333

Swahili

333. YESU ANAWAFUNZA WANAFUNZI WAKE JINSI YA KUOMBA

“Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe"

Katika Hotuba ya Mlimani, Yesu anawapa wanafunzi wake muundo wa jinsi sala zinapaswa kuwa. Mungu anena na binadamu kupitia Neno lake, na binadamu anajibu kwa Maombi. Neno linamwonyesha Mungu kama Baba yetu mpendwa aliye mbiguni, anayejali kuhusu binadamu na ambaye wanapaswa kumtegemea. Hivyo maombi ni imani inayofanya kazi na inapaswa kuongezeka jinsi tunavyotambua Mungu akifanya kazi katika maisha yetu na akijibu maombi yetu.

Lengo la somo hili ni kuongozwa na Yesu kwa njia ya haki ya kuomba.

Mathayo 6

NJIA ISIYOPASA NA INAYOPASA YA KUOMBA (Mt. 6:5-8)

Yesu anaanza maelekezo yake kuhusu maombi na onyo: "usalipo, usiwe kama wanafiki; kwa maana wao wanapenda kuomba wakiwa wamesimama katika sinagogi na pembe za njia, ili wapate kuonekana na watu”. Wakati wanaonekana kama wanamwabudu Mungu, lakini wanatafuta kupendwa na watu,  na hii ilikuwa wazi kwa mahali hadharani walikochagua kufanya maombi. Walikuwa kama waigizaji wanaochukua tabia za kigeni na kuzifanya zao. Kwa uigizaji wao walipokea sifa kutoka kwa binadamu zawadi walioitamani, hawangetumainia chochote kutoka kwa Mungu; “walikuwa washapata zawadi yao.”

Mahali pa sala ya kweli ni pa siri ambapo mlango umefungwa na nafsi iko pekee na Mungu. Maombi kama yale ya Elisha yalipata majibu yaliyotaka kutoka kwa Mungu katika kesi ya Shunamite (2 Fal. 4: 33-37). Tayari Yesu alikuwa amewafunza  mitume wake kwa mfano huu kama amri. Walikuwa wametafuta  na kumpata katika "mahali pa faragha", akipata nguvu katika maombi ili aweze kupata nguvu ya kufanya kazi ingine ngumu ya siku hio (Mk.1:35) na wakaelewa uhusiano wake na Baba yake na na utegemezi wake juu yake.

Yesu anaongezea onyo la pili: Msipayuke payuke bure, kama watu wa mataifa, kwani wanadhani watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi”. Lazima tuepuke maombi ya “kuigiza” ambapo ni jambo moja linalosemwa tena na tena kama vile kasuku anavyopenda kurudia rudia. Maneno yetu lazima yawe maelezo ya tamaa zetu za dhati za mioyo yetu. Mungu “hutafuta moyo” na kama maombi yetu hayana tamaa zetu ya ndani basi, yatakataliwa na Mungu. Kurudia rudia kunamaanisha kwamba Mungu si mjua yote kwa sababu hakusikia mara ya kwanza, au “anajua mahitaji yetu kabla tumuulize”. Jambo hili linaonyesha kukosa imani. Hivyo ibada imeshushwa kwa kiwango cha “watu wa mataifa”. Hivyo basi jibu kutoka kwa Mungu litakuwa kama lile la  Baali, wakati waabudu wake walitiwa kwenye aibu mbele ya Elisha.

SALA YA BWANA (Mt. 6:9-15)

Baada ya Bwana kuwapatia maonyo mawili kuhusu maombi, aliwaeleezea mitume wake kwa njia ipasavyo ya kuomba. Umuhimu wa “Muundo wa Sala” unaweza kuonekana kutoka kwa kuwa katika matukio tofauti wakati Bwana aliulizwa jinsi ya kuomba, alirudia sala moja (Lk 11: 1-4). Ikumbukwe kwamba lugha iliyotumika ni “Rahisi” kama mtoto akinena na baba yake, na ILIOKAMILIKA, ingawa fupi. Wakati Bwana alisema sala inapaswa kuwa kwa “kwa muundo huu” hakumaanisha kwamba maombi yote yanapaswa kuwa sawa na hii, lakini kwa misingi ya kuwa- na uwiano wa umuhimu,unyenyekevu, na wepesi-kufanana na sala hii. Kwa sababu ni fupi, tunaweza ichambua kwa haraka na kijifunza mengi kuhusu nafasi ya binadamu mbele ya Mungu na utengemezi wake Kwake, kwani kwa sala hii utukufu wa Mungu na kusudi lake zimewekwa mbele ya mahitaji ya binadamu.

Sala hii imegawanywa kwa sehemu nne:-

1.   Hotuba ya Ufunguzi—"Baba yetu, Aliye Mbiguni":

Maombi  yanaanza na ibada, sio kuuliza. Mitume wanaweza jiunga na Yesu katika kuongea na Mungu kama “Baba” ingawa Mungu katika matukio manne ameelezewa hivyo chini ya Agano la Kale (linganisha 1 Nya 29:10; Isa. 63:16; 64. 8; Kum. 32: 6), kwa kuja kwa Mwana wa Mungu kuna sisitizo zaidi- waumini wanahimizwa kumwita Mungu, “Baba”: “kwa sababu sote ni wana wake, Mungu ametuma Roho wa Mwana wake katika mioyo yetu, akilia, Abba, Baba” (Gal 4: 4-6). Katika Kristo tunafurahia urafiki na faida inayotokana katika “uhusiano wa Baba na Mwana” Huduma (6:26, 30, 32; 7:11), huruma (Zab 103: 13), uridhi (Rom 8:17. ) na hata adhabu (Ebr.12: 4-9). Kutajwa kwa maskani yake “Mbiguni”, mara moja inatufanya kuwaza kuhusu Nguvu na Utakatifu wake, na hivyo kutuonya dhidi uzoefu (linganisha Mhu. 5: 2).

2.   Maombi matatu yanayomhusu Mungu

i) " Jina lako litukuzwe”: maneno haya yanaonekana kutoka katika mistari ya ufunguzi ya Zaburi 103, ambayo ni tafakari juu ya jina na tabia ya Mungu kama inavyoonyeshwa na Musa (Kut. 34: 6-8). Tizama jinsi mawazo mengi katika Zaburi hii yanapatikana katika Sala ya Baba. Mzaburi “anatukuza” jina la Baba kwa kutaja sifa zake za ajabu ambazo ndizo msingi wa ukombozi wa binadamu (Mst.12)-Msamaha, mapenzi, huruma-  ni lazima zipatikane katika tabia ya wale wanaojiita wana Wake. Lakini leo jina la Mungu linatajwa vibaya na binadamu kwa sababu wanamdharau na kutomtii (linganisha Amo. 2:7; 52 Isa: 5). Dua hii inatafuta siku ya Ufalme wakati binadamu “watamjua Bwana” na kumwabudu katika utakatifu. Maneno ya wimbo wetu yanaelezea wazo vizuri: “Jina lako litukuzwe mbali na karibu: kwa mataifa yote”.

ii) "Ufalme wako uje. mapenzi yako yatimizwe duniani kama ilivyo mbiguni": Badala ya maombi ya binafsi, kwa mara nyingine Baba anawekwa mwanzo.  Hivyo kwa akili ya mitume walielewa nia na utukufu wa Mungu ambayo Anatamani itimizwe kwa dhati. Utawala wa binadamu umeshindwa kuleta haki na usawa; utawala wa Mungu ni muhimu.

Yule ambaye “anatafuta kwanza Ufalme wa Mungu na haki yake", kama vile Yesu alishauri (Mst.33), anaweza na akiwa na nafsi nzuri taja maneno haya. Yesu  akasema “si mapenzi yangu, bali yako yatimizwe" na huu lazima uwe ndio ulikuwa msemo wa mitume wake wote. Hatuwezi kwa dhati omba mapenzi ya Mungu yafanyike duniani katika siku zijazo, kama leo tunashindwa kufanya hivyo wenyewe.

  1. Maombi matatu yanayohusu mahitaji ya binadamu
     

i) "Utupe leo mkate wetu wa kila siku": “mkate wetu wa kila siku” unaonekana kama chakula kilichopewa watumwa, askari au wafanyakazi na kilitolewa siku moja awali (linganisha. Lk. 12:42). Katika dua hii mtume anatambua utengemezi wake kwa Mungu kwa ajili ya mahitaji yake. Amejifunza kumwamini Mungu na kutosheka kwa chakula na mavazi. Wasiwasi mwingi kuhusu siku za usoni kunaonyesha ukosefu wa imani katika utunzaji wa Baba na uwezo wa kutoa. Je tuna imani kwa Baba yetu wa Mbiguni ambayo inatupa hakikisho, na kutuwezesha kutia kikomo maombi yetu kwa mahitaji ya sasa pekee, tukiwa na ujuzi kwamba anatupenda na atatuhifadhi? Lakini binadamu hawana haja ya mkate wa kuokwa pekee: wanahitaji pia "mkate wa mbinguni" ili wapate maisha ya milele. Baba mwenye upendo wa mbinguni ametoa yote haya.

ii) "Utusamehe madeni Yetu, kama vile tunawasamehe wadeni wetu": Hapa kuna kukiri haja ya huruma ya Mungu na neema, ambayo sasa inapatikana bure kwa wale waliobatizwa kwa Jina la Yesu Kristo: hakuna msamaha isipokuwa kwake (Yn. 8:24; Mdo. 4:12). Maombi ya kweli lazima yatolewe kwa sauti ya unyenyekevu na  kutubu, lakini  kiwango cha vile Mungu atasamehe itategemea nia ya mwombaji ya kusamehe. Mtu anaweza weka kikomo kwa neema ya Mungu kwake mwenyewe kwa sababu ya ukali na machungu kwa wengine! “Yeye atakuwa na hukumu bila huruma, kwa yule hakuonyesha huruma" (Yak 2:13). Hili ni la maana kwani Bwana alirirejelea, hilo pekee, katika mwisho wa sala (mistari 14 na 15 soma kuanzia mstari wa 12). Wanafunzi wote ingawa wametukuka katika macho ya binadamu, lazima wakumbuke kwamba wamesamehewa na wanahitaji msamaha, na hivyo lazima wasemehe wenzao. Mfano wa Mkopeshaji asiye samehe Unaelezea somo hili vyema (Mat.18: 23-35, angalia somo la 16) na mtume Paulo anaendeleza funzo hili la maana katika Efe. 4:32 na Kol 3:13. mfano wa Mfarisayo na mtoza ushuru wanaonyesha mtu mmoja  aliye omba bila kutambua dhambi  na mahitaji yake, na mwingine, licha ya dhambi zake, alikuwa mwadilifu "kuliko yule mwengine" (Lk. 18:11 -14).

iii) "Usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule Mwovu": Mtume anafahamu udhaifu wake katika majaribu na uwezekano wa kushindwa. Kwa sababu hii anakataa majaribu, na kuomba kutotiwa ndani yake. Lakini anajua kwamba ni, “kwa kupitia dhiki nyingi” kwamba ataingia katika Ufalme (Mdo.14:22), na ambaye “  Yule Bwana anampenda, amemtakasa (Ebr. 12: 6). Hivyo anaomba “kuokolewa kutoka kwa uovu” mafunzo ni-kutambua udhaifu na wakati wa shida kumwomba Mungu (linganisha 2 Tim 4:18; Zab 34:6-7, 17-18).

Hitimisho: Sifa kwa Mungu —"Kwa kuwa ufalme ni wako,nguvu na utukufu hata milele. Amina": Kama sala inavyoanza, ndivyo inavyoisha kwa ibada kwa Mungu. Mungu lazima “azunguke” na kutawala maombi yetu yote; Lazima asikize matumaini yetu kwa sababu “Ufalme wake” utayatimiza-Wana wake watakombolewa kwa “nguvu", na "utukufu" wake na atakuwa pamoja na wao (Rom. 2: 7; 5: 2; 8:18). Maneno haya ya mwisho ni sawa na yale yaliyonenwa na mfalme Daudi katika tukio wakati yeye na watu wa Israeli walitoa kwa hiari kwa Hekalu na Sulemani akafanywa kuwa mfalme.  Ufahamu wa Daudi kama unavyoonekana katika sala hii, udogo wa binadamu mbele ya Ukuu wa Mungu, unatupa sisi tafakari zaidi (tazama 1 Nya 29: 10-19).


MAAGIZO ZAIDI KUHUSU SALA.

Sala ya Bwana ni mwongozo wetu, ni muhimu kutumia masomo haya kwetu wenyewe. Bwana alikuwa na mambo mengine ya kusema kuhusu maombi, pia mitume na itakuwa nzuri kwetu sisi kuyaelezea kwa kifupi:
Tunapaswa kumwomba Mungu kwa jina la Bwana Yesu Kristo, mpatanishi maalumu, kuhani, na wakili (Yn.16:23; 1 Tim 2:5; Heb.7: 25; 1Yn 2: 1).
• Tunapaswa kuwa bidii na wakweli katika maombi (Yak. 5: 16-18; Mt.7: 7-11).
• Tunapaswa kuomba mara kwa mara  (Lk 18: 1, 1 The. 5:17).
• Lazima tuendelee katika sala kama ushahidi wa dhamira ya kweli (Lk.11: 5-13).
• Lazima tutoe dua katika imani na bila shaka yoyote juu ya uwezo wa Mungu na nia ya kutoa (Mt. 7: 9-11; Mk 11:24; Jas.1. 6-8).
• Lazima kuomba kile ambacho kinalingana na mapenzi ya Baba (1 Yn 5:14; Yak 4: 3).
• Lazima tukumbuke kushukuru kwa zawadi zote kutoka kwa Mungu (Efe. 5:20; Flp. 4: 6; 1 Tim. 4: 3-5).
• Tunapaswa kuwa waangalifu na sio wenye usingizi (Kol. 4: 2).

Hakutakuwa na jibu kwa maombi kama yatafanywa kwa kupayuka na kurudia rudia, kama lengo ni la kidunia, na kama kuna uasi (1 Sam 28: 6), au kama kuna mashaka yoyote.

MAMBO TUNAYOJIFUNZA:

  • Yesu ametupa sala ya kielelezo ambapo mtazamo wa haki ya mja mbele ya Mungu unaweza kuonekana.
  • Lazima tushike kile Yesu anasema, kwa maana jinsi tunavyokuwa ndani ya Kristo, sala hii lazima ionyeshe hisia zetu: hatuwezi kamwe "kuiboresha"
  • Maombi yanatoa ushahidi kumtegemea Mungu, na ni kipimo cha ukuaji wetu wa kiroho.
  • Chochote tunafanya au kuamua, lazima kwanza tukipeleke kwa Baba kwa maombi.
  • Maombi lazima yawe ya kweli, rahisi, yenye unyenyekevu, yasiyopimika na  tukeshe.
  • Maombi ni haja ambayo hatuwezi kuacha. Nguvu zetu kidogo, kukosa uwezo wa kuwafariji wengine, ni lazima iimarishwe kwa maombi ya dhati ya kila siku. Lazima iwe sehemu ya maisha yetu, si tu jambo la kawaida lakini kitu cha muhimu na maana. Tuna uhakika kwamba maombi yetu yatasikilizwa na Baba wa mbinguni mwenye upendo.

 

MAKTABA YA KUREJELEA:

"Teaching of the Master" (L. G. Sargent)—Sehemu IV, Sura 2-7

"A Life of Jesus" (M. Purkis)—Kurasa 143-144

"A Prayer: Studies in Principle and Practice" (M. Purkis and C. Tennant)

"Making Prayer Powerful" (H. P. Mansfield)

"The Sermon on the Mount (J. Luke) Kurasa 25-41

 

MASWALI YA AYA:

  1. Yesu alisema nini katika Hotuba ya Mlimani kuhusu mtazamo wetu wa akili tunapoomba?
  2. Nini thamani ya maombi?
  3. "Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje, Utakalo lifanyike duniani kama mbinguni". Toa maoni kuhusu maneno haya katika Sala ya Bwana.
  4. Yesu aliwafundisha wanafunzi wake wasali hivi: "Utusamehe madeni yetu kama sisi tunavyo wasamehe wadeni wetu." Je, hii inatufundisha nini? onyesha jibu lako kwa kurejelea mfano wa mkopeshaji asiyesamehe (Mat. 18).

 

MASWALI YA INSHA:

  1. Chagua vifungu vitatu katika Sala ya Bwana na utoe maoni juu yake, Onyesha masomo ambayo tunajifunza.
  2. Nukuu Sala ya Bwana na uonyeshe jinsi gani inaweka mtu katika uhusiano na Mungu.
  3. Andika insha kuhusu jinsi kanuni ya Sala ya Bwana inavyoathiri mtizamo wako.

 

SEHEMU 3

KUTANGAZA UFALME WA MUNGU

Mwanzoni mwa huduma yake ya umma, Yesu alinukuu muhtasari wa Isaya kuhusu huduma yake ya Sabato katika Nazareti;

"Roho wa Bwana yu juu yangu kwa sababu amenitia mafuta kuwahubiria maskini habari njema, amenituma kuwatangazia wafungwa  kufunguliwa kwao, vipofu kupata kuona tena na  kuhubiri ukombozi kwa mateka na kuhubiri mwaka wa neema ya Bwana. "
(Lk 4: 17-19.; Isa 61: 1-2).

Wakati macho yalikuwa yameelekezwa kwake, Yesu akasema, “ Siku hii andiko hili limetimizwa mbele ya masikio yenu” (4:21) Huyu hakuwa mwana wa Yosefu miongoni mwao. Huyu alikuwa Mwana wa Mungu, Immanueli ('Mungu pamoja nasi') ambaye, kama Petro alivyosema “alienda akitenda mema, na kuponya wale wote waliokuwa wamenyanyaswa na shetani, kwani Mungu alikuwa na yeye”.

Kwa miaka mitatu na nusu Bwana alitimiza kazi yake kwa uaminifu, akifundisha habari njema ya Ufalme, kuwafariji maskini, kuwapa matumaini wale waliokuwa wamelemewa na dhambi, kuponya baadhi yao kuonyesha mamlaka yake ya kimungu, hadi hatimaye akaelekeza uso wake Yerusalemu kwa kifo. Sehemu ya tatu ya masomo yetu inaelezea kipindi hiki katika maisha ya Bwana.
 

 

 

Swahili Title
333. YESU ANAWAFUNZA WANAFUNZI WAKE JINSI YA KUOMBA
Sub type
Sub sub type