348. KARAMU YA MWISHO NA GETHSEMANE
"Si mapenzi yangu,bali ako yatimizwe ..."
Jukumu la kwanza la Masihi lilikuwa kufa kwa ajili ya dhambi za dunia. Kufanya hivyo ilibidi kuchukua asili kama ya binadamu wote, ili aweze kujua na kushinda matamanio yake na madhaifu. Jukumu kama hili lilikuwa mzigo mkuu kwa Bwana na ilikuwa katika Gethsemane ambapo ilifikia kilele. Upendo wake mkuu ulionekana katika karamu iliotangulia.
Lengo la somo hili ni kuelewa umuhimu wa karamu ya ukumbusho ambayo Bwana alianzisha kabla ya kifo chake.
Mathayo 26: 1-56
NJAMA YA CHUKI (Mt. 26:1-5)
Hiki kilikuwa ni kipindi cha wasiwasi kwa wakuu wa Wayahudi. Tangu Yesu alipofika Yerusalemu umaarufu wake na watu wa kawaida ulikuwa umeongezeka. Walikuwa wameimba nyimbo za sifa wakati alipoingia katika mji, na walisikiza majibu yake dhabiti katika vita vya maneno na Mafarisayo, Masaduayo na waandishi. Wakiwa wamejawa na wivu, makuhani wakuu, walimu wa Sheria na wazee walifanya mkutano katika nyumba ya Kayafa kupanga njama ya mauaji (Zab. 27:4) Sherehe ya Pasaka ilikuwa imebaki siku mbili pekee na waliogopa kwamba Yesu angepata sifa zaidi mbele ya macho ya watu (linganisha Yn. 6:15). Lazima wangemkamata Yesu kabla ya sikukuu ya Pasaka ili kuzuia maandamano kutoka kwa watu.
HARUFU YA UPENDO (Mt. 26:6-13)
Tofauti na madhumuni haya yenye giza, Mathayo anatueleza kuhusu kitendo cha upendo kilichotendeka katika nyumba ya Simoni mwenye Ukoma katika kijiji kidogo cha Bethania kilomita Tatu kaskazini mwa Yerusalemu. Katika mazingira ya kawaida Yesu alitoa mfano mzuri wa imani na mapenzi ambao uliwekwa kama kumbukumbu ya milele (Mst.13). Alipokuwa akikula, mwanamke aitwaye Mariamu alikuja na kumwagilia marhamu ya thamani sana juu ya kichwa chake (Yn.12: 3). Matendo yake yalikuwa yaonyeshe upako wa mwili wake kwa ajili ya mazishi na hivyo ya muhimu zaidi (Mt. 26:12). Hakuna mtu hata mmoja, hata wale kumi na wawili ambao alikuwa amewaelekeza mara nyingi, alikuwa ameelewa umuhimu wa kifo chake kama hali ya kutimiza wajibu wa Masihi.
Hili lilikuwa tendo la kujitolea ambalo lilimgusa Bwana. Lakini pia, lilikuwa tendo la kukemea kwa wale, ambao walikuwa na fursa nyingi ya kufanya, walikosa mtazamo huo na ukarimu. Wakiongozwa na Yuda, wanafunzi walianza kukosoa matendo yake kama uharibifu wa mafuta na kumtaja mwanamke yule kama asiye wajali maskini (Mst.8-9: 12 Yn. 4-6). Harufu nzuri ya marashi, hivyo kama roho ya Mariamu, ilijaa kwa chumba hicho; lakini sasa ilikuwa imeharibiwa na mgogoro na tamaa. Yesu alikabiliana na upinzani, akabaini unafiki duni uliokuwepo, na kumsifu mwamamke yule mwaminifu (Mst.10-13).
KWA VIPANDE THELATHINI VYA FEDHA (Mt. 26:14-16).
Hii ilikuwa kukumea kulikokuwa wazi kwa Yuda Iskarioti ambayo inaonekana kuwa kichocheo mwisho. Kilichompelekea kutoka kwa kundi la upendo hadi kwa baraza la wauaji. Pale ilichukua vipande thelathini vya shaba kumsaliti Yesu, ili waweze kumkamata âmbali na umatiâ (Lk 22: 6) akiwacha makuhani wakuu na matumaini makuu, Yuda alirudi kwa wenzake na kusubiri fursa ya kumsaliti Mwana wa Mungu.
CHAKULA CHA MWISHOâKI WAPI CHUMBA CHA WAGENI? (Mt. 26:17-19)
Upendo wa Yesu ulikuwa mkubwa kwa wanafunzi wake! Kwa kumkubalia Yuda kurudi miongoni mwao akijua uovu aliotaka kutenda, na akiwa na dhiki ya kifo kilichokuwa kinakaribia, Mungu alitayarisha akili yake kwa ajili ya Pasaka. Alitamani kutumia muda huu pamoja nao kwa hivyo akawalelekeza wanafunzi wake wawili kutayarisha chumba cha wageni. Aliwapa maagizo machache kuhusu eneo lake (Lk. 22:15; Mt. 26: 17-19; Mk 14: 13-15). Kwa hivyo Yuda alisitishwa japo kwa muda kuandaa mipango yake kwa wakati huu. Pasaka yao haingesitishwa.
CHAKULA CHA BWANA (Mt. 26:20-30)
Pasaka baada kutayarishwa, Yesu alikuja na kukaa na wale kumi na wawili. Walishangazwa kwa kuambiwa kwamba ni mmoja wao ambaye atamsaliti. Wote walianza kutilia shaka na kuuliza, "Bwana, ni mimi?" "Yeye Atakayechovya mkate pamoja nami katika bakuli ndiye atakayenisaliti." Yuda, "mmoja wa wale kumi na wawili" (Mk. 14:10, 17, 43), atakaye kunywa kutoka kwa kikombe kimoja, atatenda kitendo hiki cha unyama. Kwani imeandikwa, ârafiki yangu, ambaye namwamini, aliyekula chakula changu, ameniinulia kisigino chakeâ. (Zab 41: 9, tazama pia Zab 55: 12-14).
MKATE ULIMEGWA.
Katikati ya Pasaka, Yesu alianzisha Agano Jipya: âNa walipokuwa wakila, Yesu alitwaa mkate, akashukuru, na kuumega, na akawapa wanafunzi wake, akasema, 'Twaeni mle; huu ni mwili wangu". Wote walikuwa na mazoea ya maelezo ya Pasaka, lakini hapa palikuwa na mtizamo mpya! Katika nafasi ya mwanakondoo wa Pasaka, Yesu alikuwa anatoa âMwiliâ wake mbele yao. Kisha akachukua kikombe cha mvinyo na kusema, "Hii ni damu yangu ya agano jipya". Hivyo katika mtu wa mwili na damu â âMwili Tayariâ (Ebr 10: 5, 8-10) ingekuwa kutolewa kwa Mwanakandoo wa Pasaka asiye na kasoro, na hivyo sadaka zote za Agano la Kale (Zab. 40: 6-8). Yohana Mbatizaji alikuwa ametangaza hili pale aliposema, âTazama Mwana-kondoo wa Mungu ambayo huondoa dhambi ya ulimwengu" (Yn.1:29 chapa).
Chini ya kivuli cha Mlima Sinai, Musa alikuwa amechukua bakuli na kunyunyiza damu ya Agano la Kale juu ya watu wa Israeli. Walikiri imani yao kwa Mungu na nia yao ya kuwa watiifu (Kut. 24: 3-8). Hata hivyo manabii walikuwa wametabiri kuhusu Agano jipya, hivyo kuonyesha kukatizwa kwa Agano la Kale (Yer 31: 31-33; Isa 59: 20-21). Agano Jipya lingekuwa âjipyaâ kwa sababu, baadaye, lingetoa Msamaha wa dhambi (Yer 31:34 Isa 27: 9; Zek. 9:11) na kipengele hiki kimetiliwa mkazo na Bwana âDamu yangu imemwagwa kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambiâ (Mst.28) Maneno yake yalikuwa na tofauti na masharti ya Agano la Kale la Musa. Mkate na mvinyo haukua wa wale kumi na wawili pekee, au wa Israeli, bali kwa âWengiâ ambao hawakutajwa. Katika maneno haya Yesu anaungana na Roho katika Isaiya: âKwa maarifa yake mtumishi wangu mwenye haki atawafanya wengi kwani atayachukua maovu yao.â (Isa. 53:11). Angekuwa âMwokozi wa ulimwengu", kwa ajili âkila mtu amwaminiyeâ atapata ondoleo la dhambi na ahadi ya uzima wa milele (Yn. 4:42;. 3:15, 16; 12:32; Rum. 3:21. -22, 10: 11-13).
KIKOMBE CHA MVINYO.
kikombe cha mvinyo kilifuatia ishara ya damu yake (Mt. 26: 27-28) Damu inaashiria âmaishaâ na hivyo kwa njia hii, Yesu alionyesha kwamba âangetoa uhai kwa kifoâ (Law 17:11; Mwa. 9: 4; Isa 53:12, 10). Katika Yohana 6:53 anawahimiza wanafunzi wake kunywa damu yake ili waishi: âIsipokuwa kwa kunywa damu ya Mwana wa Mtu hamtakuwa na maisha ndani yenu!â kwa Myahudi hii ingeonekana kama dhambi kwani Mungu alikuwa amekataza kunywa damu (Law 17: 10-11; Kum 12:23; Mdo 15: 20-22). Hapa palikuwa na tofauti ya maksudi: Damu ya sadaka ya Sheria haingeweza kuondoa dhambi, Lakini damu ya Kristo ingeweza kufanya hivyo na kuleta uhai! âKunywaâ âDamuâ hii ni âKuishi ndani yakeâ Naye âAishi dani Yetuâ (Yn. 06:56). Maneno yake, kanuni zake, zinapaswa kuishi ndani yetu, na kuleta umoja pamoja naye na wenzetu. Nembo hizi walipewa katika usiku wa mateso ya Bwana na kifo (Lk. 22:15). Paulo anatoa maoni âKwa maana kama mnapokula mkate huu na kunywa kikombe hiki, mwaitangaza mauti ya Bwana mpaka ajapoâ (1 Kor. 11:23, 26). Kwanini utangulizi kama huu ulitolewa kuhusu kifo cha Bwana, wakati kanuni za mkate na mvinyo zinaonekana katika maisha yake? Ni kwa sababu kwa msalaba ulionekana kama âUshindi wa Mwisho juu ya dhambiâ. Alipokata roho Yesu alisema : âImekwishaâ (Yoh 19:30). Hivo katika kifo chake, kanuni zilizoonekana katika maisha yake ziliwekwa wazi.
Aya inayofuata imeandikwa katika suala ambalo zinahusiana na waleâwaliobatizwa kwa Kristoâ Wanafunzi ambao hawajafika katika kiwango hicho katika maisha yao, hata hivyo, fikiria kanuni zilizoelezewa na hivyo kuelewa kwao kunaongezeka.
Wakati tunakutana na kushiriki mkate na mvinyo fikra zetu zinapaswa kuzingatia kifo cha Bwana. Ilikuwa hapo ambapo mwili wake âulitolewaâ kwa ajili ya uhai wa ulimwengu na damu yake âilimwagwaâ ili wengine wapate kunywa (Yn 6:51;. Mat 26:28). Paulo anahimiza kwamba tunapaswa kujichunguza kabla ya kuchukua nembo. Kufanya vinginevyo ni âkunywa isivyostahiliâ na âanajipatia hatia ya mwili na damu ya Bwanaâ, na kuungana na wauaji wake (1 Kor 11: 27-29). Kwa upande mwingine kama tutazingatia kanunu za kifo chake, tunafaidika na hatimaye kupokea maisha ya milele (Yn 6: 54-57). Watu wa Kristo lazima watembee katika hatua zake; na hao walio wa Kristo wameusulubisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake (Gal 5:24). Sikukuu ya Ukumbusho inapaswa kudumishwa âmpaka atakapokujaâ (1 Kor. 11:26). Ilikuwa ni Yesu mwenyewe ambaye alihusisha utukufu wa siku zijazo na usiku ule wa mateso, wakati aliahidi kwamba hatakunywa matunda ya mzabibu mpaka pale atakapokunywa âupyaâ na wanafunzi wake katika Ufalme (Mt. 26:29).
GETHSEMANE (Mt. 26:36-46).
Baada ya kuhitimisha Pasaka hii ya kipekee na Zaburi ya sifa (Zab 118), wote waliondoka chumba cha juu na kuingia katika kiza cha usiku, walielekea hadi mteremko wa bonde la Kidroni hadi kwenye bustani ya Gethsemane chini ya Mlima wa Mizeituni. Yuda alikuwa ameondoka hapo mapema na alikuwa tayari anapanga pamoja na makuhani wakuu mipango ya kumkamata Yesu. Alikuwa anaelewa bustani ya Gethsemane kwani âmara nyingi Yesu na wanafunzi wake walikutana hukoâ (Yn 18: 1-2; Lk 22:39). Huu ulikuwa wakati mmbaya na Yesu alihisi haja ya kupata nguvu kutoka kwa Baba yake wa Mbiguni. Alijua kile Manabii walikuwa wameandika. Alijua kwamba Yuda alikuwa anapanga mauaji yake na alionya kwamba wanafunzi wale wengine wangemtoroka- andiko lazima litimizwe (Mst.31: Zek. 13: 7).
Akihitaji usuhuba Yesu aliwachukua wanafunzi wake watatu, Petro, Yakobo na Yohana, na akaingia kwenye bustani. Aliwaelezea kina cha huzuni yake. Aliwaambia wakeshe na yeye wakati anasonga mbele kidogo kunena na Baba yake. Maombi yake yalikuwa ya ukombozi kutokana na kikombe cha kutisha cha majonzi kama ingekuwa sambamba na mapenzi ya Baba yake, ambayo hangeweza kukataa, akisema, â sio kulingana na mapenzi yangu, bali mapenzi yako yatimieâ. Hakukuwa na njia nyingine. Mungu alimjibu kwa kumtuma malaika, âkumwongeza nguvuâ (Lk 22:43; 91:11 Zab, 14; 34: 7-8). Aliporudi kwa wale watatu aliwakuta wamelala-Petro, pia ambaye alikuwa amekiri waziwazi uaminifu wake (Mst.33, 35, 40). Yesu, licha ya huzuni yake ya kibinafsi, aliwajali: Kesheni na kuomba msiingie majaribuni: Roho iko tayari lakini mwili ni dhaifu" (Mst.41, linganisha Rum. 7: 17-23;. Efe. 6:18). Mara tatu aliomba akitumia maneno yale yale na kila wakati waliporudi aliwakuta wanafunzi wake wamelala (Mst.42-44). Ilikuwa saa yake ya huzuni na upweke (Zab 69: 1-4., 13-20). Jasho lake halikuwa la kawaida, kama matone makubwa ya damu yalianguka ardhini (Lk. 22:44). Hata hivyo kutokana na hili aliinuka akiwa na ushirika ulioimarika na Baba yake, na ushujaa katika uamuzi wake. "Tazama, Bwana Mungu atanisaidia, ni nani huyo atakaye nihukumu (Isa 50: 7-9). "Inukeni, Twende" (mst.46).
UMATI MKUBWA WA WATU WENYE MAPANGA NA MARUNGU (Matt. 26:47-56)
Yuda, "mmoja wa wale kumi na wawili", aliwasili pamoja na walinzi waliotenda amri ya wakuu wa makuhani (linganisha Yohana 7:32; Mat 26:47). Katika mwanga wa tochi na taa Yuda alimsaliti Bwana wake kwa kumbusu. Ilikuwa ishara ya kuhakikisha kwamba wamempata Yesu (Yn. 18:3). Upendo wa Petro na hasira zikapanda. Alichukua upanga wake akamkata sikio mmoja wa watumishi wa makuhani wakuu (Mst.51, Yn. 18:10) Hiki kilikuwa kitendo cha kuonyesha uaminifu kwa Yesu lakini hakikufaa. Akiponya sikio, Yesu alimkumbusha Petro kwamba makundi kumi na mawili ya malaika wapo kwa Ajili yake kama angewahitaji (Lk 22:51; Mat. 26:53), lakini huu haukuwa wakati wa pingamizi. Aidha â Wote ambao huishi kwa upanga wataangamia kwa upangaâ (Mst.52-53). Kisha wanafunzi wote wakamwacha, wakakimbia" (Mst.56).
MAMBO TUNAYOJIFUNZA:
- Ni rahisi kupitisha hukumu kali dhidi ya maneno ya upendo ambayo tunashindwa kuelewa.
- Mkutano wa kumbukumbu lazima uhudhuriwe kwa njia ipasayo.
- Maombi ni msaada mkubwa dhidi ya majaribu, na ni lazima tuwe macho wakati tunamwendea Mungu.
- Tunatakiwa "kupinga uovu", kisasi ni cha Mungu pekee.
- "Malaika wa Bwana hufanya kituo, akiwazungukia wamchao na kuwaokoa."
MAKTABA YA KUREJELEA:
"Nazareth Revisited" (R. Roberts)âSura 52 na 56
"A Life of Jesus" (M. Purkis)âKitabu 7, Sura 9, 10 na 11
"The Gospel of the Son of God" (L. G. Sargent)âKitabu VII, Sura 1-2
MASWALI YA AYA:
- Jinsi gani agano jipya ambalo Yesu alianzisha katika chakula cha mwisho ni tofauti na agano la kale lililotolewa na Musa katika Kutoka 24?
- Yesu alimaanisha nini aliposema: "Hii ni damu yangu ya agano jipya, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi" (Mt. 26: 2. 8)?
- Yesu alimaanisha nini aliposema, "Yeye ambaye... anakunywa damu yangu hukaa ndani yangu, nami ndani yake" (Yn. 6:56)
- Kwa nini Yesu alimwambia Petro, katika bustani ya Gethsemane, aweke upanga wake nyuma katika ala yake?
- Jinsi gani upendo wa Kristo wetu uonekana katika matukio yaliyotokea katika bustani ya Gethsemane?
MASWALI YA INSHA
- Ni maelekezo gani yameachwa kwa wale walio katika Kristo kukumbuka Yesu wiki kwa wiki?
- Je, chakula na mvinyo kilicholiwa na Yesu na wanafunzi wake wakati wa karamu ya mwisho kiliashiria?
- Elezea matukio yaliyotokea katika bustani ya Gethsemane, 'ikiwa ni pamoja na kukamatwa kwa Bwana. Weka maneno mengi ya Yesu kama unavyoweza kukumbuka.