CSSA 3-2-294 - DAVID—CHOSEN BY GOD

Swahili

294. DAUDI—ALIYECHAGULIWA NA MUNGU

"Binadamu anatazama uzuri wa nje, lakini Mungu anaangalia roho"

 

Amri ya Mungu ya kuangamizwa kabisa kwa watu waMaleki haukusikilizwa na Sauli. Badala yake alifanya kulingana na mapenzi yake. Hakutambua kwamba Mungu anapenda moyo wa kumtumikia. Tabia aliyokuwa nayo Sauli katika utawala wake ilikuwa ni ile ya kutotii (1 Sam. 13:08, 9, 14) (15:16-23) kwa sababu hii alikataliwa kama mfalme wa Israeli.

Hata hivyo Mungu alikuwa na nia ya kutawala watu wake kupitia mtu atakayejichagulia yeye mwenyewe(1 Sam 13:14;. Mat. 13:22) Mflame huyu angekuwa “Mtu anayependwa na moyo wa Mungu”. Chaguo lake lilikuwa Daudi aliyekuwa mchugaji na ambaye maisha yake yalikuwa yanamfaa mpaka pale alipokuwa Mfalme wa Israeli  na kuwaangamiza Maadui wa Mungu.

Lengo letu katika somo hili ni kuona kwamba Mungu anataka tuwe watiifu kwa maagizo yake na kwamba uchaguzi wake unafanywa kwa misingi ya ujuzi wa nia za kidani lakini sio mtazamo wa nje.

 

1 Samweli 16: SAMWELI ANATUMWA BETHLEHEMU (1 Sam. 16:1-5)

Samweli alikuwa bado anaomboleza mfalme aliyepotea wakati alisikia neno kutoka Kwa Mungu “kwa muda gani utazidi kuomboleza Sauli, na unaona nimemkataa kama Mfalme wa Israeli? Jaza upembe wako mafuta uondoke, nakutuma kwa Yese Mbethlehemu; kwa maana kuna mfalme  kwa mmoja wa wanawe” baadaye iliandikwa kwa zaburi “ nimempata Daudi mtumishi wangu, na nimemchagua kwa mafuta yangu matakatifu” (Zab. 89:20)

Samweli alikuwa anaogopa kwenda kumteua hadharani mfalme mpya wakati mfalme wa zamani akiwa bado anatawala, sababu kuu ilikuwa Sauli alikuwa amegeuka na kuwa mtu mwenye vurugu, wivu, hasira na hofu. Kwa hivyo Samweli alienda hadi Bethlehemu kwa amri ya Mungu ili akatoe sadaka lakini ilikuwa kwa njia ya siri kumchagua mtu aliyezaliwa kuwa Mfalme. Alipowaona wana wale aliwaona wasiofaa kuchukua jukumu hili kuu. Lazima tuangalie suala hili kulingana na mazingira ya wakati ule. Kumtangaza Daudi hadharani kama mridhi wa Sauli ungeleta maafa Bethlehemu hasa kwa familia ya Yese, kwani miaka iliyofuata tunaona Herode akiwauwa watoto wote katika sehemu hii akijaribu kumuua Yesu aliyekuwa amezaliwa.

Kuwasili kwa Samweli Bethlehemu kulileta hali ya mshtuko kwani Bethlehemu haikuwa miji ambayo alipitia sana katika safari zake. (1 Sam. 7:16).

Wakuu wa Bethlehemu walidhania kwamba Samweli alikuwa amekuja kuchunguza uovu uliokuwa umejificha. “ je umekuja kwa imani?”  walifurahi waliposikia nabii akisema “kwa imani, nimekuja kumtolea Mungu sadaka”

UCHAGUZI WA MUNGU (1 Sam. 16:6-11)

Jesse na wanawe walipata mwaliko maalum kwenda kwa mlo wa sadaka. Samweli aliwahesabu wana wa Yese. Kifungua mimba aliitwa Eliabu ndiye alionekana kama anaweza kuwa Mfalme.  Nabii alimtizama kwa furaha mtu ambaye kwa umbo na kimo angeweza kuwa mfalme.

Samweli aliomba ushauri wa Mungu. Asili ya mazungumzo haya yanaonekana wazi. Sauti ya Mungu ilikuwa iko wazi na ya kueleweka na inaonekana kama ilikuwa nafsi ya pili ya Samweli.  Hii haikuwa fikra ya kiroho lakini ilikuwa sauti ya Mungu kama vile Samweli alivyoisikia na kuielewa. Isitoshe yale Samweli aliyoyasikia hakuyatarajia. “usiangalia uso wala urefu wa mwili wake kwani nimemkataa; Mungu haangalii kama vile binadamu anavyoangalia umbo la nje lakini Mungu anaangalia roho. (Mst.7) Huu ilikuwa msingi wa kanuni za Kimungu na sio tu kwa kuchanguliwa kwa  Daudi kama kiongozi bali ni kwa kila mtu atakayekuwa katika Ufalme wa Mungu. (Ufu. 2:23) “ Nimemkataa” ilimaanisha kwamba roho yake haikukubalika machoni mwa Mungu.

Kila moja wa vijana saba walikuwa nyumbani mwa Yese walikataliwa “Yahweh hajawachagua” Samweli akamwambia Yese. Samweli alikataa kukaa chini ili ale chakula mpaka kijana wa nane ambaye familia yake haikuona haja ya kumwalika kwa karamu ya sadaka aletwa kutoka malishoni.

UPAKO (1 Samweli 16:12-13)

Ingawa Daudi alikuwa "mdogo"  kuwa mamlakani, alikuwa mtu aliyependwa na Moyo wa Mungu (13:14) Daudi alituza kondoo wa baba yake na hii ingekuwa iwe kazi yake ya maisha (Zab. 78:70-72) Watu mashuhuri waliokuja mbele walikuwa wametayarishwa kwa mabadiliko ambayo yangefuata- Abeli, Ibrahimu, isaka, Yakobo na Musa. Daudi aliwatambua kondoo wake kwa jina na aliwaongoza kupata malisho na maji. Alitibu vidonda vyao na kuwalinda na maisha yake kutokana na wanyama wa mwitu kumaanisha walikuwa na maisha sawa usiku na mchana. Kazi hii ya uchungaji iliunda tabia na kukuza akili yake awe mtu wa kutegemewa na mwenye kuwajali wengine, upendo na kujitolea zilibaki ndani yake mpaka siku za mwisho wa maisha yake.(Linganisha 2 Sam. 24:17) Alitambua jinsi Mungu alikuwa mchungaji mkuu wa Israeli.

Maisha yake Kama mchungaji pia yalimfanya kuelewa ukuu wa Mungu kama Muumbaji. Alipokuwa amelala katika vilima vya Judea usiku aliwaza kuhusu kazi ya ajabu ya Mungu na akavutiwa kujifunza sharia zake. (Zab. 19; 119:9)

Daudi alikuwa na jicho kali, mwili mwepesi na nywele ya kupendeza kama rekodi inavyoonyesha, Daudi alisimama mbele ya Samweli. Amri ya Mungu katika masikio ya Samweli ilikuwa kali na ya haraka “Amka, mmwangilie mafuta, kwani yeye ndiye” (16:12). Upembe wa mafuta ulimwangiliwa kwa kichwa chake akiwa amesima kati ya ndugu zake. Kile walichokuwa wakifikiria hakikurekodiwa. Maneno na vitendo vya baadae vinaonyesha wivu kama uliokuwa na ndugu za Yosefu. (17:28;.. Linganisha Zab 23:05) kile ambacho Daudi alifikiria kingeweza kuadhimisha neema hii haijandikwa katika maandiko lakini katika Zaburi 23 haya yameandikwa. Hii ilikuwa moja ya pako nne za Daudi, kati ya hizo tatu zilifanywa na binadamu Bethlehemu, Hebroni and Yerusalemu na ingine ulifanywa na roho wa Mungu kwa mkono wa Samweli pale nyumbani.

 

 

                                                                  DAUDI NA MWANAWE MKUU ZAIDI

    Chati Ifuatayo inaonyesha mfano kati ya Daudi na Yesu kristo, kuanzia mwanzo wa maisha ya Daudi.

DAUDI

YESU KRISTO

Alitambuliwa katika nyumba ya Yese Bethlehemu na Samweli ambaye alifanya kazi sawa na Yohana mbatizaji.

Mwana mkuu wa Daudi alizaliwa Bethlehemu (Lk. 2:04) na alitambulika kama Messia na Yohana mbatizaji (Yohana 1:29, 31, 36)

Kama mchungaji alitayarishwa kuwaongoza waIsraeli  (Zab. 78:70-72)

Mchungaji wa binadamu (Mko 6:34;. Isa 40:11), Mchungaji mzuri atatoa maisha yake kwa ajili ya kondoo wake (Yohana 10:11).

Hakuwa amependwa na Ndugu zake

Ndugu zake hawakumjali (Zab. 69:7-9;. Isa 53:2-4; Yohana 7:05)

Alipata upako wa roho uliokuwa mfano wa mafuta ya upako

Alipata upako kwa njia ya roho wakati wa ubatizo (Mat. 3:16-17) na alipofufuka akawa "kristo" —"mwenye Upako'* (Mat. 2:36).

 

 

UMUHIMU WA KIROHO WA UPAKO WA DAUDI

Upako kwa kutumia mafuta ilikuwa njia ya Mungu rasmi ya kuwachagua wafalme na makuhani kwenye vyeo (linganisha Law. 8:12) Mafuta inaonyesha roho wa Mungu (2 Kor. 1:21-22) na kumwangiliwa kwenye kichwa kunaonyesha kukubaliwa na Mungu. Maana yake Mungu anamtenga mtu kwa kazi maalum) baada ya kupewa roho kwa Daudi upako ulifuata (1 Sam. 16:13) Upako huu wa Daudi unatabiria ule wa Messiah. Yesu alipata upako wa kiroho wakati wa ubatizo na Mungu alionyesha kumkubali  kwa maneno haya “ Huyu ni mwanangu mpendwa, ambaye ninapendezwa naye” (Mat. 3:17; kuona pia Isa 61:1;. Heb . 1:09;. Yn 3:34) Mwishowe alikubalika na Mungu kwa utii wake hadi kifo wakati Mungu alimfufua kutoka kwa wafu. Alipewa sifa na nafsi ya kuishi milele.Petro alisema kwamba kwa kufufuka Mungu alimfanya Bwana na Kristo” (Mdo 2:36; 3:13)

 

MAFUNZO KWETU

  • Kijana au binti wa kweli wa Mungu, kama Samweli ataomboleza  wakati  wengine kama Sauli wanapotoka kwenye njia nyembamba. Wanaomboleza jamii isiyo na tamaa ya Sayuni.
  • Hali ya nje haimfurahishi  Mungu. Anaangalia roho na anatamani wale ambao wanajitolea kufuata njia zake na kutenda kwa njia ya hiari.
  • Tunaweza kushiriki  katika kutoa sadaka ya kristo tukiwa pamoja na ndugu zetu iwapo tunaweza kukubali nguvu ya neno la Mungu kushawishi maish yetu.
  • Wanadamu katika dunia wanaweza tukosea dhamani kama vile ndugu wa Daudi walifanya, lakini ni  maoni ya Mungu na wala sio maoni ya binadamu yanayoamua hatima yetu.
  • Wale ambao wanatambua kwamba Yahweh “anaangalia roho” watajitahidi na kubadili maisha yao kufananisha na Daudi “mtu aliyependwa na moyo wa Mungu” na mwanawe mkuu Yesu kristo Mteuliwa.
     

MAKTABA YA KUREJELEA:

"The Ways of Providence" (R. Roberts)—sura 15

"The Visible Hand of God" (R. Roberts)—sura 23

“The Story of the Bible” (H. P. Mansfield)—Tol. 3, Nam. 8

"The Man David" (H. Tennant)—kur. 19-23

 

MASWALI YA AYA:

  1. Kwa nini Samweli alisita kwenda Bethlehemu, kumpaka mafuta Daudi? Nini ilikuwa sababu yake halisi ya kukataa kwenda?
  2. Kuna somo gani kwetu katika uchaguzi wa Daudi  kama mfalme badala ya ndugu zake?
  3. Jinsi gani maisha ya Daudi ya awali kama mchungaji kulimtayarisha kuwa Mfalme?

MASWALI YA INSHA:

  1. Linganisha tabia ya Sauli na Daudi
  2. Ni sifa gani zilimfanya Daudi kuwa Mfalme?
  3. Linganisha kuchanguliwa na upako wa Daudi na ule wa Yesu Kristo.
  4. “Binadamu anaangalia hali ya nje lakini Yahweh anaangalia roho” (1 Sam 16:07.); kwa wingi wa roho mdomo hunena (Mat. 12:34) ni kanuni gani zinazotumika katika nukuu hizi? Kwa njia gani nukuu hizi zinaonekana katika uchanguzi wa Daudi na kukataliwa kwa Saul?
  5. Elezea upako wa Daudi na Samweli.

 

 

  1. Samweli anamteua Daudi mbele ya familia yake kule Bethlehemu kisha anarudi nyumbani Rama (1 Sam. 16:1, 13).
  2. Daudi anacheza kinubi chake mbele ya Mfalme Sauli kule Gibea (16:21; 15:34).
  3. Daudi anapigana na Goliathi kwenye bonde la Elani (17:1-2, 20). Wafilisiti wanafukuzwa hadi Ekroni (17:52).
  4. Daudi anarudi kwenye ikulu ya Sauli (18:2) ambapo anapata rafiki Jonathani lakini hii inakuwa chanzo cha wivu kwa Sauli, baada ya mafanikio yake ya wafilisiti (18:3-8).
  5. Kwa Msaada wa Mikaeli, Daudi anatoroka na kwenda kwa Samweli kule Naiothi in Rama (19:18).
  6. Baada ya kupokea ishara kutoka Jonathani kwamba maisha yake yako hatarini kutoka kwa Saul (20:1, 33-37), Daudi alikimbilia Nob, mahali kwa makuhani (21:1).
  7. Akichukua mkate uliokwa na upanga wa goliath, anatoroka kwa Mfalme wa Akishi Gathi ambapo aliweza kutoroka kwa kujifanya kichaa. (21:10-13).

 

 

Swahili Title
294. DAUDI—ALIYECHAGULIWA NA MUNGU
English files
Swahili file
Sub type
Sub sub type