332

Swahili

332. YESU ANAWAFUNZA WANAFUNZI WAKE

(b) Kanuni za Uanafunzi Zikifanya Kazi

“Kila asikiaye maneno haya na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye busara"

Yesu alikuwa amemaliza kuelezea sifa za mtu kamili. Sasa akaendelea kutoa muhtasari wa maadili yanayotokana na tabia hiyo. Heri ni mbegu ambayo mambo mengine yanapata njia ya kujionyesha. Sifa zinazohitajika zinaonekana katika masuala ya utendaji.

Lengo letu katika somo hili ni kuona masuala haya  kama yanavyoadhiri maisha yetu wenyewe.

Mathayo 5, 6, 7

KRISTO NA MUSA

Sheria ya Musa ilihukumu vitendo vya nje, lakini Sheria ya Kristo inahukumu fikra ambapo vitendo hutokea. Yesu alichukua masuala kutoka mtazamo wa nje hadi mtazamo wa ndani, kutoka nje hadi ndani. Ni katika akili ambapo mbegu za dhambi huota na kukua (Yak.1: 14-15). Kama zinaweza kungolewa, matendo ya dhambi hayawezi pata nafasi ya kujiendeleza. Kuonyesha kauli hii, Yesu mara kwa mara anatofautiana na sheria ya Musa.

HASIRA INAKATAZWA (Mt.5: 21-24).

Wakati Sheria ya Musa iliwahukumu wauaji, Yesu aliona hasira ndiyo sababu ya mauaji, na akakemea hilo. Kama mmoja atapatanishwa na Mungu, lazima awe na hamu ya kupatana na  ndugu yake. Ibada inayokubalika haiwezekani wakati kuna kosa linalojulikana na halijarekebishwa. Hata kwa kile kinachoonekana kama wakati takatifu zaidi ("sadaka ya zawadi"), maridhiano na mtu ni muhimu kwa Mungu kuliko sadaka (linganisha Efe. 4: 26-27).

KUWA MPOLE WAKATI UMEKOSEA (Mt. 5:25-26; Linganisha Zab. 25:8).

Yesu anashirikisha unyenyekevu na utiifu ambapo kosa linapatikana kwa watumishi wake. Maringo na ukaidi zinaweza sababisha matokea mabaya na kuleta aibu kwa jina lake.

FIKRA YA UZINIFU ZIMEKATAZWA (Mt. 5:27-32)

Kutafakari  kuhusu zinaa ni sawa na kutenda. Kutizama kunaleta tamaa na tamaa inasababisha mtu azini moyoni mwake. Ni bora kutoa angalia (Ayu. 31: 1). Kizuizi kilichopo katika hamu ya kutenda ni kukosekana kwa nafasi, hivyo katika macho ya Mungu tamaa ni jambo moja na kutenda.

Na kanuni hii inatumika katika kitendo chochote ambapo imani inadhoofishwa. Yesu anapanua upeo huu. "Jicho" na "mkono" zimewekwa kwa ajili ya tamaa na matendo. Ni bora kujinyima sehemu ya  maisha haya mafupi kuliko kupoteza maisha ya uzima wakati ukifika.

Funzo ni, kosa linawezwa kuepukwa kwa uamuzi wa kutii Neno la Mungu. Kama nafasi  katika mioyo na akili zetu imejaa mambo mazuri ya Haki, fikra mbaya hazitapata nafasi (Rom. 13:14).
 

KUAPA UWONGO KUMEKATAZWA (Mt. 5:33-37)

Kama maneno hayo yaliyonenwa kwa kiapo yalichukuliwa kisheria kwa mtu, je na maneno yasiyo na kiapo? Je mtu katika tukio hilo amewekwa huru kutoka kwa majukumu yake? La hasha, Viapo  vilikuwa vinatumika kwa wepesi sana na uwepo wa Mungu ulitiwa kwenye maswali wakati ulitanguliwa na viapo vya aina hii, "Kama Mungu aishivyo" haikutendeka. Hili lilikuwa jambo kubwa. “Hebu mawasiliano yako yawe, Naam, Naam, La, La: kwani chochote kilicho zaidi ya haya huleta uovu.

NJIA YA KUTOKATAA (Mt. 5:38-42)

Katika Kristo, lafudhi ni juu ya mtu binafsi, si taifa au serikali. Hivyo, “jicho kwa jicho” haitumiki tena. Katika Kristo, imetoweka na haitonekana tena hadi pale Ufalme utakapo anzishwa. Mtu binafsi ni msafiri, na Kristo anaamuru mwenendo wake mbele ya watu wengine.

Katika  mifano mitatu ya lazima, Yesu anshauri upinzani dhidi ya mabaya, kuumia (Mst.39), kutoza kwa nguvu (Mst.40), na kulamisha “kwa kutumia nguvu” (Mst.41) Katika kesi ya nne (Mst.42) hakuna kulazimishwa. Mtume ana uhuru wa kukubali au kukataa na hivyo mtihani mgumu zaidi. Lakini ni lazima awe mkarimu moyoni kwa wote watakao muuliza, sio kuwapa hasa kile wanachohitaji, lakini kwa hakika kuwapa kile kitakacho saidi yule anayeuliza. Lengo la kukosa upinzani ni kuondoa uchungu wa mtu binafasi, na kuchukua hatua kutoka kwa mkosaji na kumshinda kupitia kanuni za wokovu.
 

SHERIA YA UPENDO (Mt. 5:43-48)

Mbali na kuwa na maaadui, Yesu alikuwa anasababisha mambo mazuri kama “Kupenda.....kubariki.....kutenda mema...kuomba...” Hiki ni kitendo cha mapenzi ambapo wanafunzi walichukua hatua kutoka kwa mkosaji na kupigana naye wakitumia vifaa ambavyo mkosaji hakuelewa. Hii ndio njia ambayo  haki inashinda uovu. Mabaya hayana jibu kwa shambulizi la upendo. Haki inaweza tizama mtenda maovu kwa woga, lakini upendo unamshinda.

Katika kufanya hivyo, mitume walionyesha Baba anayefanya jua kuchomoza na anawanyeshea mvua wale wenye haki  na wasio haki. Hii inamaanisha Mungu anawaonyesha Upendo “Adui zake” na anatumainia wokovu wao, kwa kufanya hivyo, anaweka mfano wa maadili kwa watoto wake (5 Rom: 8-10; Yn. 3:16). Kama upendo utafungiwa katika duara la familia  na kwa wale wanaotupenda, basi hatuna tofauti na wanafiki wa mataifa ambao hawampendi Baba. Upendo wetu kama jua, lazima uangaze kwa wote, kama sisi tunaweza kuwa kamili, kama ni Baba yetu aliye mbinguni (Mst.46-48).
 

DHAMBI YA UNAFIKI (Mt. 6:1-18)

Neno "sadaka" katika mstari wa kwanza inapaswa kuwa “Haki”. Katika kile kinafuatia, Yesu anasisitiza zaidi. Katika Mst 2-4 anakemea hadharani hali ya kujioyesha hadharani Mst.5-6 kuomba katika maeneo ya wazi na katika Mst. 16-18 Kufunga kwa bandia.  Katika kila kesi anakashifu dini hiyo, akiwa ametiwa motisha na maslahi ya kibinafsi, kwamba haina maana katika kupata zawadi ya Baba.  Sadaka hizo, sala na kufunga hazikuwa zinatokana na  upendo wao kwa Mungu, lakini bei iliyowabidi kulipa ili wapate maoni mazuri kutoka kwa binadamu. Lilikuwa tolea ambalo halikutolewa kwa Mungu bali kwao wenyewe. Ilikuwa kama kitendo cha kuigiza ambacho walishangaliwa na watu, na hilo ndilo wangepata pekee.

Kimsingi, dhambi ya unafiki inatoka katika hali yakutoamini. Haiwezekani kumtumikia Mungu kama tunajishughulisha na kupata sifa kutoka kwa binadamu (linganisha Lk 16:15; Yn 5:44; Yuda. 16).

IMANI NA UTAJIRI WA KWELI (Mt. 6:19-21)

Ibada ya kweli imetofautishwa na unafiki na sasa hazina ya kweli imetofautishwa na tamaa. Unafiki na tamaa ni hatari mbili katika hali ya kutafuta haki. “Haki” kwa wanafiki ni bure hata utajiri wao. Utajiri wao ni ishara kwa dunia hii ambayo itaangamia na wale wanaoweka roho yao ndani yake (Mst.19) Moyo utageuka kama sindano ya dira kwa kile tunacho dhamini kwa dhati (Mst.20-21).

ZAWADI YA BABA NA JIBU LA MWANA (Mt. 7:7-12)

Mwanafunzi anatiwa moyo kuendelea- kuuliza, kutafuta, na kubisha- kwa maana kutokufa moyo kunashinda binadamu waovu, "kwa kiasi gani zaidi" Baba yenu aliye mbinguni atazidi kuwapa zawadi nzuri (linganisha Yak 1: 5-7;Mt. 15: 21-28; Lk 11: 5-13). Kama utundu wa binadamu unaweza punguzwa, basi Baba yetu wa Mbiguni atakuwa tayari zaidi kujibu maombi yetu. Tofauti hizi ni za kushangaza. Katika mstari wa 12 kuna kanuni kuu: Kwa hiyo yale yote mtakayotaka mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo. Kwa maana hiyo ndiyo torati na manabii”. Hii ni uendelezi wa sura ya 6: 14-15. Mfano wa Mungu unatupa motisha na nguvu za kutii. Asili nzito ya giza ya binadamu inafanywa kuwa nyeupe na  upendo wa Mungu (2Kor. 5:14-15). Huu ni ujumbe wa maana wa sheria na manabii: na ndio msingi wa amri mbili kuu (Linganisha Mt. 22:37-40)


NJIA MBILI, MITI MIWILI, WAJENZI WAWILI (Mt. 7:13-27)

Kwa kumalizia, Yesu anatoa mifano mitatu:

  1. Njia mbili (Mst.13-14):  kama Musa,  Yesu anaweka mbele ya wanafunzi wake njia mbili na walipaswa kufanya uchaguzi(Kum. 30: 15-20). Hakungekuwa na njia ya katikati na njia inaoyostahili haingekuwa maarufu.
  2. Miti Miwili (Mst.15-20) ili kuwaongoza katika njia, makundi mawili ya binadamu wangetoa huduma yao.  Ili kutambua wakweli kutoka kwa wadanganyifu, ingepaswa mitume kuchunguza matunda yao, kwani kama mti, tunda linafanana na aina yake (Mwa 1:12). Matunda yanaonekana katika  maneno na kazi, kama maneno hayalingani na “Sheria na ushuhuda” na kazi yao sio kama mfano wa Kristo, basi watakataliwa (linganisha Isa. 8:20;1 Pet. 4:11).
  3. Wajenzi wawili (Mst. 24-27): Neno linawagawanyisha binadamu, wenye busara na wapumbavu. Wale ambao wanafanya kulingana na Neno ("hayo maneno yangu")  wanajenga msingi dhabiti (linganisha. 1 Kor. 3:11). Hivi karibuni dhoruba itajaribu kila nyumba na wajenzi wenye busara watajenga wakitilia hili maanani (linganisha. 2 Tim. 2:15).
     

MAMBO TUNAYOJIFUNZA:

  • Katika kuonyesha maadili ya ufalme, Yesu alielezea sifa za wale wanaostahili ufalme wake.
  • Wakati huo huo, yeye anaweka wazi kwamba atakuwa hakimu wa wote ambao watajaribu kuingia kwenye Ufalme (7:21). Hakuwezi kuwa na motisha mkuu zaidi kwa sifa  anazo hitaji zaidi ya haya.
  • Tunapaswa kuwa kama mtu mwenye busara aliyejenga juu ya msingi imara - msingi wa Kweli, aliyeamini, na kuelewe, na kutenda.

MAKTABA YA KUREJELEA:

"The Teaching of the Master" (L. G. Sargent)—Sehemu III-VI

"A Life of Jesus" (M. Purkis)—Kitabu 4, Sura 11, 12

"The Story of the Bible" (H. P. Mansfield)—Tol. 8, Kurasa 152-159

"The Sermon on the Mount" (J. Luke)—Kurasa 9-24

MASWALI YA AYA:

  1.  Ni wapi dhambi huanzia na jinsi gani inaweza epukwa? Tumia mafundisho ya Yesu katika Hotuba  ya Mlimani kuelezea jibu lako.
  2. Je, Yesu anasema nini kuhusu imani na utajiri katika Hotuba ya Mlimani?
  3. Baba "anawanyeshea mvua watu wenye haki na waovu”. Nini Yesu alikuwa akifundisha kwa kauli hii katika Hotuba ya Mlimani?

MASWALI YA INSHA:

  1. Kwa njia ngani mafundisho ya Yesu yalilinganishwa na Sheria ya Musa? Toa mifano minne kutoka kwa Hotuba ya Mlimani.
  2. Elezea kile unachokijua kuhusu “njia” mbili, "miti" miwili na "wajenzi" wawili katika Mahubiri ya Mlimani.
  3. Fananisha tabia iliyo elezewa katika heri na maelekezo kwa vitendo juu ya kuishi katika sehemu ya mwisho ya hotuba ya mlimani.

 

 

Swahili Title
332. YESU ANAWAFUNZA WANAFUNZI WAKE
Sub type
Sub sub type