350. HAI KUTOKA KWA WAFU
âNa kama Yesu hakufufuliwa,imani yenu ni bure;mngali bado katika dhambi zenu"
Kwa maneno yaliyo hapo juu ni ya Mtume Paulo yanayosisitiza umuhimu wa mafundisho ya ufufuo wa Kristo. Kupatikana kwa kaburi tupu kumetengeneza historia ya miaka elfu mbili, na imeamua mtawala wa miaka elfu moja ijayo, kwani Bwana aliyetukuka atarudi na kutawala katika haki na amani; Mungu ametoa hakikisho kwa hili âkwa ajili ya watu wote amemfufua kutoka kwa wafuâ.
Lengo la somo hili ni kuonyesha ushahidi dhabiti kwamba Yesu alifufuka kutoka kwa wafu, na umuhimu wa hili kwetu sisi.
Mt. 27: 62-66; Lk. 24: 1-47
ONYO LA MWISHO
Yesu alikufa katika Siku Maandalizi na siku iliofuata ilikuwa siku ta Sabato (Mt. 27:62; Lk 23:54). Makuhani wakuu na Mafarisayo walikuwa na wasiwasi kwamba mipango yao kumkamata haingefaulu. Woga uliwakumba kwani walivyokuwa wanamdhihaki Yesu, mbingu zikawa na giza na ardhi ikatetemeka. Walishtuka zaidi pale pazia la Hekalu lilipopasuka kuanzia juu mpaka chini (Mt. 27:51). Hizi zilikuwa ishara za kuonywa (linganisha Zab 18:6-8). Kama wangefaulu (dhidi ya Mungu) basi ingewabidi kuchukua kila onyo. Hivyo wakamuuliza Pilato mlinzi maalum na askari wa Kirumi ili kuhakikisha kwamba kaburi litakuwa limefungwa mpaka siku ya tatu. Walihofia kwamba wanafunzi wake wangeiba mwili kutoka kaburini na kudai kwamba âmdanganyifuâ amefufuka kutoka kwa wafu. Gavana alikubali ombi lao: â mna askari, nendeni mkalilinde salama kadiri mjuavyoâ. Na wakafanya hivyo kwa kutia jiwe alama na kulinda kaburi.
Ni jambo la kuchukiza kuona kwamba viongozi wa taifa lililochaguliwa walikuwa wanafanya wawezavyo kuzuia kufufuka kwa Masihi wao! Ilhali vitendo vyao vilikuwa vinadhibitisha ukweli wa kihistoria wa ufufuo wa Yesu. Kwani hakuna yeyote aliye mchukia Yesu kama wazee hawa? Nani katika karne zote angekuwa na makini ya kulinda kaburi? Kama jiwe hilo lingesonga, basi ingekuwa ni Mungu ambaye angekuwa amesababisha!
WANAWAKE WAFIKA KWANZA KABURINI (Lk. 24:1-10)
Wakati wanawake wa Galilaya waliondoka kaburini baada ya kutizama kwa makini mazishi yaliofanywa na Yosefu na Nikodema, waliamua kurudi na manukato na marhamu kukamilisha kuhifadhiwa kwa mwili wa Yesu (Lk 23:55-56; Mk 16:1) na hivyo, baada ya kumzika Sabato, wakaja asubuhi na mapema (RV) ya siku ya kwanza ya wiki , wakijiuliza wao wenyewe nani aliyeliondoa jiwe (linganisha Mk 16:3). Walipowasili, walikuta kwa mshangao wao kwamba jiwe lilikuwa limeondolewa kutoka kwa mlango wa kaburi na, zaidi ya hapo, mwili wa Bwana haukuwa katika kaburi! Mshangao wao uligeuka na kuwa woga kwani ndani ya kaburi kulikuwa na malaika wawili wenye mavazi ya kumeremeta wakatangaza kwamba Bwana amefufuka: âKwa nini mnamtafuta aliye hai kati ya wafu Hayupo hapa amefufuka!â Hivyo kaburi la kifo lilikuwa limeshindwa na kuwa mahali pa kuzaliwa kwa uzima (2 Tim. 1:10). Dhambi, mshika mateka wa binadamu, alikuwa sasa ameshikwa mateka (Efe. 4: 8; 1 Kor 15:55). Ni jambo la kutambua kwamba malaika walitambua Uongozi wa Kristo, na jinsi wanavyorejelea kwa heshima maneno yake ya hapo awali kuhusu kufufuka kwa wafu (linganisha Mathayo 28: 6; Lk 24: 7-8).
Kwa hofu na mshangao wanawake wale walirudi walikotoka kupitia mitaa ya utulivu wa Yerusalemu. Walikutana na kundi la wanafunzi waliokuwa na huzuni na waliopoteza mwelekeo (linganisha. Mk. 16:10). Habari hizi zilikuwa nzuri kuwa kweli, na hivyo ripoti ya wanawake hawa âkwao ilionekana maneno ya upuuzi na hawakuamini!â (Mst.11) Petro, pengine akiwa anafuatana na Yohana (linganisha Yohana 20:3-4) wakaelekea kaburini. Kule kwenye giza la kaburi angeweza kuona mavazi aliyo kuwa amevaa yamekunjwa vizuri na kuwekwa upande mmoja; lakini aliondoka kama hajaridhika licha ya kwamba Yesu alikuwa alikuwa amewaambia mara nyingi kuhusu ufufuko wake (Mk. 8:31; 9:31; 10:33-34).
MGENI KATIKA BARABARA YA EMMAU (Lk. 24:13-35; Mk. 16:12)
Huzuni iliyowakumba kundi la wanafunzi ililibadilika na kuwa kuchanganyikiwa. Matumaini yao yote yalikuwa kwa huyu Yesu wa Nazarethi: alikuwa Masihi mshindi aliyeahidiwa. Walikuwa wamemwona akichukuliwa na kusulubiwa.Na sasa hawakujua hata mwili wake ulikokuwa (Yn 20) Heshima yao kwake sasa ilikuwa imechanganyika na matumaini yaliyofifia, na wakaanza safari ya kuondoka Yerusalemu wakiwa na nyoyo nzito. Wanafunzi wawili walikuwa wanelekea Emmau, kijiji kidogo kilomita 11 kutoka Yerusalemu, pale mgeni alipo jiunga nao na kuwauliza ni jambo gani hilo la huzuni walilokuwa wakijadiliana (Lk 24: 13-17). Mmoja wao, Kleopa, alishangaa kwamba mgeni hakujua matukio ya kushangaza ya siku za hivi karibuni ambayo yalikuwa yamejaa Yerusalemu- kuhusu, Yesu wa Nazarethi, ânabii mwenye uwezo wa kutenda na kufundisha mbele ya Mungu na watu wote", na jinsi wakuu wa Kiyahudi walikuwa wamemtoa asulibishwe. Kleopa alielezea wazi imani yao ya hapo awali, âTuliamini yeye ndiye angeokoa Israeliâ. Ilikuwa siku ya tatu tangu Yesu asulubiwe, walikuwa wamepoteza imani katika madai yake ya Umasihi. Ingawa kulikuwa na mwanga wa matumaini kwamba wanawake fulani walikuwa wameelezea kuwepo kwa Malaika katika kaburi na kudai kwamba walikuwa wamepokea ujumbe kwamba Yesu alikuwa hai, hata hivyo wengine hawakuweza kumpata ingawa walipata kaburi likiwa tupu kama ilivyo ripotiwa (Mst.19-24)!
Mgeni alisikiza kwa makini mpaka pale Kleopa alimaliza kusimulia. Kisha akasema "Mbona mu wapumbavu na mioyo yenu ni mizito hivyo kusadiki yote yaliyonenwa na manabii: hayapaswi Kristo ( Gk. Ya âMesihi) kupitia mateso haya na kuingia katika utukufu?â kisha kwa njia kuu. Mgeni aliwaelezea ukweli wa Kristo kutoka kwa Musa na manabii wote. Wote wakashtuka na kushanga. Matamshi haya yalikuwa moja ya yaliyo makubwa katika historia ya Israeli. Agano la kale la Israeli likiwa na marejeleo ya ya mflame mwenye utukufu ambaye angeinua taifa na kuleta haki na amani kwa wote (Hes. 23:21; 24:17-19; 2 Sam 7; Zab 2; Mai 4: 1 -2). Hivyo Israeli walijua na walisubiri kutimizwa kwake. Hata hivyo kwa uwazi andiko linaongea kuhusu mtu wa chini ambaye atateswa na kufa kwa ajili ya dhambi, na kisha kufufuka kutoka kwa wafu.(Kut.12; Zab 22, 69, 118;. Isa 42, 50, 53;. Zek.13 : 7; Dan 9:26) kazi ya hapo awali ya Messia haikueleweka. Manabii na malaika walikuwa wameuliza maana ya mpangilio wa pande hizi mbili za kazi kuu ya Masihi (1 Pet 1: 10-12). Yesu, hata hivyo, alikuwa amewaambia mara kwa mara kuhusu udhalilishaji unaokuja, kifo chake na kufufuka kwake; upofu uliwazuia kukubali mambo haya. Sasa alikuwa nao, akiwa amefufuka kutoka kwa wafu, akielezea zaidi mambo yale walikuwa wameona na kusikia kutoka kwake katika siku zake za mwisho.
Muda ulipita haraka na kundi lile likafika Emau wakati wa jioni. Kleopa na mwenzake wakafanikiwa kumsihi âmgeniâ kukaa nao. Kulikuwa na kitu cha kuvutia kumhusu. Ingawa alikuwa amewaonyesha kutojua kwao, kitendo chake kilichofuata kilifufua matumaini yao ndani ya Yesu (mst.32). hivyo walitamani uwepo wake jioni hio, na watatu wale wakakaa chini na kula nyama pamoja (linganisha Ebr. 13: 2; Yn 14:23; Ufu 3:20). Mtakatifu Marko anatuambia katika tukio hili Yesu alionekana katika âumbo lingineâ (16:12). Na haikuwa mpaka pale alipochukua mkate,akaubariki, akaumega, akawapa,ndipo walipojua kwamba likuwa Bwana wao! Mara nyingi walikuwa wameshuhudia kitendo hiki cha kumega mkate (Mk 6:41; 8: 6; 14:22).
Kutokea kwa Bwana kulikuwa ni ushahidi dhahiri kwamba alikuwa amefufuka kutoka kwa wafu. Baada ya kutambulika alitoweka, akiwaacha na hali ya msisimko: âJe, mioyo yetu haikuwa inawaka ndani yetu hapo alipokuwa akisema nasi njiani, na wakati yeye alifungua kwetu maandiko?" (Mst.32). Wakaondoka na kushika njia yenye giza na kurudi Yerusalemu kuwapa habari njema wanafunzi wake
YESU ANAWATOKEA WANAFUNZI WAKE (Lk. 24:33-43)
Walipofika Yerusalemu, Kleopa, na wenzake waliwakuta wanafunzi wa Yesu wakiwa hai na ukweli kwamba Yesu alikuwa amefufuka, na alikuwa amemtokea Simoni" (linganisha 1 Wakorintho 15: 5)! Kwa furaha waliongeza ushahidi wa matukio yao wenyewe. Ghafla walipokuwa wakiongea Bwana akatokea miongoni mwao, baada ya kuona wasiwasi wao akasema, â Imani iwe kwenu...Tizameni mikono na miguu yangu, ya kuwa ni mimi mwenyewe: nishikeni na muone; kwani roho haina mwili wala mifupa kama ninayo mimiâ (Mst.36-39; 1 Yn 1: 1-2; linganisha 1 Kor.15:50). Wakatazama mikono na miguu iliyokuwa imechomwa misumari, hivyo kuashiria kubadilika kunakokuja kwa Israeli (Mst.10, Zk. 12:10). Ilikuwa jambo la ajabu kupokewa na mioyo yenye shaka ya binadamu. Hivyo wakati "hawakuwa wameamini kwa furaha", Yesu aliangiza chakula na akala mbele yao, kudhibitisha uwepo wake wa kimwili na uhai (Mst.41-43).
Lazima iwe Toma hakuweko wakati wa mkutano huu wa kwanza, lakini siku nane baadaye alihakikishiwa pia na akaamini ndani ya Mwana wa Mungu aliyefufuka kwa maneno, âBwana wangu na Mungu wangu" (Yn 20: 24-28 linganisha Yohana 10: 34-36). Mashaka yake ya hapo awali yakatumika kuonyesha kwamba kweli Yesu alikuwa amefufuka.
UFUFUKO WA YESUâJIWE LA MSINGI LA INJILI
Umuhimu wa mafundisho ya ufufuo hauwezi kusisitizwa zaidi. Kupinga ni kugeuza injili, kwani bila injili hakuna tumaini: "Kwa maana kama wafu hawafufuliwi, basi naye Kristo hakufufuka na kama Kristo hakufufuliwa, basi, imani yenu ni ya bure; mngali bado katika dhambi zenu" (1 Kor 15: 14-18; 2 Tim 2: 16-18). Ilikuwa msingi wa injili ya kitume. Bila kifo cha Yesu tamaa za mwili hazingeshindwa, wala bila ya haki ya Baba haki kwa ondoleo la dhambi haungetangazwa. Ufufuko wa Yesu ulikuwa majibu ya Mungu kwa ajili ya utiifu wa Mwana wake (1 Pet. 1:21). Haikuwa sawa kwa mwenye Haki ashikwe na machungu ya Kifo (1 Pet.1:21). Hivyo akatengeneza njia ya uzima kwa njia ya kaburi (1 Tim. 6:16; Yn 5:26). Maisha ya milele yanaweza kupatikana kupitia Jina la Kristo aliyefufuka (Mdo 4:12). Ubatizo unamtambulisha muumini na kuzikwa na kufufuka kwa Kristo: â"tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, na ili kama vile Yesu alifufuka kutoka kwa wafu kwa utukufu wa Mungu hata sisi pia tuweze kutembea katika uzima mpyaâ (Rum 6: 4; Kol 2: 12-13; 3: 1; Yn. 3: 5).
Katika wakati huu wa dhana za kijinga ni vyema kuchunguza hali ya kujiamini wanafunzi walikuwa nayo kuhusu ufufuko wa Kristo. Kwa ajili walisema: "Yesu huyu, Mungu alimfufua, na sisi sote ni mashahidi wa tukio hilo. Maneno haya yalielekezwa kwa kizazi kile kingepinga ukweli huu, na ambacho viongozi wake walikuwa na nia ya kufanya hivyo (Mdo 2:32). Lakini walikuwa kimya. Wanafunzi waliwafanya wengi kuwa na ujasiri na kuamini ufufuko wa Bwana (Mdo 2:24; 3:15, 26; 4:10, 33; 5:30; 10:40; 13:30, 33; 26:26 ). Tunaweza ondoa wasiwasi kwamba Yesu amefufuka na tuzidishe imani yetu kwake na katika ujio wake kama Mfalme juu ya ulimwengu hautakuwa wa bure.
MAMBO TUNAYOJIFUNZA:
- Ufufuo wa Kristo ukageuza huzuni kuwa furaha kwa mashaka ya wanafunzi.Inaweza kufanya hivyo kwa ajili yetu leo.
- Si wenye hekima na elimu wa dunia hii waliotafuta nguvu za ufufuo: wanawake na wavuvi wanyenyekevu walikuwa wa kwanza kuamini.
- Hatupaswi kuwa "wajinga na mioyo mizito kusadiki yote ambayo manabii walinena" (Lk. 24:25).
- Ufufuko wa Kristo ndio msingi wa kweli wa injili na historia. Hakuna hekima katika mfumo wowote wa mawazo ambayo haujajengwa juu yake.
MAKTABA YA KUREJELEA:
"A Life of Jesus" (M. Purkis)âKitabu 8, Sura 1 na 2
"Nazareth Revisited" (R. Roberts)âSura 59
"The Story of the Bible" (H. P. Mansfield)âTol. 12, Kurasa 150-158
MASWALI YA INSHA:
- Ni hatua gani wakuu walichukua kuhusu mwili wa Yesu? Jinsi gani hili linaimarisha imani yetu katika ufufuo wake?
- Ni wakati gani wanafunzi waliona majeraha katika mikono na miguu ya Yesu na wakaamini.Jinsi gani hili linatangulia ugeuzi wa Israeli?
- Kufa na kufufuka kwa Kristo ni mfano wa nini kwa muumini?
- Nini umuhimu wa ufufuo wa Kristo?
MASWALI YA AYA:
- Andika insha kuhusu mfufulizo ambao Yesu aliwatokea wanafunzi baada ya kufufuka kwake (kama katika Lka 24).
- Elezea matukio yaliyofuata wakati Yesu alijiunga na wanafunzi wawili akiwa njiani kuelekea Emau. Kwa jinsi gani kuelewa kwao kuhusu Masihi kulikuwa tofauti na maelezo yake ya kazi yake Umasihi?
- Ni ushahidi gani upo kwa ajili kuamini katika ufufuo wa Yesu Kristo kutoka kwa wafu? Nini tofauti gani hii inafanya katika maisha yetu?
- Andika matukio yaliyotokea wakati wanawake walikwenda kaburini la Kristo siku ya kwanza ya juma.