330

Swahili

330. YESU ANAWAITA WANAFUNZI WAKE

"Kama mtu yeyote anataka kuwa mfuasi wangu, lazima ajikane mwenyewe ..."

Wanafunzi wa Yesu hawakuchaguliwa wote wakati mmoja, lakini mmoja mmoja ama wawili wawili. Wa kwanza kati ya wanafunzi alikuwa Yohana Mbatizaji, ambaye aliwaongoza kwa Yesu.. Jinsi Wanafunzi waliandamana na Yesu ujuzi wao wa Neno la Mungu uliongezeka, na  walijifunza kutoka kwake kwamba unafunzi wa kweli unahitaji kwamba binadamu aweke Mungu mwanzo katika maisha yake. Kama vile wakati ulivyosonga, ilikuwa ni muhimu kwa Yesu kuchagua kutoka miongoni mwao wanafunzi kumi na wawili ambao watakuwa na jukumu la kuhubiri na kudumisha ukweli. Hawa watu waliitwa mitume. Lengo la somo hili ni kuona jibu kamili ambalo watu lazima watoe kwa Mwana wa Mungu.

Yohana 1:29-51; Luka 5:1-11, 27-28; 6:12-16

"MWANAKONDOO WA MUNGU" (Yn.1:29-30)

Ilikuwa ni siku baada ya Yohana Mbatizaji kukutana na wajumbe kutoka Sanhedrini(baraza) alipomwona Yesu akimjia, na akatangaza kwa umati uliokusanyika kwamba  “Mwana-kondoo wa Mungu, aondoaye dhambi za dunia”. Hili lilikuwa tangazo kwamba alikuwa yule ambaye kupitia kwake binadamu wangepatanishwa na Mungu. Katika Edeni, Adamu aliambiwa kwamba majani ya mtini hayawezi kufunika dhambi yake- ila tu ngozi za wanyama( kutoka kwa kondoo waliotolewa na Mungu) zingefanya hivyo (Mwa. 3: 7, 21).  Kondoo pia walichinjwa kuokoa kifungua mimba wote wa Israeli wakati wale wa Wamisri waliangamizwa  (Kut. 12:12, 13), Wakati kondoo walitolewa kila asubuhi na jioni kama sadaka ya kuteketezwa (Hes 28: 3, 4). Kondoo walionyesha Wayahudi jukumu la Masihi, lakini kazi ya Yesu ilikuwa kuleta majibu makubwa, kwani alikuwa Mwanakondoo wa Mungu anayechukua “DHAMBI YA ULIMWENGU".

MWANAFUNZI WA KWANZA (Yohana 1: 35-42).

Siku nyingine ikapita na Yohana Mbatizaji alikuwa amesimama na wanafunzi wake wawili- Andrea (ndugu yake Simoni Petro) na pengine Yohana, mwandishi wa Injili (13:23 linganisha Yohana 19:26). Kuona Yesu akipita, Mbatizaji akanyoosha kidole kwa wanafunzi wake, akisema kwa mara nyingine, "Tazama Mwana-kondoo wa Mungu",na mara hio Andrea na Yohana wakajiondoa kwake na kumfuata Yesu. Wanafunzi hawa wakati huo hawakujua msiba ambao ungemkumba Yesu (Linganisha.Lk. 18:34). Ilikuwa inatosha kwao  kwamba Yohana alikuwa ameongea kuhusu Masihi wa Israeli, Mwana wa Mungu, na  yule aliye onyeshwa kwao.  Wangemfuata. Yesu aligeuka na kuwauliza kuhusu nia yao na walitaka mahojiano na yeye ili waweze kujadiliana kwa kina asili ya  wito wake: "Mwalimu", walisema, “unaishi wapi”. Akajibu “Njooni nanyi mtaona” na  ilikuwa mchana- “saa kumi”- waliongea na Bwana na kukaa na yeye usiku mzima. Mtu anaweza kufikiria  jinsi roho zao zilishangaa kama vile Yesu alivyowafunza. Wakiwa wamesisimuliwa na mjadala wao na Bwana, Andrea akampata Simeoni ndugu yake na kusema, "Tumemwona Masihi" Wangekuwa mara nyingi wamejadili kuja kwa Masihi wa Israeli, hivyo Simeoni hakusita kumfuata Andrea.  Ghafla alifanywa kupata ufahamu wa uwepo wa Bwana, bila utambulisho rasmi, Yesu alimwambia Simeoni kwamba alimjua tayari: "Wewe ni Simoni mwana wa Yohane," alisema. “na wewe utaitwa Kefa, ambayo kwa ufafanuzi wake,  Jiwe”. Uzoefu wa maisha, katika huduma kwa Bwana wake,  ungefanya alama kwa  Simeoni. Jina lake kama tabia yake, ingebadilika. Angekuwa Kefa, au Petro. Hamu yake, tabia yake ya haraka hatimaye ingebadilishwa na  utulivu wa mwamba ulio  muhimu katika kudumisha ukweli (Mt. 16: 16-18).

WITO WA FILIPO NA NATHANIELI (Yn. 1:43-51)

Kesho yake Yesu alitamani kutoka Yudea na kwenda Galilaya umbali wa kilomita 80 au 90 kaskazini. Andrea, Yohana na Simoni, kama yeye, walikuwa wametoka Galilaya. Walikuwa wamekuja kusikiza mahubiri ya Mbatizaji, ambaye alikuwa amewaongoza kwa Kristo, na ambaye kazi yake na wao ilikuwa imekamilika. Ilikuwa inatarajiwa kwamba  wangerudi na yeye hadi Galilaya. Wakiwa njiani, Yesu alisimama kupata Mwanafuzi mwengine. Mazingira ya wito wake hayajawekwa wazi; kwa kifupi Yesu alimwambia Filipo, “Nifuate” inawezekana alikuwa ameonyeshwa na Andrea na Simoni Petro kwani wote walikuwa wametoka Bethsaida (mji wa Samaki). Walikuwa wanapitia wimbi la shauku kubwa. Filipo aliharakisha kumtafuta rafiki yake Nathanieli, "Tumemwona yule ambaye Musa katika Sheria na manabii waliandika habari zake, Yesu wa Nazareti mwana wa Yusufu." Lakini Nathanaeli akauliza zaidi. Nazareti alijua kama sehemu ya kudharauliwa Galilaya (linganisha 1 Fal. 9:12, 13). Masihi alikuwa aje kutoka Yerusalemu, hivyo akauliza "Je, kuna kitu chema chaweza toka Nazareti?" "Njoo, uone, " alisema. Yesu alijua nyoyo za watu wote.

Jinsi Nathanieli alivyokaribia alisikia  Yesu akisema: “Tazama Mwisraeli kweli kweli hamna hila ndani yake” Nathanieli alikuwa miongoni mwa wale waliokuwa na moyo wa dhati na wale ambao hawakutishwa na kile kilichoonekana kama hila ama undanganyifu. Akajibu: “umepataje kunitambua”, na aliambiwa, “kabla Filipo kukuita ulikuwapo chini ya mtini, nilikuona”. Nathanieli alishangaa. Mashaka yake yote yakapotea. Hili lilikuwa onyesho la nguvu ambalo lilionyesha mkono wa Mungu. Hapa hapakuwa “Mwana wa Yusufu”, hivyo akakiri: Rabi wewe u Mwana wa Mungu; ndiwe mfalme wa Israeli”. Aliweza kuona yule aliyekuwa mbele yake kama utimizo wa sheria na manabii- mridhi wa Daudi na mflame wa Isreali aliyeahidiwa (linganisha Zab 2: 2, 7, 2 Sam 7:14; Isa 9: 6-7) . Lakini Yesu aliendelea zaidi. “ kwa sababu nilikuambia nilikuona chini ya mtini, wamini? Utaona mambo makuu kuliko haya. Akamwambia, amini amini, nakwambia, mtaziona mbigu zimefunguka na malaika wa Mungu wakishuka na kupaa juu ya Mwana wa Adamu” "(linganisha. Mwa 28:12). Inaonekana kwamba Nathanieli alikuwa anasoma chini ya mtini, ambayo Yesu alikuwa anaashiria Mwanzo 28. Yakobo alikuwa ameondoka  kwa wazazi wake na ilibidi kuishi Padanaramu na mjomba wake Labani kwa njia ya hila yake. Baadaye alifunzwa kumtegemea Mungu na hili lilidhibitswa wakati jina lake lilibadilishwa kutoka Yakobo hadi (“Mshika kisigino”) kwa Israeli ("mkuu na Mungu") Yesu alimtaja Nathanieli kama “Mwisraeli wa Kweli, ambaye ndani yake hamna hila” inataja maisha ya Yakobo. Kama kweli akili ya Nathanieli ilikuwa imezama katika sehemu hii ya andiko, fikiria jinsi alivyochukulia jambo hili. Yule aliyekuwa mbele yake, hakujua tu pale alipokuwa bali alijua mpaka fikra zake. Si ajabu alikiri kwamba Yesu alikuwa Mwana wa Mungu na Mfalme wa Israeli (Mst. 49).

KIINI CHA UANAFUNZI WA KWELI (Lk. 5:1-11, 27, 28).

Yesu, akaenda mbele, maneno yake na kazi yake yalivutia watu kwake. Polepole idadi ya wanafunzi ikaongezeka, kwa mfano wakati Mathayo aliacha chombo chake kule Kapernaumu. Yesu alimwambia, "Nifuate! Akayaacha yote, akaondoka, akamfuata". Kulikuwa na hali ya kuhitimisha katika uamuzi wake ambao ulikosekana katika majibu ya wanafunzi wake wa kwanza, kwani wakati walirudi Galilaya na Yesu, wachache ndio waliobaki kwa upande wake, wale wengine walirudi kwa kazi zao wakati Yesu aliendelea kuhubiri na kutenda miujiza. Walikuwa waonyeshwe kwamba uanafunzi katika Kristo ulihusisha kumweka Mungu mbele na mwanzo katika maisha. Rekodi katika Luka 5 inasimamia Mt. 4: 18-22 na Mk. 1: 16-20. Simoni, Andrea,  Yakobo na Yohana walikuwa wanafanya kazi karibu na kingo za mto, na walimsikia  Yesu. Walikuwa wamevua usiku mzima, lakini hawakushika chochote. Na sasa, alfajiri, watu walimsogelea kusikia neno la Mungu, mashua  zilikuwa zimetiwa nanga karibu na kingo za mto na wavuvi wanne walikuwa wanajishughulisha na kuosha na wakitengeneza nyavu zao. Umati uliongezeka na kuwa mkubwa hadi Yesu akapanda Mashua ya Simoni na kusonga mbali na kingo ya mto ili aweze kuongea na watu akiwa ndani ya mashua. Alipomaliza kuongea, akamwambia Simoni apeleke mashua  ndani zaidi mtoni na ashushe nyavu zake avue samaki. Walikuwa wamekesha usiku mzima bila kupata chochote. Ilionekana bure kurudi tena. Matokeo yalikuwa ya ajabu. Idadi kubwa ya smaki walishikwa, hivyo kwamba mashua ingine ilitafutwa na pia hio ikajaa samaki- nyavu ikakatika na mashua ilikuwa katika hatari ya kuzama. Wanafunzi  walishangaa. Simoni Petro alishikwa na hali ya kutofaa, lakini Yesu akamwambia "Usiogope, tangu sasa utakuwa ukivua WATU." Baada ya kuleta mashua ukingoni, “wakaachavyote wakamfuata”. Somo walilofuzwa liliwafurahisha sana. Na hatupaswi kusahau hili. Ni rahisi kufikiria Mungu anapendezwa nasi wakati tunafanya kazi yetu ya kila siku, wakati kila saa, tunasimama bila kufanya chochote katika uwanja wa injili. Mara nyingi, hata juhudi zetu katika kazi zetu za kila siku hazifauli kwani Mungu hajahusishwa. Kama  wanafunzi, tunapaswa kukumbuka kwamba Mungu ana haja ya sisi “kuvua” watu kuliko samaki. Atatutumia katika kusudi hili kama sisi “(kama wanafunzi) tutaweka maisha yetu katika Neno, na sio katika Dunia

WALE KUMI NA WAWILI (Lk. 6:12-13)

Idadi ya wanaume na wanawake ambao walijiunga na Yesu iliongezeka kwa haraka jinsi alivyo hubiri injili ya Ufalme na kufanya miujiza. Jinsi muda ulivyosonga ikabidi ili kulinda kazi yake kuhifadhi wale kumi na wawili- moja kwa kila kabila la Israeli (Mt.19:28). Wangekuwa wanafunzwa na yeye- kuwa “wanafunzi wake”- ili  baadaye  “watumwe” na yeye ili kuwafunza wengine- wawe “Mitume”. Hii haikuwa kazi rahisi kufanya uchanguzi na kwa sababu ni muhimu Yesu alienda Mlimani “ na kuendelea usiku kucha akimwomba Mungu”. Asubuhi yake alifanya uamuzi. Tunajua machache kuhusu wengi wao. Tunajua  kwamba Yuda asipokuwepo, wote walikuwa waaminifu kwa majukumu yaliyowekwa juu yao. Walionyesha udahifu wa binadamu na wakashindwa mara nyingi kutimiza maagizo ya Bwana wao, lakini walijifunza kutoka kwa makosa yao. Hawakuwa na elimu ya juu, wala hawakuchaguliwa  kwa sababu ya uwezo wao wa kunena, lakini kwa sababu ya tabia yao (Mdo. 4:13).

 

KUMI NA WAWILI WALIKUWA:

  1. SIMONI PETRO - Pia alijulikana kama Kefa, jiwe (kutoka Aramaia kwa Petro Yn. 1:42). Alikuwa mwana wa Yonas ("Bar-Yona" katika Mt.16:17), Mvuvi wa Bethsaida (Mat, 4:18; Yn. 1:44). Awali alikuwa mwanafunzi wa Yohana Mbatizaji na alikuwa ameoa (Mk. 1:30; 1 Kor, 9: 5). Yeye aliandika 2 nyaraka na alimhimiza Marko kuandika Injili yake.
  2. ANDREA- Ndugu ya Petro aliyekuwa mwanafunzi wa Yohana Mbatizaji (1:35 Yn. 40). Yeye iliwaleta Wagiriki kwa Yesu (Yn.12: 20-23).
  3. YOHANA - pia mvuvi, mwana wa Zebedayo, mwenyeji wa Bethsaida (Mt.4:21, Lk 5:10). Kwa Yakobo ndugu yake, huyo aliitwa Boanerges - "mwana wa radi" (Mk. 3:17). Huenda alikuwa binamu wa Yesu, na ambaye Yesu alimpenda. Yeye aliandika Injili, Nyaraka tatu na Ufunuo.
  4. YAKOBO - ndugu Yohana (Mk. 1:19). Mama yao alikuwa pengine Salome, dada ya Maria (linganisha Mt. 27:56; 15:40 Mk, 16: 1; Yn. 19:25).
  5. FILIPO - pia mwenyeji wa Bethsaida katika Galilaya (Yn. 1:44).
  6. BATHOLOMEO - Maana yake ni mtoto wa Tolmai. Alikuwa mwenyeji wa Kana Galilaya anafikiriwa na wengi kuwa Nathanaeli. Na ametajwa mara mbili tu (Yohana 1:45, 21: 2).
  7. MATHAYO - Alijulikana kama Lawi (Mt. 9: 9; Lk. 5:27). Alikuwa mwana wa Alfayo. Alikuwa mchukua ushuru au kodi katika Galilaya na aliandika Injili ya kwanza.
  8. TOMA - aitwaye pia Pacha, maana yake "pacha" (Yn. 11:16). Yeye awali alikuwa na mashaka kwamba Yesu alikuwa amefufuliwa kutoka kwa wafu, lakini akaamini wakati Bwana alitokea mbele yake (Yn. 20: 24-29).
  9. YAKOBO - Mwana wa Alfayo:, pengine "Yakobo mdogo" au "mdogo" (Mt. 10 3) (Mt. 27:56; Mk.15:40; 16: 1; Lk 24:10)
  10. LEBAU: Thadayo - pia aitwaye Yuda, lakini si yule Iskarioti (Lk 6:16; Yn. 14:22). Anafikiriwa na baadhi kuwa ndugu yake Yakobo, "ndugu yake Bwana" (Yuda 1;. Lk 6:16;. Gal 1:19).
  11.  SIMONI ZELOTE - Mwanachama wa chama cha siasa kilichoitwa Zealots (Lk. 6:15) Neno Mkanaani lilitumika kwake  kama mkaanaani kutoka Kanaani, Kiaramu kwa Kigiriki "Zelote" (Mt.10: 4).
  12.  YUDA ISKARIOTI - Mwana wa Simoni Iskarioti (Yn. 6:71). Iskarioti ni "ish Keruthi", yaani mtu wa Keruthi katika kusini mwa Yuda (Yos. 15:25). Yeye aliyemsaliti Yesu, na baadaye kubadilishwa na Mathia (Mdo 1: 23-26).

MAMBO TUNAYOJIFUNZA:

  • Yesu ilitangazwa na Yohana kama "Mwanakondoo wa Mungu anayeondoa dhambi ya ulimwengu".
  • Yesu, kwa mwenendo wake na vitendo, alitambuliwa wazi na wanafunzi wake wa mapema si tu kama Masihi, lakini pia kama Mwana wa Mungu.
  • Muujiza ya samaki uliwafundisha wanafunzi umuhimu wa dhamira ya jumla, na "waliacha yote na kumfuata".
  • Yesu aliwavuta watu aliowachagua yeye mwenyewe, watu aliojua kwamba wataendeleza kazi yake baada ya kifo chake. isipokuwa mmoja wao, watu hawa wengine wote walikuwa waaminifu kwa wito wao, na waliacha mfano kwa wanafunzi wote kupitisha kwa vizazi vyote.

MAKTABA YA KUREJELEA:

"A Life of Jesus" (M. Purkis)—Kurasa 61-65, 95-98

"Nazareth Revisited" (R. Roberts)—Kurasa 12, 16, 22

"The Gospel of John" (J. Carter)—Kurasa 28-29

"The Story of the Bible" (H.P. Mansfield)—Tol. 8, Kurasa 90-94, 117-120, 143-145

 

MASWALI YA AYA:

  1. Kwa jinsi gani Yohana Mbatizaji alimtambulisha Yesu kwa wanafunzi wake? Maneno aliyotumia yanatufunza nini kumhusu Yesu?
  2.  Elezea wito wa Nathanieli.
  3. Baada ya wito wao wa awali, baadhi ya wanafunzi wa Yesu wakarudi kwa kazi zao ya awali. Jinsi gani Yesu alionyesha kwamba wao lazima wawe na hali ya kujitolea kamili katika kazi yao kwa ajili ya Mungu?        

MASWALI YA INSHA:

  1. Elezea njia ambayo kazi ya Yohana Mbatizaji iliwatayari watu ambao walimfuata Yesu.
  2.  Taja wanafunzi kumi na wawili, na uelezee baadhi ya vipengele mashuhuri na tabia za watu hawa.
  3. Toa muhtasari wa wito wa wanafunzi na uteuzi wa wale kumi na wawili.

 

 

Swahili Title
330. YESU ANAWAITA WANAFUNZI WAKE
Sub type
Sub sub type