337. KULISHA UMATI
"Mimi ni mkate wa uzima"
Watu elfu tano walilishwa na Bwana Yesu Kristo katika kingo za mashariki za mto Galilaya. Hakutoa chakula hiki kutosheleza njaa yao: kulikuwa na maana ya ndani ya kiroho ambayo alitaka wanafunzi wake na watu kwa jumla watambue: Alikuwa Mkate wa Uzima. Wale ambao walielewa maana ya maneno yake na kumkubali kama mwokozi wangejiunga na yeye katika uzima wa milele.
Lengo letu katika somo hili ni kuona kwamba ni kwa kuja kwa Yesu kristo pekee na kukubali mafunzo yake tunaweza kuwa na matumaini ya uzima pale anaporudi.
Yohana 6:1-14; Mark 6:31-44
NJOONI NYINYI PEKE YENU FARAGHANI (Mk. 6:31-34)
Miaka miwili ilikuwa imepita katika huduma ya Bwana Yesu na umaarufu wake ulikuwa unafikia kilele. Umati uliokuweko kila wakati wakiwa na tamaa na mahitaji tofauti walikuwa wanachukua raslimali nyingi za Mwalimu. Mitume walikuwa wamerejea kutoka kuhubiri na walikuwa na hamu ya kuripoti mambo ya ajabu ambayo walikuwa wamekamilisha (Mk. 6:12, 13, 30). Kwa wakati huu ujumbe kuhusu kifo cha Yohana mbatizaji zikawasili, mtagulizi mkuu wa Bwana na binamu yake. Ikawa dhahiri kwamba lazima angejitenga na umati na msisimko, Yesu alihitaji kuongea na wanafunzi wake na kujenga mtazamo wao wa kiroho kwa matukio yalikuwa mbele yao. Akawaambia âNjooni ninyi mahali pasipokuwa na watu mkapumzike kidogoâ. Wakachukua mashua na kuondoka hadi upande mwingine wa bahari ya Galilaya. Umati ulingundua kuondoka kwao, na wakawafuata hadi kingo za kaskazani mwa bahari ya Galilaya, mpaka walipofika alipokuwa Yesu na mitume wake. Wangine kutoka miji jirani walijiunga na umati huu mpaka idadi ikafikia watu elfu tano (Mst.33) hivyo faragha ya Yesu ikaingiliwa.
Walikuwa wamekuja kwa sababu walikuwa wamefurahishwa na miujiza ya uponyaji (Yn 6: 2), Lakini hawakutambua Haja yao kubwa. Bwana aliguswa na hali yao ya kujitolea. Aliwaona kama âKondoo bila mchungajiâ (Mst.34), na Marko alielezea maoni yake: âYesu aliwaonea hurumaâ Japo alikuwa na mahitaji yake, alionyesha sifa za mchungaji wa kweli pale alipoweka mahitaji yake kando kwa ajili ya wengine. Hakuna mwengine ambaye watu wangemgeukia, kwani masinagogi na mahekalu yalikuwa yanaongozwa na watu waliongozwa na maslahi yao ya kibinafsi na ambao waliwanyanyasa maskini na wenye haja.Hivyo akaanza kuwafunza mambo mengi, kiwapa chakula cha kiroho na kinywaji cha kuwatosheleza kiroho (linganisha Zab. 23: 2-3; Eze.34: 23-24; Yn. 10:11; Lk 9 : 11).
KUWALISHA WATU ELFU TANO (Yn. 6:5-14).
Aliwafundisha na kuwaponya saa baada ya saa mpaka jioni ikakaribia (Lk. 9:12). Hawakua wamekula na wanafunzi wakafikia wanapaswa kufanya jambo la kawaida kwa Bwana wao. Walikuwa wamekosea kufikiria walikuwa wanajua zaidi yake yeye. Walimwambia Bwana awatawanye watu kwa haraka ili waende wakanunue mikate katika sehemu jirani (Lk. 9:12). Lakini Bwana alielewa mgogoro uliokuwa umetokea, na alichukia kuwafukuza watu waliokuja kusikiza neno lake. Akawajibu wanafunzi wake: âwapeni ninyi chakulaâ. Walishindwa kutambua ukuu wa Mwana wa Mungu kati yao, na walianza kufikiria fedha ambazo zingehitajika kuwalisha watu hawa wote. Mitume hawa walikosa imani, ingawa walikuwa wameona yale aliyokuwa na uwezo wa kufanya (Mk. 6:30). Walifikiria kwamba hakukuwa na njia ya kutoa mkate ila kwa gharama kubwa, na walikuwa na fedha kidogo kwenye vibindo vyao (Mk. 10:28).
Bwana aliwauliza wana mikate mingapi, na kuwaambia waende wakaangalie (Mk 6:38). Andrea ndiye aliyekuja na jibu. âkuna kijana hapa, ambaye ana mikate mitano, na samaki wawili wadogo; lakini haiwezi watosha watu hawa wote? (Yn.6: 9). Jukwaa lilikuwa sasa limewekwa wazi kwa moja kati ya miujiza mikuu ya Bwana. Aliwaelekeza wanafunzi wake kuwagawanyisha na kuwakalisha katika makundi ya watu mia moja na hamsini kwenye nyasi. Jioni ilipofika waume kwa wake elfu tano walishuhudia Mwana wa Mungu akichukua mikate na samaki, akatazama mbiguni na kuzibariki kisha akavunja mikate na kuwapa wanafunzi wake wawape watu. Pia aligawayisha samaki wale wawili na kuwazidisha ili watoshe kila mtu. Matokeo yake yamefupishwa: "Nao wote wakala wakashiba" (Mk; 6:42). Tafakari mshangao wa umati uliokuwepo. Wakati walipokua wamekula âmpaka wakatoshekaâ, Bwana akawaambia wanafunzi wake wakusanye mabaki, âkisipotee kitu chochoteâ Vikapu kumi na viwili vya mabaki vilikusanywa. Waliokuweko walipoona ishara hii walisema "ni ukweli kwamba huyu ndiye nabii anayekuja ulimwenguni" (Yn.6:14). Waliamini kwamba alikuwa nabii mkuu ambaye Musa alikuwa ametangaza kwamba atatokea miongoni mwa ndugu zao (Kum.18: 15-18).
UMUHIMU WA ISHARA (Yn. 6:30-40, 47-58).
Mwaka mmoja baadaye, wakati wa pasaka, Yesu kwa mara nyingine alichukua mkata na kuubariki, kisha akaumega, na kuwapa wanafunzi wake, na kusema, Twaeni, mle: kwani huu ni mwili wanguâ (Mk 14:22). Alitumia lugha sawa, na hii inatupa funguo ya kufungua na kuelewa maana ya kweli ya kulisha watu elfu tano: alikuwa anafunza kwamba kwa kuvunja mwili wake wakati wa kifo atakuwa anatoa mkate wa kweli ambao ungewatosheleza wengi wakielekea uzima wa milele. Mafunzo sawia yanapatikana katika chakula cha Bwana ambapo kifo chake kinakumbukwa katika ugawaji wa mkate.
Kama mikate mitano ilivyogawanywa kwa watu elfu tano, hivyo ndivyo neema ya Mungu kupitia Kristo imesambaa kwa mataifa (Ufu 7: 9; Rum 5:15). Watakombolewa miongoni mwa watu na hawatahisi njaa wala kiu tena, kwani Mwana wa Mungu atawakusanya kama kondoo wake na kuwalisha na kuwangoza hadi kisima cha maji ya uzima (Ufu.7: 16-17; 1 Pet. 2:25 5: 4).
Kanuni hizi zilifunzwa watu siku iliofuatia walipomkuta katika Sinagogi kule Kapernaumu upande wa pili wa ziwa. Jambo la kusiskitisha ni kwamba hawakuwa wamejifunza maana halisi ya muujiza wao, kwani walikuwa wanatafuta utoshelezi zaidi wa njaa yao. Yesu aliwakemea: Msifanye kazi kwa ajili ya chakula kinacho haribika, lakini kwa chakula kile kinachodumu milele, ambacho Mwana wa Mtu anawapa ninyiâ (Yn 6:27; linganisha Isa. 55:1-3) .
Alijitambulisha kama mkate wa kweli: Mimi ndiye mkate wa uzima: yule atakaye kuja kwangu kamwe hatahisi njaa; na yule atakaye niamini kamwe hatahisi kiuâ (Mst.35). Usambazaji wa mikate ulikuwa mfano wa kuonyesha utoaji wa mwili wake kwa ajili ya uzima wa dunia (Mst.51) Kushindwa kumtambua kama mkate wa kweli kutoka mbiguni kungeleta madhara makubwa: âmsipokula mwili wa Mwana wa Mtu, na kuinywa damu yake, basi hamna uzima ndani yenuâ (Mst.53).
MABAKI
Baada ya kulisha umati Bwana akawambia mitume wake kuokota mabaki, âkisipotee chochoteâ. Katika maelelezo yake siku iliofuatia Bwana alitamka maneno yaliyojaza ombi hili na maana. âNa haya ni mapenzi ya Bwana ambaye amenituma mimi, ili kwa wote alionipa nisipoteze hata mmoja, bali nimfufue siku ya mwishoâ (Mst.39, linganisha 17:12). Ukuu wa akili ya Bwana, alipotenda miujiza katika kingo za Galilaya zinaweza sasa tambulika: aliona matukio haya kama utangulizi wa kifo chake mwaka mmoja ujao. Aliona kwamba katika utoaji wa mkate, uzima haungekuwa wa kondoo waliopotea wa nyumba ya Isralei, bali pia wa watu wa mataifa- hakuna kipande kilipaswa kupotea- kwani mabaki haya yangewatosheleza watu wa mataifa (Mk 7:28;. rejelea Somo la 13). Katika hotuba yake alisisitiza kwamba yeye ni Mkate wa Kweli ambao ungepatikana kwa âwoteâ au âulimwenguâ (Mst.33, 39, 40, 51). Injili ya Yohana inaweka mkazo mkubwa katika kuongezwa kwa watu wa mataifa katika tumaini la Israeli kwa njia ya imani katika Yesu Kristo (linganisha 3:15, 16; 4:23; 12:32; 20:31).
Ni muhimu kwamba muda mfupi baadaye katika sehemu ya watu wa mataifa iitwayo Dekapoli alirudia muujiza ule ule, wakati wanaume elfu nne, bila kuhesabuwanawake na watoto walilishwa (Mk 8: 1-9; Mt. 15:38 ). Maneno na matendo yake yalikuwa karibu kufanana- Bwana alikuwa nafundisha kwamba âkondoo wengineâ, ambao ni watu wa mataifa, walikuwa bado waingie katika tumaini la Israeli.
Ukweli ni kwamba kulikuwa na vikapu kumi na viwili vya mabaki vilivyokusanywa kusisitiza tabia za tumaini la Kiisraeli. Watu wa mataifa wangeokolewa lakini ni kwa kuwa âIsraeli ya Munguâ kwa njia ya amani (Linganisha. Efe. 2:12; Yn. 4:22; Gal.6:16).
MKUU KULIKO MUSA
Katika historia yote ya Israeli ni tukio moja linaloweza kufananishwa na muujiza wa Yesu. Kupitia mkono wa Musa Mungu hakuwalisha watu 5,000 kwa siku moja, lakini taifa zima katika jagwa la sinai kwa miaka 40. Watu walifanya ulinganishi wa haraka. Mwanzoni walimtaja kama nabii aliyeahidiwa na Musa, na hata walitaka kumchukua kwa nguvu na kumfanya mfalme (Yn. 6:14-15). Sasa wakati alipokemea nia zao za kumtafuta, walihitaji ishara kutoka kwake ili wadhibitishe mamlaka yake, wakisema Musa alidhibitishwa kwa kuwapa mababa zao mkate kutoka mbiguni! Ulinganishi wao ulisisitiza mapungufu yao. Mungu ndiye alikuwa amewapa mababa zao mkate wakiwa jagwani, sio Musa: na ulinganishi wa kweli haukua kati ya Musa na Yesu, lakini kati ya Manna, ambayo ilitolewa na Mungu, na Yesu Mwana ambaye Mungu alimtuma ulimwenguni (Mst.39). Alikuwa mkate wa kweli kwa sababu angewapa uzima wa milele (wakati kizazi kulichokula Manna jagwani kilikuwa kimekufa, Mst.49) na Neno na sio kizazi kimoja au taifa moja lingefaidika: "Maana mkate wa Mungu ni yule anayeshuka kutoka mbiguni, na aupaye ulimwengu uzima wa milele (Mst.33). Kweli mkuu kuliko Musa alikuwa amekuja!
UMAARUFU UNAPUNGUA (Yn. 6:59-69)
Hotuba haikupokelewa vyema na wengi waliokuwa kwenye umati. Walikuwa wamekuja kwa Yesu wapate chakula zaidi na wajifurahishe, lakini Yesu aliwaagiza na kutoa mwito dhidi ya nia na kuelewa kwao wakati alisema maneno haya, "msipokula mwili wa Mwana wa Mtu na kuinywa damu yake, hamna uzima ndani yenu "(Yn.6:52, 60-61). Kauli hii iliwakasirisha Wayahudi kwani sheria iliwakataza kunywa damu (Law. 17:10). Walichukua maneno yale jinsi yalivyo, na unyonge wao wa Kiyahudi ukasisimuliwa. Yesu aliwaelezea maana yake. Hakuwa anarejelea kitendo cha kula mwili wake halisi na kunywa damu yake, kwani âmwili haufai kituâ (Mst.63). wanapaswa kuchukua maneno haya wayatafakari, ili wapate mafundisho yake halisi: âmaneno ninayo waambia, ni roho na ni uzima. âSikizeniâ, akasema Isaiya, âna nyoyo zenu zitaishiâ (55: 3).
Kuanzia wakati huo wengi wa wanafuzi wake waliondoka (Mst.66). kilele cha umaarufu wake kilikuwa kimepita. Hata kati ya wale kumi na wawili kulikuwa na shaka. Usiku uliopita Yesu alitembea juu ya maji walipokuwa ziwani kuelekea Kapernaumu. Alituliza nyoyo zao zenye hofu kwa maneno haya: âNi mimi, Msiogopeâ (Yn.6: 20), lakini hata wao waliona vigumu kuamini alikuwa Yesu, kwani âhawakufikiria kuhusu muujiza wa mikate, kwani nyoyo zao zilikuwa nzitoâ (Mk.6: 52). Mara mbili katika kipindi cha masaa ishirini na nne waliona nguvu za Muumbaji, sasa swali likatoka kwa Yesu, âje nyinyi mwataka kwenda zenu pia?â
Petro alijibu kwa haraka, âBwana, ni kwa nani tutaenda? Wewe unayo maneno ya uzima wa milele, na sisi tunaamini na tuna uhakika kwamba wewe ndiwe yule Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai "(Mst.68-69).
MAMBO TUNAYOJIFUNZA:
- Kama Bwana wetu sisi hatupaswi kuwafukuza watu lakini kuwavuta kwa Injili, tukionyesha wema na huruma kama wachungaji wema.
- Kristo ni mkate wa kweli kutoka mbinguni; nje yake kifo kinatawala, kwani hakuna mtu mwingine tunaweza kugeuka kwa ajili ya "maneno ya uzima wa milele".
- Ni kwa utafiti wa makini wa maneno ya Yesu tutaona na kufahamu maana yake.
- Kifo cha Kristo kinakumbukwa katika kushiriki chakula cha Bwana, hata kama kulisha umati wa watu kunatabiri hili.
MAKTABA YA KUREJELEA:
"Gospel of John" (J. Carter)âSura 6
"The Story of the Bible" (H. P. Mansfield) -Tol. 9, Kurasa 113-131
MASWALI YA AYA:
- Kwa nini Yesu alitaka kuwapeleka wanafunzi mbali katika mahali pa faragha jagwani kabla ya kuwalisha watu 5,000?
- Elezea kwanini uaminifu wa wafuasi wa Yesu ulipungua wakati aliongea nao katika sinagogi kule Kapernaumu baada ya kulisha watu 5,000.
- "Mimi ni mkate wa uzima", alisema Yesu Kristo katika hotuba iliyofuata kulisha watu 5,000. Onyesha jinsi wazo hili lilionekana kupitia miujiza.
MASWALI YA INSHA:
- Elezea muujiza wa kulisha watu 5,000. Nini maana ya kiroho ya muujiza huu?
- Kwa nini idadi ya wale miongoni mwa 5,000 ambao Yesu aliwalisha walimtafuta siku ya pili? Jinsi gani walimganisha na Musa na majibu yake yalikuwa yapi?
- "Bwana kwa nani tutakwenda? Wewe unayo maneno ya uzima wa milele". Ni wakati gani Petro alisema maneno haya kwa Yesu na nini kilisababisha? Ni somo gani tunajifunza kutokana na tukio hili?
- Wale kumi na wawili walirejelea kazi yao ya kuhubiri na habari za kifo cha Yohana zinamfikia Yesu. Hivyo wanaamua kuvuka mto kuelekea jagwani karibu na Bethsaida (6:16 Mk., 30-31).
- Umati unamfuata hadi kingo za ziwa (Mk 6: 32-33).
- Baada ya kulisha watu 5,000 wale kumi na wawili walivuka ziwa. Bwana alitembea juu ya maji (Yohana 6: 15-21). Wanafika Kapernaumu.
- Bwana anawaponya wengi katika nchi ya Genesareti (Mk 6: 53-56).
- Anatoa hotuba yake kuhusu mkate wa uzima kayika Sinagogi kule Kapernaumu (Yohana 6:59).
Matukio ya Somo la 13 yanafuatia