Nani awezaye Kuhubiri?
Anayehubiri lazima aelewe kile anachohubiri. Ni lazima wajue mafundisho vizuri na wafahamu vifungu vinavyohusika.
Mhubiri si lazima awe mzungumzaji mzuri. Mtume Paulo alikuwa mhubiri mkuu, lakini hakuwa mzungumzaji mzuri. “Lakini nijapokuwa mimi ni mtu asiyejua kunena, hii si hali yangu katika elimu; ila katika kila neno tumedhihirishwa kwenu.” (2 Wakorintho 11:6). Wala hakuwa mzuri kwa maneno, “sikuja niwahubiri siri ya Mungu kwa ufasaha wa maneno” (1 Wakorintho 2:1).
Mhubiri hana budi kuwa mfano wa tabia njema. Watu hawatasikiliza ikiwa mhubiri hatatekeleza kwa vitendo kile anachohubiri.
Paulo aliweka mfano mzuri wa tabia alipowafundisha wengine. Alitoa ushauri huu, “katika mambo yote ukijionyesha wewe mwenyewe kuwa kielelezo cha matendo mema, na katika mafundisho yako ukionyesha usahihi na ustahivu, na maneno yenye uzima yasiyoweza kuhukumiwa makosa, ili yule mwenye kupinga atahayarike, kwa kuwa hana neno baya la kunena juu yetu.” (Tito 2:7,8).
Mhubiri hufundisha kwa maneno yake NA tabia yake.
Mafarisayo walikuwa walimu waliozoezwa na wasemaji wazuri. Lakini hawakuweka mfano sahihi. Yesu alisema, “lakini kwa mfano wa matendo yao, msitende; maana wao hunena lakini hawatendi.” (Mathayo 23:3).
Ni kwa matendo mhubiri anajulikana kweli. Kama tunavyoijua miti kwa matunda yake, vivyo hivyo walimu hujulikana kwa matunda yake, “Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri; na mti mwovu huzaa matunda mabaya. Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mwovu kuzaa matunda mazuri. Kila mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwa motoni. Ndiposa kwa matunda yao mtawatambua.” (Mathayo 7:17-20).
Ni lazima tujitayarishe kwa kuhubiri kama Paulo alivyoshauri, “Hata nitakapokuja, ufanye bidii katika kusoma na kuonya na kufundisha... Jitunze nafsi yako, na mafundisho yako. Dumu katika mambo hayo; maana kwa kufanya hivyo utajiokoa nafsi yako na wale wakusikiao pia.” (1 Timotheo 4:13,16).
Ni lazima wahubiri waendelee kuishi katika njia ifaayo na Mungu la sivyo hawataokolewa. Paulo alijua hili. Alisema, “bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwahubiri wengine, mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa.” (1 Wakorintho 9:27).