Correspondance Course - Lesson 54

SOMO LA 54

KUCHAGUA MCHUMBA

SOMO: 1 Wakorintho 7

Mungu alipokuwa akiwaumba watu, alimuumba kwanza mwanamume. Baada ya hapo alimuumba mwanamke kwa namna aliyoona inafaa, baada ya kuona haifai mwanamume awe peke yake (Mwanzo 2:18). Kwa hiyo mpango wa uumbaji ni wa mume na mke kuwa wamoja katika maisha yao yote.

Correspondance Course - Lesson 53

SOMO LA 53

KUJAMIIANA, Zawadi kutoka kwa Mungu

SOMO: Mwanzo 19

Kama unaamini kwamba Mungu alimuumba mwanadamu awe kiumbe aliye bora zaidi kati ya wanyama wengine, utaamini pia kwamba ndiye aliyeubuni mwonekano wa miili yetu ya ajabu; ndiye aliyetupa miguu na mikono na viungio vyake na misuli. Alitupa akili yetu na uwezo wa kufikiri na kupanga, kutii au kutotii.

Correspondance Course - Lesson 52

SOMO LA 52

MFUASI NA NCHI

SOMO: Warumi 13

Mtume Petro alipokuwa akiziandikia eklesia zote katika Asia alisema kwamba, wafuasi wa Yesu ni lazima wamche Mungu na kumheshimu mfalme (1 Petro 2:13-17). Kwa wakati huo, mfalme pekee alikuwa Mfalme wa Kirumi, na kwa wakati huo wa mwisho-mwisho wa maisha ya Petro, mfalme huyo alikuwa Nero, aliyekuwa ‘balaa’ kwa ukatili wake na kwa jinsi alivyowatesa Wakristo.

Correspondance Course - Lesson 51

SOMO LA 51

MATUMIZI NA UDHIBITI WA HASIRA

SOMO: Mwanzo 34

Hasira ni hisia ya ajabu sana ndani ya uanadamu wetu. Pengine ina nguvu hata zaidi katika ulimwengu wa wanyama, ndege na samaki. Katika Biblia kuna ushauri mzuri unaotolewa wa namna ya kuidhibiti hasira, na kuna maonyo kadhaa ya wazi kuhusiana na nini kitatokea kama tukiiachia hasira itutawale.

Correspondance Course - Lesson 50

SOMO LA 50

UAMINIFU MBELE YA MUNGU NA MBELE YA MWANAWE YESU KRISTO

SOMO: Matendo 5

Katika somo hili, nataka tuangalie kwa makini mambo tunayofanya kila siku. Baadhi yake yatakuwa ni kwa ajili ya Mungu na Yesu, kama kuhubiri kwa wengine au kuwasaidia wagonjwa na wazee. Mengine yatakuwa ni kwa kuhudumia familia au kuipa mwelekeo fulani, au wale tunaowajibika kwao.

Matendo mengine yote yatakuwa yakiwahusu watu tunaokutana nao kila siku kwenye shughuli, au safari au kwenye lolote linaloweza kutokea.

Correspondance Course - Lesson 49

SOMO LA 49

NI SAWA KUWA NA TAMAA?

SOMO: Mathayo 18

Maelezo ya Mathayo juu ya maisha na mafundisho ya Yesu, ni pamoja na misemo kadhaa inayohusu tamaa za kibinadamu. Maelezo hayo yote yanalaani au kutuonya dhidi ya msukumo wa tamaa, ambao ni kitu chenye nguvu katika hulka yetu.

Wanafunzi wa Yesu walielekea kuwa na tatizo la: nani angekuwa mkubwa zaidi katika kikundi chao, ukimwondoa Yesu? Inaonekana lilikuwa jambo waliloliona la muhimu kwao kwa wakati huo, na inaelekea walibishania mara nyingi.

Correspondance Course - Lesson 47

SOMO LA 47

MAFUNDISHO YA BIBLIA KUHUSU MATESO

SOMO: Waebrania 12

Mateso ni tatizo katika maisha na yanaweza kumpata mtu yeyote. Mtoto anazaliwa kipofu, au amelemaa na tunajiuliza, ni kwa nini? Mtoto hajakosea kitu. Wanaume kwa wanawake, vijana kwa wazee, matajiri kwa maskini, wanapatwa na maumivu ya magonjwa ya hatari yanayoweza tu kuishia kwenye kufa. Kwa nini wateseke?

Correspondance Course - Lesson 46

Somo la 46

KUMPENDA JIRANI YAKO

Somo: Luka 10

Katika somo hili tutaangalia zaidi maagizo ya Yesu kuwa, kama kweli tunataka tuwe wafuasi wake, ni lazima tuoneshe katika maisha yetu kiwango kisicho cha kawaida cha upendo kwa watu wengine. Mahali pa kuanzia pa somo hili ni mfano wa Msamaria-mwema uliotajwa katika somo letu lililopita. Tunapoangalia kwa ukaribu maneno ya Yesu katika Luka 10:30-37, tunaona mambo kadhaa ya muhimu.        

Correspondance Course - Lesson 45

Somo la 45

NAMNA TUNAVYOWAFIKIRIA WATU WENGINE NI MUHIMU KWA MUNGU

Somo: Yakobo 2

Yesu alipojaribiwa siku moja  na mmoja wa madaktari wa Sheria ya Kiyahudi, juu ya amri iliyo kuu kuliko zote, alijibu kuwa ni kumpenda  Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, nguvu zako zote, na akili yako yote, na jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe. Kwa ajili ya kuelezea maana aliyokuwa nayo ya ‘jirani’, aliendelea kwa kutoa mfano wa Msamaria aliyekuwa mwema. Unaweza kusoma juu yake katika Luka 10:25-37.