajaa hekima, na neema ya Mungu ilikuwa juu yake" (Lk 2:40).

Isaya anahusisha ukuaji huu wa Mwana wa Mungu katika sura ya 11: 2-3. Ilikuwa ni katika miaka hii ya matayarisho, ambapo Yesu alipata tabia muhimu ya ushirika na Baba yake na kutafakari juu ya Neno lake ambalo lilikuwa chanzo cha nguvu katika huduma yake. Tunaweza kumfikiria akiwa kwenye milima iliozunguka Nazareti asubuhi mapema akitafakari juu ya historia ya Mungu ambayo ilikuwa imetokea katika nyika ya Esdraloni, Mlima Tabori, Mlima Karmel na maeneo mengine aliyoweza kuona. Kwa miaka hio alitafakari umuhimu wa unabii kuhusu kazi yake. Wakati wa huduma yake ilikuwa ni kawaida yake kutumia nyakati za asubuhi katika ushirika wake na Babake. Kiwango cha elimu ya Yesu imeonyeshwa na tukio la muhimu katika maisha yake alipokuwa na umri wa miaka kumi na miwili.

PASAKA YA KWANZA YA YESU (Lk. 2:42-50)

Kila mwaka wazazi wake walihudhuria sikukuu ya Pasaka. Wakati vijana wa kiyahudu walitimiza miaka 12 walichukua jukumu la kulinda Sheria za Musa. Jinsi wakati huu muhimu ulivyokaribia, muda mwingi na jitihada zilitumika katika kukariri sheria. Ni jambo la kushangaza kuona kuelewa kwa hali ya juu alikokuwa nao Mwana wa Mungu kwa umri huu, hadi wakuu wa Sheria wakashangaa. Tunaweza kufikiria mazingira ya matumaini wakati familia ilikuwa inajitayarisha kwa safari ya Yerusalemu. Kwa jinsi gani angeweza kutafakari umuhimu wa Pasaka, Kwa mazingira yake ya kihistoria, na jinsi miaka ilivyosonga awe na hali ya kuelewa kwa kina jinsi yeye mwenyewe anavyohusika. Pasaka hii ya Yerusalemu lazima iwe ilikuwa tukio lenye furaha. Kurudi nyumbani akiwa miongoni mwa marafiki na jamaa, Yosefu na Mariamu wakumkosa Yesu mpaka pale walikuwa washafanya safari ya siku moja (Mst. 43-45). Walipomkosa walirejea Yerusalemu kwa haraka. Lakini hata hivyo haikuwa hadi siku ya tatu ambapo walimpata katika Hekalu, akiulizwa na kujibu maswali ya Madaktari wa Sheria (Mst. 46-47).

Yusufu na Mariamu walipata nafuu lakini walishangazwa kwa hali yake ya kutojali. Mariamu alimwendea mwanawe kwa maneno haya “Kwa nini umetutenda hivyo sisi? Tazama, baba yako na mimi tumekuwa tukikutafuta kwa huzuni "(Mst. 48) matamshi kama haya yalikuwa ya kawaida kulingana na mazingira lakini hawakuwa wanaongea na Mwana wao pekee bali mwana wa Mungu pia. Yesu alionyesha kuelewa kwake kwa uhusiano huu katika jibu lake ambapo alimkumbusha Mariamu kwa upole kwamba hakuwa mwana wa Yosefu: “Hamkujua kwamba inanipasa kuwa katika nyumba ya Baba yangu ", au katika nakala mpya," Je, hamjui kwamba ni lazima niwe katika nyumba Baba yangu? Hofu ya Bwana ilionekana wazi kwake na ilionekana wazi kwamba anafaa kuhusishwa katika masuala ya Baba yake (Mst 49-50).

KUKUA HADI KUWA MTU MZIMA (Lk. 2:51-52)

Hakuna mambo zaidi yamesemwa kuhusu maisha ya Yesu kutoka Pasaka hii hadi anapotokea katika kingo za mto Yorodani akiwa na umri wa 30, ila tu muhtasari wa kumbukumbu katika (Lk. 2:52), na kile kinaweza hitimishwa kutoka kwa maoni yake wakati wa huduma yake. Hakuhudhuria vituo vyovyote vya mafunzo lakini mara kwa mara alihudhuria sinagogi (Lk. 4:16, 22). Yesu alimfuata Yusufu na akawa seremala. Inaonekana kama Yosefu alifariki katika kipindi hiki kwani hakuna rekodi yake wakati wa huduma ya Yesu. Yesu alikuwa kifungua mimba wa familia kubwa ilikuwa na ndugu wanne na angalau madada wawili (Mk 6: 3). Kuwekwa mahali pa majukumu kama kiongozi na anayetoa, alijifunza mengi kuhusu asili ya binadamu na kuongeza utambuzi wake kuhusu hukumu, na rehema, inayobainika wazi katika huduma yake. Mafumbo mengi aliyotumia na mifano bila shaka ilikuwa na asili wakati wa maisha yake ya awali Nazareti

MAMBO TUNAYOJIFUNZA:

  • Yesu alitahiriwa na sisi tunafuata mfano wake kwa kusulibisha anasa na tamaa za mwili (Gal. 5:24, 25; Kol. 3: 1-5).

  • Wayahudi wachache wajawazito, kama Simeoni na Anna, walisubiri kuja kwake. Tunapaswa kuwa na roho ile ile ya msisimko na kuishi kama tunasubiri kuja kwake mara ya pili (2 Tim. 4: 8., Mt. 24: 42-47; Lk 21: 34-36).

  • Mungu alimlinda Mwana wake kutoka mikono katili ya Herode. Kama wana wake pia tunaweza kuchukua faraja kwamba Baba atatulinda na kututunza sisi pia (Zab. 34: 6-8; Rum. 8: 31-39).
    • Kama Yesu alivyotoka Misri, hivyo sisi tunaacha giza la dunia na kuja katika mwanga wa utukufu wa kweli (2 1 Pet. 9-10; 1 The. 5: 4-6).

  • Katika hekima yake Mungu alichagua Nazareti ilio dharauliwa kama sehemu ya maandalizi kwa ajili ya Mwana wake. Utajiri, heshima, hadhi, kwa mara nyingi ni vikwazo katika njia ya ukuaji wa kiroho (Flp. 3: 7-8; 1 Kor.1: 17-18, 26-31).

  • Hali ya kuwajibika ya Yesu ilikuwa dhahiri katika umri mdogo. Hata ingawa alikuwa chombo kilichotayarishwa kwa ajili ya Bwana, tunapaswa kukumbuka maneno ya Sulemani, "Kumbuka Muumba wako katika siku za ujana wako .." (Mhu. 12: 1). Mungu ana kusudi na sisi pia.

 

MAKTABA YA KUREJELEA:

"The Story of the Bible" (H.P. Mansfield)—Tol. 8, Kurasa 29-67

"A Life of Jesus" (M. Purkis)—Kitabu 1, Sura 2-5

"Nazareth Revisited" (R. Roberts)—Sura 8-10

MASWALI YA AYA:

  1. Ni matukio gani yalitokea wakati Yesu alipelekwa Hekaluni kufuatia kipindi cha utakaso cha mama yake?

  2. Ni zawadi gani Mamamjusi walimletea mtoto Yesu na umuhimu wake ulikuwa upi?

  3. Ni mambo gani yalisaidia maendeleo ya Yesu kabla ya huduma yake akiwa na umri wa miaka 30?

  4. Ni tukio gani muhimu lilifanyika katika Hekalu wakati Yesu alikuwa na miaka 12? Je, linaonyesha nini kuhusu tabia ya Yesu?

MASWALI YA INSHA:

  1. Jadili riziki ya Bwana katika maisha yake ya awali.

  2. Elezea ziara ya mamajusi katika kumtafuta Yesu na masomo kwetu katika kwenda kwao kwake.

  3. Orodhesha matukio ambayo yalisababisha Yesu kuchukuliwa na Yusufu na Mariamu kutoka Bethlehemu hadi Misri halafu Nazareti. Ni unabii upi wa Agano la Kale uliotimizwa katika harakati hizi?

  4. Orodhesha mambo ambayo sisi tunajua kuhusu ujana waYesu na ukuaji wake hadi akawa mtu mzima. Tabia ya Maria kwa hayo ilikuwa ipi? Ni masomo gani tunayojifunza kutokana na hili?

 

Swahili Title
326. MAISHA YA AWALI YA YESU
Sub type
Sub sub type