328

Swahili

328. NIKODEMA ANAMJIA YESU USIKU

"Tunajua kwamba wewe ndiye mwalimu aliyetumwa na Mungu"

Baada ya Yesu kufanya  muujiza wake wa kwanza wa kubadili maji kuwa pombe katika Kana, alisafiri kaskazini kwenda Kafarnaumu. Kule alikaa na mamake, ndugu zake na wanafunzi wake, kwa muda mfupi. Wakati Pasaka ilikaribia, Yesu alisafiri kusini hadi Yerusalemu. Hivyo akaanza iliojulikana kama huduma yake ya kwanza ya Yudea, matukio ambayo yameandikwa katika kitabu cha Yohana pekee. Pasaka hii ilikuwa sherehe yake ya kwanza ya  huduma yake katika mji mkuu. Yohana amerekodi matukio mawili makuu: utakaso wa hekalu na ziara ya Nikodemo 'usiku.

Lengo la somo hili ni kuona kwamba Mungu lazima abudiwe kwa utakatifu na kuelewa haja ya kujibu kazi iliyofanywa na Mwana Wake.

Yohana 2:13-25; 3:1-21

UTAKASO WA HEKALU (Yn. 2:13-22)

Hapakuwa na nafasi sahihi ya Yesu kujionyesha kupita Yerusalemu, na kukiwa na watu waliokuwa wamekusanyika kwa sherehe ya Pasaka, wakati ulikuwa umefika. Watawala walipaswa kupewa nafasi ya kwanza ya kumkubali Masihi. Lakini kwa njia gani angetokea? Malaki alikuwa amewaonya kwamba “mjumbe wa agano" angekuja kwa ghafla na bila kutarajiwa kwa Hekalu yake, na kama moto wa mtu asafishaye na sabuni ya dobi, hivyo angeweza kuondoa rushwa (Mal. 3:1-3). Katika wakati ufao “Bwana ambaye walimtafuta akaja hekaluni mwake”, na kile alichokifanya kilitazamwa? Mahakama ilikuwa imetengewa kwa watu wa mataifa ilikuwa imejaa vibanda vya wanyama na meza za wabadili fedha! Ilikuwa ni jambo la Busara kwamba wale waliokuwa wa nchi za mbali waweze kufanya biashara katika mahali palipofaa wanyama wa sadaka, na ilikuwa muhimu kwamba walikuwa waweze kubadili sarafu zao ili waweze kufanya biashara. Lakini kile kilichoanza kama jambo lisilo baya, kwa muda likawa na ufisadi- watu wa mataifa hawangeweza kumwabudu Mungu katika mahali walipotengewa, na wanyama wa sadaka wangeweza kununuliwa tu kwa sarafu za Hekalu, ambazo zilibadilishwa kwa riba ya juu ili kuleta faida kubwa kwa makuhani! Hivyo wacha Mungu walinyanyaswa bila ya  aibu na huduma ya hekalu ikahusishwa na matatizo. Mungu aliona yote haya; kati ya makelele ya  sauti za wanyama na milio ya sarafu zikibadilishwa na wale walikuwa na “jicho ovu” la faida, ilikuwa haiwezekani  “kumwabudu Bwana kwa uzuri wa utakatifu" (Zab. 96: 9).

Ghadhabu ya Bwana iliwaka na hakuwa na huruma. Akisokota baadhi ya kamba na kutengeneza mijeledi, aliwafukuza wote kutoka Hekaluni, kondoo na ngombe; alirusha meza kando, akatawanya makundi ya sarafu, wakati watu wakitoroka kwa woga. Akiwageukia wale waliosalia, wale waliouza njiwa, akawapa amri, "Ondoeni vitu hivi hapa: msiifanye nyumba ya Baba yangu kuwa nyumba ya biashara” pole pole dhoruba ikatulia. Hakuna mtu aliyempinga. Wale waliokuwa wahusika wakaja lakini shambulio lao lilisitishwa hata kabla lianze na umbo lililokuwa kimya mbele yao, macho yake yakiwaka kwa hasira na changamoto. Inaonekana walihisi wenye hatia- pengine alikuwa Masihi, kwani Yohana mbatizaji alikuwa amewaambia kwamba atakuja. Waliimuuliza “awaonyeshe” ishara ya kile alichokuwa amefanya (linganisha Kum.13: 1-2). Yesu aliwapa ishara. "Vunjeni Hekalu hili (Gk" naos ") na kwa siku tatu nitalisimamisha tena". Hii haikuwa changamoto ya bure lakini unabii. Yesu alikuwa anatabiri kifo chake kwa mikono yao na pia kwa kufufuka kwake baada ya siku tatu. Hangejifufua kutoka kwa  wafu, lakini kwa “utii wa mauti” angepata neema ya Baba yake ambaye angemfufua (Yn.10: 17-18; Flp. 2: 8-11). maneno yake ya hukumu na upinzani kwa watawala wa Yerusalemu yalikuwa hatua za awali katika njia ambayo ingempeleka hadi msalabani, na maneno ya Yesu yalionyesha kwamba alielewa hili. Sio hio tu, lakini mateso ya Mwana wa Mungu yangekuwa dhambi ambayo ingefuatia majanga ya mwaka 70 BK wakati, Heklu, mji na nchi ingepotea kati ya maovu yasiyoelezeka. Hekalu hatimaye ilibadilishwa na mahali papya patakatifu, jiwe la msingi ambalo lilikuwa Mwana wa Mungu; “Tazama, naweka jiwe la Msingi Sayuni,  jiwe lililojaribiwa, msingi dhabiti” (Isa. 28:16). Ni dhahiri kwamba wakati Yesu aliashiria hekalu la mwili wake, alitumia neno (Gk. "Naos") ambalo inaelezea mahali pa ndani patakatifu ambapo Mungu anaishi, palipo patakatifu zaidi,  ilhali aliongea kuhusu hekalu kama “nyumba” au “makazi” (Gk. "oikon").

Mungu alikuwa ameondoka kwa mmoja na sasa alikuwa anaishi katika mwingine, mwili wa Mwana wake (Yn. 1:14). Tamko la Yesu katika mstari wa 20 halijasahaulika na Wayahudi wala Wanafunzi. Baada ya miaka mitatu ilielezewa visivyo na Wayahudi katika juhudi za kumtuhumu, na hivyo ukweli wa maneno yenyewe yakaanzishwa kwa makosa. Walikuwa wale watakao mwangamiza(Mt. 26:61). Wanafunzi waliyakumbuka kwa kusudi bora: wakati hali ya kukata tamaa ilikuwa imebadilishwa na furaha ya kumwona Bwana aliyefufuka, wanafunzi “walikumbuka alikuwa amewaambia; na waliamini maandishi na neno ambalo Yesu alikuwa amesema” (Mst. 22). Kwao, kauli ya Yesu ikawa ishara ya utawala wake na Umasihi. Utakaso wa Hekalu ulifuatiwa na matendo ya  nguvu (Mst.23). Hapa palikuwa na ushahidi wa kutosha wa mamlaka yake kwa wale waliokuwa na macho ya kumwona. Wengi waliamini walipoona kazi hizi, lakini ilikuwa tu utambuzi wa juu wa nguvu zake. Israeli ilikuwa imeona majanga ya ajabu yaliyotokea Misri, lakini walirudi na kukosa imani baadaye kidogo wakiwa jagwani (Zab. 95: 8-11). Yesu, ambaye alijua kila mtu, “ hakuwa na imani nao” (Mst. 24. RSV) alijua  utii wao ulikuwa na chanzo kwa mshangao, na wala sio kwa imani, na alitenda kuelekea kwao ipasavyo.

NIKODEMA ANAKUJA KWA YESU (Yn. 3:1-21).

Yesu alijua kwamba kukubaliwa na watu kutabadilika haraka na kuwa chuki kubwa, hakuwa kwa njia yeyote akibangua. Alikuwa na uwezo wa kutafuta mioyo ya watu, hivyo wakati Nikodemo alikuja kwake alitambua kwa mtu huyu sio tu udhaifu wake lakini uwezekano wa imani yenye nguvu. Katika tafsiri ya Rotherhamu, Nikodema analinganishwa na wasikilizaji wake kwa ujumla kwa Yohana 3:1 inasoma “ basi palikuwa na mtu mmoja Mfarisayo, jina lake Nikodemo” hata hivyo  kulikuwa ISIPOKUWA mtu miongoni mwa  Wafarisayo...” tathmini ya Yesu ya Nikodemo ilikuwa ya kweli, kwani jinsi muda ulivyo songa tunapata imani yake ikiimarika kwa nguvu na, licha ya matatizo ya nafasi yake kama kiongozi wa Israeli, alichukua msimamo dhabiti na Bwana katika:

  1. Akipinga dhidi ya mbinu haramu za Baraza wakati walitaka kumhukumu Yesu (7:51); na
  2. Kuungana na Yusufu wa Arimathaya kumpa Bwana Mazishi ya heshima (19:39).

Aliongea kama mwakilishi wa Wafarisayo: "Mwalimu, tunajua kwamba wewe ni mwalimu ..." (Mst. 2) na maelezo yaliyokuwa yametolewa kumhusu ni “Mtu (kutoka) Farisayo" (Mst.1 ). Labda aliwakilisha mmoja kati ya wale viongozi waliokuwa na fikra nzuri katika kuuliza kuhusu huduma ya Yesu, katika njia sawa kwa wajumbe waliokuwa wametumwa kwa Yohana (1:19). Mahojiano yalifanyika "usiku" na inaonekana alitaka kuzuia makabiliano ya moja kwa moja na Yesu- imani yake haikuwa imetosha kumkubalia aharibu msimamo wake. Baadaye Yesu alisema kwamba watu “wanapenda giza kuliko mwangaza” inaonekana alikuwa anarejelea kitendo cha Nikodema cha kumtembelea usiku  (Mst. 19). Nikodemo akamwambia, "Tunajua kwamba wewe ni mwalimu uliyetumwa na Mungu, maana hakuna mtu awezaye kufanya ishara unazozifanya, Mungu asipokuwa pamoja nawe" (Mst. 2). Yesu akamjibu “amini, amini, nakuambia, mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi akauona ufalme wa Mungu (Mst.3) Mshangao wa Nikodema unaonekana katika swali lake. “awezaje kuzaliwa akiwa mzee? Awezaje kuingia katika tumboni mwa mamake kwa mara ya pili akazaliwa (Mst.4) Yesu akaelezea maneno yake zaidi; “ Mtu asipozaliwa kwa maji na Roho matakatifu hawezi kuingia katika ufalme wa Mungu.

Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa na Roho ni Roho” (Mst.5 -6). Yesu alitarajia Nikodema kuelewa maneno yake, inaonekana wazi katika karipio lake katika mistari 10 na 12. Yesu alizungumza kuhusu vizazi vitatu- ya mwili (wakati wa kujifungua), ya maji, na ya Roho (yaani ubatizo) muhimu kwa wakovu (Mst. 3; Mk. 16:16; Gal. 3:27-29).  Bila unyenyekevu, toba na imani inayoashiria, kiingilio kwa Ufalme wa Mungu haiwezekani. Ubatizo kwa mara nyingi unafananishwa na kuzaliwa upya (Tit. 3: 5 Roth, 1 Pet.1:23; 2: 1-2), kwani ndani yake muumini anatambua asili yake ya mwili haina maana kwake wakati  uzima wa milele unahusika, na kwamba ni kiumbe kipya, mwana wa Mungu anayetegemea Neno la Mungu. Lakini hakuna kubadilika kwa asili au hali ya mwili wakati wa ubatizo.

Hii huja wakati “binadamu anachukua hali ya uzima wa milele” baada ya  kufufuka na anakuwa roho. Hii ndio Yesu alitaja kama “kuzaliwa kwa Roho”. Mtume Paulo alitilia mkazo hili kwa kusema "mwili na damu haziwezi kuridhi ufalme wa Mungu; wala uharibufu kuridhi kutokuharibu” (1 Kor. 15:50). Yesu aliendelea kueleza, “Yule aliyezaliwa kwa Roho” ni kama upepo, anaweza kutoka sehemu moja hadi nyingine akisikika lakini bila kuonekana (linganisha Mst.7-8; malaika katika Zab 104:4 Roth, 2 Sam 5:24) kufuatia “Kuzaliwa kwake kwa Roho” au kufufuka, Yesu alichukua mwili wa “ nyama na mifupa”, na uwezo wa kuonekana na kugusika lakini akiwa na uwezo wa kusafiri bila kuonekana (Lk. 24:39, 40;.Yn 20:19).kwa mara nyingine Nikodemo alishangaa na Bwana, kama Malaki akamkaripia (Mst.9-10; Mal. 2: 7). Alifananisha ujinga wa Nikodema na maarifa yao  (sisi katika Mst.11 ni pamoja na Yohana Mbatizaji) na anamshutumu Nikodema kama mwakilishi wa Wayahudi kwa kumkataa shahidi au ushuhuda wa Yesu na Yohana. Bwana kisha alizungumza kuhusu kile kukataa kwao kungesababisha, yaani kusulubiwa kwake: Na kama vile Musa alivyomwinua yule nyoka jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa" (Mst.14). Kulikuwa na tukio wakati Sheria na  ukuhani wake ulikuwa umeonyesha hali ya kushindwa kutoa wokovu na hio ilikuwa Jagwani wakati Israeli walikuwa wametenda dhambi na “nyoka wakali” walitumwa miongoni mwa watu (Hes. 21: 4-9).

Sadaka maalum ya dhambi ya kitaifa ilikuwa imepitishwa na makuhani, njia nyingine ilitolewa na Mungu. Wale walioumwa na nyoka wangepata wokovu kwa kumwangalia kwa imani nyoka  wa shaba aliyeinuliwa juu ambapo uchungu wa dhambi haungepatikana. Imani katika ufanisi wake ilileta  wokovu kwa “kila mtu” na sio waisraeli pekee (Hes. 21: 8, 9). Haya yalikuwa mafunzo ya kiroho,  “Mambo ya Mbiguni”, ambayo Yesu alikuwa anamfundisha Nikodema kwani Yesu pia angetundikwa na kuinuliwa juu. Angalia jinsi Bwana alisisitiza kwamba wokovu ambao ungekuja kupitia kwake ungekuwa wa Wayahudi pamoja na Watu wa mataifa. Hautakuja kwa njia ya Sheria, bali kwa "mlango wa imani." (Maneno "dunia" na "yeyote" katika mstari 15-16 yanaunganisha, Mataifa na vilevile Wayahudi; linganisha Rum. 10: 11-13). Ilikuwa kwa furaha ya Nikodema kwamba hatimaye alimkubali Yesu na hakuwa miongoni mwa wale waliomsulubisha Bwana. Kwa hivyo alitimiza kila neno alilokuwa amesikia hapo awali na hivyo imani yake ikakua na akaweza kuchukua  msimamo dhabiti na kusimama na Yusufu wa Arimathaya. Yesu akahitimisha kwa kusisitiza upendo wa Mungu kwa kumtoa Mwanawe. Ingawa Yesu angechukuliwa na mkono mwovu na kuuawa, kifo chake kilikuwa kinahitajika kwani kilikuwa kimeamuliwa na Mungu, kwamba aonyeshwe kuwa mwenye haki wakati anahalalisha wale watakaokuja kwake kupitia Mwana wake.

Lakini wakati Mungu katika upendo alimtuma Mwana wake ili kuwaokoa watu, lakini matokea yake yaliona wengi “wakianguaka” Kushindwa kuamini lazima kumaanishe kulaaniwa; uwepo wa Mwana wa Mungu ungesababisha uamuzi kwa upande wa binadamu! Yesu alionyesha wazi kwamba Babake, alikuwa mwanga gizani (Mst. 19; 1: 8-9). Kiwango cha uwajibikaji wa binadamu uliongezeka kwani hakuweza kudai ujinga kama udhuru kwa dhambi (linganisha 15:22; Mdo.17: 30-31). Matokea ya kutisha ya mwanga juu ya wanadamu ni kuwamulika wakiwa gizani; kwa sababu tabia mbaya huongopa kumulikwa na  mwanga na hivyo kukataa kuelimishwa na kuokolewa (Mst.20) Kwa upande mwingine, wachache wanaotafuta ukweli watakuja kwa Mungu kwa Mungu(Mst. 21).

MAMBO TUNAYOJIFUNZA:

  • Yesu hakuweza kuvumilia rushwa katika ibada, na hata leo atakubali sisi kumwabudu Mungu pekee "kwa uzuri wa utakatifu".
  • Yesu alielewa asili ya binadamu kikamilifu, na yeye kama mwamuzi wetu, tunapaswa kujitahidi kusafisha mawazo yetu, maneno na matendo.
  • Ingawa Nikodemo alishangazwa mno na maneno ya Yesu, hakukata tamaa. Kwa kirefu alikuwa tayari kuchukua msimamo chini ya msalaba. Hivyo pia, lazima imani yetu na ujasiri kwa ajili ya Kristo ikue.
  • Upendo wa Mungu umeonyeshwa katika zawadi ya Mwana wake, na Yeye anataka watu kujibu katika imani na kuokolewa badala ya kuhukumiwa.
  • Uwepo wa "mwanga" (au maarifa ya Mungu) unafanya watu kuwa jukumu la Mungu.

MAKTABA YA KUREJELEA:

"A Life of Jesus" (M. Purkis)—Kitabu 3, Sura 1, 2

"The Gospel of John" (J. Carter)—Kurasa 42-63

"Nazareth Revisited" (R. Roberts)—Sura 12 na 13

MASWALI YA AYA:

  1.  Kwa nini Yesu alitakasa Hekalu alipofika Yerusalemu mwanzoni mwa huduma yake ya hadharani?
  2. Ni "ishara" gani Yesu alitoa baada kusafisha Hekalu mwanzoni mwa huduma yake?  Nani ambaye baadaye alikumbuka kile alichosema kuhusu ishara hii?
  3. Elezea kauli ifuatayo ambayo ilitolewa na Yesu kwa Nikodemo: "Mtu asipozaliwa kwa maji na Roho, hawezi kamwe kuingia katika ufalme wa Mungu."

MASWALI YA INSHA

  1. Malaki nabii alisema: "Bwana mnayemtafuta atakuja kwa ghafla katika hekalu lake". Andika insha juu ya maoni haya kuhusiana na huduma ya Kristo.
  2.  Andika insha juu ya mazungumzo ambayo yalifanyika wakati Nikodemo alimwendea Yesu usiku.
  3. Yesu alisema nini kwa Nikodemo kuhusu yeye "kuinuliwa"? Taja katika jibu lako tukio muhimu lililotokea Jagwani na pia masomo ya tukio hili na maneno ya Yesu kwetu sisi.

 

 

Swahili Title
328. NIKODEMA ANAMJIA YESU USIKU
Sub type
Sub sub type