344

Swahili

344. "TAZAMA, MFALME WENU"

"Heri ni kwa yule anayekuja kwa jina la Bwana”

Yesu kumfufua Lazaro kulianzisha vurugu na maisha yake yalikuwa hatarini (Yn. 11:53, 57).  Kuepuka  nia za mauaji za Wayahudi, Yesu alisafiri Kaskazini katika mji wa Ephraimu. Wakati wake haukuwa umefika, na ingawa “Pasaka ilikuwa imekaribia”,  ilikuwa ni muhimu kwamba “mambo yote yaliyoandikwa katika Sheria na Manabii yatimie”. Alitoroka kama mkimbizi, lakini pamoja na wanafunzi kumi na wawili-alirejea kufa. Lakini kurudi kwake kuonyesha siku kuu inayokuja yeye kama mfalme ataingia katika mji wake kwa nguvu na utukufu mkubwa, akiwa pamoja na watakatifu waliokusanyika kwake (Mt. 21: 1-11; Zab 24.: 7-10).

Lengo la somo ni kuona jinsi Yesu alionyesha kwamba alikuwa kweli Mwana wa Daudi ambaye atakuja katika jina la Bwana.

Mathayo 21:1-22

YESU ANAINGIA YERIKO (Lk. 18:35-19:10)

Pasaka ilikuwa imebaki wiki moja pekee wakati Bwana alisafiri kusini kuelekea Yeriko. Njia aliyotumia ilikuwa imejaa mahujaji, wote wakilelekea Yerusalemu kusherehekea sikukuuu. Alipokaribia mji, alikutana na mtu aliyekuwa kipofu na akamponya (Lk 18: 35-43). Muujiza huu ulisisimua umati na kuongeza hamu yao kwa Bwana Yesu. Alipokuwa anatembea katika njia nyembamba katikati mwa mji wa Yeriko, watu walimzingira, kwamba wale waliokuwa mbali na umati hawakuweza kumwona.

Mmoja kati ya matajiri wa Yeriko, aliyechukiwa na kudharauliwa alikuwa mtoza kodi mkuu, alitamani sana kumwona Yesu. Lakini Zakayo alikuwa mfupi wa umbo. Alijaribu kufika pale mbele ya umati lakini alishindwa kwani umati ulikuwa umesongamana. Kwa msisimko kuhusu kufika kwa Yesu, Zakaria alikuwa na nia kubwa ya kumwona. Mbele yake kulikuwa na mti wa Mkuyu, umejaa matawi na majani makubwa. Hapa palikuwa na jibu lake. Kwa juhudi, alipanda juu ya mti ule na kusubiri, akiamini kwamba hakuna mtu amgeweza kumwona. Yesu alikaribia na alipofika chini ya mti ule, alisimama na kutizama juu. Waliokuwa naye pia walifuata macho ya Yesu hadi kwa mtu yule mdogo aliyejishikilia kwa tawi la mti ule. Zakayo alionekana mpumbavu! Watu walifuruhia kumwona akiabika!  "Zakayo, fanya haraka, shuka, kwa kuwa leo imenipasa kushinda nyumbani mwako," alisema Bwana (Lk. 19: 5). Mtoza mshuru huyu hakuamini masikio yake. Aliharakisha kushuka, akijua kwa moyo wake kwamba mabadiliko makubwa yalikuwa karibu kutokea katika maisha yake. Umati ulinungunika kwa uchaguzi wa Yesu, lakini Bwana alijua nyoyo ya binadamu na kwamba Zakayo alikuwa naweza kutenda mambo mazuri. Uchanguzi wake ulidhibitishwa kwa Zakayo,ambaye alimtambua Yesu kama Bwana, na akaahidi kurudisha chochote alichochukua kwa njia za udanganyifu mara nne zaidi na kutoa mali yake kwa maskini. Zakayo alikuwa ameinu mzigo wa nafsi mbaya kutoka kwa mabega yake; sasa alikuwa “huru” na mwana wa Abrahamu. Linganisha badiliko lake mpya na mtazamo wa Abrahamu dhidi ya Mfalme wa Sodomu (Mwa 14:21), na mbele ya wana wa Hethi (Mwa 23). Zakayo alikuwa “amepotea”, lakini Bwana alimtafuta na kumpata; kwa hili, huduma ya Yesu kama Mwokozi ulitimia. Anaelezea vizuri “Mfano wa Wapotevu” ambao Yesu alikuwa amenena kuhusu (Lk. 15).

 

SAFARI YA MTU KABAILA (Lk. 19:11-27)

Bwana alikaa na Zakayo usiku mzima. Angeingia Yerusalemu mchana wa siku iliofuatia. Kwa sababu ya matukio yajayo na kwa sababu wanafunzi walifikiria kwamba mda ulikuwa unafaa kwa kuanzishwa kwa ufalme (Mst.11). Yesu akawaelezea kuhusu mfano wa mtu kabaila. Alijionyesha kama mtu kabaila aliye safiri hadi nchi za mbali (mbinguni) ili kupokea mamlaka na kisha arudi. Hii ilifunza wazi kwamba  katika kipindi hicho mda ulipita kabla arudi kutawala dunia kutoka Yerusalemu, mji ambao ulikuwa “karibu sana nao” kwa wakati huu. Mtazamo wa watumishi wake katika kipindi ambacho hangekuwepo ingeamua hatma yao wakati atakapo rudi.  Hii pia ni sambamba na jukumu la Wanafunzi wa Yesu. Watahukumiwa wakati Bwana atarudi kulingana na kazi zao (2 Kor. 5:10).

YESU ANAFIKA BETHANIA (Yn. 12:1-9).

Bwana aliondoka Yeriko na kuchukia safari yenye uchovu kupitia barabara ilioinuka katika milima mieupe ya Yudea hadi mji mkuu Yerusalemu, umbali wa kilomita thelethini. Ilikuwa “siku sita kabla ya Pasaka” (Mst.l) wakati Yesu alipofika nyumbani mwa Martha katika kijiji kidogo cha Bethania karibu na Mlima wa Mizeituni.

Waty wengi walikuwa wamejaa katika mji wa Yerusalemu kutoka kila upande. Msisimko wa kawaida unaokuwepo wakati wa Pasaka ulitiliwa mkazo na swali ambalo lilikuwa kinywani mwa kila mtu. Lilimhusu Yesu, na lilionyeshwa kwa swali moja pekee, “je atakuja kwenye sikukuu” (Yn. 11:56)

TAZAMA MFALME WENU ANAKUJA (Mt. 21:1-5).

Yesu alielewa kile sheria, katika Zaburi na Manabii walikuwa wameshuhudia kumhusu, na matendo yake yote na kwa hivyo walikuwa wameelekezwa na Neno la Mungu. Alipofika Bethfage, aliwatuma wanafunzi wake kijijini na watampata mwanapunda aliyefungwa. “mfunguueni na mkalete hapa”, akasema.

Mwanapunda alikuwa ishara ya heshima ya kifalme (2 Sam 16: 1-2; 1Fal. 1:33, 38), na kwa hili ni muhimu kama matendo ya Yesu yalitimia katika Zek 9:9. Yesu alitaka kuonyesha bila shaka kwamba alikuwa mfalme wa laini ya Daudi, na kwa njia ambayo ingeonyesha kwamba hangeongoza mageuzi ya kijeshi dhidi ya Roma.

KUINGIA KWA USHINDI (Mat. 21:6-11)

Habari ya kuja kwa Yesu kulisababisha watu kutoka Yerusalemu na kupanda mlima wa Mizeituni kukutana naye. Walipiga kelele za ushindi huku wakimkaribisha kama mshindi huku wakiyatandaza mavazi na makuti mbele yake.  Wakapiga kelele wakisema "Hosana" Mwana wa Daudi, "Heri ni kwa yule ajaye kwa jina la Bwana" (Zab 118: 26). Nia ya Israeli ilikuwa MFALME, Masihi. Utawala wa Kiyahudi walikubwa na wasiwasi kwamba watu walikuwa wanahusisha Umasihi na Yesu. Lakini Mfalme wa Israeli, akionyesha neema na huruma ya Baba alikuwa amekuja kwao. Hata hivyo, kuelewa kwa watu kulikuwa hafifu. Baada ya siku chache msisimko wao ungegeuka na kuwa chuki kwani wangemsulubisha mfalme wao. Jinsi gani binadamu alikuwa na asili ya kugeuka!

Alipofika Hekaluni, Yesu “ akatazama pande zote”. Hakuna kitu kilichokuwa kimebadilika- Nyumba ya Mungu bado ilikuwa mahali pa ubadilishanaji wa sarafu na biashara (Yn.2:16) Uamuzi wake ungeonekana katika matukio ya siku iliofuatia. Usiku huo alirudi Bethania pamoja na wanafunzi wake (Mk. 11:11).

 

KUTAKASA HEKALU (Mt. 21:12-19)

Kesho yake asubuhi akiwa njiani kuelekea Yerusalemu alihisi njaa (mst.18). Kandokando ya barabara kulikuwa na mti wa mtini akauendea. Mti huu ulikuwa katika msimu wa mazao na kwa hivyo ulipaswa kuwa na matunda. Lakini haukuwa hata na tunda moja. Ingawa ulionekana mkubwa, mti huu haukuwa na matunda. Kulingana na wanafunzi Kristo alinena na mti ule : “Yasipatikane matunda kwako tangu leo na hata milele”.

Akiuacha Mtini, Bwana alipita kwenye mji akielekea katika hekalu alipokuta imejaa shughuli nyingi, makelele, tamaa, uchoyo na faida. Yesu alipita katika mahakama, akawafukuza wote waliokuwa wakiuza na kununua,alitawanya sarafu kwa kupindua meza za wabadili fedha. Sauti yake ilisikika, “Je, si imeandikwa. nyumba yangu itaitwa nyumba ya maombi: lakini nyinyi mmeifanya kuwa pango la wezi (Mst.13). Utakaso uliashiria utakaso wa Wayahudi kutoka Yerusalemu miaka Arubaini baadaye na Warumi. Wakati alipomnukuu Yer. 7:11 na kuita Hekalu “pango la wezi” alikuwa anatumia maneno ambayo nabii alikuwa ametumia kuhusu hekalu ya Sulemani- na hatma ya Hekalu hilo ingekuwa sawa katika hekalu ambalo Herode alikuwa amejenga. Lakini Yesu pia aliona wazi siku inayokuja pale Hekalu ya Bwana itakuwa kitovu cha ibada duniani kote (Isa 56:7).

Wakati waovu na wenye tamaa waliondolewa kutoka kwa hekalu walibadilishwa na wale waliokuwa wanahitaji hifadhi ya Mungu. Vipofu, vilema walikuja kwake naye aliwaponya. Alikuwa na wengine pia Wale ambao kwa uwongo walijiita wana wa Mungu waliondolewa na wana waliompenda walichukua nafasi yao. Wakifananisha sauti waliokuwa wamesikia siku iliopita, wakapiga kelele na kusema “Hosana Mwana wa Daudi!" (Mst15) na wakati viongozi wa hekalu waliyaona haya wakakasirika, “wasikia hawa wasemavyo?” “Ndio” akajibu “Hamkupata kusoma, kwa vinywa vya watoto wachanga na wanaonyonya umekamilisha sifa?” (Mst.16).

MTI WA MTINI ULIONYAUKA (Mt. 21:20-22)

Walikuwa njiani kutoka Bethania siku iliofuatia ambapo wanafunzi walishangazwa na mtini ulionyauka. Kwa ishara mti huu wa Mtini uliwakilisha Israeli  (Yoe.1:7 Lk.13: 5-9) - Kumbukumbu imerekodi mfano wa Mtini Tasa. Kama mti huu ungezaa matunda baada ya kuwekwa mbolea basi haungeadhibiwa. Yesu katika tukio hilo hakumaliza mfano wake. Ingebidi muda upite kabla ya hatma kujulikana. Katika tukio hili Yesu alionyesha kwamba mti wa Mtini ungebaki bila mazao na ungeharibiwa. Hivyo akakamilisha mfano.

Kama Waisraeli wa kweli tunapaswa kuzaa matunda “wakati wa msimu na usio wa msimu” au hukumu sawa itatuangukia  (2 Tim 4: 2). Lazima tuendeleze imani ya Mungu ndani yetu na tujifunze kutizama maisha kutoka kwa mtizamo wake  (Mk. 11:22). Kupitia nguvu za utakaso wa Neno na maombi tunaweza shinda dhambi na kuzaa matunda yatakayomfurahisha Mungu  (Mk 11: 23-24).

MAMLAKA YA YESU YANAPATA CHANGAMOTO (Mt. 21:23-27)

Wakati Yesu aliingia Hekaluni tena, maadui zake walikuwa  tayari “ni kwa amri gani unatenda mambo haya” wakamuuliza (Mst.23). Yesu alijibu swali hili kwa kuwauliza swali lingine, akiahidi kwamba wakimjibu naye atawajibu swali lao: hata hivyo swali lake lilikuwa ni jibu kwa swali lao na pia onyesho la nia zao za kinafiki. “ubatizo wa Yohana, ulitoka mbiguni au kwa binadamu?”. Kwa kurejelea Yohana, Yesu alirejelea yule ambaye binadamu wote walimwona kama nabii, ambaye huduma yake ilikuwa kwa ajili ya utambulisho wa Kristo. Hapa palikuwa na mamlaka ya kazi yake. Yesu aliwatia changamoto kutaja maoni yao kuhusu ujumbe wa nabii. Kumtambua Yohana (kusema kwamba ubatizo wake “ulikuwa wa Mbiguni”) ilikuwa kumtambua Yesu kama Kristo: hili hawakuwa tayari kufanya. Lakini kupinga huduma ya Yohana (kusema ubatizo wake ulikuwa wa “Binadamu) haingewezekana katika mtizamo dhabiti wa watu kumhusu. Jibu lao lilikuwa kukiri kwamba “ Sisi hatujui”, kukiri ambako kungemdanganya yeyote, na pia kusisitiza kushindwa kwao. “Wala mimi siwaambii ninyi ni kwa amri gani nafanya mambo haya” (Mst.27).

Kisha Yesu akaongea kuhusu mifano mitatu:-

  1. Wana Wawili (Mst. 28-32)
  2. Wakulima wakaidi (Mst. 33-46)
  3. Ndoa ya Mwana Mfalme (22: 1-14).


Katika mifano hii anaonyesha maarifa yake katika nia zao za mauaji, hukumu ambayo wangepata na wito wa Watu wa mataifa.
 

MAMBO TUNAYOJIFUNZA:

  • Kama Zakayo, kama sisi tutamfuta Yesu kwa moyo wetu wote, tutampata na kupatikana na yeye.
  • Leo sisi tunasubiri kurudi kwa mkuu ambaye atawalipa watumishi wake waaminifu na mahali katika hekalu lake.
  • Yesu alisema kwamba katika vinywa vya watoto wadogo sifa imekamilika. Mungu anafurahi katika sifa na shukrani ya watoto wake.
  • Ni muhimu kwetu sisi kuzaa matunda katika utumishi wa kweli, vinginevyo hatma ya mtini itakuwa yetu pia.

MAKTABA YA KUREJELEA:

"The Story of the Bible" (H. P. Mansfield)—Tol. 10, Kurasa.186-188; Tol. 11, Kurasa. 33-71

"A Life of Jesus" (M. Purkis)—Kitabu 7, Sura 3-6 "Nazareth Revisited" (R. Roberts)—Sura 48

MASWALI YA AYA:

  1. Nini ilikuwa kusudi la Yesu katika kuingia kwa ushindi Yerusalemu?
  2. Nini Yesu alikuwa akifunza kwa kulaani mti wa Mtini?
  3. Ni mambo gani tunayojifunza kutokana na kubadilika kwa Zakayo?

MASWALI YA INSHA:

  1. Elezea kuingia kwa ushindi kwa Yesu, Yerusalemu. Nini Yesu alikuwa anaonyesha kwa kuingia amepanda punda Yerusalemu?
  2. Elezea tukio ambapo Yesu alitakasa hekalu mara ya pili. Elezea maneno yake na sababu ya matendo yake.
  3. Jinsi gani laana kwa mti wa Mtini inatimiza mfano wa Mtini Tasa?
  4. Jinsi gani Yesu aliwaaibisha wale ambao walimwambia, "Kwa mamlaka gani unatenda mambo haya?"

 

 

Swahili Title
344. "TAZAMA, MFALME WENU"
Sub type
Sub sub type