318. UFALME UNAAGUSHWA
"Nitaipindua, nitaipindua; na haitakuwa tena, mpaka atakapokuja yule ambaye ana haki; nami nitampa"
Kifo cha haraka cha mgeuzi aliyejitolea wa Yuda, Yosia, aliyetengeneza njia ya hukumu ya Bwana juu Yuda. Mfalme wao alikuwa, kwa bidii amesima kwa ajili ya Ukweli ili azuie hukumu inayokuja. Lakini miaka 120 baada ya kuanguka kwa Israeli, Yuda pia iliingia kwa rushwa ya uasi. Walikuwa wamepata upendeleo wa umuhimu katika akili ya Mungu kwa ajili ya Daudi na agano lake, kwa Yerusalemu kuwa âmji uliochanguliwa na Jina lake kuwekwa paleâ, na kwa sababu ya makuhani na Walawi waliojaribu kuimarisha mambo yaliyobakia. Licha ya haya, wafalme wanne baada ya Yosia walikuwa waovu. Waliharakisha kiwango cha uozo wa kiroho na hivyo siku ya uhamisho ikakaribia.
Lengo letu katika somo hili ni kuona jinsi hukumu iliotangazwa na Mungu dhidi ya Yuda ilifikia kwa mujibu na maneno ya manabii wake. Neno hilo limetaja uharibifu wa watu wa mataifa katika siku ya mwisho.
ASHURU INAANGUKA, BABELI INAIMARIKA.
Ngome ya Mwashuri ya Nineve ilishikwa katikati, wakati Cyaxeres wa Media na Nabopolassar wa Babeli (Babake Nebukadreza) walishambulia mji. Nineve ilianguka katika mwaka wa 612 kabla Yesu. Utawala ukagawanyika na Media ikanyakua upande wa kaskazini na kaskazini Mashariki, na Babeli Kusini na Kusini Magharibi. Hii ni pamoja na Ashuru, Palestina na Misri. Jeshi la Ashuru lilikuwa dhaifu likaondoa nguvu zake hadi kaskazini mwa Shami kule Harani.
Misri ilitaka kuhifadhi Ashuru kama nguzo ya mji, na kwa hivyo wakaenda kuwasaidia Washuru (2 Fal. 23. 29-30). Kama Farao â Neko alielekea Kaskazini, Yosia aliamua kuingilia kati, licha ya onyo la Wamisri walishambulia Misri kule Megido. Yosia alijeruhiwa vibaya vitani.
Hivyo wakati wa mgogoro wa kimataifa, Yuda ilikosa mgeuzi wake aliyejitolea. Hii ilikuwa hasara kubwa na ilimaanisha kifo kwa Yuda. Nabii Hulda alikuwa amemwambiaYosia, âmacho yako hataona mabaya yote ambayo mimi nitaleta mahali hapaâ (2 Fal. 22:20); Wanawe waovu walikuwa wajiletee wenyewe majanga yaliyokuja (Sef. 1: 8.).
WAFALME WANNE WALIO ZIDISHA UOVU WA YUDA.
Yosia aliwaacha wanawe watatu, Eliakim, miaka 25, (2 Fal. 23:36.), Shalumu, wenye umri 23 (2 Fal. 23:31; Yer. 22:11) Na mwana mdogo, Matania wenye umri 10 (2 Fal. 24: 17-18).
Shalumu: Kufuatia kifo cha Yosia, watu wa Yuda walimteua mwanawe wa pili wa Yosia, Shalumu, kama mfalme wao. Walibadilisha jina lake kutoka Shalumu hadi Yehoahazi ("Bwana huidhinishaâ). Alionekana kama âsimba mchangaâ (Eze. 19:. 3, 5), lakini alishindwa kuishi kulingana na jina lake na pia kulingana na matarajio ya watu. Mungu hakumuidhinisha, kwani baada Farao Neko alishindwa katika msaada wake wa Ashuru ( Baada ya Nabopolassar kumaliza kuangushwa Ashuru) Wamisri walirudi na kuweka Yuda chini ya Kodi. Walimwondoa Yehoahazi, ambaye alitawala miezi mitatu pekee, walamtupa jela Ribla na hatimaye wakamtorosha hadi Misri alikofia (2 Fal. 23:33; 2 Nya. 36: 1-3; Yer. 22:12).
Eliakimu: Mwana mkuu wa Yosia, Eliakimu ("El ataanzisha") ilianzishwa na Farao-Neko kama mfalme- kibaraka (2 Nya. 36:. 4-8). Wamisri walibadilisha jina lake na kumuita Yehoyakimu ("Yah anaanzisha"), lakini, kama mtangulizi wake, yeye pia hakufaa jina lake. Alihitajiwa kulipa kodi ya juu kwa Misri. Kuwezesha hili aliweka kodi ya juu kwa taifa na wakati huu ulikuwa wakati wa ukame (Yer.14: 1.). Nabii Yeremia alishutumu tamaa ya Yehoyakimu. Alijenga majumba ya kifahari katika wakati huo mgumu na kufanyisha watu kazi ya lazima (Yer. 22: 13-19).
Mbali na kurudi katika njia za Yosia, kama alivyoelekezwa na manabii, alirudia tabia mbovu za Manase. Alikuwa âmwovu na asiye na haki, wala mtakatifu kwa Mungu, wala mvumilivu kwa watuâ akaandika Yosephus (Ant. X, 5, 2). Kiwango cha haraka cha uoza wa kiroho ulisisitiza haja ya haraka ya kuondoa, aliokuwa nayo Mungu.
Ilikuwa katika mwaka wa tatu wa utawala wa miaka kumi na moja ya utawala wa Yehoyakimu wakati Nebukadreza alienda kuunganisha nguvu, hasa dhidi ya Wamisri (Dan. 1: 1, 2 Fal. 24: 1). Majeshi mawili makuu yalipambana katika vita vikuu vya Karmeshi katika Frati. Nebukadreza alipata ushindi, hivyo kutimiza utabiri wa nabii Yeremia (46: 5-11). Akiwa na nia ya kuongeza ushindi wake, Mbabiloni alielekea kusini na kuteka Yerusalemu. Hata hivyo alisimamishwa kwa ghafla katika kampeni yake ya kusini na kifo cha babake kule Babeli. Kwa haraka alimweka Yehoyakimu chini ya kodi, na alidai kwamba kodi iliokuwa inapelekwa Misri, ipelekwe Babeli. Alinyakua baadhi ya vyombo vya Hekalu kama nyara za vita (2 Nya. 36: 7), akachukua mateka wachache kutoka kwa familia ya kifalme hadi Babeli. Danieli alikuwa miongoni mwa wale waliofukuzwa kutoka uhamisho wa Kibabeli (Dan. 1: 1-3.).
MFALME MUASI WA YUDEA NA MTAWALA MNYENYEKEVU WA BABELI
Katika mwaka wa nne na wa tano wa utawala wa Yehoyakimu, Yeremia aliweka kumbukumbu ya ujumbe wa Mungu katika kitabu, akiwa na matumaini ya kwamba Yuda watashika onyo hili la hukumu inayokuja na kutubu. Hata hivyo, mfalme wao mwenye kiburi na wa kidunia, aliposikia kilichosomwa kutoka kwa kitabu, alikikatakata vipande and kukiharibu kwa moto (Yer. 36: 20-26). Kwa kiburi alifikiria kwamba angeweza kudharau na kubughudhu hukumu ya Bwana.
Na bado katika mwaka huo huo (mwaka wa tano wa Yehoyakimu ulilingana na mwaka wa pili wa utawala wa Nebukadreza), Mfalme wa Babeli, mkuu wa himaya ya dunia, alitambua kwamba Mungu ni âMungu wa miungu, na Bwana wa Wafalme, na mfumbuzi wa siri"(Dan. 2:47). Tazama tofauti â mflame mwovu, na muasi Yehoyakimu, na mnyenyekevu mfalme Nebukadneza: mmoja aliye dharau Neno la Mungu na mwengine aliye heshimu Neno la Mungu. Majibu ya Yehoyakimu ya kukataa ushauri wa Bwana ulisababisha kuongezeka kwa nia yake ya kutoa adhabu dhidi yake. Biblia inatuonyesha ujinga wa Mfalme na taifa kwa kina kwa ajili ya kusoma kwetu na kutuonya. âWacha tutambue kwamba hakuna hekima, wala ufahamu, wala ushauri, juu ya Bwana" (Mit. 21:30, tazama pia 1: 27-30; 5: 11-12; 13:13; 19:21; 29: 1 ).
Yehoyakimu alilipa kodi kwa miaka mitatu, mpaka Nebukadreza alipopata kikwazo katika shambulizi lake la Wamisri. Akiwa tayari kugeukia Misri, Yehoyakimu bila kujali alidhania kwamba nguvu za Babeli zilikuwa zimeshindwa. Lakini Nebukadreza aliunganisha majeshi yake na alikuwa tayari kumwadhibu Yehoyakimu na majeshi ya kawaida (2 Fal. 24. 1, 2). Hatimaye Nebukadreza aliamua kumwangamiza muasi Yehoyakimu yeye mwenyewe. Akamfunga na minyororo ili kumpeleka Babeli, lakini akaonekana kubadilisha fikra zake na kumtupa juu ya ukuta wa Yerusalemu, ambapo alipotelea kama vile Yeremia alikuwa ametabiri (Yer. 22:18, 19; 36:30; 2 Nya. 36: 6).
YEHOYAKINI: Mabwana wa Babeli walimweka Yehoyakini, aliyejulikana kama Yekonia ama Konia (1 Nya. 3:16; Yer. 22: 24-28) mwana wa miaka kumi na nane wa Yehoyakimu, kama mridhi wa kiti. Jina lake lilimaanisha âYah ataanzishaâ, lakini utawala wake wa miezi mitatu na siku kumi uliashiria tofauti (2 Nya. 36: 9; 2 Fal. 24: 8.). Nebukadreza alibadilisha fikra zake kuhusu uteuzi wa Yehoyakini, akarejea na kumchukua yeye, mamake na mateka wengine 10,000 hadi Babeli. Mji ukaanguka katika mwaka wa 597 Kabla ya Yesu na kati ya mateka hawa wengi walikuwa matajiri na wakutajika. Miongoni mwa mateka walikuwa Ezekiali na Mordekai.
Yekonia aliendelea kuishi miaka mingi Babeli na kupokea mambo mazuri kutoka kwa Wana wa Nebukadreza. Ni jambo la kuvutiaa kuona mjukuu wake, Zerubabeli, alikuwa mmoja wa viongozi wa kurudi kutoka uhamishoni (Ezra 3: 2; Hag. 1: 1).
SEDEKIA: Mfalme wa mwisho wa Yuda na mwana mchanga wa Yosia, Matania, aliwekwa na Wababeli juu ya taifa lililofifia. Ezekieli alimwita, sio mflame, bali âmkuu mwovuâ (21:25).Jina lake lilibadilishwa na akaitwa Sedekia ("Mwenye haki wa Yahâ) kama ishara ya ushirikiano wake na Wababeli.
Siku hizi za mwisho zilikuwa na alama ya uasi wa kiroho na uozo wa kimaadili (Eze. 8-11;. 22). Sedekia, kwa msaada wa mahakama ya kimisri, alikuwa anasumbuliwa kwa ajili ya nira ya Wababeli na kugeukia Misri kwa msaada (Yer. 27). Upande huu hakuwa wa kisiasa tu, bali ulikuwa ukiukaji wa kiapo chake cha utii kwa Nebukadreza (Eze. 17). Uzito kamili wa hasira za Mungu ulikuwa tayari kumwangiliwa juu ya Yuda.
Utawala wa miaka kumi na moja wa Sedekia ulifikia kikomo wakati Nebukadreza alipoizinguka Yerusalemu kwa miezi kumi na minane yenye machungu. Mji uliadhirika na ukame na ukaanguka mwaka wa 586 Kabla Kristo (2 Fal. 24: 18-25: 7; 2 Nya. 36: 10-21; Yer. 52: 1-11.). Sedekia alijaribu kutoroka akijificha gizani lakini alikamatwa. Alivurutwa mbele ya Nebukadreza, akalazimishwa kutizama kuuawa kwa wanawe wawili. Kisha macho yake yakangolewa. Kama mfungwa mnyonge alipelekwa Babeli pamoja na wale walionusirika mauaji haya ya kutisha ya kuangushwa kwa Yerusalemu. Walio maskini ndio walioachwa katika nchi.
"NITAPINDUA . . . HADI ATAKAPOKUJA".
Hadi mwisho wenye machungu, huruma ya Bwana ilionekana katika kutuma manabii kuwaonya na kuwahimiza watu wa Yuda. Huruma yake ilikuwa kwa watu wake na katika makao yake. Lakini âwalimdhihaki mjumbe wa Mungu, na kudharau maneno yake, na kuwacheka manabii wake, mpaka hasira ya Bwana ilipoinuka dhidi wa watu wake, mpaka kukawa hakuna msamahaâ (2 Nya. 36:15, 16). Hivyo kutimiza unabii, â kiondoe kilemba, ivue taji...... nitakipindua, nitakipindua, nitakipindua" (Eze. 21: 26-27).
Nchi ilifurahia Sabato, hata kipindi cha miaka sabini ya mapumziko (2 Nya. 36:21;. 25:11 Yer.12; 29:12). Kiti cha Daudi kingebaki bila mfalme mpaka, kama ilivyotabiriwa katika Eze. 21: 25-27, mmoja atatokea â ambaye ni haki yake; na nitampaâ. Hii haingetokea kama matokeo ya kurudi kutoka utumwani, kwani ilikuwa ni alama ya heshima ya mpango wa baadaye. Yeye âambaye ana hakiâ alikuwa Mwana mkuu wa Daudi na mwana wa Mungu (2 Sam. 7 12-14.), mtawala mwenye haki (2 Sam. 23: 3; Isa. 11: 1-15) Masihi aliye uawa(Zab. 22; Isa. 53) na Mfalme aliyefufuka wa laini ya Melkizedeki (2 Sam. 07:16; Zab. 110: 1-4). Katika Yeremia 23: 5, 6 na 33: 14-16 na 33: 14-16 mfalme huyu mkuu wa laini ya Daudi anaelezewa kama âTawi la Hakiâ kuinuliwa juu hadi kwa Daudi. Kutawala na kufanikiwa na kuunganisha Israeli na Yuda chini ya jina lake la kifalme la "Bwana haki yetu ". Atakuwa mwaminifu kwa jina hili. Jina Sedekia pia linaanisha "Haki ya Yah", lakini hakuishi kulingana na maana ya jina yake.
Huyu Mfalme, ni Bwana Yesu Kristo na kama ilivyoahidiwa kwa Maria, "Yeye atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa Aliye juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake" (Lk. 1: 31-33). Yeye aliye uliwa atarudi hivi karibuni na âkutawala kwa hakiâ (Isa. 32: 1.). Hapo ndipo âWenye haki watanawiriâ na kufurahia katika "wingi wa amani" (Zab. 72: 7.; 37:11).
MAMBO TUNAYOJIFUNZA:
- Ulimwengu wa Mataifa ambayo sisi tunaishi unakaribia siku maalumu wakati Mungu atahukumu ulimwengu kwa haki.
- Tufanye bidii kushikilia imani, kama alivyofanya Yeremiah, au tupotoshwe na mvuto wa nyakati zetu wa kuharibu imani.
- Je, tunaweza kumwamini Bwana au tutaweka imani yetu katika Misri, kama walivyofanya wafalme wa Yuda?
- Ni lazima tuamue "kuimarisha mambo ambayo ni ya kubaki" na kuwasaidia wale wa imani ya thamani.
- Ni hivyo tu, tunaweza kuangalia zaidi ya mawingu na dhoruba ya hukumu zinazatokea, kwa ushiriki katika utawala wakati nguvu za Daudi zinaanzishwa upya.
MAKTABA YA KUREJELEA:
"The Story of the Bible" (H.P. Mansfield) â Tol. 6, Nam. 5-9
"Josephus" (Antiquities) â Kitabu 10, Sura. 5-8
"The Ministry of the Prophets â Jeremiah" (C.C. Walker)
"The Book of the Prophet Ezekiel" (W.H. Boulton)
MASWALI YA AYA:
- Nini maana ya jina la Mfalme Sedekia? Jinsi gani hii ilifanywa kuwa somo katika unabii?
- Andika maelezo mafupi juu ya Mfalme Yehoyakimu na utawala wake.
- Elezea ushindani wa nguvu kati ya Misri, Ashuru na Babeli kuhusiana na Yuda wakati wa uhamisho wake.
MASWALI YA INSHA:
- Ni lipi kosa thabiti katika mitazamo ya wafalme wa mwisho wa Yuda?
- Kwa kifupi onyesha jinsi wana watatu wa Yosia walishindwa kuishi kulingana na majina yao yaliyobadilishwa.
-
"Mimi nitakipindua, nitakipindua, nitakipindua; na hakitakuwa tena, hata atakapokuja yeye ambaye ni haki yake; nami nitampa" (Eze. 21: 25-27.).
(a) Wakati gani maneno haya yalisemwa na kwa nani?
(b) Nani anayezungumziwa katika maneno "mpaka yeye atakapokuja"?
(c) Ni nini yeye atapewa na nafasi yake itakuwa ipi?
4. Elezea mashambulizi yaliyofanywa na Babeli dhidi ya Yuda ambayo yalielekea kutekwa mateka kwa Babeli.
SEHEMU YA 3: UHAMISHO NA KURUDI
Adhabu ilikuwa kidonda kwa taifa la Israeli. Wimbi baada ya wimbi la watekaji nyara walishuka kutoka kaskazini, wakiwachukua watu kutoka kwa nyumba, mashamba, miji na hata hekalu zao. Vichwa vyao viliinamia chini wakilia walipokaa chini katika mito ya Babeli na kukumbuka Sayuni.
Hata hivyo, katikati ya ukosefu wa uhamisho, mabadiliko yalikuja juu ya watu. Ezekieli nabii alinena kuhusu sababu ya uhamisho, haja ya kutubu na utukufu wa taifa katika siku za usoni. Marafiki wa Danieli walijitenga na ibada ya sanamu wa Babeli na kuonyesha utii wa amri za Mungu. Danieli mwenyewe, kwa hekima aliyopewa na Mungu, alifanya hata mtawala mkuu wa Babeli kukiri kwamba kulikuwa na mfalme Mbiguni ambaye ana udhibiti wa vyote duniani.
Polepole watu waliokuwa uhamishoni walirudishwa kwa Mungu wao, hivyo kwamba wakati miaka 70 ilikamilika na Koreshi na Ferushi wakatoa amri, na malefu walifurahia kumfuata Zerubabeli hadi nchi ya baba zao na kujenga tena hekalu la Mungu wao.
Ezra aliwasili katika eneo, kisha Nehemia, na kwa umbali walisikia sauti za manabii Hagai, Zekaria na Malaki. Juhudi za kishujaa za watu hawa waaminifu chini ya magumu ya kufanya kazi ya Mungu inatupa kumbukumbu ya kufurahisha, na mfano wenye nguvu kwa wale wote ambao katika umri wowote, wanajenga kwa ajili ya Ukweli.