338. UNAJISI NA UNAFIKI
"Kile kitokacho kinywani, ndicho kinanajisi binadamu"
Ukuu wa umaarufu wa Bwana ulikuwa umefika kwa kulisha watu 5,000. Kisha ikafikia hatua ya kugeuka kwa utoaji wa hotuba yake Kapernaumu ambayo iliwakasirisha wengi wa wanafunzi wake hivyo hawakutembea tena naye. Kufuatia tukio hili nguvu za upinzani zikaanza kujiunga.
Kundi la Waandishi na Wafarisayo wakaja kwa Yesu kuhusu swala la unajisi kwa kutoosha mikono. Yesu akawakemea kwa unafiki wao, akielezea kwamba unajisi unatoka kwa kutoosha nyoyo na fikra zao.
Kukataliwa kwa Yesu na Wayahudi kulikuwa faida kwa Watu wa Mataifa, kwani Yesu alielekea Kaskazini hadi mipaka ya Tiro na Sidoni kule alipopata mwanamke mwaminifu wa Mataifa. Aliporudi Galilaya alipata Watu wa Mataifa waliomsifu Mungu wa Israeli na ambao katika umati wa 4,000 walipokea mkate kutoka mbiguni.
Lengo la somo hili ni kuonyesha kwamba utamaduni wa binadamu anaweza kukandamiza amri za Mungu na kwamba unajisi una asili yake katika moyo wa binadamu.
Mathayo 15: 1-31
MASHINDANO YA DINI (Mathayo. 15:1).
Wafarisayo walikuwa wametengeneza dini kulingana na utaratibu. Ingawa njia yao ilikuwa na misingi ya Sheria za Musa na viwango vya maadili walivyoweka vilikuwa juu (Mt. 23: 3) lakini walikuwa wamepuuza nguvu iliokuwa nyuma ya sheria- "Mpende Bwana Mungu kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili yako yote, na kwa nguvu zako zote "(Mk.12:30). Walikuwa wanashughulika na sheria na taratibu za nje na hizi zikawa dini yenyewe.
Kwa akili wa Wafarisayo mbinu hii alikuwa na "faida"; ilifanya âdiniâ rahisi kuadhimisha, na cha muhimu zaidi, ilifanya rahisi kuchunguza mapungufu ya wengine. (kama wafarisee walivyowaona) ikiwa ni pamoja na Bwana Yesu Kristo!
Suala liliungana ambapo Waandishi na Wafarisayo ambao walikuwa wameumwa kutoka Yerusalemu walimkabili Yesu: "Kwa nini wanafunzi wako wanadharau tamaduni za wazee?â ilikuwa ni mashindano ya dini ambapo hakungekuwa na maelewano. Aidha madai ya Mungu yanahusisha utiifu wa sheria na maadili ya nje, bila kujali mawazo na makusudi ya moyo, zilikuwa na utiifu uliotoka mioyoni na akilini ukizingatia maadili ya Mungu.
UTAMADUNI WA VIONGOZI (Mt. 15:2).
Mafarisayo walihisi kwamba walikuwa na kesi kuu dhidi ya Kristo; â Wanafunzi wako hawanawi mikono wanapokula mkateâ. Yesu alikuwa amewalisha watu 5,000 jagwani (Mt.14:20, 21). Hawangeweza kufuata njia ya Mafarisayo ya kuoga, kwa kuinua mikono yao juu kwa utaratibu baada ya kuoga ili mikono yote ijae maji na ili maji yaliyochafuka yasishuke hadi kwa vidole vyao na kuwachafua tena.
Kwa kuzingatia mambo hayo madogo, Mafarisayo walisahau maswala yenye maana ya Sheria, haki, huruma na imani (Mt. 23: 23-24). Walionekana wasafi kwa samani zao, lakini hawakujali kwamba chakula ambacho walikuwa wanakula kilikuwa kimepatikana kwa njia ya hila na udanganyifu (Mk 7: 4).
UTIIFU UNAKANDAMIZWA NA TAMADUNI (Mt. 15:3-9).
Yesu hakusimama kuhalalisha wala kuomba msamaha kwa wanafunzi wake. Badala yake aligeuza swali lile kwa Waandishi na Mafarisayo; âKwa nini ninyi mnavunja amri ya Mungu kwa tamaduni zenu?â kulikuwa na tofauti kati ya âtamaduni za binadamuâ na âamri za Munguâ. Tamaduni za binadamu ziliweka kando amri za Mungu, na pia kuzibadilisha ili ziweze kutosheleza tamaa za kibinafsi za binadamu.
Yesu alitoa mfano wa jinsi tamaduni za wazee zilitofautiana na Sheria ya Mungu. Mungu aliamuru kwamba Baba na Mama waheshimiwe kwa matendo na maneno, ili, katika wakati wa haja, wanapaswa kusaidiwa. Zaidi ya hayo, ilitishia adhabu kali dhidi ya wale ambao waliwadharau ou kuongea kwa dharau dhidi ya wazazi wao- kanuni ambazo zinatumika leo kama wakati wa Musa (Met 20:20; 30:17; Efe 6:2). Hata hivyo tamaduni za wazee ziliwaepusha wanadamu kutoka kwa majukumu haya kama wangetoa kwa ukarimu kwa hazina za Hekalu. Hivyo amri za Mungu zilifutiliwa mbali na tamaduni za binadamu (Mst.6) Yesu aliwaita Mafarisayo âwanafikiâ, kwani ingawa walijifanya waabudu wa Mungu, walikuwa wanaweka tamaduni za binadamu mbele.
Isaya alitabiri kuhusu kundi kama hilo la binadamu, âWatu hawa wananitaja kwa vinywa vyao, na kunisifu kwa vinywa vyao; lakini nyoyo zao ziko mbali nami. Wananiabudu bure, wakifunza mafundisho yaliyo maagizo ya binadamuâ(29:13).
UNAJISI NA CHANZO CHAKE (Mt. 15:10-20)
Basi, Yesu akageuka na kuita umati uje kwake, akitangaza, âSi kile kiingiacho kinywani kimtiacho mtu unajisi, bali kile kitokacho kinywani ndicho kimtiacho mtu unajisi." Kimsingi waandishi walikuwa wamekosea. Walifikiria kwamba maadhimisho yangeweza watakasa nafsi ya ndani. Lakini Yesu aliweka rekodi sawa- hakuna haja kuacha nyama chafu kama matendo sio katika kuweka kanuni zilizoonyeshwa. Sheria ya Mungu imewekwa ili kugeuza nyoyo na hivyo kubadili fikra, maneno na matendo ambayo ni masuala ya moyoni.
Lakini baadhi ya wanafunzi wa Yesu hawakuwa wanazingatia mafunzo yake. Walikuwa na wasiwasi zaidi kuhusu mbinu yake ya moja kwa moja. Isitoshe, Mafarisayo walikuwa adui mwenye nguvu na hatari. Hivyo, pengine kwa sauti ya upinzani, walimwonya Yesu, âWajua ya kwamba Mafarisayo wamechukizwa?" Walitaka Ukweli alionena ukarabatiwe ili uwe âunakubalikaâ katika macho ya dunia. Lakini hili halingewezekana. Katika uchambuzi wa mwisho ni Mafarisayo na wala sio Kristo ambaye angebanduliwa: âwaacheni, wao ni viongozi vipofu wa vipofu. Na kama kipofu anamwongoza kipofu, wote wataanguka kwenye shimoâ.
Hata wanafunzi wa karibu walishtuka. Baada ya kurudi kwa nyumba walitaka kuelezwa zaidi. Maelezo yalikuwa rahisi lakini ya msingi. Chochote kiingiacho ndani ya binadamu kutoka nje huenda tumboni, bila kupitia moyoni. Chakula chote ni safi, kwani zinawezaje kuadhiri jinsi ya kufikiri kwa binadamu?
Chanzo cha unajisi kiko kwa binadamu mwenyewe. Moyo wa binadamu unakabiliwa na dhambi. Umekosa ufahamu wa Neno la Mungu, na utazaa fikra ambazo zitawaelekeza kutenda matendo ya dhambi. Yereremia aliuta âunafikiâ (Yer. 17:9). Binadamu hahitaji shetani wa nje kumfanya atende dhambi, tamaa yake inamfanya kutenda dhambi (Yak.1:14-15).
Kisha Yesu akaorodhesha mambo ambayo yalikuwa yamefichwa moyoni. Moyo ni chanzo cha âmauajiâ na, zaidi ya hayo chanzo cha mawazo yote yakipata nafasi ya kuendelea, yanasababisha mauaji. "Uzinzi" na "uasherati" zimetajwa. Uzinzi unahusisha uvunjaji wa ahadi takatifu inayofanywa na mshirika mwengine wa ndoa; uasherati unahusisha ukosefu wa uaminifu kwa mchumba wa ndoa wa siku za usoni, na zote ni dhambi dhidi ya Mungu (Mwa. 39: 9; Zab. 51: 4). Hivyo aina zote za uovu wa kijinsia umegusiwa. âWiziâ unahusisha kumwibia Mungu pamoja na wanadamu wenzetu. âUshahidi wa Uwongoâ ni kuharibu sifa ya mwengine. âkufuruâ ni dhambi dhidi ya Mungu.
Na hivyo uovu wa Moyo unaendelea. Marko katika maelezo yake anahusisha orodha kamili (Mk 7: 21-22). Ni dhahiri kwamba katika orodha za dhambi Yesu alihusisha fikra, maneno na matendo. Kwa hivyo dhambi zinapinga sheria za Mungu katika fikra, maneno na matendo. Mtu ananajisiwa na mambo haya, wala sio kula kwa âmikono michafuâ
IMANI YA MWANAMKE WA MATAIFA (Mt. 15:21-28)
Mgongano na Waandishi na Mafarisayo ulikuwa na matokeo ya ajabu. Hatari iliyomkabili Yesu ilimfanya aondoke na kuelekea Kaskazini hadi mipaka ya Tiro na Sidoni. Sehemu hii ilikuwa ya watu wa Mataifa ilio wachiwa wale âwalionajisiwaâ. Hakuna Mfarisayo ama Mwaandishi angepatikana huko.
Lakini kwa Yesu, Tiro na Sidoni haikuwa mbaya kuliko Korazini na Bethsaida (Mt.11:21). kwa matendo yake Yesu aliondoa tofauti zilizokuwepo kati ya watu kama vile maneno yake yalikuwa yameondoa tofauti kati ya chakula.
Wakati huo huo mwanamke wa Kifinisia aliyejaa mashaka alikuwa anamsumbua Yesu. Binti yake alikuwa mgonjwa sana. Matumaini yake yalikuwa kwa Yesu pekee. Alijitupa miguuni mwake: "Unirehemu, Bwana, Mwana wa Daudi".
Lakini hakukuwa na jibu. Hakuna neno la kufariji lililotajwa.
"Mwambie aende zake" huu ulikuwa ushauri wa wanafunzi wake waliokosa subira. Waliunga mkono wazo la Mafarisayo; alikuwa wa taifa chafu (Kum 7: 1-2).
Kwa Yesu hakukuwa na mgawanyiko kama huo. Imani, na wala sio mahali pa kuzaliwa, ilimfanya mtu kukubalika na Mungu. Hata hivyo imani yake ilihitaji kuimarishwa- alihitaji kufahamu uhusiano wake na Israeli: "Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli", Yesu alisema.
Aliendelea kwa maombi yake ya dhati, âBwana, nisaidieâ. Hiki kilikuwa kilio cha wokovu, lakini wokovu ulikuwa wa âWayahudi pekeeâ (Yn. 4:22). âsi vizuri kuchukua chakula cha watoto (Israeli), na kuwatupia mbwa (Mataifa)". Mwanamke alirejelea maneno ya Yesu: â Ni kweli, Bwana: lakini hata mbwa hula makombo yanayoanguka kutoka meza ya bwana waoâ. Maneno yake yalikuwa na uzito, pengine hata zaidi ya alivyoelewa. âWatotoâ walikuwa wamekataa âmkate wa uzima (Yn. 6). Yesu alikuwa amesukumwa hadi kwenye ukingo wa âmezaâ. Na âMakomboâ yalikuwa yameanguka kwa Mwanamke kutoka Watu wa Mataifa miguuni mwake.
Yesu aliguswa na jibu lake; Ewe, Mwanamke, imani yako ni kubwa; na iwe kwako hata kama utakavyo wewe". Kwa imani na sio matendo ya Sheria âMwanamke wa Kaananiâ alikubalika mbele ya macho ya Mungu (linganisha Efe. 2:8-9; Mdo 14:27). Na katika upande huo wa mpaka, katika nchi ya Galilaya iliyodharauliwa, msichana mdogo alihisi nguvu na uhai ukurudi katika mwili wake.
KUREJEA DEKAPOLI (Mt. 15:29-31)
Kutoka mipaka ya Tiro na Sidoni, Yesu aliongoza kundi dogo la wanafunzi mpaka kwa kingo za magahribi za ziwa la Galilaya, katika sehemu ya Dekapoli, kipande cha ardhi kilichomilikiwa na Watu wa Mataifa: Isaiya aliita "Galilaya ya mataifa"(9: 1).
Kulikuwa na mlima katika eneo ambalo lingewachukiza Mafarisayo lakini kuwachangamsha wale waliojua kwamba uanafunzi ulitegemea mawazo ya moyo, na sio kabila wala ibada. Kwani katika mlima âumati mkubwaâ wa Watu wa Mataifa âulijitupa chini ya miguu ya Yesu; naye aliwaponyaâ.
Kulikuwa na tofauti kubwa, wale waliweza, kutembea, kuona na kunena katika Israeli waligeuza nyoyo zao dhidi ya Yesu: lakini "vilema, vipofu, na bubu" wa Mataifa walijitahidi kufika juu ya mlima kuja kwa Yesu. Wakamwabudu "Mungu wa Israeli".
MAMBO TUNAYOJIFUNZA:
- Hatupaswi kuona Ukweli kama mfululizo wa sheria ambazo tunaweza kutumia kuwahukumu wengine.
- Ukweli unapaswa kuathiri makusudi ya mioyo yetu na kupata kuelezwa kwa maneno na matendo kwa mujibu wa amri za Mungu.
- Kama moyo wa mtu haudhibitiwi na sheria za Mungu, basi ni chanzo cha uovu wote.
- Kwa nje, kabila au rangi hazina tofauti katika macho ya Mungu-mkate wa uzima unapatikana kwa wote.
MAKTABA YA KUREJELEA:
"A Life of Jesus" (M. Purkis)âKitabu 5, Sura 4 na 5
"The Gospel of the Son of God" (L. G. Sargent) Sehemu IV, Sura 2, 3
MASWALI YA INSHA:
- Yesu alisema nini kuhusu moyo wa binadamu wakati alipokuwa akifundisha juu ya chanzo cha unajisi?
- Jinsi gani amri "Waheshimu baba yako na mama yako" ilifutilia mbali na "tamaduni za wazee"?
- Ni kwa misingi gani ombi la mwanamke Mkanaani lilijibiwa na Yesu? Yesu alisema nini?
MASWALI YA INSHA:
- Kwa njia gani "Tamaduni za wazee" zinaenda kinyume na amri za Mungu? Toa mfano.
- Yesu aliwaonyesha Mafarisayo kwamba mawazo yao kuhusu kunajisi yalikuwa na makosa. Elezea kile alifundisha kuhusu udhalilishaji na chanzo cha dhambi.
- Elezea kile kilichotokea wakati Yesu alifuatwa na "Mwanamke Mkanaani" wakati alikuwa katika mkoa wa Tiro na sidoni.